Surah: AL-AN’AAM 

Ayah : 86

وَإِسۡمَٰعِيلَ وَٱلۡيَسَعَ وَيُونُسَ وَلُوطٗاۚ وَكُلّٗا فَضَّلۡنَا عَلَى ٱلۡعَٰلَمِينَ

Na Ismaili na Alyasaa na Yunus na Lutwi. Na wote (hao) tumewafanya bora kuliko walimwengu (wengine wa zama zao)



Surah: AL-AARAAF 

Ayah : 80

وَلُوطًا إِذۡ قَالَ لِقَوۡمِهِۦٓ أَتَأۡتُونَ ٱلۡفَٰحِشَةَ مَا سَبَقَكُم بِهَا مِنۡ أَحَدٖ مِّنَ ٱلۡعَٰلَمِينَ

Na (kumbuka Mtume) Lutwi wakati alipowaambia watu wake (kwamba): Hivi mnafanya uchafu ambao hajakutangulieni yeyote miongoni mwa walimwengu kuufanya?



Surah: AL-AARAAF 

Ayah : 81

إِنَّكُمۡ لَتَأۡتُونَ ٱلرِّجَالَ شَهۡوَةٗ مِّن دُونِ ٱلنِّسَآءِۚ بَلۡ أَنتُمۡ قَوۡمٞ مُّسۡرِفُونَ

Hakika, nyinyi mnawaendea (mnawatamani) wanaume kimatamanio badala ya wanawake? Ama kweli ninyi ni watu mliokiuka mipaka (katika uovu)



Surah: AL-AARAAF 

Ayah : 82

وَمَا كَانَ جَوَابَ قَوۡمِهِۦٓ إِلَّآ أَن قَالُوٓاْ أَخۡرِجُوهُم مِّن قَرۡيَتِكُمۡۖ إِنَّهُمۡ أُنَاسٞ يَتَطَهَّرُونَ

Na halikuwa jibu la watu wake isipokuwa tu walisema (kwamba): Watoeni (wafukuzeni) katika mji wenu, maana wao ni watu wanaojifanya wasafi



Surah: AL-AARAAF 

Ayah : 83

فَأَنجَيۡنَٰهُ وَأَهۡلَهُۥٓ إِلَّا ٱمۡرَأَتَهُۥ كَانَتۡ مِنَ ٱلۡغَٰبِرِينَ

Basi tulimuokoa yeye na familia yake isipokuwa mkewe tu; alikuwa miongoni mwa waliobaki (katika adhabu)



Surah: AL-AARAAF 

Ayah : 84

وَأَمۡطَرۡنَا عَلَيۡهِم مَّطَرٗاۖ فَٱنظُرۡ كَيۡفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلۡمُجۡرِمِينَ

Na tukawamiminia mvua (ya mawe). Basi tazama; ni namna gani ulikuwa mwisho wa waovu?



Surah: HUUD 

Ayah : 74

فَلَمَّا ذَهَبَ عَنۡ إِبۡرَٰهِيمَ ٱلرَّوۡعُ وَجَآءَتۡهُ ٱلۡبُشۡرَىٰ يُجَٰدِلُنَا فِي قَوۡمِ لُوطٍ

Na pindi hofu ilipomuondoka Ibrahimu, na ikamjia ile bishara (ya kupata mtoto), alianza kujadiliana nasi kuhusu watu wa Lutwi’



Surah: HUUD 

Ayah : 75

إِنَّ إِبۡرَٰهِيمَ لَحَلِيمٌ أَوَّـٰهٞ مُّنِيبٞ

Hakika Ibrahimu alikuwa mpole, ana huruma, na mwepesi wa kurejea kwa Allah



Surah: HUUD 

Ayah : 76

يَـٰٓإِبۡرَٰهِيمُ أَعۡرِضۡ عَنۡ هَٰذَآۖ إِنَّهُۥ قَدۡ جَآءَ أَمۡرُ رَبِّكَۖ وَإِنَّهُمۡ ءَاتِيهِمۡ عَذَابٌ غَيۡرُ مَرۡدُودٖ

(Malaika walimwambia): Ewe Ibrahimu! Hili liache! Kwa hakika kabisa amri ya Mola wako mlezi imeshafika, na hakika hao itawafika adhabu isiyo rudi nyuma



Surah: HUUD 

Ayah : 77

وَلَمَّا جَآءَتۡ رُسُلُنَا لُوطٗا سِيٓءَ بِهِمۡ وَضَاقَ بِهِمۡ ذَرۡعٗا وَقَالَ هَٰذَا يَوۡمٌ عَصِيبٞ

Na pindi wajumbe wetu walipo kuja kwa Lutwi’ alijihisi huzuni na akawaonea dhiki. Na akasema: Hii leo ni siku ngumu sana!



