Surah: AL-AHZAAB 

Ayah : 40

مَّا كَانَ مُحَمَّدٌ أَبَآ أَحَدٖ مِّن رِّجَالِكُمۡ وَلَٰكِن رَّسُولَ ٱللَّهِ وَخَاتَمَ ٱلنَّبِيِّـۧنَۗ وَكَانَ ٱللَّهُ بِكُلِّ شَيۡءٍ عَلِيمٗا

Muhammad si baba wa yeyote katika wanaume wenu, bali ni Mtume wa Allah na Mwisho wa Manabii, na Allah ni Mjuzi wa kila kitu



Surah: AL-AHZAAB 

Ayah : 45

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّبِيُّ إِنَّآ أَرۡسَلۡنَٰكَ شَٰهِدٗا وَمُبَشِّرٗا وَنَذِيرٗا

Ewe Nabii! Hakika Sisi tume-kutuma uwe shahidi na mbashiri na muonyaji,



Surah: AL-AHZAAB 

Ayah : 46

وَدَاعِيًا إِلَى ٱللَّهِ بِإِذۡنِهِۦ وَسِرَاجٗا مُّنِيرٗا

Na mwitaji kumwendea Allah kwa idhini yake, na taa yenye kutoa nuru



Surah: SABAA 

Ayah : 28

وَمَآ أَرۡسَلۡنَٰكَ إِلَّا كَآفَّةٗ لِّلنَّاسِ بَشِيرٗا وَنَذِيرٗا وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يَعۡلَمُونَ

Na hatukukutuma ila kwa watu wote, uwe mbashiri, na muonyaji. Lakini watu wengi hawajui



Surah: SABAA 

Ayah : 46

۞قُلۡ إِنَّمَآ أَعِظُكُم بِوَٰحِدَةٍۖ أَن تَقُومُواْ لِلَّهِ مَثۡنَىٰ وَفُرَٰدَىٰ ثُمَّ تَتَفَكَّرُواْۚ مَا بِصَاحِبِكُم مِّن جِنَّةٍۚ إِنۡ هُوَ إِلَّا نَذِيرٞ لَّكُم بَيۡنَ يَدَيۡ عَذَابٖ شَدِيدٖ

Sema: Mimi nakunasihini kwa jambo moja tu - ya kwamba msimame kwa ajili ya Allah, wawili-wawili na mmoja-mmoja; kisha mfikiri. Mwenzenu huyu hana wazimu. Yeye si chochote ila ni Muonyaji kwenu kabla ya kufika adhabu kali



Surah: YAASIIN 

Ayah : 3

إِنَّكَ لَمِنَ ٱلۡمُرۡسَلِينَ

(Kwamba) Hakika kabisa, wewe ni miongoni mwa Mitume



Surah: YAASIIN 

Ayah : 4

عَلَىٰ صِرَٰطٖ مُّسۡتَقِيمٖ

(Uko) Juu ya njia iliyo nyooka



Surah: FUSSWILAT 

Ayah : 6

قُلۡ إِنَّمَآ أَنَا۠ بَشَرٞ مِّثۡلُكُمۡ يُوحَىٰٓ إِلَيَّ أَنَّمَآ إِلَٰهُكُمۡ إِلَٰهٞ وَٰحِدٞ فَٱسۡتَقِيمُوٓاْ إِلَيۡهِ وَٱسۡتَغۡفِرُوهُۗ وَوَيۡلٞ لِّلۡمُشۡرِكِينَ

Sema: Hakika ilivyo ni kwamba, mimi ni mtu kama nyinyi; inafunuliwa kwangu kwa njia ya Wahyi ya kwamba Mungu wenu ni Mungu Mmoja tu. Basi nyookeni sawa kumwendea Yeye, na muombeni msamaha. Na ole wao wenye kufanya ushirikina (wa kumshirikisha Allah na vitu vingine)



