Surah: AL-BAQARAH 

Ayah : 255

ٱللَّهُ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ ٱلۡحَيُّ ٱلۡقَيُّومُۚ لَا تَأۡخُذُهُۥ سِنَةٞ وَلَا نَوۡمٞۚ لَّهُۥ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِۗ مَن ذَا ٱلَّذِي يَشۡفَعُ عِندَهُۥٓ إِلَّا بِإِذۡنِهِۦۚ يَعۡلَمُ مَا بَيۡنَ أَيۡدِيهِمۡ وَمَا خَلۡفَهُمۡۖ وَلَا يُحِيطُونَ بِشَيۡءٖ مِّنۡ عِلۡمِهِۦٓ إِلَّا بِمَا شَآءَۚ وَسِعَ كُرۡسِيُّهُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَۖ وَلَا يَـُٔودُهُۥ حِفۡظُهُمَاۚ وَهُوَ ٱلۡعَلِيُّ ٱلۡعَظِيمُ

Allah, hakuna anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Yeye tu. Yeye ndiye Mwenye uhai wa milele, Mwenye kusimamia kila kitu. Hapatwi na kusinzia wala kulala. Ni vyake yeye tu vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini. Ni nani awezaye kuombea mbele yake bila ya idhini yake? Anayajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao, wala hawajui kitu katika elimu yake isipokuwa atakacho tu. Kursi yake imezienea mbingu na ardhi wala hakumchoshi kuzihifadhi (mbingu, ardhi na vilivyomo), na Yeye ndiye aliye juu na ndiye aliye Mkuu



Surah: ANNISAI 

Ayah : 85

مَّن يَشۡفَعۡ شَفَٰعَةً حَسَنَةٗ يَكُن لَّهُۥ نَصِيبٞ مِّنۡهَاۖ وَمَن يَشۡفَعۡ شَفَٰعَةٗ سَيِّئَةٗ يَكُن لَّهُۥ كِفۡلٞ مِّنۡهَاۗ وَكَانَ ٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ مُّقِيتٗا

Yeyote atakayeombea maombezi mazuri (atakayeingilia kati katika kufanikisha jambo jema) atapata fungu katika jambo zuri hilo, na yeyote atakayeombea maombezi maovu (atakayeingilia kati katika kufanikisha jambo ovu) atapata fungu katika jambo ovu hilo. Na Allahni Mwenye uweza na ujuzi juu ya kila kitu



Surah: AL-AN’AAM 

Ayah : 51

وَأَنذِرۡ بِهِ ٱلَّذِينَ يَخَافُونَ أَن يُحۡشَرُوٓاْ إِلَىٰ رَبِّهِمۡ لَيۡسَ لَهُم مِّن دُونِهِۦ وَلِيّٞ وَلَا شَفِيعٞ لَّعَلَّهُمۡ يَتَّقُونَ

Na waonye kwayo (Qur’ani) wale wanao ogopa kukusanywa kwa Mola wao wakiwa hawana msimamizi wala muombezi isipokuwa yeye (Allah), ili wamche Allah



Surah: AL-AN’AAM 

Ayah : 70

وَذَرِ ٱلَّذِينَ ٱتَّخَذُواْ دِينَهُمۡ لَعِبٗا وَلَهۡوٗا وَغَرَّتۡهُمُ ٱلۡحَيَوٰةُ ٱلدُّنۡيَاۚ وَذَكِّرۡ بِهِۦٓ أَن تُبۡسَلَ نَفۡسُۢ بِمَا كَسَبَتۡ لَيۡسَ لَهَا مِن دُونِ ٱللَّهِ وَلِيّٞ وَلَا شَفِيعٞ وَإِن تَعۡدِلۡ كُلَّ عَدۡلٖ لَّا يُؤۡخَذۡ مِنۡهَآۗ أُوْلَـٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ أُبۡسِلُواْ بِمَا كَسَبُواْۖ لَهُمۡ شَرَابٞ مِّنۡ حَمِيمٖ وَعَذَابٌ أَلِيمُۢ بِمَا كَانُواْ يَكۡفُرُونَ

Na waache wale walioifanya dini yao mchezo na pumbao, na yamewahadaa maisha ya dunia. Na kumbusha kwayo (Qur’ani ili), isije nafsi ikaangamizwa kwasababu ya (madhambi) waliyoyachuma, haina mlinzi yeyote wala muombezi yeyote. Na hata kama (nafsi hiyo) itatoa fidia ya aina yoyote (ili isiadhibiwe) haitachukuliwa. Hao ndio wale walioangamizwa kwa (sababu ya madhambi) waliyoyachuma. Watapata kinywaji cha maji ya moto na adhabu iumizayo sana kwa (sababu) ya walivyokuwa wanakufuru



