Surah: AL-HIJRI 

Ayah : 73

فَأَخَذَتۡهُمُ ٱلصَّيۡحَةُ مُشۡرِقِينَ

Basi (ghafla) Ukelele mkali uliwachukua kipindi cha mapam-bazuko



Surah: AL-HIJRI 

Ayah : 74

فَجَعَلۡنَا عَٰلِيَهَا سَافِلَهَا وَأَمۡطَرۡنَا عَلَيۡهِمۡ حِجَارَةٗ مِّن سِجِّيلٍ

Na tukaigeuza nchi (yao) juu chini chini juu, na tukawanyeshea (mvua ya) mawe ya udongo wa Motoni



Surah: AL-HIJRI 

Ayah : 75

إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَٰتٖ لِّلۡمُتَوَسِّمِينَ

Hakika katika hiyo (adhabu iliyowapata watu wa Lutwi) zipo ishara kwa wanaozingatia



Surah: AL-HIJRI 

Ayah : 76

وَإِنَّهَا لَبِسَبِيلٖ مُّقِيمٍ

Na (kitongoji cha watu wa Lutwi) kipo kwenye barabara ipitwayo (na watu wanaokwenda Sham)



Surah: AL-HIJRI 

Ayah : 77

إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةٗ لِّلۡمُؤۡمِنِينَ

Hakika katika hiyo (adhabu) ipo ishara (na mazingatio) kwa Waumini



Surah: AL-ANBIYAA 

Ayah : 74

وَلُوطًا ءَاتَيۡنَٰهُ حُكۡمٗا وَعِلۡمٗا وَنَجَّيۡنَٰهُ مِنَ ٱلۡقَرۡيَةِ ٱلَّتِي كَانَت تَّعۡمَلُ ٱلۡخَبَـٰٓئِثَۚ إِنَّهُمۡ كَانُواْ قَوۡمَ سَوۡءٖ فَٰسِقِينَ

Na Lutwi tukampa hukumu na elimu na tukamuokoa na ule mji ulio kuwa ukifanya maovu. Hakika hao walikuwa watu wabaya, wachafu



Surah: AL-ANBIYAA 

Ayah : 75

وَأَدۡخَلۡنَٰهُ فِي رَحۡمَتِنَآۖ إِنَّهُۥ مِنَ ٱلصَّـٰلِحِينَ

Na tukamuingiza katika rehema yetu. Hakika yeye ni miongoni mwa watenda mema



Surah: ASH-SHUARAA 

Ayah : 160

كَذَّبَتۡ قَوۡمُ لُوطٍ ٱلۡمُرۡسَلِينَ

Watu wa Lutwi waliwakanusha Mitume



Surah: ASH-SHUARAA 

Ayah : 161

إِذۡ قَالَ لَهُمۡ أَخُوهُمۡ لُوطٌ أَلَا تَتَّقُونَ

Alipo waambia ndugu yao, Lutwi: Je! Hamumchi Allah?



Surah: ASH-SHUARAA 

Ayah : 162

إِنِّي لَكُمۡ رَسُولٌ أَمِينٞ

Hakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu



Surah: ASH-SHUARAA 

Ayah : 163

فَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَأَطِيعُونِ

Basi mcheni Allah na nitiini mimi



Surah: ASH-SHUARAA 

Ayah : 164

وَمَآ أَسۡـَٔلُكُمۡ عَلَيۡهِ مِنۡ أَجۡرٍۖ إِنۡ أَجۡرِيَ إِلَّا عَلَىٰ رَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ

Wala mimi sikutakini ujira juu yake; ujira wangu hauko ila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote



Surah: ASH-SHUARAA 

Ayah : 165

أَتَأۡتُونَ ٱلذُّكۡرَانَ مِنَ ٱلۡعَٰلَمِينَ

Je! mnawaingilia wanaume katika walimwengu?



Surah: ASH-SHUARAA 

Ayah : 166

وَتَذَرُونَ مَا خَلَقَ لَكُمۡ رَبُّكُم مِّنۡ أَزۡوَٰجِكُمۚ بَلۡ أَنتُمۡ قَوۡمٌ عَادُونَ

Na mnaacha alicho kuumbieni Mola wenu Mlezi katika wake zenu? Ama kweli nyinyi ni watu mnaoruka mipaka!



Surah: ASH-SHUARAA 

Ayah : 167

قَالُواْ لَئِن لَّمۡ تَنتَهِ يَٰلُوطُ لَتَكُونَنَّ مِنَ ٱلۡمُخۡرَجِينَ

Wakasema: Ewe Lutwi! Usipo acha, hapana shaka utakuwa miongoni mwa wanao tolewa mji!



Surah: ASH-SHUARAA 

Ayah : 168

قَالَ إِنِّي لِعَمَلِكُم مِّنَ ٱلۡقَالِينَ

Akasema: Hakika mimi ni katika wanao kichukia hichi kitendo chenu



Surah: ASH-SHUARAA 

Ayah : 169

رَبِّ نَجِّنِي وَأَهۡلِي مِمَّا يَعۡمَلُونَ

Mola wangu Mlezi! Niokoe mimi na ahali zangu na haya wayatendayo



Surah: ASH-SHUARAA 

Ayah : 170

فَنَجَّيۡنَٰهُ وَأَهۡلَهُۥٓ أَجۡمَعِينَ

Basi tukamwokoa yeye na ahali zake wote,



Surah: ASH-SHUARAA 

Ayah : 171

إِلَّا عَجُوزٗا فِي ٱلۡغَٰبِرِينَ

Isipokuwa kikongwe katika waliokaa nyuma



Surah: ASH-SHUARAA 

Ayah : 172

ثُمَّ دَمَّرۡنَا ٱلۡأٓخَرِينَ

Kisha tukawaangamiza wale wengine



Surah: ASH-SHUARAA 

Ayah : 173

وَأَمۡطَرۡنَا عَلَيۡهِم مَّطَرٗاۖ فَسَآءَ مَطَرُ ٱلۡمُنذَرِينَ

Na tukawanyeshea mvua, basi ni mbaya mno mvua ya waliyoonywa



Surah: ASH-SHUARAA 

Ayah : 174

إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةٗۖ وَمَا كَانَ أَكۡثَرُهُم مُّؤۡمِنِينَ

Hakika katika hayo ipo Ishara. Na hawakuwa wengi wao wenye kuamini



Surah: ASH-SHUARAA 

Ayah : 175

وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ

Na hakika Mola wako Mlezi bila ya shaka ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu



Surah: ANNAMLI 

Ayah : 54

وَلُوطًا إِذۡ قَالَ لِقَوۡمِهِۦٓ أَتَأۡتُونَ ٱلۡفَٰحِشَةَ وَأَنتُمۡ تُبۡصِرُونَ

Na Lutwi alipo waambia watu wake: Je! Mnafanya uchafu nanyi mnaona?



Surah: ANNAMLI 

Ayah : 55

أَئِنَّكُمۡ لَتَأۡتُونَ ٱلرِّجَالَ شَهۡوَةٗ مِّن دُونِ ٱلنِّسَآءِۚ بَلۡ أَنتُمۡ قَوۡمٞ تَجۡهَلُونَ

Hivyo nyinyi mnawaingilia wanaume kwa matamanio badala ya wanawake? Hakika nyinyi ni watu mnao fanya ujinga kabisa!



Surah: ANNAMLI 

Ayah : 56

۞فَمَا كَانَ جَوَابَ قَوۡمِهِۦٓ إِلَّآ أَن قَالُوٓاْ أَخۡرِجُوٓاْ ءَالَ لُوطٖ مِّن قَرۡيَتِكُمۡۖ إِنَّهُمۡ أُنَاسٞ يَتَطَهَّرُونَ

Basi haikuwa jawabu ya watu wake ila ni kusema: Wafukuzeni wafwasi wa Lutwi katika mji wenu. Hao ni watu wanao jitia usafi



Surah: ANNAMLI 

Ayah : 57

فَأَنجَيۡنَٰهُ وَأَهۡلَهُۥٓ إِلَّا ٱمۡرَأَتَهُۥ قَدَّرۡنَٰهَا مِنَ ٱلۡغَٰبِرِينَ

Basi tukamwokoa yeye na ahali zake, isipo kuwa mkewe; tukamkadiria katika walio baki nyuma



Surah: ANNAMLI 

Ayah : 58

وَأَمۡطَرۡنَا عَلَيۡهِم مَّطَرٗاۖ فَسَآءَ مَطَرُ ٱلۡمُنذَرِينَ

Na tukawanyeshea mvua. Ni mbaya kweli kweli hiyo mvua ya walio kwisha onywa



Surah: AL-ANKABUUT 

Ayah : 26

۞فَـَٔامَنَ لَهُۥ لُوطٞۘ وَقَالَ إِنِّي مُهَاجِرٌ إِلَىٰ رَبِّيٓۖ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡحَكِيمُ

Lutwi akamuamini, na akasema: Mimi nahamia kwa Mola wangu Mlezi. Hakika Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hekima



Surah: AL-ANKABUUT 

Ayah : 31

وَلَمَّا جَآءَتۡ رُسُلُنَآ إِبۡرَٰهِيمَ بِٱلۡبُشۡرَىٰ قَالُوٓاْ إِنَّا مُهۡلِكُوٓاْ أَهۡلِ هَٰذِهِ ٱلۡقَرۡيَةِۖ إِنَّ أَهۡلَهَا كَانُواْ ظَٰلِمِينَ

Na wajumbe wetu walipo mjia Ibrahim na bishara, walisema: Hakika sisi hapana shaka tutawaangamiza watu wa mji huu, kwani watu wake hakika wamekuwa madhaalimu