Surah: AL-JAATHIYA 

Ayah : 18

ثُمَّ جَعَلۡنَٰكَ عَلَىٰ شَرِيعَةٖ مِّنَ ٱلۡأَمۡرِ فَٱتَّبِعۡهَا وَلَا تَتَّبِعۡ أَهۡوَآءَ ٱلَّذِينَ لَا يَعۡلَمُونَ

Kisha tukakuweka wewe juu ya Njia ya haya mambo, basi ifuate, wala usifuate matamanio ya wasio jua kitu



Surah: AL-AHQAAF 

Ayah : 9

قُلۡ مَا كُنتُ بِدۡعٗا مِّنَ ٱلرُّسُلِ وَمَآ أَدۡرِي مَا يُفۡعَلُ بِي وَلَا بِكُمۡۖ إِنۡ أَتَّبِعُ إِلَّا مَا يُوحَىٰٓ إِلَيَّ وَمَآ أَنَا۠ إِلَّا نَذِيرٞ مُّبِينٞ

Mimi si kiroja miongoni mwa Mitume. Wala sijui nitakavyo fanywa wala nyinyi. Mimi nafuata niliyo funuliwa tu kwa Wahyi, wala mimi si chochote ila ni mwonyaji wa wazi



Surah: AL-FAT-HI 

Ayah : 8

إِنَّآ أَرۡسَلۡنَٰكَ شَٰهِدٗا وَمُبَشِّرٗا وَنَذِيرٗا

Hakika tumekutuma wewe uwe Shahidi, na Mbashiri, na Mwonyaji



Surah: AL-FAT-HI 

Ayah : 28

هُوَ ٱلَّذِيٓ أَرۡسَلَ رَسُولَهُۥ بِٱلۡهُدَىٰ وَدِينِ ٱلۡحَقِّ لِيُظۡهِرَهُۥ عَلَى ٱلدِّينِ كُلِّهِۦۚ وَكَفَىٰ بِٱللَّهِ شَهِيدٗا

Yeye ndiye aliye mtuma Mtume wake kwa uongofu na Dini ya Haki, ili aitukuze juu ya dini zote. Na Allah anatosha kuwa Shahidi



Surah: AL-FAT-HI 

Ayah : 29

مُّحَمَّدٞ رَّسُولُ ٱللَّهِۚ وَٱلَّذِينَ مَعَهُۥٓ أَشِدَّآءُ عَلَى ٱلۡكُفَّارِ رُحَمَآءُ بَيۡنَهُمۡۖ تَرَىٰهُمۡ رُكَّعٗا سُجَّدٗا يَبۡتَغُونَ فَضۡلٗا مِّنَ ٱللَّهِ وَرِضۡوَٰنٗاۖ سِيمَاهُمۡ فِي وُجُوهِهِم مِّنۡ أَثَرِ ٱلسُّجُودِۚ ذَٰلِكَ مَثَلُهُمۡ فِي ٱلتَّوۡرَىٰةِۚ وَمَثَلُهُمۡ فِي ٱلۡإِنجِيلِ كَزَرۡعٍ أَخۡرَجَ شَطۡـَٔهُۥ فَـَٔازَرَهُۥ فَٱسۡتَغۡلَظَ فَٱسۡتَوَىٰ عَلَىٰ سُوقِهِۦ يُعۡجِبُ ٱلزُّرَّاعَ لِيَغِيظَ بِهِمُ ٱلۡكُفَّارَۗ وَعَدَ ٱللَّهُ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّـٰلِحَٰتِ مِنۡهُم مَّغۡفِرَةٗ وَأَجۡرًا عَظِيمَۢا

Muhammad ni Mtume wa Allah. Na walio pamoja naye wana nguvu mbele ya makafiri, na wanahurumiana wao kwa wao. Utawaona wakiinama na kusujudu wakitafuta fadhila na radhi za Allah. Alama zao zipo katika nyuso zao, kwa athari ya kusujudu. Huu ndio mfano wao katika Taurati. Na mfano wao katika Injili ni kama mmea ulio toa chipukizi lake, kisha ukalitia nguvu, ukawa mnene, ukasimama sawa juu ya ubuwa wake, ukawafurahisha wakulima, ili kuwakasirisha kwa ajili yao makafiri. Allah amewaahidi walio amini na wakatenda mema katika wao msamaha na ujira mkubwa



