Allah amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao. Wawe wananiabudu Mimi, wala wasinishirikishe na chochote. Na watao kufuru baada ya hayo, basi hao ndio wapotovu”. Surat Nuur: 55
Ahadi ya Allah kwa Waumini ambao wanatenda mema ni kuwafanya makhalifa katika ardhi, na kuwapa amani na usimamizi
Kuwa muaminifu kwa Allah na kushikamana na utiifu ni njia ya kupata ahadi hiyo
Tunajifunza kuwa
Ahadi ya Allah ni kuwamakinisha Waumini katika ardhi.
Thibiti katika imani na kutenda mema, Allah amekuahidi kuwa na amani na utulivu baada ya hofu
Tambua kuwa njia yako ya kuwa msimamizi wa mambo inaanza kwa wewe kuwa na yakini na kufanya ibada
mmekuwa bora ya umma walio tolewa watu, kwa kuwa mnaamrisha mema na mnakataza maovu, na mnamuamini Allah. Na lau kwa Watu wa Kitabu nao wangeamini ingeli kuwa bora kwao. Wapo miongoni mwao waumini, lakini wengi wao wapotovu”.Surat Aal- Imran: 110.
Wewe - Muumini - ni mtu bora katika umma huu kwa watu, majukumu yako makubwa ni kuamrisha mema na kukataza maovu
Basi, kuwa wewe ni nuru ya kuongoza katika haki na kutenda mema daima
Tunajifunza kuwa:
Ubora wa umma huu ni kusimamia majukumu ya imani.
Ubora wako - ewe Muumini - unapatikana kwa imani yako na kueneza kheri na kwa kupambana na maovu. Kuwa mfano bora wa kuigwa katika mema, kwani jamii inahitaji kuona manufaa yako kwa kutenda mema
“Enyi mlio amini! Msiingie nyumba za Nabii ila mpewe ruhusa kwenda kula, sio kungojea kiwive. Lakini mtakapo itwa basi ingieni, na mkisha kula tawanyikeni, wala msiweke mazungumzo. Hakika hayo yanamuudhi Nabii naye anakustahini, lakini Allah hastahi kwa jambo la haki. Na mnapo wauliza wakeze haja waulizeni nyuma ya mapazia, hivyo ndio usafi zaidi kwa nyoyo zenu na nyoyo zao. Wala haifai kwenu kumuudhi Mtume wa Allah, wala kuwaoa wake zake baada yake kabisa. Hakika jambo hilo ni kubwa mbele ya Allah”. Surat Al-Ahzaab: 53.
Usafi unaanza-kwako- kwa kushikamana na tabia njema za kuamiliana na kuchunga mipaka ya adabu.
Kushikamana na mambo hayo kutausafisha moyo wako na kulinda usafi wa mioyo ya wengine.
Basi, fanya usafi huo ni anuani ya mahusiano yako wakati wote.
Tunajifunza kuwa:
Usafi wa nyoyo huleta adabu za kuamiliana vizuri.
Kujiheshimu na kuwa na heshima katika kuamiliana ni msingi imara wa kuzisafisha nyoyo.
Basi, weka kizuizi kati yako, kwa kushikamana na adabu njema zinazo leta nuru katika moyo wako na mioyo ya walio kuzunguka, kwani hayo ndiyo mafanikio yako.
Tunajifunza kuwa:
Kushikamana na tabia njema ni msingi wa kuzisafisha nyoyo.
Na waambie Waumini wanawake wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao, wala wasioneshe uzuri wao isipo kuwa unao dhihirika. Na waangushe shungi zao juu ya vifua vyao, wala wasioneshe uzuri wao ila kwa waume zao, au baba zao, au baba wa waume zao, au watoto wao, au watoto wa waume zao, au kaka zao, au wana wa kaka zao, au wana wa dada zao, au wanawake wenzao, au iliyo wamiliki mikono yao ya kuume, au wafuasi wanaume wasio na matamanio, au watoto ambao hawajajua mambo yaliyo khusu uke. Wala wasipige chini miguu yao ili yajulikane mapambo waliyo yaficha. Na tubuni nyote kwa Allah, enyi Waumini, ili mpate kufanikiwa”. Surat Nuur: 31
Maendeleo ya kitabia yana maanisha kupupia juu ya kuto onesha wazi mambo yanayo takiwa kufichwa.
