Surah: AL-FAATIHA 

Ayah : 4

مَٰلِكِ يَوۡمِ ٱلدِّينِ

Mmiliki wa Siku ya Malipo



Surah: AL-BAQARAH 

Ayah : 107

أَلَمۡ تَعۡلَمۡ أَنَّ ٱللَّهَ لَهُۥ مُلۡكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۗ وَمَا لَكُم مِّن دُونِ ٱللَّهِ مِن وَلِيّٖ وَلَا نَصِيرٍ

Je, hujui kwamba Allah ndiye Mwenye ufalme wa mbinguni na ardhini? Na nyinyi hamna mlinzi wala msaidizi mwingine badala ya Allah



Surah: AL-IMRAN 

Ayah : 26

قُلِ ٱللَّهُمَّ مَٰلِكَ ٱلۡمُلۡكِ تُؤۡتِي ٱلۡمُلۡكَ مَن تَشَآءُ وَتَنزِعُ ٱلۡمُلۡكَ مِمَّن تَشَآءُ وَتُعِزُّ مَن تَشَآءُ وَتُذِلُّ مَن تَشَآءُۖ بِيَدِكَ ٱلۡخَيۡرُۖ إِنَّكَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٞ

Sema: Ewe Mola wangu, Mmiliki wa ufalme, unampa ufalme umtakaye, na unamuondolea ufalme umtakaye, na unamtukuza umtakaye, na unamfanya dhalili umtakaye. Kheri zote zipo mkononi mwako tu. Hakika, wewe ni Muweza sana wa kila kitu



Surah: AL-IMRAN 

Ayah : 180

وَلَا يَحۡسَبَنَّ ٱلَّذِينَ يَبۡخَلُونَ بِمَآ ءَاتَىٰهُمُ ٱللَّهُ مِن فَضۡلِهِۦ هُوَ خَيۡرٗا لَّهُمۖ بَلۡ هُوَ شَرّٞ لَّهُمۡۖ سَيُطَوَّقُونَ مَا بَخِلُواْ بِهِۦ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِۗ وَلِلَّهِ مِيرَٰثُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۗ وَٱللَّهُ بِمَا تَعۡمَلُونَ خَبِيرٞ

Na kamwe wasidhani ambao wanafanya ubakhili kwa kile alichowapa Allah katika fadhila zake kuwa ni kheri kwao, bali hiyo ni shari kwao watafungwa kongwa kwa vile walivyovifanyia ubakhili siku ya kiama na ni wa Allah pekee urithi wa Mbingu na Ardhi, na Allah ni mwenye khabari kwa yale mnayoyatenda



Surah: AL-IMRAN 

Ayah : 189

وَلِلَّهِ مُلۡكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۗ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٌ

Na ufalme wa Mbingu na Ardhi ni wa Allah, na Allah ni muweza wa kila kitu



Surah: AL-MAIDA 

Ayah : 17

لَّقَدۡ كَفَرَ ٱلَّذِينَ قَالُوٓاْ إِنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلۡمَسِيحُ ٱبۡنُ مَرۡيَمَۚ قُلۡ فَمَن يَمۡلِكُ مِنَ ٱللَّهِ شَيۡـًٔا إِنۡ أَرَادَ أَن يُهۡلِكَ ٱلۡمَسِيحَ ٱبۡنَ مَرۡيَمَ وَأُمَّهُۥ وَمَن فِي ٱلۡأَرۡضِ جَمِيعٗاۗ وَلِلَّهِ مُلۡكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَمَا بَيۡنَهُمَاۚ يَخۡلُقُ مَا يَشَآءُۚ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٞ

Kwa yakini kabisa, wamekufuru wale waliosema: “Hakika Allah (Mungu) ndio Masihi bin Mariamu.” Sema: “Ni nani anayemiliki kuzuia jambo lolote litokalo kwa Allah akitaka kumuangamiza Masihi Mwana wa Mariamu na mama yake na wote waliomo ardhini (duniani)? Na ufalme wa mbinguni na ardhini na vilivyomo kati yake ni wa Allah (tu peke yake); anaumba atakacho. Na Allah ni Muweza wa kila kitu