Surah: ANNAJMI 

Ayah : 56

هَٰذَا نَذِيرٞ مِّنَ ٱلنُّذُرِ ٱلۡأُولَىٰٓ

Huyu (Mtume þ) ni muonyaji miongoni mwa waonyaji wa awali



Surah: AL-HADIID

Ayah : 8

وَمَا لَكُمۡ لَا تُؤۡمِنُونَ بِٱللَّهِ وَٱلرَّسُولُ يَدۡعُوكُمۡ لِتُؤۡمِنُواْ بِرَبِّكُمۡ وَقَدۡ أَخَذَ مِيثَٰقَكُمۡ إِن كُنتُم مُّؤۡمِنِينَ

Na mna nini nyinyi hamu-muamini Allah, na hali yakuwa Mtume anakuiteni ili mumua-mini Bwana wenu, na hali Amekwi-shachukua ahadi yenu mkiwa nyinyi ni Waumini



Surah: ASSWAFF 

Ayah : 6

وَإِذۡ قَالَ عِيسَى ٱبۡنُ مَرۡيَمَ يَٰبَنِيٓ إِسۡرَـٰٓءِيلَ إِنِّي رَسُولُ ٱللَّهِ إِلَيۡكُم مُّصَدِّقٗا لِّمَا بَيۡنَ يَدَيَّ مِنَ ٱلتَّوۡرَىٰةِ وَمُبَشِّرَۢا بِرَسُولٖ يَأۡتِي مِنۢ بَعۡدِي ٱسۡمُهُۥٓ أَحۡمَدُۖ فَلَمَّا جَآءَهُم بِٱلۡبَيِّنَٰتِ قَالُواْ هَٰذَا سِحۡرٞ مُّبِينٞ

Na (kumbuka Mtume) Isa, Mwana wa Mariamu aliposema: Enyi Wana wa Israili: Hakika, mimi ni Mtume wa Allah kwenu, nikithibitisha Taurati iliyokuwepo kabla yangu, na nikitoa bishara (habari njema) ya Mtume atakayekuja baada yangu; jina lake ni Ahmad. Lakini (Mtume huyo) alipowaletea hoja zilizo wazi, walisema: Huu ni uchawi ulio dhahiri



Surah: ASSWAFF 

Ayah : 9

هُوَ ٱلَّذِيٓ أَرۡسَلَ رَسُولَهُۥ بِٱلۡهُدَىٰ وَدِينِ ٱلۡحَقِّ لِيُظۡهِرَهُۥ عَلَى ٱلدِّينِ كُلِّهِۦ وَلَوۡ كَرِهَ ٱلۡمُشۡرِكُونَ

Yeye ndiye aliye mtuma Mtume wake kwa uwongofu na Dini ya haki ili ipate kuzishinda dini zote, ijapo kuwa washirikina watachukia



Surah: AL-JUMUA 

Ayah : 2

هُوَ ٱلَّذِي بَعَثَ فِي ٱلۡأُمِّيِّـۧنَ رَسُولٗا مِّنۡهُمۡ يَتۡلُواْ عَلَيۡهِمۡ ءَايَٰتِهِۦ وَيُزَكِّيهِمۡ وَيُعَلِّمُهُمُ ٱلۡكِتَٰبَ وَٱلۡحِكۡمَةَ وَإِن كَانُواْ مِن قَبۡلُ لَفِي ضَلَٰلٖ مُّبِينٖ

Yeye (Allah) ndiye aliye mpeleka Mtume kwa watu wasiojua kusoma wala kuandika, awasomee Aya zake na awatakase na awafunze Kitabu na hekima, japokuwa kabla ya haya walikuwa katika upotevu ulio wazi kabisa



