Surah: AL-AN’AAM 

Ayah : 31

قَدۡ خَسِرَ ٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ بِلِقَآءِ ٱللَّهِۖ حَتَّىٰٓ إِذَا جَآءَتۡهُمُ ٱلسَّاعَةُ بَغۡتَةٗ قَالُواْ يَٰحَسۡرَتَنَا عَلَىٰ مَا فَرَّطۡنَا فِيهَا وَهُمۡ يَحۡمِلُونَ أَوۡزَارَهُمۡ عَلَىٰ ظُهُورِهِمۡۚ أَلَا سَآءَ مَا يَزِرُونَ

Hakika, wamepata hasara wale waliopinga kukutana na Allah, hadi kitakapowajia Kiyama ghafla watasema: Eee! Majuto ni yetu kwa (sababu ya) yale tuliyoyafanyia uzembe humo (duniani), na huku wanabeba mizigo (makosa) yao migongoni mwao. Elewa kwamba, ni mabaya mno hayo (madhambi) wanayoyabeba



Surah: AL-AN’AAM 

Ayah : 40

قُلۡ أَرَءَيۡتَكُمۡ إِنۡ أَتَىٰكُمۡ عَذَابُ ٱللَّهِ أَوۡ أَتَتۡكُمُ ٱلسَّاعَةُ أَغَيۡرَ ٱللَّهِ تَدۡعُونَ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ

Sema: Hivi mnaonaje itakapokujieni adhabu ya Allah (hapa duniani) au kitakapokujieni Kiyama, hivi mtawaomba (Miungu wengine) badala ya Allah kama kweli nyinyi ni wakweli?



Surah: AL-AARAAF 

Ayah : 187

يَسۡـَٔلُونَكَ عَنِ ٱلسَّاعَةِ أَيَّانَ مُرۡسَىٰهَاۖ قُلۡ إِنَّمَا عِلۡمُهَا عِندَ رَبِّيۖ لَا يُجَلِّيهَا لِوَقۡتِهَآ إِلَّا هُوَۚ ثَقُلَتۡ فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۚ لَا تَأۡتِيكُمۡ إِلَّا بَغۡتَةٗۗ يَسۡـَٔلُونَكَ كَأَنَّكَ حَفِيٌّ عَنۡهَاۖ قُلۡ إِنَّمَا عِلۡمُهَا عِندَ ٱللَّهِ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يَعۡلَمُونَ

Wanakuuliza kuhusu Kiyama; ni lini? Sema: Ilivyo ni kwamba ujuzi wake upo kwa Mola wangu Mlezi. Hakuna wa kuuweka wazi wakati wake isipokuwa yeye tu. Limekuwa jambo zito mno mbinguni na ardhini. Hakitakujieni isipokuwa tu kwa ghafla. Wanakuuliza kuhusu hicho (Kiyama) kama vile wewe umekitafiti (na ukakijua bara bara). Sema (uwaambie): Ujuzi wake uko kwa Allah na lakini watu wengi hawajui



Surah: YUSUF 

Ayah : 107

أَفَأَمِنُوٓاْ أَن تَأۡتِيَهُمۡ غَٰشِيَةٞ مِّنۡ عَذَابِ ٱللَّهِ أَوۡ تَأۡتِيَهُمُ ٱلسَّاعَةُ بَغۡتَةٗ وَهُمۡ لَا يَشۡعُرُونَ

Je, hivi wamejiaminisha kuwa haitowajia adhabu ya Allah ya kuwagubika au hakitawafikia Kiyama kwa ghafla na hali hawatambui?



Surah: ANNAHLI 

Ayah : 77

وَلِلَّهِ غَيۡبُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۚ وَمَآ أَمۡرُ ٱلسَّاعَةِ إِلَّا كَلَمۡحِ ٱلۡبَصَرِ أَوۡ هُوَ أَقۡرَبُۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٞ

Na ni Allah tu anayejua visivyoo-nekana mbinguni na ardhini na halikua jambo la kutokea Kiyama (uharaka wa kutokea) kwake isipokuwa tu ni kama kupepesa jicho au ni haraka zaidi ya hivyo. Hakika Allah ni muweza wa kila kitu



Surah: TWAHA 

Ayah : 15

إِنَّ ٱلسَّاعَةَ ءَاتِيَةٌ أَكَادُ أُخۡفِيهَا لِتُجۡزَىٰ كُلُّ نَفۡسِۭ بِمَا تَسۡعَىٰ

Hakika Saa (Kiyama) kitakuja bila ya shaka. Nimekaribia kukificha, ili kila nafsi ilipwe kwa iliyo yafanya



Surah: AL-HAJJ 

Ayah : 1

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ ٱتَّقُواْ رَبَّكُمۡۚ إِنَّ زَلۡزَلَةَ ٱلسَّاعَةِ شَيۡءٌ عَظِيمٞ

Enyi watu, mcheni Mola wenu Mlezi. Hakika tetemeko la Kiyama ni jambo kubwa mno



Surah: ARRUUM 

Ayah : 12

وَيَوۡمَ تَقُومُ ٱلسَّاعَةُ يُبۡلِسُ ٱلۡمُجۡرِمُونَ

Na itaposimama Saa wakosefu watakata tamaa



Surah: ARRUUM 

Ayah : 14

وَيَوۡمَ تَقُومُ ٱلسَّاعَةُ يَوۡمَئِذٖ يَتَفَرَّقُونَ

Na siku itaposimama Saa, siku hiyo watagawanyika



Surah: AL-AHZAAB 

Ayah : 63

يَسۡـَٔلُكَ ٱلنَّاسُ عَنِ ٱلسَّاعَةِۖ قُلۡ إِنَّمَا عِلۡمُهَا عِندَ ٱللَّهِۚ وَمَا يُدۡرِيكَ لَعَلَّ ٱلسَّاعَةَ تَكُونُ قَرِيبًا

Watu wanakuuliza khabari ya Saa (ya Kiyama). Sema: Ujuzi wake uko kwa Allah. Na nini kitakujulisha? Pengine hiyo Saa iko karibu



Surah: SABAA 

Ayah : 3

وَقَالَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ لَا تَأۡتِينَا ٱلسَّاعَةُۖ قُلۡ بَلَىٰ وَرَبِّي لَتَأۡتِيَنَّكُمۡ عَٰلِمِ ٱلۡغَيۡبِۖ لَا يَعۡزُبُ عَنۡهُ مِثۡقَالُ ذَرَّةٖ فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَلَا فِي ٱلۡأَرۡضِ وَلَآ أَصۡغَرُ مِن ذَٰلِكَ وَلَآ أَكۡبَرُ إِلَّا فِي كِتَٰبٖ مُّبِينٖ

Na walisema walio kufuru: Haitatufikia Saa (ya Kiyama). Sema: Kwani? Hapana shaka itakufikieni, naapa kwa haki ya Mola wangu Mlezi, Mwenye kujua ya ghaibu! Hapana kinacho fichikana kwake hata chenye uzito wa chembe tu, si katika mbingu wala katika ardhi, wala kilicho kidogo kuliko hivyo, wala kikubwa zaidi; ila vyote hivyo vimo katika Kitabu chake chenye kubainisha



Surah: GHAAFIR 

Ayah : 59

إِنَّ ٱلسَّاعَةَ لَأٓتِيَةٞ لَّا رَيۡبَ فِيهَا وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يُؤۡمِنُونَ

Hakika Saa (ya Kiyama) itafika, nayo haina shaka. Lakini watu wengi hawaamini



Surah: FUSSWILAT 

Ayah : 47

۞إِلَيۡهِ يُرَدُّ عِلۡمُ ٱلسَّاعَةِۚ وَمَا تَخۡرُجُ مِن ثَمَرَٰتٖ مِّنۡ أَكۡمَامِهَا وَمَا تَحۡمِلُ مِنۡ أُنثَىٰ وَلَا تَضَعُ إِلَّا بِعِلۡمِهِۦۚ وَيَوۡمَ يُنَادِيهِمۡ أَيۡنَ شُرَكَآءِي قَالُوٓاْ ءَاذَنَّـٰكَ مَامِنَّا مِن شَهِيدٖ

Ujuzi wa kuijua Saa ya Kiyama unarudishwa kwake tu Allah. Na matunda hayatoki katika mafumba yake, wala mwanamke hachukui mimba, wala hazai, isipokuwa (Allah) anajua. Na siku atakayo waita, akawaambia: Wako wapi washirika wangu? Hapo watasema: Tunakiri kwako ya kwamba hapana miongoni mwetu anaye shuhudia hayo



Surah: AZZUKHRUF 

Ayah : 66

هَلۡ يَنظُرُونَ إِلَّا ٱلسَّاعَةَ أَن تَأۡتِيَهُم بَغۡتَةٗ وَهُمۡ لَا يَشۡعُرُونَ

Je! Nini wanangojea ila Saa (Kiyama) kiwajie kwa ghafla na wala wao hawatambui?



