Surah: AL-BAQARAH 

Ayah : 20

يَكَادُ ٱلۡبَرۡقُ يَخۡطَفُ أَبۡصَٰرَهُمۡۖ كُلَّمَآ أَضَآءَ لَهُم مَّشَوۡاْ فِيهِ وَإِذَآ أَظۡلَمَ عَلَيۡهِمۡ قَامُواْۚ وَلَوۡ شَآءَ ٱللَّهُ لَذَهَبَ بِسَمۡعِهِمۡ وَأَبۡصَٰرِهِمۡۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٞ

Umeme unakaribia kupofoa macho yao. Kila unapowaangazia wanatembea katika mwanga huo, na pale unapowazimikia wanasimama. Na kama Allah angelitaka basi, kwa yakini kabisa, angeondoa kusikia kwao na macho yao. Hakika, Allah ni muweza wa kila kitu



Surah: AL-BAQARAH 

Ayah : 148

وَلِكُلّٖ وِجۡهَةٌ هُوَ مُوَلِّيهَاۖ فَٱسۡتَبِقُواْ ٱلۡخَيۡرَٰتِۚ أَيۡنَ مَا تَكُونُواْ يَأۡتِ بِكُمُ ٱللَّهُ جَمِيعًاۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٞ

Na kila umma una upande unaoelekea. Kwa hiyo, shindaneni kufanya kheri. Popote mtakapokuwa, Allah atakuleteni nyote. Hakika, Allah nimuweza wa kila kitu



Surah: AL-IMRAN 

Ayah : 26

قُلِ ٱللَّهُمَّ مَٰلِكَ ٱلۡمُلۡكِ تُؤۡتِي ٱلۡمُلۡكَ مَن تَشَآءُ وَتَنزِعُ ٱلۡمُلۡكَ مِمَّن تَشَآءُ وَتُعِزُّ مَن تَشَآءُ وَتُذِلُّ مَن تَشَآءُۖ بِيَدِكَ ٱلۡخَيۡرُۖ إِنَّكَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٞ

Sema: Ewe Mola wangu, Mmiliki wa ufalme, unampa ufalme umtakaye, na unamuondolea ufalme umtakaye, na unamtukuza umtakaye, na unamfanya dhalili umtakaye. Kheri zote zipo mkononi mwako tu. Hakika, wewe ni Muweza sana wa kila kitu



Surah: AL-IMRAN 

Ayah : 27

تُولِجُ ٱلَّيۡلَ فِي ٱلنَّهَارِ وَتُولِجُ ٱلنَّهَارَ فِي ٱلَّيۡلِۖ وَتُخۡرِجُ ٱلۡحَيَّ مِنَ ٱلۡمَيِّتِ وَتُخۡرِجُ ٱلۡمَيِّتَ مِنَ ٱلۡحَيِّۖ وَتَرۡزُقُ مَن تَشَآءُ بِغَيۡرِ حِسَابٖ

Unauingiza usiku ndani ya mchana[1], na unauingiza mchana ndani ya usiku, na unatoa (kiumbe) hai kutoka katika (kiumbe) mfu, na unatoa (kiumbe) mfu kutoka katika (kiumbe) hai. Na unampa riziki umtakaye bila ya hesabu


1- - Allah anauingiza usiku katika mchana na unakuwa mrefu katika kipindi fulani na pia anauingiza mchana
katika usiku na unakuwa mrefu katika kipindi kingine. Allah anaelezea uweza wake mkubwa unaotoa
kiumbe hai kutoka katika kinachoonekana kama kiumbe mfu, na anatoa kiumbe mfu katika kiumbe hai!
Hapa Allah anelezea uwezo wake mkubwa katika kinachoitwa “Mfuatano na muendelezo wa maisha ya
viumbe hai”.


Surah: ANNISAI 

Ayah : 133

إِن يَشَأۡ يُذۡهِبۡكُمۡ أَيُّهَا ٱلنَّاسُ وَيَأۡتِ بِـَٔاخَرِينَۚ وَكَانَ ٱللَّهُ عَلَىٰ ذَٰلِكَ قَدِيرٗا

(Allah) Akitaka atakuondoeni enyi watu na ataleta wengine. Na Allah analiweza sana hilo



Surah: AL-MAIDA 

Ayah : 40

أَلَمۡ تَعۡلَمۡ أَنَّ ٱللَّهَ لَهُۥ مُلۡكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ يُعَذِّبُ مَن يَشَآءُ وَيَغۡفِرُ لِمَن يَشَآءُۗ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٞ

Hivi hujui ya kwamba, ni wa Allah tu ufalme wa mbinguni na ardhini? Anamuadhibu amtakaye na anamsamehe amtakaye. Na Allah ni Muweza wa kila kitu



Surah: AL-AN’AAM 

Ayah : 37

وَقَالُواْ لَوۡلَا نُزِّلَ عَلَيۡهِ ءَايَةٞ مِّن رَّبِّهِۦۚ قُلۡ إِنَّ ٱللَّهَ قَادِرٌ عَلَىٰٓ أَن يُنَزِّلَ ءَايَةٗ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَهُمۡ لَا يَعۡلَمُونَ

Na walisema: (ingekuwa vizuri) lau kama (Mtume Muhammad) angeteremshiwa Aya (Muujiza) kutoka kwa Mola wake. Sema: Hakika, Allah ni mwenye uwezo wa kuteremsha Aya (Muujiza wanaoutaka) lakini wengi wao hawajui (kitakachowakuta kama wakiteremshiwa muujiza na wasiamini)



Surah: AL-AN’AAM 

Ayah : 65

قُلۡ هُوَ ٱلۡقَادِرُ عَلَىٰٓ أَن يَبۡعَثَ عَلَيۡكُمۡ عَذَابٗا مِّن فَوۡقِكُمۡ أَوۡ مِن تَحۡتِ أَرۡجُلِكُمۡ أَوۡ يَلۡبِسَكُمۡ شِيَعٗا وَيُذِيقَ بَعۡضَكُم بَأۡسَ بَعۡضٍۗ ٱنظُرۡ كَيۡفَ نُصَرِّفُ ٱلۡأٓيَٰتِ لَعَلَّهُمۡ يَفۡقَهُونَ

Sema: Yeye tu ndiye Muweza wa kuleta kwenu adhabu itokayo juu yenu au chini ya miguu yenu, au kukuvalisheni nguo ya mfarakano wa makundi na kukuonjesheni mkong’oto wa (nguvu za) wengine. Ona, namna tunavyozifafanua Aya (hoja) ili wapate kufahamu



Surah: AL-AN’AAM 

Ayah : 73

وَهُوَ ٱلَّذِي خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ بِٱلۡحَقِّۖ وَيَوۡمَ يَقُولُ كُن فَيَكُونُۚ قَوۡلُهُ ٱلۡحَقُّۚ وَلَهُ ٱلۡمُلۡكُ يَوۡمَ يُنفَخُ فِي ٱلصُّورِۚ عَٰلِمُ ٱلۡغَيۡبِ وَٱلشَّهَٰدَةِۚ وَهُوَ ٱلۡحَكِيمُ ٱلۡخَبِيرُ

Na yeye ndiye aliyeumba mbingu na ardhi kwa haki. Na (kumbuka) siku (Allah) anaposema (kuliambia jambo): Kuwa, basi linakuwa. Kauli yake ni haki. Ni wake yeye tu ufalme siku litakapopulizwa baragumu. Ni mjuzi wa Ghaibu (yaliyofichika) na yaliyo bayana. Na yeye ni Mwenye hekima, Mjuzi wa habari (zote)



Surah: ATTAUBA 

Ayah : 39

إِلَّا تَنفِرُواْ يُعَذِّبۡكُمۡ عَذَابًا أَلِيمٗا وَيَسۡتَبۡدِلۡ قَوۡمًا غَيۡرَكُمۡ وَلَا تَضُرُّوهُ شَيۡـٔٗاۗ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٌ

Kama hamtatoka (kwenda kupambana kwenye Jihadi basi Allah) atakuadhibuni adhabu inayoumiza mno, na atabadilisha (na kuleta) watu wengine wasiokuwa nyinyi (wenye utayari wa kwenda Jihadi) na nyinyi hamtamdhuru chochote Allah (kwa kuikimbia kwenu Jihadi). Na Allah ni Muweza wa kila kitu



Surah: AL-KAHF 

Ayah : 45

وَٱضۡرِبۡ لَهُم مَّثَلَ ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا كَمَآءٍ أَنزَلۡنَٰهُ مِنَ ٱلسَّمَآءِ فَٱخۡتَلَطَ بِهِۦ نَبَاتُ ٱلۡأَرۡضِ فَأَصۡبَحَ هَشِيمٗا تَذۡرُوهُ ٱلرِّيَٰحُۗ وَكَانَ ٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ مُّقۡتَدِرًا

Na wapigie mfano wa maisha ya dunia. Hayo ni kama maji tunayo yateremsha kutoka mbinguni, yakachanganyika na mimea ya ardhi, kisha hiyo mimea ikawa vibuwa vinavyo peperushwa na upepo. Na Allah ni Mwenye uweza juu ya kila kitu