Surah: AL-MAIDA 

Ayah : 18

وَقَالَتِ ٱلۡيَهُودُ وَٱلنَّصَٰرَىٰ نَحۡنُ أَبۡنَـٰٓؤُاْ ٱللَّهِ وَأَحِبَّـٰٓؤُهُۥۚ قُلۡ فَلِمَ يُعَذِّبُكُم بِذُنُوبِكُمۖ بَلۡ أَنتُم بَشَرٞ مِّمَّنۡ خَلَقَۚ يَغۡفِرُ لِمَن يَشَآءُ وَيُعَذِّبُ مَن يَشَآءُۚ وَلِلَّهِ مُلۡكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَمَا بَيۡنَهُمَاۖ وَإِلَيۡهِ ٱلۡمَصِيرُ

Na Wayahudi na Wanaswara (Wakristo) walisema: “Sisi ni Wana wa Allah (Mungu) na vipenzi vyake”. Sema: “Basi ni kwa nini anakuadhibuni kwa dhambi zenu? Bali nyinyi ni watu (tu) miongoni mwa (watu wengine) aliowaumba. (Allah) Anamsamehe amtakaye (anapotubu) na anamuadhibu amtakaye (asipotubu). Na ni wa Allah tu ufalme wa mbinguni na ardhini na vilivyomo baina yake, na marejeo ni kwake tu



Surah: AL-MAIDA 

Ayah : 120

لِلَّهِ مُلۡكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَمَا فِيهِنَّۚ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرُۢ

Ni wa Allah tu ufalme wa mbinguni na ardhini na vilivyomo ndani yake. Na yeye ni Muweza wa kila kitu



Surah: AL-AN’AAM 

Ayah : 73

وَهُوَ ٱلَّذِي خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ بِٱلۡحَقِّۖ وَيَوۡمَ يَقُولُ كُن فَيَكُونُۚ قَوۡلُهُ ٱلۡحَقُّۚ وَلَهُ ٱلۡمُلۡكُ يَوۡمَ يُنفَخُ فِي ٱلصُّورِۚ عَٰلِمُ ٱلۡغَيۡبِ وَٱلشَّهَٰدَةِۚ وَهُوَ ٱلۡحَكِيمُ ٱلۡخَبِيرُ

Na yeye ndiye aliyeumba mbingu na ardhi kwa haki. Na (kumbuka) siku (Allah) anaposema (kuliambia jambo): Kuwa, basi linakuwa. Kauli yake ni haki. Ni wake yeye tu ufalme siku litakapopulizwa baragumu. Ni mjuzi wa Ghaibu (yaliyofichika) na yaliyo bayana. Na yeye ni Mwenye hekima, Mjuzi wa habari (zote)



Surah: AL-AARAAF 

Ayah : 158

قُلۡ يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ إِنِّي رَسُولُ ٱللَّهِ إِلَيۡكُمۡ جَمِيعًا ٱلَّذِي لَهُۥ مُلۡكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۖ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ يُحۡيِۦ وَيُمِيتُۖ فَـَٔامِنُواْ بِٱللَّهِ وَرَسُولِهِ ٱلنَّبِيِّ ٱلۡأُمِّيِّ ٱلَّذِي يُؤۡمِنُ بِٱللَّهِ وَكَلِمَٰتِهِۦ وَٱتَّبِعُوهُ لَعَلَّكُمۡ تَهۡتَدُونَ

Sema: Enyi watu, hakika mimi ni Mtume wa Allah kwenu nyote[1]. (Allah) Ambaye ni wake pekee ufalme wa mbinguni na ardhini. Hapana mwenye haki ya kuabudiwa isipokuwa yeye tu. Anahuisha na anafisha. Basi muaminini Allah na Mtume wake, Nabii ambaye hasomi kilichoandikwa, ambaye anamuamini Allah na maneno yake, na mfuateni ili mpate kuongoka


1- - Aya hii ni tangazo rasmi kwamba, Uislamu ni dini ya ulimwengu wote na sio ya taifa fulani, kabila fulani au jamii fulani.


