Surah: AL-INSAAN

Ayah : 28

نَّحۡنُ خَلَقۡنَٰهُمۡ وَشَدَدۡنَآ أَسۡرَهُمۡۖ وَإِذَا شِئۡنَا بَدَّلۡنَآ أَمۡثَٰلَهُمۡ تَبۡدِيلًا

Sisi tumewaumba, na tukavitia nguvu viungo vyao. Na tukitaka tutawabadilisha mfano wao wawe badala yao



Surah: AL-INSAAN

Ayah : 29

إِنَّ هَٰذِهِۦ تَذۡكِرَةٞۖ فَمَن شَآءَ ٱتَّخَذَ إِلَىٰ رَبِّهِۦ سَبِيلٗا

Hakika haya ni mawaidha; basi anaye taka atashika Njia ya kwenda kwa Mola wake



Surah: AL-INSAAN

Ayah : 30

وَمَا تَشَآءُونَ إِلَّآ أَن يَشَآءَ ٱللَّهُۚ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَلِيمًا حَكِيمٗا

Wala hamuwezi kutaka ila atakapo Allah. Hakika Allah ni Mwenye elimu, Mwenye hekima



Surah: AL-INSAAN

Ayah : 31

يُدۡخِلُ مَن يَشَآءُ فِي رَحۡمَتِهِۦۚ وَٱلظَّـٰلِمِينَ أَعَدَّ لَهُمۡ عَذَابًا أَلِيمَۢا

Humuingiza amtakaye katika rehema zake. Na wenye kudhulumu amewawekea adhabu iumizayo



Surah: A’BASA

Ayah : 22

ثُمَّ إِذَا شَآءَ أَنشَرَهُۥ

Kisha Atakapotaka, Atamfufua



Surah: ATTAK-WIIR 

Ayah : 29

وَمَا تَشَآءُونَ إِلَّآ أَن يَشَآءَ ٱللَّهُ رَبُّ ٱلۡعَٰلَمِينَ

Wala nyinyi hamtataka isipo kuwa atake Allah Mola wa Walimwengu wote



Surah: AL-INFITWAAR 

Ayah : 8

فِيٓ أَيِّ صُورَةٖ مَّا شَآءَ رَكَّبَكَ

Katika sura yoyote aliyo ipenda akakujenga



Surah: AL-BURUJI 

Ayah : 16

فَعَّالٞ لِّمَا يُرِيدُ

Atendaye ayatakayo