Surah: AL-HAJJ 

Ayah : 39

أُذِنَ لِلَّذِينَ يُقَٰتَلُونَ بِأَنَّهُمۡ ظُلِمُواْۚ وَإِنَّ ٱللَّهَ عَلَىٰ نَصۡرِهِمۡ لَقَدِيرٌ

Wameruhusiwa kupigana wale wanao pigwa vita kwa sababu wamedhulumiwa - na kwa yakini Allah ni Muweza wa kuwasaidia



Surah: ALMUUMINUUN 

Ayah : 18

وَأَنزَلۡنَا مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءَۢ بِقَدَرٖ فَأَسۡكَنَّـٰهُ فِي ٱلۡأَرۡضِۖ وَإِنَّا عَلَىٰ ذَهَابِۭ بِهِۦ لَقَٰدِرُونَ

Na tumeteremsha kutoka mbinguni maji kwa kiasi na tukayatuliza katika ardhi. Na hakika Sisi tunaweza kuyaondoa



Surah: ALMUUMINUUN 

Ayah : 95

وَإِنَّا عَلَىٰٓ أَن نُّرِيَكَ مَا نَعِدُهُمۡ لَقَٰدِرُونَ

Na hakika Sisi ni waweza wa kukuonyesha tuliyo waahidi



Surah: ANNAMLI 

Ayah : 60

أَمَّنۡ خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ وَأَنزَلَ لَكُم مِّنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءٗ فَأَنۢبَتۡنَا بِهِۦ حَدَآئِقَ ذَاتَ بَهۡجَةٖ مَّا كَانَ لَكُمۡ أَن تُنۢبِتُواْ شَجَرَهَآۗ أَءِلَٰهٞ مَّعَ ٱللَّهِۚ بَلۡ هُمۡ قَوۡمٞ يَعۡدِلُونَ

Au nani yule aliye ziumba mbingu na ardhi, na akakute-remshieni maji kutoka mbinguni, na kwa hayo tukaziotesha bustani zenye kupendeza? Nyinyi hamna uwezo wa kuiotesha miti yake. Je! Yupo mungu pamoja na Allah? Bali hao ni watu walio potoka



Surah: ANNAMLI 

Ayah : 61

أَمَّن جَعَلَ ٱلۡأَرۡضَ قَرَارٗا وَجَعَلَ خِلَٰلَهَآ أَنۡهَٰرٗا وَجَعَلَ لَهَا رَوَٰسِيَ وَجَعَلَ بَيۡنَ ٱلۡبَحۡرَيۡنِ حَاجِزًاۗ أَءِلَٰهٞ مَّعَ ٱللَّهِۚ بَلۡ أَكۡثَرُهُمۡ لَا يَعۡلَمُونَ

Au nani yule aliye ifanya ardhi mahali pa kutua, na akajaalia ndani yake mito, na akaweka milima? Na akaweka baina ya bahari mbili kiziwizi? Je! Yupo mungu pamoja na Allah? Bali wengi wao hawajui



Surah: ANNAMLI 

Ayah : 62

أَمَّن يُجِيبُ ٱلۡمُضۡطَرَّ إِذَا دَعَاهُ وَيَكۡشِفُ ٱلسُّوٓءَ وَيَجۡعَلُكُمۡ خُلَفَآءَ ٱلۡأَرۡضِۗ أَءِلَٰهٞ مَّعَ ٱللَّهِۚ قَلِيلٗا مَّا تَذَكَّرُونَ

Au nani yule anaye mjibu mwenye shida pale anapo muomba, na akaiondoa dhiki, na akakufanyeni warithi wa ardhi? Je! Yupo mungu pamoja na Allah? Ni machache mnayo yazingatia



Surah: ANNAMLI 

Ayah : 63

أَمَّن يَهۡدِيكُمۡ فِي ظُلُمَٰتِ ٱلۡبَرِّ وَٱلۡبَحۡرِ وَمَن يُرۡسِلُ ٱلرِّيَٰحَ بُشۡرَۢا بَيۡنَ يَدَيۡ رَحۡمَتِهِۦٓۗ أَءِلَٰهٞ مَّعَ ٱللَّهِۚ تَعَٰلَى ٱللَّهُ عَمَّا يُشۡرِكُونَ

Au nani yule anaye kuongoeni katika giza la bara na bahari, na akazipeleka pepo kuleta bishara kabla ya rehema zake? Je! Yupo mungu pamoja na Allah? Ametukuka Allah juu ya wanao washirikisha naye



