إِذۡ قَالَتِ ٱمۡرَأَتُ عِمۡرَٰنَ رَبِّ إِنِّي نَذَرۡتُ لَكَ مَا فِي بَطۡنِي مُحَرَّرٗا فَتَقَبَّلۡ مِنِّيٓۖ إِنَّكَ أَنتَ ٱلسَّمِيعُ ٱلۡعَلِيمُ
(Kumbuka) Aliposema mke wa Imrani (kwamba): Ewe Mola wangu, hakika mimi nimeweka nadhiri kwa aliyemo tumboni mwangu kwa ajili yako akiwa Wakfu, basi nikubalie. Hakika, wewe ni Msikiaji mno, Mjuzi sana
فَلَمَّا وَضَعَتۡهَا قَالَتۡ رَبِّ إِنِّي وَضَعۡتُهَآ أُنثَىٰ وَٱللَّهُ أَعۡلَمُ بِمَا وَضَعَتۡ وَلَيۡسَ ٱلذَّكَرُ كَٱلۡأُنثَىٰۖ وَإِنِّي سَمَّيۡتُهَا مَرۡيَمَ وَإِنِّيٓ أُعِيذُهَا بِكَ وَذُرِّيَّتَهَا مِنَ ٱلشَّيۡطَٰنِ ٱلرَّجِيمِ
Alipomzaa alisema: Ewe Mola wangu, hakika nimezaa (mtoto) mwanamke, na Allah anamjua zaidi (mtoto) aliyemzaa. Na (mtoto) mwanaume sio sawa na (mtoto) mwanamke. Na kwa hakika, mimi nimempa jina la Mariamu, na kwa hakika mimi nakuomba umkinge yeye na kizazi chake dhidi ya shetani aliyelaaniwa
فَتَقَبَّلَهَا رَبُّهَا بِقَبُولٍ حَسَنٖ وَأَنۢبَتَهَا نَبَاتًا حَسَنٗا وَكَفَّلَهَا زَكَرِيَّاۖ كُلَّمَا دَخَلَ عَلَيۡهَا زَكَرِيَّا ٱلۡمِحۡرَابَ وَجَدَ عِندَهَا رِزۡقٗاۖ قَالَ يَٰمَرۡيَمُ أَنَّىٰ لَكِ هَٰذَاۖ قَالَتۡ هُوَ مِنۡ عِندِ ٱللَّهِۖ إِنَّ ٱللَّهَ يَرۡزُقُ مَن يَشَآءُ بِغَيۡرِ حِسَابٍ
Basi Mola wake akampokea kwa mapokezi mazuri na akamkuza makuzi mazuri na akampa Zakaria jukumu la kumlea. Zakaria kila alipoingia kwa Mariamu katika Mihirabu[1] alikuta ana riziki (ya vyakula). Akasema: Ewe Mariamu, unavipata wapi (vyakula) hivi? Akasema: Vinatoka kwa Allah. Hakika Allah anampa riziki amtakaye bila ya hesabu
1- - Mihirabu ni chumba kinachokuwepo ndani ya msikiti kwa madhumuni ya kukaa faragha ili kumuabudu
Allah. Pia mihirabu ni sehemu anayosimama imamu katika kuongoza Swala msikitini.
وَإِذۡ قَالَتِ ٱلۡمَلَـٰٓئِكَةُ يَٰمَرۡيَمُ إِنَّ ٱللَّهَ ٱصۡطَفَىٰكِ وَطَهَّرَكِ وَٱصۡطَفَىٰكِ عَلَىٰ نِسَآءِ ٱلۡعَٰلَمِينَ
Na (kumbuka) Malaika walipo-sema: Ewe Mariamu, hakika Allah amekuteua na amekutakasa, na amekuteua kuliko wanawake wa walimwengu wote
يَٰمَرۡيَمُ ٱقۡنُتِي لِرَبِّكِ وَٱسۡجُدِي وَٱرۡكَعِي مَعَ ٱلرَّـٰكِعِينَ
Ewe Mariamu, mnyenyekee Mola wako na sujudu na rukuu pamoja na wenye kurukuu
ذَٰلِكَ مِنۡ أَنۢبَآءِ ٱلۡغَيۡبِ نُوحِيهِ إِلَيۡكَۚ وَمَا كُنتَ لَدَيۡهِمۡ إِذۡ يُلۡقُونَ أَقۡلَٰمَهُمۡ أَيُّهُمۡ يَكۡفُلُ مَرۡيَمَ وَمَا كُنتَ لَدَيۡهِمۡ إِذۡ يَخۡتَصِمُونَ
Hizo ni baadhi tu ya habari za Ghaibu tunazokufunulia, na hukuwa nao wakati wakitupa kalamu zao (kwa kupiga kura); ni nani kati yao atamlea Mariamu. Na hukuwa nao walipokuwa wakigombana
إِذۡ قَالَتِ ٱلۡمَلَـٰٓئِكَةُ يَٰمَرۡيَمُ إِنَّ ٱللَّهَ يُبَشِّرُكِ بِكَلِمَةٖ مِّنۡهُ ٱسۡمُهُ ٱلۡمَسِيحُ عِيسَى ٱبۡنُ مَرۡيَمَ وَجِيهٗا فِي ٱلدُّنۡيَا وَٱلۡأٓخِرَةِ وَمِنَ ٱلۡمُقَرَّبِينَ
(Kumbuka) Malaika waliposema: Ewe Mariamu, hakika Allah anakubashiria (mtoto atakayepatikana) kwa neno kutoka kwake. Jina lake ni Masihi Isa bin Mariamu. Ni mwenye heshima duniani na akhera, na ni miongoni mwa watakaokurubishwa
وَيُكَلِّمُ ٱلنَّاسَ فِي ٱلۡمَهۡدِ وَكَهۡلٗا وَمِنَ ٱلصَّـٰلِحِينَ
Na atazungumza na watu akiwa mtoto mchanga na akiwa mtu mzima, na atakuwa miongoni mwa watu wema
قَالَتۡ رَبِّ أَنَّىٰ يَكُونُ لِي وَلَدٞ وَلَمۡ يَمۡسَسۡنِي بَشَرٞۖ قَالَ كَذَٰلِكِ ٱللَّهُ يَخۡلُقُ مَا يَشَآءُۚ إِذَا قَضَىٰٓ أَمۡرٗا فَإِنَّمَا يَقُولُ لَهُۥ كُن فَيَكُونُ
Mariamu akasema: Ewe Mola wangu, nitapataje mtoto na ilhali hajanigusa mtu yeyote na sikuwa mzinifu? Akasema: Hivyo ndivyo Allah anaumba atakavyo; pindi anapohukumu jambo huliambia: Kuwa na linakuwa
وَيُعَلِّمُهُ ٱلۡكِتَٰبَ وَٱلۡحِكۡمَةَ وَٱلتَّوۡرَىٰةَ وَٱلۡإِنجِيلَ
Na atamfundisha kitabu na hekima na Taurati na Injili
وَرَسُولًا إِلَىٰ بَنِيٓ إِسۡرَـٰٓءِيلَ أَنِّي قَدۡ جِئۡتُكُم بِـَٔايَةٖ مِّن رَّبِّكُمۡ أَنِّيٓ أَخۡلُقُ لَكُم مِّنَ ٱلطِّينِ كَهَيۡـَٔةِ ٱلطَّيۡرِ فَأَنفُخُ فِيهِ فَيَكُونُ طَيۡرَۢا بِإِذۡنِ ٱللَّهِۖ وَأُبۡرِئُ ٱلۡأَكۡمَهَ وَٱلۡأَبۡرَصَ وَأُحۡيِ ٱلۡمَوۡتَىٰ بِإِذۡنِ ٱللَّهِۖ وَأُنَبِّئُكُم بِمَا تَأۡكُلُونَ وَمَا تَدَّخِرُونَ فِي بُيُوتِكُمۡۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةٗ لَّكُمۡ إِن كُنتُم مُّؤۡمِنِينَ
Na ni Mjumbe kwa Wana wa Israili (akiwa na ujumbe kwamba) hakika: Mimi nimekuleteeni muujiza kutoka kwa Mola wenu; hakika mimi nawaumbieni kutoka katika udongo umbile kama la ndege kisha na mpulizia na anakuwa ndege kwa idhini ya Allah. Na ninaponya kipofu na mwenye ukoma, na ninafufua wafu kwa idhini ya Allah, na nitawaambia kile mnachokula na mnachoweka akiba majumbani mwenu. Hakika, katika haya yote kuna ishara kwenu mkiwa ni wenye kuamini
وَمُصَدِّقٗا لِّمَا بَيۡنَ يَدَيَّ مِنَ ٱلتَّوۡرَىٰةِ وَلِأُحِلَّ لَكُم بَعۡضَ ٱلَّذِي حُرِّمَ عَلَيۡكُمۡۚ وَجِئۡتُكُم بِـَٔايَةٖ مِّن رَّبِّكُمۡ فَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَأَطِيعُونِ
Na ni mwenye kusadiki Taurati iliyoteremshwa kabla yangu, na ili ni kuhalalishieni baadhi ya yale yaliyoharamishwa kwenu, na nimekujieni na ishara kutoka kwa Mola wenu. Basi mcheni Allah na mnitii
إِنَّ ٱللَّهَ رَبِّي وَرَبُّكُمۡ فَٱعۡبُدُوهُۚ هَٰذَا صِرَٰطٞ مُّسۡتَقِيمٞ
Hakika Allah ndiye Mola wangu na Mola wenu, basi muabuduni. Hii ndiyo njia iliyonyooka
وَبِكُفۡرِهِمۡ وَقَوۡلِهِمۡ عَلَىٰ مَرۡيَمَ بُهۡتَٰنًا عَظِيمٗا
Na (pia hawaamini isipokuwa kidogo sana) kwasababu ya ukafiri wao na kumsingizia kwao Mariamu uzushi mkubwa sana
يَـٰٓأَهۡلَ ٱلۡكِتَٰبِ لَا تَغۡلُواْ فِي دِينِكُمۡ وَلَا تَقُولُواْ عَلَى ٱللَّهِ إِلَّا ٱلۡحَقَّۚ إِنَّمَا ٱلۡمَسِيحُ عِيسَى ٱبۡنُ مَرۡيَمَ رَسُولُ ٱللَّهِ وَكَلِمَتُهُۥٓ أَلۡقَىٰهَآ إِلَىٰ مَرۡيَمَ وَرُوحٞ مِّنۡهُۖ فَـَٔامِنُواْ بِٱللَّهِ وَرُسُلِهِۦۖ وَلَا تَقُولُواْ ثَلَٰثَةٌۚ ٱنتَهُواْ خَيۡرٗا لَّكُمۡۚ إِنَّمَا ٱللَّهُ إِلَٰهٞ وَٰحِدٞۖ سُبۡحَٰنَهُۥٓ أَن يَكُونَ لَهُۥ وَلَدٞۘ لَّهُۥ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِۗ وَكَفَىٰ بِٱللَّهِ وَكِيلٗا
Enyi Watu wa Kitabu, msichupe mipaka katika dini yenu na msimsemee Allah isipokuwa haki tu. Hakika, ilivyo ni kwamba Masihi, Issa Mwana wa Mariamu ni Mtume wa Allah na neno lake alilompelekea Mariamu, na ni roho iliyotoka kwake. Basi muaminini Allah na Mitume wake, na msiseme: Miungu ni watatu. Acheni (kuamini hivyo) itakuwa kheri kwenu. Hakika, ilivyo ni kwamba, Allah ni Mungu mmoja tu, ametakasika (kwa) kutokuwa na mwana. Ni vyake yeye tu vyote vilivyomo mbinguni na ardhini. Na imetosha kwamba, Allah ni Mwenye kutegemewa
وَإِذۡ قَالَ ٱللَّهُ يَٰعِيسَى ٱبۡنَ مَرۡيَمَ ءَأَنتَ قُلۡتَ لِلنَّاسِ ٱتَّخِذُونِي وَأُمِّيَ إِلَٰهَيۡنِ مِن دُونِ ٱللَّهِۖ قَالَ سُبۡحَٰنَكَ مَا يَكُونُ لِيٓ أَنۡ أَقُولَ مَا لَيۡسَ لِي بِحَقٍّۚ إِن كُنتُ قُلۡتُهُۥ فَقَدۡ عَلِمۡتَهُۥۚ تَعۡلَمُ مَا فِي نَفۡسِي وَلَآ أَعۡلَمُ مَا فِي نَفۡسِكَۚ إِنَّكَ أَنتَ عَلَّـٰمُ ٱلۡغُيُوبِ
Na (kumbuka) Allah aliposema: Ewe Issa bin Mariamu, hivi wewe uliwaambia watu: Nifanyeni mimi na mama yangu Miungu badala ya Allah? (Issa) akasema: Subhanaka (utakatifu ni wako wewe tu) Haiwi kwangu mimi kusema ambayo si haki yangu (kuyasema). Ikiwa nilisema basi bila ya shaka umekwishayajua. Wewe unayajua yaliyomo ndani ya nafsi yangu, na mimi siyajui yaliyomo katika nafsi yako. Hakika, Wewe ndiye Mjuzi wa yaliyofichikana
وَٱذۡكُرۡ فِي ٱلۡكِتَٰبِ مَرۡيَمَ إِذِ ٱنتَبَذَتۡ مِنۡ أَهۡلِهَا مَكَانٗا شَرۡقِيّٗا
Na mtaje Maryamu katika Kitabu, pale alipo jitenga na jamaa zake mahali upande wa mashariki
فَٱتَّخَذَتۡ مِن دُونِهِمۡ حِجَابٗا فَأَرۡسَلۡنَآ إِلَيۡهَا رُوحَنَا فَتَمَثَّلَ لَهَا بَشَرٗا سَوِيّٗا
Na akaweka pazia kujikinga nao. Tukampelekea Roho wetu (Malaika Jibrili), akajifananisha kwake sawa na mtu
قَالَتۡ إِنِّيٓ أَعُوذُ بِٱلرَّحۡمَٰنِ مِنكَ إِن كُنتَ تَقِيّٗا
(Maryamu) akasema: Hakika mimi najikinga kwa Mwingi wa Rehema aniepushe nawe, ukiwa ni mcha Mungu
قَالَ إِنَّمَآ أَنَا۠ رَسُولُ رَبِّكِ لِأَهَبَ لَكِ غُلَٰمٗا زَكِيّٗا
(Malaika) akasema: Hakika mimi ni mwenye kutumwa na Mola wako Mlezi ili nikubashirie tunu ya mtoto aliye takasika
قَالَتۡ أَنَّىٰ يَكُونُ لِي غُلَٰمٞ وَلَمۡ يَمۡسَسۡنِي بَشَرٞ وَلَمۡ أَكُ بَغِيّٗا
Akasema: Nitampataje mtoto hali mwanaadamu yeyote hajanigusa, wala mimi si kahaba?
قَالَ كَذَٰلِكِ قَالَ رَبُّكِ هُوَ عَلَيَّ هَيِّنٞۖ وَلِنَجۡعَلَهُۥٓ ءَايَةٗ لِّلنَّاسِ وَرَحۡمَةٗ مِّنَّاۚ وَكَانَ أَمۡرٗا مَّقۡضِيّٗا
(Malaika) akasema: Ndio hivyo hivyo! Mola wako Mlezi amesema: Haya ni mepesi kwangu! Na ili tumfanye kuwa ni Ishara kwa watu, na Rehema itokayo kwetu, na hilo ni jambo lilio kwisha hukumiwa
۞فَحَمَلَتۡهُ فَٱنتَبَذَتۡ بِهِۦ مَكَانٗا قَصِيّٗا
Basi akachukua mimba yake, na akaondoka nayo mpaka mahali pa mbali
فَأَجَآءَهَا ٱلۡمَخَاضُ إِلَىٰ جِذۡعِ ٱلنَّخۡلَةِ قَالَتۡ يَٰلَيۡتَنِي مِتُّ قَبۡلَ هَٰذَا وَكُنتُ نَسۡيٗا مَّنسِيّٗا
Kisha uchungu ukampeleka kwenye shina la mtende; akasema: Laiti ningelikufa kabla ya haya, na nikawa niliye sahaulika kabisa!
فَنَادَىٰهَا مِن تَحۡتِهَآ أَلَّا تَحۡزَنِي قَدۡ جَعَلَ رَبُّكِ تَحۡتَكِ سَرِيّٗا
Pakatangazwa kutoka chini yake: Usihuzunike! Hakika Mola wako Mlezi amejaalia chini yako kijito kidogo cha maji!
وَهُزِّيٓ إِلَيۡكِ بِجِذۡعِ ٱلنَّخۡلَةِ تُسَٰقِطۡ عَلَيۡكِ رُطَبٗا جَنِيّٗا
Na litikise kwako hilo shina la mtende, utakuangushia tende nzuri zilizo mbivu
فَكُلِي وَٱشۡرَبِي وَقَرِّي عَيۡنٗاۖ فَإِمَّا تَرَيِنَّ مِنَ ٱلۡبَشَرِ أَحَدٗا فَقُولِيٓ إِنِّي نَذَرۡتُ لِلرَّحۡمَٰنِ صَوۡمٗا فَلَنۡ أُكَلِّمَ ٱلۡيَوۡمَ إِنسِيّٗا
Basi kula, na kunywa, na litue jicho lako. Na pindi ukimwona mtu yeyote basi sema: Hakika mimi nimeweka nadhiri kwa Allah ya kufunga; kwa hivyo leo sitasema na mtu
فَأَتَتۡ بِهِۦ قَوۡمَهَا تَحۡمِلُهُۥۖ قَالُواْ يَٰمَرۡيَمُ لَقَدۡ جِئۡتِ شَيۡـٔٗا فَرِيّٗا
Akenda naye (mwanawe) kwa jamaa zake amembeba. Wakasema: Ewe Maryamu! Hakika umeleta kitu cha ajabu!
يَـٰٓأُخۡتَ هَٰرُونَ مَا كَانَ أَبُوكِ ٱمۡرَأَ سَوۡءٖ وَمَا كَانَتۡ أُمُّكِ بَغِيّٗا
Ewe dada yake Harun! Baba yako hakuwa mtu muovu, wala mama yako hakuwa kahaba
فَأَشَارَتۡ إِلَيۡهِۖ قَالُواْ كَيۡفَ نُكَلِّمُ مَن كَانَ فِي ٱلۡمَهۡدِ صَبِيّٗا
Akawaashiria kwa mtoto. Wakasema: Vipi tumsemeshe aliye bado mdogo yumo katika bebeo