Surah: ANNAAZIAAT 

Ayah : 37

فَأَمَّا مَن طَغَىٰ

Basi yule aliyepindukia mipaka na kuasi



Surah: ANNAAZIAAT 

Ayah : 38

وَءَاثَرَ ٱلۡحَيَوٰةَ ٱلدُّنۡيَا

Na akapenda zaidi maisha ya dunia



Surah: ANNAAZIAAT 

Ayah : 39

فَإِنَّ ٱلۡجَحِيمَ هِيَ ٱلۡمَأۡوَىٰ

Kwa hakika Jahannamu ndiyo makaazi yake!



Surah: AL-FAJRI 

Ayah : 20

وَتُحِبُّونَ ٱلۡمَالَ حُبّٗا جَمّٗا

Na mnapenda mali mapenzi ya kupita kiasi



Surah: AL-AADIYAAT 

Ayah : 8

وَإِنَّهُۥ لِحُبِّ ٱلۡخَيۡرِ لَشَدِيدٌ

Naye hakika bila ya shaka anapenda sana (kheri) mali!



Surah: ATTAKAATHUR

Ayah : 1

أَلۡهَىٰكُمُ ٱلتَّكَاثُرُ

Kumekushughulisheni kutafuta wingi



Surah: ATTAKAATHUR

Ayah : 2

حَتَّىٰ زُرۡتُمُ ٱلۡمَقَابِرَ

Mpaka mje makaburini!