Surah: YUNUS 

Ayah : 3

إِنَّ رَبَّكُمُ ٱللَّهُ ٱلَّذِي خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٖ ثُمَّ ٱسۡتَوَىٰ عَلَى ٱلۡعَرۡشِۖ يُدَبِّرُ ٱلۡأَمۡرَۖ مَا مِن شَفِيعٍ إِلَّا مِنۢ بَعۡدِ إِذۡنِهِۦۚ ذَٰلِكُمُ ٱللَّهُ رَبُّكُمۡ فَٱعۡبُدُوهُۚ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ

Hakika, Mola wenu Mlezi ni Allah ambaye ameumba mbingu na ardhi katika siku sita, kisha akalingana sawa juu ya Arshi, anaendesha mambo yote, hakuna muombezi yeyote (atakayekubaliwa uombezi wake) isipokuwa baada ya idhini yake tu. Huyo, kwenu nyie, ndiye Allah, Mola wenu mlezi, basi muabuduni. Hivi hamuonyeki?



Surah: AL-ANBIYAA 

Ayah : 28

يَعۡلَمُ مَا بَيۡنَ أَيۡدِيهِمۡ وَمَا خَلۡفَهُمۡ وَلَا يَشۡفَعُونَ إِلَّا لِمَنِ ٱرۡتَضَىٰ وَهُم مِّنۡ خَشۡيَتِهِۦ مُشۡفِقُونَ

Anayajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao. Wala hawam-wombei yeyote ila yule anaye mridhia Yeye, nao kwa ajili ya kumwogopa wananyenyekea



Surah: ASSAJDAH 

Ayah : 4

ٱللَّهُ ٱلَّذِي خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ وَمَا بَيۡنَهُمَا فِي سِتَّةِ أَيَّامٖ ثُمَّ ٱسۡتَوَىٰ عَلَى ٱلۡعَرۡشِۖ مَا لَكُم مِّن دُونِهِۦ مِن وَلِيّٖ وَلَا شَفِيعٍۚ أَفَلَا تَتَذَكَّرُونَ

Allah ndiye aliye umba mbingu na ardhi na vilivyomo baina yao kwa siku sita, na akatawala kwenye Kiti cha Enzi. Nyinyi hamna mlinzi wala mwombezi isipokuwa Yeye tu. Basi, je, hamkumbuki?



Surah: YAASIIN 

Ayah : 23

ءَأَتَّخِذُ مِن دُونِهِۦٓ ءَالِهَةً إِن يُرِدۡنِ ٱلرَّحۡمَٰنُ بِضُرّٖ لَّا تُغۡنِ عَنِّي شَفَٰعَتُهُمۡ شَيۡـٔٗا وَلَا يُنقِذُونِ

Je! Niishike miungu mingine badala yake? Arrahmani, Mwingi wa Rehema, akinitakia madhara uombezi wa hao hautanifaa kitu, wala hawataniokoa



Surah: AZZUMAR 

Ayah : 43

أَمِ ٱتَّخَذُواْ مِن دُونِ ٱللَّهِ شُفَعَآءَۚ قُلۡ أَوَلَوۡ كَانُواْ لَا يَمۡلِكُونَ شَيۡـٔٗا وَلَا يَعۡقِلُونَ

Au ndio wanachukua waombezi badala ya Allah? Sema: Ingawa hawana mamlaka juu ya kitu chochote, wala hawatambui lolote?



Surah: AZZUMAR 

Ayah : 44

قُل لِّلَّهِ ٱلشَّفَٰعَةُ جَمِيعٗاۖ لَّهُۥ مُلۡكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۖ ثُمَّ إِلَيۡهِ تُرۡجَعُونَ

Sema: Uombezi wote uko kwa Allah. Ni wake Yeye tu ufalme wa mbingu na ardhi. Kisha mtarejeshwa kwake



Surah: AZZUKHRUF 

Ayah : 86

وَلَا يَمۡلِكُ ٱلَّذِينَ يَدۡعُونَ مِن دُونِهِ ٱلشَّفَٰعَةَ إِلَّا مَن شَهِدَ بِٱلۡحَقِّ وَهُمۡ يَعۡلَمُونَ

Wala hao mnao waomba badala yake hawana uwezo wa kumwombea mtu, isipo kuwa anayeshuhudia kwa haki, na wao wanajua



Surah: ANNAJMI 

Ayah : 26

۞وَكَم مِّن مَّلَكٖ فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ لَا تُغۡنِي شَفَٰعَتُهُمۡ شَيۡـًٔا إِلَّا مِنۢ بَعۡدِ أَن يَأۡذَنَ ٱللَّهُ لِمَن يَشَآءُ وَيَرۡضَىٰٓ

Na kuna malaika wengi mbinguni hainufaishi chochote uombezi wao ila baada ya kupewa idhini na Allah kwa amtakaye na amridhie



Surah: ALMUDDATH-THIR 

Ayah : 48

فَمَا تَنفَعُهُمۡ شَفَٰعَةُ ٱلشَّـٰفِعِينَ

Basi haitowafaa uombezi wowote wa waombezi