Surah: AL-BAQARAH 

Ayah : 25

وَبَشِّرِ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّـٰلِحَٰتِ أَنَّ لَهُمۡ جَنَّـٰتٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُۖ كُلَّمَا رُزِقُواْ مِنۡهَا مِن ثَمَرَةٖ رِّزۡقٗا قَالُواْ هَٰذَا ٱلَّذِي رُزِقۡنَا مِن قَبۡلُۖ وَأُتُواْ بِهِۦ مُتَشَٰبِهٗاۖ وَلَهُمۡ فِيهَآ أَزۡوَٰجٞ مُّطَهَّرَةٞۖ وَهُمۡ فِيهَا خَٰلِدُونَ

Na wape bishara wale walioamini na kufanya matendo mema kuwa, watapata bustani zitiririkazo mito chini yake. Kila wanapopewa riziki ya matunda humo wanasema: Hii ndio ile riziki tuliyopewa kabla. Na wamepewa riziki hiyo ikiwa inafanana. Na watapata humo wake waliotwaharishwa, na watabaki humo daima



Surah: AL-IMRAN 

Ayah : 15

۞قُلۡ أَؤُنَبِّئُكُم بِخَيۡرٖ مِّن ذَٰلِكُمۡۖ لِلَّذِينَ ٱتَّقَوۡاْ عِندَ رَبِّهِمۡ جَنَّـٰتٞ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ خَٰلِدِينَ فِيهَا وَأَزۡوَٰجٞ مُّطَهَّرَةٞ وَرِضۡوَٰنٞ مِّنَ ٱللَّهِۗ وَٱللَّهُ بَصِيرُۢ بِٱلۡعِبَادِ

Sema: Je, nikupeni habari ya vilivyo bora zaidi kuliko hivyo? Wenye ucha Mungu tu watapata kwa Mola wao bustani zipitazo mito chini yake, watakaa humo milele na (pia watapata) wake waliotakaswa na radhi za Allah, na Allah ni Mwenye kuwaona sana waja



Surah: AL-IMRAN 

Ayah : 16

ٱلَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَآ إِنَّنَآ ءَامَنَّا فَٱغۡفِرۡ لَنَا ذُنُوبَنَا وَقِنَا عَذَابَ ٱلنَّارِ

Ambao wanasema: Ewe Mola wetu, hakika sisi tumeamini, hivyo tusamehe dhambi zetu na tukinge na adhabu ya Moto



Surah: AL-IMRAN 

Ayah : 17

ٱلصَّـٰبِرِينَ وَٱلصَّـٰدِقِينَ وَٱلۡقَٰنِتِينَ وَٱلۡمُنفِقِينَ وَٱلۡمُسۡتَغۡفِرِينَ بِٱلۡأَسۡحَارِ

Na wafanyao subira na wasemao kweli na wanaotii na wanaotoa (walivyojaaliwa na kuwapa wengine) na wanaoomba msamaha usiku wa manane



Surah: AL-IMRAN 

Ayah : 133

۞وَسَارِعُوٓاْ إِلَىٰ مَغۡفِرَةٖ مِّن رَّبِّكُمۡ وَجَنَّةٍ عَرۡضُهَا ٱلسَّمَٰوَٰتُ وَٱلۡأَرۡضُ أُعِدَّتۡ لِلۡمُتَّقِينَ

Na ukimbilieni msamaha wa Mola wenu Mlezi na Pepo (ambayo) upana wake ni mbingu na ardhi, iliyoandaliwa kwa ajili ya wacha Mungu



Surah: ANNISAI 

Ayah : 57

وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّـٰلِحَٰتِ سَنُدۡخِلُهُمۡ جَنَّـٰتٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ خَٰلِدِينَ فِيهَآ أَبَدٗاۖ لَّهُمۡ فِيهَآ أَزۡوَٰجٞ مُّطَهَّرَةٞۖ وَنُدۡخِلُهُمۡ ظِلّٗا ظَلِيلًا

Na walioamini na wakatenda mema tutawaingiza katika Pepo zipitazo mito chini yake, wakibaki humo milele. Katika Pepo hizo watakuwa na wake waliotakaswa, na tutawaingiza katika vivuli vinavyofunika daima



Surah: ATTAUBA 

Ayah : 72

وَعَدَ ٱللَّهُ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ وَٱلۡمُؤۡمِنَٰتِ جَنَّـٰتٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ خَٰلِدِينَ فِيهَا وَمَسَٰكِنَ طَيِّبَةٗ فِي جَنَّـٰتِ عَدۡنٖۚ وَرِضۡوَٰنٞ مِّنَ ٱللَّهِ أَكۡبَرُۚ ذَٰلِكَ هُوَ ٱلۡفَوۡزُ ٱلۡعَظِيمُ