Surah: AL-JAATHIYA 

Ayah : 32

وَإِذَا قِيلَ إِنَّ وَعۡدَ ٱللَّهِ حَقّٞ وَٱلسَّاعَةُ لَا رَيۡبَ فِيهَا قُلۡتُم مَّا نَدۡرِي مَا ٱلسَّاعَةُ إِن نَّظُنُّ إِلَّا ظَنّٗا وَمَا نَحۡنُ بِمُسۡتَيۡقِنِينَ

Na ikisemwa: Hakika ahadi ya Allah ni kweli, na Kiyama hakina shaka, nyinyi mkasema: Hatuijui hicho Kiyama, tunadhania dhana tu, wala hatuna yakini



Surah: ADH-DHAARIYAAT 

Ayah : 5

إِنَّمَا تُوعَدُونَ لَصَادِقٞ

(Kwamba) Hakika ilivyo ni kwamba, mnachoahidiwa ni kweli kabisa



Surah: ADH-DHAARIYAAT 

Ayah : 6

وَإِنَّ ٱلدِّينَ لَوَٰقِعٞ

Na Hakika, malipo (Siku ya Kiyama) kwa yakini kabisa yatakuwepo



Surah: AL-QAMAR

Ayah : 1

ٱقۡتَرَبَتِ ٱلسَّاعَةُ وَٱنشَقَّ ٱلۡقَمَرُ

Kimekaribia Kiyama na mwezi umepasuka



Surah: AL-QAMAR

Ayah : 2

وَإِن يَرَوۡاْ ءَايَةٗ يُعۡرِضُواْ وَيَقُولُواْ سِحۡرٞ مُّسۡتَمِرّٞ

Na (Makafiri kila) wanapoona Aya yoyote (ishara/muujiza) wanakengeuka na kusema: (Huu) Ni uchawi endelevu



Surah: AL-QAMAR

Ayah : 3

وَكَذَّبُواْ وَٱتَّبَعُوٓاْ أَهۡوَآءَهُمۡۚ وَكُلُّ أَمۡرٖ مُّسۡتَقِرّٞ

Na wamekadhibisha (haki) na wamefuata utashi wa nafsi zao. Na kila jambo (la kheri au la shari) litatulia (mahali pake. Watu wema watalipwa wema na watu wabaya watalipwa ubaya)



Surah: AL-QAMAR

Ayah : 4

وَلَقَدۡ جَآءَهُم مِّنَ ٱلۡأَنۢبَآءِ مَا فِيهِ مُزۡدَجَرٌ

Na kwa yakini kabisa, katika habari muhimu, imekwishawajia habari ambayo ndani yake mna makemeo makali



Surah: AL-QAMAR

Ayah : 5

حِكۡمَةُۢ بَٰلِغَةٞۖ فَمَا تُغۡنِ ٱلنُّذُرُ

Ni hekima ya kiwango cha juu kabisa, lakini maonyo (wanayopewa) hayasaidii kitu



Surah: AL-MULK 

Ayah : 25

وَيَقُولُونَ مَتَىٰ هَٰذَا ٱلۡوَعۡدُ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ

Na wanasema: Ni lini hiyo ahadi (ya kufufuliwa), mkiwa ni wasemao kweli?



Surah: AL-MULK 

Ayah : 26

قُلۡ إِنَّمَا ٱلۡعِلۡمُ عِندَ ٱللَّهِ وَإِنَّمَآ أَنَا۠ نَذِيرٞ مُّبِينٞ

Sema: Hakika ujuzi wake uko kwa Allah; na hakika mimi ni muonyaji tu mwenye kubainisha



Surah: AL-MULK 

Ayah : 27

فَلَمَّا رَأَوۡهُ زُلۡفَةٗ سِيٓـَٔتۡ وُجُوهُ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ وَقِيلَ هَٰذَا ٱلَّذِي كُنتُم بِهِۦ تَدَّعُونَ

Basi watakapoiona (adhabu ya Kiyama) inakaribia, zitahuzunika nyuso za wale waliokufuru, na itasemwa: Hii ndio ambayo mliyokuwa mkiiomba