Surah: ANNAMLI 

Ayah : 64

أَمَّن يَبۡدَؤُاْ ٱلۡخَلۡقَ ثُمَّ يُعِيدُهُۥ وَمَن يَرۡزُقُكُم مِّنَ ٱلسَّمَآءِ وَٱلۡأَرۡضِۗ أَءِلَٰهٞ مَّعَ ٱللَّهِۚ قُلۡ هَاتُواْ بُرۡهَٰنَكُمۡ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ

Au nani anaye uanzisha uumbaji, kisha akaurejesha? Na nani anaye kuruzukuni kutoka mbinguni na kwenye ardhi? Je! Yupo mungu pamoja na Allah? Sema: Leteni hoja zenu kama nyinyi ni wasema kweli



Surah: ANNAMLI 

Ayah : 88

وَتَرَى ٱلۡجِبَالَ تَحۡسَبُهَا جَامِدَةٗ وَهِيَ تَمُرُّ مَرَّ ٱلسَّحَابِۚ صُنۡعَ ٱللَّهِ ٱلَّذِيٓ أَتۡقَنَ كُلَّ شَيۡءٍۚ إِنَّهُۥ خَبِيرُۢ بِمَا تَفۡعَلُونَ

Na unaiona milima unaidhania imetulia; nayo inakwenda kama mwendo wa mawingu. Huo ndio ufundi wa Allah aliye tengeneza kila kitu kwa ubora. Hakika Yeye anazo khabari za yote myatendayo



Surah: FAATWIR 

Ayah : 44

أَوَلَمۡ يَسِيرُواْ فِي ٱلۡأَرۡضِ فَيَنظُرُواْ كَيۡفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡ وَكَانُوٓاْ أَشَدَّ مِنۡهُمۡ قُوَّةٗۚ وَمَا كَانَ ٱللَّهُ لِيُعۡجِزَهُۥ مِن شَيۡءٖ فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَلَا فِي ٱلۡأَرۡضِۚ إِنَّهُۥ كَانَ عَلِيمٗا قَدِيرٗا

Je! Hawakusafiri katika ardhi wakaona vipi ulikuwa mwisho wa walio kuwa kabla yao? Na hao walikuwa wana nguvu zaidi kuliko wao. Na hapana kitu kinacho weza kumshinda Allah mbinguni wala katika ardhi. Hakika Yeye ni Mwenye kujua, Mwenye uweza



Surah: AZZUKHRUF 

Ayah : 42

أَوۡ نُرِيَنَّكَ ٱلَّذِي وَعَدۡنَٰهُمۡ فَإِنَّا عَلَيۡهِم مُّقۡتَدِرُونَ

Au tutakuonyesha tuliyo waahidi. Nasi bila ya shaka tuna uwezo juu yao



Surah: AL-HASHRI 

Ayah : 6

وَمَآ أَفَآءَ ٱللَّهُ عَلَىٰ رَسُولِهِۦ مِنۡهُمۡ فَمَآ أَوۡجَفۡتُمۡ عَلَيۡهِ مِنۡ خَيۡلٖ وَلَا رِكَابٖ وَلَٰكِنَّ ٱللَّهَ يُسَلِّطُ رُسُلَهُۥ عَلَىٰ مَن يَشَآءُۚ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٞ

Na ngawira yeyote ile Aliyoileta Allah Kwa Mtume Wake kutoka kwao; basi hamkuyaendea mbio Kwa farasi Na wala vipando vya ngamia. Lakini Allah Huwapa mamlaka na nguvu Mitume Wake dhidi ya Amtakaye. Na Allah juu ya kila kitu ni Muweza



Surah: AL-MULK 

Ayah : 1

تَبَٰرَكَ ٱلَّذِي بِيَدِهِ ٱلۡمُلۡكُ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٌ

Ametakasika (Allah) Ambaye ufalme umo mikononi Mwake yeye tu, Naye ni Muweza sana wa kila kitu



Surah: ALMA’RIJ 

Ayah : 40

فَلَآ أُقۡسِمُ بِرَبِّ ٱلۡمَشَٰرِقِ وَٱلۡمَغَٰرِبِ إِنَّا لَقَٰدِرُونَ

Basi Naapa kwa Mola wa Mashariki zote na Magharibi zote, hakika Sisi bila shaka ni Wenye kuweza



Surah: ALMA’RIJ 

Ayah : 41

عَلَىٰٓ أَن نُّبَدِّلَ خَيۡرٗا مِّنۡهُمۡ وَمَا نَحۡنُ بِمَسۡبُوقِينَ

(Tuna uwezo wa) Kuwabadili kwa walio bora kuliko wao; na Sisi hatushindwi