Surah: ALMUNAAFIQUUN 

Ayah : 8

يَقُولُونَ لَئِن رَّجَعۡنَآ إِلَى ٱلۡمَدِينَةِ لَيُخۡرِجَنَّ ٱلۡأَعَزُّ مِنۡهَا ٱلۡأَذَلَّۚ وَلِلَّهِ ٱلۡعِزَّةُ وَلِرَسُولِهِۦ وَلِلۡمُؤۡمِنِينَ وَلَٰكِنَّ ٱلۡمُنَٰفِقِينَ لَا يَعۡلَمُونَ

Wanasema: Tutakaporudi Madinah, mwenye hadhi zaidi atamfukuza humo aliye dhalili. Na hali utukufu ni wa Allah na wa Mtume Wake na wa Waumini, lakini wanafiki hawajui



Surah: ATTWALAAQ 

Ayah : 11

رَّسُولٗا يَتۡلُواْ عَلَيۡكُمۡ ءَايَٰتِ ٱللَّهِ مُبَيِّنَٰتٖ لِّيُخۡرِجَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّـٰلِحَٰتِ مِنَ ٱلظُّلُمَٰتِ إِلَى ٱلنُّورِۚ وَمَن يُؤۡمِنۢ بِٱللَّهِ وَيَعۡمَلۡ صَٰلِحٗا يُدۡخِلۡهُ جَنَّـٰتٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ خَٰلِدِينَ فِيهَآ أَبَدٗاۖ قَدۡ أَحۡسَنَ ٱللَّهُ لَهُۥ رِزۡقًا

Naye ni Mtume anaekusomeeni Aya za Allah zinazobainisha; ili kuwatoa wale walio amini na wakatenda mema kutoka kwenye giza kuingia katika Nuru. Na yeyote anayemwamini Allah na akatenda mema, atamwingiza katika Bustani zipitazo mito kati yake, wadumu humo milele. Allah amekwisha mpa riziki nzuri



Surah: AL-QALAM 

Ayah : 4

وَإِنَّكَ لَعَلَىٰ خُلُقٍ عَظِيمٖ

Na hakika wewe uko juu ya tabia njema sana



Surah: ALHAAQQA 

Ayah : 41

وَمَا هُوَ بِقَوۡلِ شَاعِرٖۚ قَلِيلٗا مَّا تُؤۡمِنُونَ

Wala si kauli ya mtunga mashairi. Ni machache sana mnayoyaamini



Surah: ALHAAQQA 

Ayah : 42

وَلَا بِقَوۡلِ كَاهِنٖۚ قَلِيلٗا مَّا تَذَكَّرُونَ

Wala si kauli ya kuhani. Ni machache mnayo yakumbuka



Surah: ALJINN 

Ayah : 19

وَأَنَّهُۥ لَمَّا قَامَ عَبۡدُ ٱللَّهِ يَدۡعُوهُ كَادُواْ يَكُونُونَ عَلَيۡهِ لِبَدٗا

Na hakika Mja wa Allah Nabii Muhammad rehma na amani ziwe juu yake alipo simama kumuomba (na kumuabudu), wao walikaribia kumzonga.!



Surah: ALJINN 

Ayah : 20

قُلۡ إِنَّمَآ أَدۡعُواْ رَبِّي وَلَآ أُشۡرِكُ بِهِۦٓ أَحَدٗا

Sema: Ewe Muhammad: Hakika mimi namuomba (na kumuabudu) Mola wangu na wala simshirikishi na yeyote



Surah: ALJINN 

Ayah : 21

قُلۡ إِنِّي لَآ أَمۡلِكُ لَكُمۡ ضَرّٗا وَلَا رَشَدٗا

Sema: Mimi sina mamlaka ya kukudhuruni wala kukuongozeni



Surah: ALJINN 

Ayah : 22

قُلۡ إِنِّي لَن يُجِيرَنِي مِنَ ٱللَّهِ أَحَدٞ وَلَنۡ أَجِدَ مِن دُونِهِۦ مُلۡتَحَدًا