Surah: ATTAUBA 

Ayah : 116

إِنَّ ٱللَّهَ لَهُۥ مُلۡكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۖ يُحۡيِۦ وَيُمِيتُۚ وَمَا لَكُم مِّن دُونِ ٱللَّهِ مِن وَلِيّٖ وَلَا نَصِيرٖ

Hakika, Allah tu ndiye Mwenye ufalme wa mbinguni na ardhini; anahuisha na anafisha. Nanyi hamna Mlinzi wala Msaidizi minghairi (badala) ya Allah



Surah: AL-ISRAA 

Ayah : 111

وَقُلِ ٱلۡحَمۡدُ لِلَّهِ ٱلَّذِي لَمۡ يَتَّخِذۡ وَلَدٗا وَلَمۡ يَكُن لَّهُۥ شَرِيكٞ فِي ٱلۡمُلۡكِ وَلَمۡ يَكُن لَّهُۥ وَلِيّٞ مِّنَ ٱلذُّلِّۖ وَكَبِّرۡهُ تَكۡبِيرَۢا

Na sema: Alhamdulillah, Himdi zote ni za Allah ambaye hana mwana, wala hana mshirika katika ufalme, wala hana rafiki wa kumsaidia kwasababu ya udhaifu wake. Na mtukuze kwa utukufu mkubwa



Surah: TWAHA 

Ayah : 114

فَتَعَٰلَى ٱللَّهُ ٱلۡمَلِكُ ٱلۡحَقُّۗ وَلَا تَعۡجَلۡ بِٱلۡقُرۡءَانِ مِن قَبۡلِ أَن يُقۡضَىٰٓ إِلَيۡكَ وَحۡيُهُۥۖ وَقُل رَّبِّ زِدۡنِي عِلۡمٗا

Ametukuka Allah, Mfalme wa Haki. Wala usiifanyie haraka hii Qur’ani, kabla haujamalizika ufunuo wake. Na sema: Mola wangu Mlezi! Nizidishie ilimu



Surah: AL-HAJJ 

Ayah : 56

ٱلۡمُلۡكُ يَوۡمَئِذٖ لِّلَّهِ يَحۡكُمُ بَيۡنَهُمۡۚ فَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّـٰلِحَٰتِ فِي جَنَّـٰتِ ٱلنَّعِيمِ

Ufalme wote siku hiyo utakuwa wa Allah. Atahukumu baina yao. Basi walio amini na wakatenda mema watakuwa katika Bustani zenye neema



Surah: ALMUUMINUUN 

Ayah : 116

فَتَعَٰلَى ٱللَّهُ ٱلۡمَلِكُ ٱلۡحَقُّۖ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ رَبُّ ٱلۡعَرۡشِ ٱلۡكَرِيمِ

Ametukuka Allah, Mfalme wa Haki, hapana mungu ila Yeye, Mola Mlezi wa A’rshi Tukufu



Surah: ANNUUR 

Ayah : 42

وَلِلَّهِ مُلۡكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۖ وَإِلَى ٱللَّهِ ٱلۡمَصِيرُ

Na ni wa Allah ufalme wa mbingu na ardhi, na kwa Allah ndio marejeo ya wote



Surah: ALFURQAAN 

Ayah : 2

ٱلَّذِي لَهُۥ مُلۡكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَلَمۡ يَتَّخِذۡ وَلَدٗا وَلَمۡ يَكُن لَّهُۥ شَرِيكٞ فِي ٱلۡمُلۡكِ وَخَلَقَ كُلَّ شَيۡءٖ فَقَدَّرَهُۥ تَقۡدِيرٗا

Ambaye ni wake yeye tu ufalme wa mbingu na ardhi, na wala hakuwa na mwana, wala hakuwa na mshirika katika ufalme, na akaumba kila kitu na akakikadiria kwa kipimo



Surah: ALFURQAAN 

Ayah : 26

ٱلۡمُلۡكُ يَوۡمَئِذٍ ٱلۡحَقُّ لِلرَّحۡمَٰنِۚ وَكَانَ يَوۡمًا عَلَى ٱلۡكَٰفِرِينَ عَسِيرٗا

Ufalme wa haki siku hiyo utakuwa wa Arrahman, Mwingi wa Rehema, na itakuwa siku ngumu kwa makafiri



Surah: FAATWIR 

Ayah : 13

يُولِجُ ٱلَّيۡلَ فِي ٱلنَّهَارِ وَيُولِجُ ٱلنَّهَارَ فِي ٱلَّيۡلِ وَسَخَّرَ ٱلشَّمۡسَ وَٱلۡقَمَرَۖ كُلّٞ يَجۡرِي لِأَجَلٖ مُّسَمّٗىۚ ذَٰلِكُمُ ٱللَّهُ رَبُّكُمۡ لَهُ ٱلۡمُلۡكُۚ وَٱلَّذِينَ تَدۡعُونَ مِن دُونِهِۦ مَا يَمۡلِكُونَ مِن قِطۡمِيرٍ

Anauingiza usiku katika mchana, na anauingiza mchana katika usiku. Na amelifanya jua na mwezi kutumikia. Kila kimojawapo kinakwenda kwa muda maalumu. Huyo ndiye Allah Mola wenu Mlezi. Ufalme ni wake. Na hao mnao waomba badala yake hawamiliki hata ugozi wa kokwa ya tende



Surah: YAASIIN 

Ayah : 83

فَسُبۡحَٰنَ ٱلَّذِي بِيَدِهِۦ مَلَكُوتُ كُلِّ شَيۡءٖ وَإِلَيۡهِ تُرۡجَعُونَ

Basi Ametakasika yule ambaye mkononi mwake umo Ufalme wa kila kitu; na kwake Yeye mtarejeshwa



Surah: AZZUMAR 

Ayah : 6

خَلَقَكُم مِّن نَّفۡسٖ وَٰحِدَةٖ ثُمَّ جَعَلَ مِنۡهَا زَوۡجَهَا وَأَنزَلَ لَكُم مِّنَ ٱلۡأَنۡعَٰمِ ثَمَٰنِيَةَ أَزۡوَٰجٖۚ يَخۡلُقُكُمۡ فِي بُطُونِ أُمَّهَٰتِكُمۡ خَلۡقٗا مِّنۢ بَعۡدِ خَلۡقٖ فِي ظُلُمَٰتٖ ثَلَٰثٖۚ ذَٰلِكُمُ ٱللَّهُ رَبُّكُمۡ لَهُ ٱلۡمُلۡكُۖ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَۖ فَأَنَّىٰ تُصۡرَفُونَ

Amekuumbeni kutokana na nafsi moja. Kisha akamfanya mwenziwe katika nafsi ile ile. Na akakuleteeni wanyama wa mifugo jozi nane. Anakuumbeni katika matumbo ya mama zenu, umbo baada ya umbo, katika viza vitatu. Huyu ndiye Allah Mola wenu Mlezi. Ufalme ni wake. Hapana mungu isipo kuwa Yeye. Basi nyinyi mnageuzwa wapi?



Surah: AZZUMAR 

Ayah : 44

قُل لِّلَّهِ ٱلشَّفَٰعَةُ جَمِيعٗاۖ لَّهُۥ مُلۡكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۖ ثُمَّ إِلَيۡهِ تُرۡجَعُونَ

Sema: Uombezi wote uko kwa Allah. Ni wake Yeye tu ufalme wa mbingu na ardhi. Kisha mtarejeshwa kwake



Surah: GHAAFIR 

Ayah : 16

يَوۡمَ هُم بَٰرِزُونَۖ لَا يَخۡفَىٰ عَلَى ٱللَّهِ مِنۡهُمۡ شَيۡءٞۚ لِّمَنِ ٱلۡمُلۡكُ ٱلۡيَوۡمَۖ لِلَّهِ ٱلۡوَٰحِدِ ٱلۡقَهَّارِ

Siku watakayo dhihiri wao. Hapana kitacho fichikana chochote chao kwa Allah. Ufalme ni wa nani leo? Ni wa Allah Mmoja Mtenda nguvu



Surah: ASH-SHUURAA 

Ayah : 49

لِّلَّهِ مُلۡكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۚ يَخۡلُقُ مَا يَشَآءُۚ يَهَبُ لِمَن يَشَآءُ إِنَٰثٗا وَيَهَبُ لِمَن يَشَآءُ ٱلذُّكُورَ

Ufalme wa mbingu na ardhi ni wa Allah; anaumba apendavyo, anamtunukia amtakaye watoto wa kike, na anamtunukia amtakaye watoto wa kiume,



Surah: AZZUKHRUF 

Ayah : 85

وَتَبَارَكَ ٱلَّذِي لَهُۥ مُلۡكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَمَا بَيۡنَهُمَا وَعِندَهُۥ عِلۡمُ ٱلسَّاعَةِ وَإِلَيۡهِ تُرۡجَعُونَ

Na ametukuka Mwenye ufalme wa mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake. Na uko kwake ujuzi wa Saa ya Kiyama, na kwake Yeye mtarudishwa



Surah: AL-JAATHIYA 

Ayah : 27

وَلِلَّهِ مُلۡكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۚ وَيَوۡمَ تَقُومُ ٱلسَّاعَةُ يَوۡمَئِذٖ يَخۡسَرُ ٱلۡمُبۡطِلُونَ

Na Allah ndiye Mwenye ufalme wa mbingu na ardhi. Na siku itakapo simama Saa ya Kiyama, siku hiyo wataangamia wenye kushikamana na upotovu



Surah: AL-FAT-HI 

Ayah : 14

وَلِلَّهِ مُلۡكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۚ يَغۡفِرُ لِمَن يَشَآءُ وَيُعَذِّبُ مَن يَشَآءُۚ وَكَانَ ٱللَّهُ غَفُورٗا رَّحِيمٗا

Na Allah ndiye mwenye ufalme wa mbingu na ardhi. Humsamehe amtakae, na humuadhibu amtakaye. Na Allah ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu



Surah: AL-HADIID

Ayah : 2

لَهُۥ مُلۡكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۖ يُحۡيِۦ وَيُمِيتُۖ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٌ

Ni Wake pekee ufalme wa mbingu na ardhi. Anahuisha na anafisha. Na yeye Muweza wa kila kitu



Surah: AL-HADIID

Ayah : 5

لَّهُۥ مُلۡكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۚ وَإِلَى ٱللَّهِ تُرۡجَعُ ٱلۡأُمُورُ

Ni Wake Pekee ufalme wa mbingu na ardhi, kwa Allah Pekee yanarejeshwa mambo yote



Surah: AL-HADIID

Ayah : 10

وَمَا لَكُمۡ أَلَّا تُنفِقُواْ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ وَلِلَّهِ مِيرَٰثُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۚ لَا يَسۡتَوِي مِنكُم مَّنۡ أَنفَقَ مِن قَبۡلِ ٱلۡفَتۡحِ وَقَٰتَلَۚ أُوْلَـٰٓئِكَ أَعۡظَمُ دَرَجَةٗ مِّنَ ٱلَّذِينَ أَنفَقُواْ مِنۢ بَعۡدُ وَقَٰتَلُواْۚ وَكُلّٗا وَعَدَ ٱللَّهُ ٱلۡحُسۡنَىٰۚ وَٱللَّهُ بِمَا تَعۡمَلُونَ خَبِيرٞ

Na mna nini hata hamtoi katika njia ya Allah, na hali urithi wa mbingu na ardhi ni wa Allah Pekee. Hawi sawa miongoni mwenu aliyetoa kabla ya Ushindi (wa Makkah) na akapigana. Hao watapata daraja kuu kabisa kuliko wale waliotoa baadae na wakapigana. Na wote Allaah Amewaahidi malipo mazuri kabisa. Na Allah kwa yale myatendayo ni Mwenye khabari nayo