Surah: ATTAGHAABUN 

Ayah : 11

مَآ أَصَابَ مِن مُّصِيبَةٍ إِلَّا بِإِذۡنِ ٱللَّهِۗ وَمَن يُؤۡمِنۢ بِٱللَّهِ يَهۡدِ قَلۡبَهُۥۚ وَٱللَّهُ بِكُلِّ شَيۡءٍ عَلِيمٞ

Haufiki msiba wowote ila kwa idhini ya Allah. Na mwenye kumuamini Allah huuongoa moyo wake. Na Allah ni Mjuzi wa kila kitu



Surah: ALJINN 

Ayah : 14

وَأَنَّا مِنَّا ٱلۡمُسۡلِمُونَ وَمِنَّا ٱلۡقَٰسِطُونَۖ فَمَنۡ أَسۡلَمَ فَأُوْلَـٰٓئِكَ تَحَرَّوۡاْ رَشَدٗا

Na hakika sisi miongoni mwetu ni Waislamu, na miongoni mwetu wapo wakengeukaji; (wanao acha haki). Hivyo atakaye silimu, hao ndio waliofuata uongofu



Surah: AL-INSAAN

Ayah : 3

إِنَّا هَدَيۡنَٰهُ ٱلسَّبِيلَ إِمَّا شَاكِرٗا وَإِمَّا كَفُورًا

Hakika, sisi tumemuongoza (tumempa mwongozo unaofikishwa na Mitume); ama awe mwenye kushukuru au mwenye kukufuru



Surah: ALLAIL 

Ayah : 12

إِنَّ عَلَيۡنَا لَلۡهُدَىٰ

Hakika ni juu yetu kuonyesha uongofu



Surah: ALLAIL 

Ayah : 13

وَإِنَّ لَنَا لَلۡأٓخِرَةَ وَٱلۡأُولَىٰ

Na hakika ni yetu Sisi Akhera na dunia