Allah amewaahidi Waumini wanaume na Waumini wanawake Pepo zipitazo mito mbele yake, watadumu humo milele, na (pia amewaahidi) makazi mazuri katika Pepo za kudumu. Na radhi za Allah ndio jambo kubwa zaidi. Huko ndiko hasa kufuzu kukubwa



Surah: AR-RA’D 

Ayah : 35

۞مَّثَلُ ٱلۡجَنَّةِ ٱلَّتِي وُعِدَ ٱلۡمُتَّقُونَۖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُۖ أُكُلُهَا دَآئِمٞ وَظِلُّهَاۚ تِلۡكَ عُقۡبَى ٱلَّذِينَ ٱتَّقَواْۚ وَّعُقۡبَى ٱلۡكَٰفِرِينَ ٱلنَّارُ

Mfano wa Pepo waliyoahidiwa wacha Mungu, inapita mbele yake mito, matunda yake hayana msimu, na pia kivuli chake. Huu ndio mwisho wa wale waliojilinda. Na mwisho wa makafiri ni Moto



Surah: AL-HIJRI 

Ayah : 45

إِنَّ ٱلۡمُتَّقِينَ فِي جَنَّـٰتٖ وَعُيُونٍ

Hakika wanaomuogopa Mola wao watakuwa katika Pepo na chemchem



Surah: AL-HIJRI 

Ayah : 46

ٱدۡخُلُوهَا بِسَلَٰمٍ ءَامِنِينَ

(Wamchao Allah wataambiwa:) Ingieni (Peponi) kwa salama na amani



Surah: AL-HIJRI 

Ayah : 47

وَنَزَعۡنَا مَا فِي صُدُورِهِم مِّنۡ غِلٍّ إِخۡوَٰنًا عَلَىٰ سُرُرٖ مُّتَقَٰبِلِينَ

Na tutaondoa (kwa watu wa Peponi) chuki iliyokuwamo vifuani mwao, wawe ndugu juu ya viti vya fahari wakiwa wameelekeana



Surah: AL-HIJRI 

Ayah : 48

لَا يَمَسُّهُمۡ فِيهَا نَصَبٞ وَمَا هُم مِّنۡهَا بِمُخۡرَجِينَ

Hautawagusa humo uchovu, wala humo hawatatolewa



Surah: AL-KAHF 

Ayah : 31

أُوْلَـٰٓئِكَ لَهُمۡ جَنَّـٰتُ عَدۡنٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهِمُ ٱلۡأَنۡهَٰرُ يُحَلَّوۡنَ فِيهَا مِنۡ أَسَاوِرَ مِن ذَهَبٖ وَيَلۡبَسُونَ ثِيَابًا خُضۡرٗا مِّن سُندُسٖ وَإِسۡتَبۡرَقٖ مُّتَّكِـِٔينَ فِيهَا عَلَى ٱلۡأَرَآئِكِۚ نِعۡمَ ٱلثَّوَابُ وَحَسُنَتۡ مُرۡتَفَقٗا

Hao watapata Bustani za milele, zinazo pita mito kati yake. Humo watapambwa kwa mavazi ya mikononi ya dhahabu, na watavaa nguo za kijani za hariri na at’ilasi, huku wakiegemea humo juu ya makochi. Ni malipo bora hayo! Na matandiko mazuri mno ya kupumzikia!



Surah: MARYAM 

Ayah : 61

جَنَّـٰتِ عَدۡنٍ ٱلَّتِي وَعَدَ ٱلرَّحۡمَٰنُ عِبَادَهُۥ بِٱلۡغَيۡبِۚ إِنَّهُۥ كَانَ وَعۡدُهُۥ مَأۡتِيّٗا

Bustani za milele alizo waahidi Rahmani waja wake katika siri. Hakika ahadi yake hapana shaka itafika



Surah: MARYAM 

Ayah : 62

لَّا يَسۡمَعُونَ فِيهَا لَغۡوًا إِلَّا سَلَٰمٗاۖ وَلَهُمۡ رِزۡقُهُمۡ فِيهَا بُكۡرَةٗ وَعَشِيّٗا

Humo hawatasikia upuuzi, ila Salama tu. Na watapata humo riziki zao asubuhi na jioni



Surah: MARYAM 

Ayah : 63

تِلۡكَ ٱلۡجَنَّةُ ٱلَّتِي نُورِثُ مِنۡ عِبَادِنَا مَن كَانَ تَقِيّٗا

Hiyo ndiyo Pepo tutakayo warithisha katika waja wetu walio kuwa wacha Mungu



Surah: AL-HAJJ 

Ayah : 23

إِنَّ ٱللَّهَ يُدۡخِلُ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّـٰلِحَٰتِ جَنَّـٰتٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ يُحَلَّوۡنَ فِيهَا مِنۡ أَسَاوِرَ مِن ذَهَبٖ وَلُؤۡلُؤٗاۖ وَلِبَاسُهُمۡ فِيهَا حَرِيرٞ

Hakika Allah atawaingiza walio amini na wakatenda mema katika Bustani zipitiwazo na mito kati yake. Watapambwa humo kwa mapambo ya mikononi ya dhahabu na lulu. Na mavazi yao humo ni hariri



Surah: AL-HAJJ 

Ayah : 24

وَهُدُوٓاْ إِلَى ٱلطَّيِّبِ مِنَ ٱلۡقَوۡلِ وَهُدُوٓاْ إِلَىٰ صِرَٰطِ ٱلۡحَمِيدِ

Na wataongozwa kwenye maneno mazuri, na wataongozwa kwenye Njia ya Msifiwa



Surah: FAATWIR 

Ayah : 33

جَنَّـٰتُ عَدۡنٖ يَدۡخُلُونَهَا يُحَلَّوۡنَ فِيهَا مِنۡ أَسَاوِرَ مِن ذَهَبٖ وَلُؤۡلُؤٗاۖ وَلِبَاسُهُمۡ فِيهَا حَرِيرٞ

Mabustani ya milele watayaingia. Huko watavikwa vikuku vya dhahabu, na lulu, na nguo zao humo ni za hariri



Surah: FAATWIR 

Ayah : 34

وَقَالُواْ ٱلۡحَمۡدُ لِلَّهِ ٱلَّذِيٓ أَذۡهَبَ عَنَّا ٱلۡحَزَنَۖ إِنَّ رَبَّنَا لَغَفُورٞ شَكُورٌ

Na watasema: Alhamdulillahi, Sifa njema zote ni za Allah aliye tuondolea huzuni zote. Hakika Mola wetu Mlezi bila ya shaka ni Mwenye kusamehe, Mwenye shukrani



Surah: FAATWIR 

Ayah : 35

ٱلَّذِيٓ أَحَلَّنَا دَارَ ٱلۡمُقَامَةِ مِن فَضۡلِهِۦ لَا يَمَسُّنَا فِيهَا نَصَبٞ وَلَا يَمَسُّنَا فِيهَا لُغُوبٞ

Ambaye kwa fadhila yake ametuweka makao ya kukaa daima; humu haitugusi taabu wala humu hakutugusi kuchoka



Surah: YAASIIN 

Ayah : 55

إِنَّ أَصۡحَٰبَ ٱلۡجَنَّةِ ٱلۡيَوۡمَ فِي شُغُلٖ فَٰكِهُونَ

Hakika watu wa Peponi leo wamo shughulini, wamefurahi



Surah: YAASIIN 

Ayah : 56

هُمۡ وَأَزۡوَٰجُهُمۡ فِي ظِلَٰلٍ عَلَى ٱلۡأَرَآئِكِ مُتَّكِـُٔونَ

Wao na wake zao wamo katika vivuli wameegemea juu ya viti vya fakhari



Surah: YAASIIN 

Ayah : 57

لَهُمۡ فِيهَا فَٰكِهَةٞ وَلَهُم مَّا يَدَّعُونَ

Watapata humo kila namna ya matunda na watapata kila watakacho kitaka



Surah: YAASIIN 

Ayah : 58

سَلَٰمٞ قَوۡلٗا مِّن رَّبّٖ رَّحِيمٖ

“Salama!” Hiyo ndiyo kauli itokayo kwa Mola Mlezi Mwenye kurehemu



Surah: ASSWAAFFAAT 

Ayah : 41

أُوْلَـٰٓئِكَ لَهُمۡ رِزۡقٞ مَّعۡلُومٞ

Hao ndio watakao pata riziki maalumu,



Surah: ASSWAAFFAAT 

Ayah : 42

فَوَٰكِهُ وَهُم مُّكۡرَمُونَ

Matunda, nao wataheshimiwa



Surah: ASSWAAFFAAT 

Ayah : 43

فِي جَنَّـٰتِ ٱلنَّعِيمِ

Katika Bustani za neema



Surah: ASSWAAFFAAT 

Ayah : 44

عَلَىٰ سُرُرٖ مُّتَقَٰبِلِينَ

Wako juu ya viti wanatazamana



Surah: ASSWAAFFAAT 

Ayah : 45

يُطَافُ عَلَيۡهِم بِكَأۡسٖ مِّن مَّعِينِۭ

Wanazungushiwa kikombe chenye kinywaji cha chemchem