Surah: HUUD 

Ayah : 78

وَجَآءَهُۥ قَوۡمُهُۥ يُهۡرَعُونَ إِلَيۡهِ وَمِن قَبۡلُ كَانُواْ يَعۡمَلُونَ ٱلسَّيِّـَٔاتِۚ قَالَ يَٰقَوۡمِ هَـٰٓؤُلَآءِ بَنَاتِي هُنَّ أَطۡهَرُ لَكُمۡۖ فَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَلَا تُخۡزُونِ فِي ضَيۡفِيٓۖ أَلَيۡسَ مِنكُمۡ رَجُلٞ رَّشِيدٞ

Watu wake wakamjia mbio mbio. Na kabla ya hapo walikuwa wakitenda maovu. (Lutwi) akawaambia: Enyi watu wangu! Hawa hapa binti zangu, ndio wametakasika zaidi kwenu. Basi mcheni Allah, na msinifedheheshe mbele ya wageni wangu. Hivi, miongoni mwenu hakuna hata mmoja aliye na akili?



Surah: HUUD 

Ayah : 79

قَالُواْ لَقَدۡ عَلِمۡتَ مَا لَنَا فِي بَنَاتِكَ مِنۡ حَقّٖ وَإِنَّكَ لَتَعۡلَمُ مَا نُرِيدُ

Wakasema: Bila shaka unajua hatuna haki juu ya binti zako, na hakika unajua tunayoyataka



Surah: HUUD 

Ayah : 80

قَالَ لَوۡ أَنَّ لِي بِكُمۡ قُوَّةً أَوۡ ءَاوِيٓ إِلَىٰ رُكۡنٖ شَدِيدٖ

(Lutwi) akasema: Laiti mimi ningekuwa na nguvu ya kuwazuia, au ningekuwa na kabila na jamaa wenye nguvu tungepambana nanyi!



Surah: HUUD 

Ayah : 81

قَالُواْ يَٰلُوطُ إِنَّا رُسُلُ رَبِّكَ لَن يَصِلُوٓاْ إِلَيۡكَۖ فَأَسۡرِ بِأَهۡلِكَ بِقِطۡعٖ مِّنَ ٱلَّيۡلِ وَلَا يَلۡتَفِتۡ مِنكُمۡ أَحَدٌ إِلَّا ٱمۡرَأَتَكَۖ إِنَّهُۥ مُصِيبُهَا مَآ أَصَابَهُمۡۚ إِنَّ مَوۡعِدَهُمُ ٱلصُّبۡحُۚ أَلَيۡسَ ٱلصُّبۡحُ بِقَرِيبٖ

(Malaika) wakasema: Ewe Lutwi›! Sisi ni wajumbe wa Mola wako mlezi, hawatakufikia. Na ondoka pamoja na watu wako katika kipande cha usiku uliobaki. Na yeyote miongoni mwenu asigeuke kutazama nyuma, isipokuwa mkeo itamfika adhabu (itakayowafika wengine). Hakika miadi yao ni asubuhi. Hivi, asubuhi si karibu?



Surah: HUUD 

Ayah : 82

فَلَمَّا جَآءَ أَمۡرُنَا جَعَلۡنَا عَٰلِيَهَا سَافِلَهَا وَأَمۡطَرۡنَا عَلَيۡهَا حِجَارَةٗ مِّن سِجِّيلٖ مَّنضُودٖ

Basi ilipofika amri yetu tulikigeza (kijiji kile) juu chini, na tukawateremshia mvua ya mawe kutoka Motoni



Surah: HUUD 

Ayah : 83

مُّسَوَّمَةً عِندَ رَبِّكَۖ وَمَا هِيَ مِنَ ٱلظَّـٰلِمِينَ بِبَعِيدٖ

(Mawe) yaliyotiwa alama maalumu kwa Mola wako mlezi. Na (mawe) hayo hayawakosi madhalimu