Sema: Hakika hakuna yeyote awezaye kunilinda na Allah na wala sitoweza kupata mahali pa kukimbilia



Surah: ALJINN 

Ayah : 23

إِلَّا بَلَٰغٗا مِّنَ ٱللَّهِ وَرِسَٰلَٰتِهِۦۚ وَمَن يَعۡصِ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ فَإِنَّ لَهُۥ نَارَ جَهَنَّمَ خَٰلِدِينَ فِيهَآ أَبَدًا

Isipokuwa nifikishe Ujumbe utokao kwa Allah, na ujumbe wake. Na wenye kumuasi Allah na Mtume wake, basi hakika hao watapata Moto wa Jahannamu wadumu humo milele



Surah: ALMUZZAMMIL 

Ayah : 15

إِنَّآ أَرۡسَلۡنَآ إِلَيۡكُمۡ رَسُولٗا شَٰهِدًا عَلَيۡكُمۡ كَمَآ أَرۡسَلۡنَآ إِلَىٰ فِرۡعَوۡنَ رَسُولٗا

Hakika Sisi tumemtuma kwenu Mtume aliye shahidi juu yenu, kama tulivyo mtuma Mtume kwa Firauni



Surah: ALMUZZAMMIL 

Ayah : 20

۞إِنَّ رَبَّكَ يَعۡلَمُ أَنَّكَ تَقُومُ أَدۡنَىٰ مِن ثُلُثَيِ ٱلَّيۡلِ وَنِصۡفَهُۥ وَثُلُثَهُۥ وَطَآئِفَةٞ مِّنَ ٱلَّذِينَ مَعَكَۚ وَٱللَّهُ يُقَدِّرُ ٱلَّيۡلَ وَٱلنَّهَارَۚ عَلِمَ أَن لَّن تُحۡصُوهُ فَتَابَ عَلَيۡكُمۡۖ فَٱقۡرَءُواْ مَا تَيَسَّرَ مِنَ ٱلۡقُرۡءَانِۚ عَلِمَ أَن سَيَكُونُ مِنكُم مَّرۡضَىٰ وَءَاخَرُونَ يَضۡرِبُونَ فِي ٱلۡأَرۡضِ يَبۡتَغُونَ مِن فَضۡلِ ٱللَّهِ وَءَاخَرُونَ يُقَٰتِلُونَ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِۖ فَٱقۡرَءُواْ مَا تَيَسَّرَ مِنۡهُۚ وَأَقِيمُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتُواْ ٱلزَّكَوٰةَ وَأَقۡرِضُواْ ٱللَّهَ قَرۡضًا حَسَنٗاۚ وَمَا تُقَدِّمُواْ لِأَنفُسِكُم مِّنۡ خَيۡرٖ تَجِدُوهُ عِندَ ٱللَّهِ هُوَ خَيۡرٗا وَأَعۡظَمَ أَجۡرٗاۚ وَٱسۡتَغۡفِرُواْ ٱللَّهَۖ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمُۢ

Hakika Mola wako anajua ya kuwa hakika wewe unakesha karibu na thuluthi mbili za usiku, na nusu yake, na thuluthi yake. Na baadhi ya watu walio pamoja nawe kadhaalika. Na Allah ndiye anaye ukadiria usiku na mchana. Anajua kuwa hamuwezi kuweka hesabu, basi amekusameheni. Basi someni kilicho chepesi katika Qurani. Anajua ya kuwa baadhi yenu watakuwa wagonjwa, na wengine wanasafiri katika ardhi wakitafuta fadhila za Allah, na wengine wanapigana katika Njia ya Allah. Kwa hivyo someni kilicho chepesi humo, na simamisheni Sala, na toeni Zaka, na mkopesheni Allah mkopo ulio mwema. Na kheri yoyote mnayo itanguliza kwa ajili ya nafsi zenu mtaikuta kwa Allah, nayo imekuwa bora zaidi, na ina thawabu kubwa sana. Na mtakeni msamaha Allah. Hakika Allah ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu