Surah: MARYAM 

Ayah : 30

قَالَ إِنِّي عَبۡدُ ٱللَّهِ ءَاتَىٰنِيَ ٱلۡكِتَٰبَ وَجَعَلَنِي نَبِيّٗا

(Issa) akasema, (hali ya kuwa ni mtoto mchanga): Mimi ni mja wa Allah, Amenipa Kitabu, (nacho ni Injili), na amenifanya Nabii



Surah: MARYAM 

Ayah : 31

وَجَعَلَنِي مُبَارَكًا أَيۡنَ مَا كُنتُ وَأَوۡصَٰنِي بِٱلصَّلَوٰةِ وَٱلزَّكَوٰةِ مَا دُمۡتُ حَيّٗا

Na amenijaalia ni mwenye kubarikiwa popote pale niwapo. Na ameniusia Sala na Zaka maadamu nipo hai



Surah: MARYAM 

Ayah : 32

وَبَرَّۢا بِوَٰلِدَتِي وَلَمۡ يَجۡعَلۡنِي جَبَّارٗا شَقِيّٗا

Na nimtendee wema mama yangu. Wala hakunifanya niwe jeuri, mwovu



Surah: MARYAM 

Ayah : 33

وَٱلسَّلَٰمُ عَلَيَّ يَوۡمَ وُلِدتُّ وَيَوۡمَ أَمُوتُ وَيَوۡمَ أُبۡعَثُ حَيّٗا

Na amani iko juu yangu siku niliyozaliwa, na siku nitakayo kufa, na siku nitakayo fufuliwa kuwa hai



Surah: MARYAM 

Ayah : 34

ذَٰلِكَ عِيسَى ٱبۡنُ مَرۡيَمَۖ قَوۡلَ ٱلۡحَقِّ ٱلَّذِي فِيهِ يَمۡتَرُونَ

Huyo ndiye Issa mwana wa Maryamu. Ndiyo kauli ya haki ambayo wanaifanyia shaka



Surah: AL-ANBIYAA 

Ayah : 91

وَٱلَّتِيٓ أَحۡصَنَتۡ فَرۡجَهَا فَنَفَخۡنَا فِيهَا مِن رُّوحِنَا وَجَعَلۡنَٰهَا وَٱبۡنَهَآ ءَايَةٗ لِّلۡعَٰلَمِينَ

Na mwanamke aliye linda uke wake, na tukampulizia katika roho yetu, na tukamfanya yeye na mwanawe kuwa ni Ishara kwa walimwengu



Surah: ALMUUMINUUN 

Ayah : 50

وَجَعَلۡنَا ٱبۡنَ مَرۡيَمَ وَأُمَّهُۥٓ ءَايَةٗ وَءَاوَيۡنَٰهُمَآ إِلَىٰ رَبۡوَةٖ ذَاتِ قَرَارٖ وَمَعِينٖ

Na tukamfanya mwana wa Mariamu na mama yake kuwa ni Ishara, na tukawapa makimbilio kwenda mahali palipo inuka penye utulivu na chemchem za maji



Surah: ATTAHRIIM 

Ayah : 12

وَمَرۡيَمَ ٱبۡنَتَ عِمۡرَٰنَ ٱلَّتِيٓ أَحۡصَنَتۡ فَرۡجَهَا فَنَفَخۡنَا فِيهِ مِن رُّوحِنَا وَصَدَّقَتۡ بِكَلِمَٰتِ رَبِّهَا وَكُتُبِهِۦ وَكَانَتۡ مِنَ ٱلۡقَٰنِتِينَ

Na Mariamu binti wa ‘Imrani ambaye amehifadhi tupu yake (aliye linda ubikira wake), Tukampulizia humo (katika nguo yake) kupitia kwa Roho Wetu (Jibrili), na akasadikisha Maneno ya Mola wake, na Vitabu Vyake, na akawa miongoni mwa watiifu na wanyenyekevu