Surah: AL-HIJRI 

Ayah : 59

إِلَّآ ءَالَ لُوطٍ إِنَّا لَمُنَجُّوهُمۡ أَجۡمَعِينَ

Isipokuwa waliomfuata Lutwi (na kumuamini). Bila ya shaka sisi tutawaokoa wote



Surah: AL-HIJRI 

Ayah : 60

إِلَّا ٱمۡرَأَتَهُۥ قَدَّرۡنَآ إِنَّهَا لَمِنَ ٱلۡغَٰبِرِينَ

Ispokuwa mkewe. Tunakadiria huyo atakuwa miongoni (mwa) watakaobakia nyuma



Surah: AL-HIJRI 

Ayah : 61

فَلَمَّا جَآءَ ءَالَ لُوطٍ ٱلۡمُرۡسَلُونَ

Basi wale wajumbe (waliotumwa) walipofika kwa Lutwi



Surah: AL-HIJRI 

Ayah : 62

قَالَ إِنَّكُمۡ قَوۡمٞ مُّنكَرُونَ

(Lutwi) Alisema: Hakika nyinyi ni watu msiojulikana (hapa kwetu)



Surah: AL-HIJRI 

Ayah : 63

قَالُواْ بَلۡ جِئۡنَٰكَ بِمَا كَانُواْ فِيهِ يَمۡتَرُونَ

(Malaika) Walisema: Bali sisi tumekuletea (adhabu ya) yale waliyokuwa wakiyatilia shaka



Surah: AL-HIJRI 

Ayah : 64

وَأَتَيۡنَٰكَ بِٱلۡحَقِّ وَإِنَّا لَصَٰدِقُونَ

Na tumefika kwako kwa Haki, na hakika sisi tunasema kweli



Surah: AL-HIJRI 

Ayah : 65

فَأَسۡرِ بِأَهۡلِكَ بِقِطۡعٖ مِّنَ ٱلَّيۡلِ وَٱتَّبِعۡ أَدۡبَٰرَهُمۡ وَلَا يَلۡتَفِتۡ مِنكُمۡ أَحَدٞ وَٱمۡضُواْ حَيۡثُ تُؤۡمَرُونَ

Basi ondoka na ahli zako kwenye sehemu ya usiku, nawe ufuate nyuma yao (huku ukiwahimiza ili waharakishe kuondoka), wala yeyote kati yenu asigeuke nyuma. Na mwende mlikoamrishwa



Surah: AL-HIJRI 

Ayah : 66

وَقَضَيۡنَآ إِلَيۡهِ ذَٰلِكَ ٱلۡأَمۡرَ أَنَّ دَابِرَ هَـٰٓؤُلَآءِ مَقۡطُوعٞ مُّصۡبِحِينَ

Na tukamfunulia Lutwi wahyi huo kwamba, mwisho wa watu hawa ikifika (mapambazuko ya) asubuhi watakuwa wameshakatiliwa mbali



Surah: AL-HIJRI 

Ayah : 67

وَجَآءَ أَهۡلُ ٱلۡمَدِينَةِ يَسۡتَبۡشِرُونَ

Na walikuja watu wa mji ule (baada ya kusikia kwa Lutu kuna wageni wazuri) huku wakifurahi



Surah: AL-HIJRI 

Ayah : 68

قَالَ إِنَّ هَـٰٓؤُلَآءِ ضَيۡفِي فَلَا تَفۡضَحُونِ

(Lutwi) Alisema (kuwaambia): Hakika hawa wageni wangu (wanahitaji kuenziwa), tafadhalini msinifedheheshe



Surah: AL-HIJRI 

Ayah : 69

وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَلَا تُخۡزُونِ

Na mcheni Allah, wala msinidhalilishe (mbele ya wageni)



Surah: AL-HIJRI 

Ayah : 70

قَالُوٓاْ أَوَلَمۡ نَنۡهَكَ عَنِ ٱلۡعَٰلَمِينَ

(Watu wa Lutwi) Walisema: Sisi situlikukataza usitie (neno tunapomtaka) yeyote katika walimwengu?



Surah: AL-HIJRI 

Ayah : 71

قَالَ هَـٰٓؤُلَآءِ بَنَاتِيٓ إِن كُنتُمۡ فَٰعِلِينَ

(Lutwi) Alisema (kuwaambia msinivunjie heshima): Hawa (hapa) binti zangu (waoeni), ikiwa nyinyi ni wafanyaji (mnaotaka kukata hamu zenu)



Surah: AL-HIJRI 

Ayah : 72

لَعَمۡرُكَ إِنَّهُمۡ لَفِي سَكۡرَتِهِمۡ يَعۡمَهُونَ

(Allah alisema) Naapia kwa umri wako! Hakika hao (watu wa Lutwi) wamepagawa katika ulevi wao, wanahangaika