Basi, jipambe kwa tabia ya aibu (hayaa), kwani hiyo ni anuani bora ya uzuri wa kweli.
Tunajifunza kuwa:
Uzuri wa aibu (hayaa) ni Mwanamke kuwa na tabia ya aibu (hayaa).
Heshima hudhihirisha uzuri wa roho na kujenga maadili mema.
Basi - Ewe Mwanamke - kuwa mfano mwema wa kuigwa kwa heshima yako, kwani aibu ni pambo la mwanamke na anuani ya maendeleo yake.
“Mitume hao ni wabashiri na waonyaji, ili watu wasiwe na hoja juu ya Allah baada ya kuletewa Mitume. Na Allah ni Mwenye nguvu, Mwenye hikima”. Surat Nisaa: 165.
Allah amewatuma Mitume ili wabashiri na waonye, na wawe ni hoja na dalili ya wazi kwa viumbe.
Basi, kuwa na pupa sana ya kufuata miongozo yao, kwani hiyo ndiyo njia ya kuijua haki.
Tunajifunza kuwa
Miongozo ya Mitume ndiyo njia ya kuijua haki.
Mitume walibeba ujumbe wa uongofu ili kusimamisha hoja juu ya watu.
Basi, kuwa mwerevu na ujifunze nuru ya ujumbe wa Mitume, ambao ndiyo wenye kukuangazia maisha yako yote.
Tunajifunza kuwa
Nuru ya ujumbe wa Mitume ni hekima (huruma) ya Allah kwa viumbe.
“Haiwi kwa Allah kuwaacha Waumini katika hali mliyo nayo mpaka apambanue wabaya na wema. Wala haiwi kwa Allah kukujulisheni mambo ya ghaibu. Lakini Allah humteua katika Mitume wake amtakaye. Basi muaminini Allah na Mitume yake. Na mkiamini na mkamchamungu mtakuwa na ujira mkubwa”. Surat Aal- Imran: 179.
Ghaibu ni ujuzi wa Allah peke yake. Lakini Mitume yake walio chaguliwa hutubebea mambo ya ghaibu yenye nuru ya uongofu.
Basi, jilazimishe kuamini hekima ya Allah na kujisalimisha mambo yako yote kwake, kwani kila kitu kwake kipo kwa makadirio.
Tunajifunza kuwa
Elimu ya ghabu ni hekima ya Allah peke yake.
Si kila kitu tunaweza kukiona au kukijua, bali Allah peke yake ndiye Mjuzi wa ghaibu, na huchagua katika Mitume yake anaye tuletea mambo ya ghaibu yaliyo ya haki.
Basi, kuamini kwako ghaibu ndiyo njia ya kukufikisha katika yakini.
Tunajifunza kuwa
Kuwa na yakini na Allah ni miongoni mwa miongozo ya Mitume.
“Hakika hii Qur’an inaongoa kwenye yale yaliyo nyooka kabisa, na inawabashiria Waumini ambao wanatenda mema ya kwamba watapata malipo makubwa”. Surat Al-Israa: 9.
Qur’an ndiyo njia yako ya kukufikisha katika maisha mazuri, inayokuongoza kwenye njia sahihi, na kukubashiria kupata malipo makubwa.
Basi, shikamana nayo ili upate utukufu na mafanikio.
Tunajifunza kuwa:
Muongozo wa Qur’an ndiyo wenye malipo makubwa.
Qur’an ni nuru inayo kuongoza katika njia sahihi, na kukuahidi kupata malipo bora ikiwa utatenda mema.
Basi, ufanye mfumo wa maisha yako uwe unatokana na maelekezo yake, kwani utukufu unapatikana kwa kuifuata.
Tunajifunza kuwa:
Qur’an ndiyo mfumo bora wa maisha na njia iliyo nyooka.
“Sema: Hakika Sala yangu, na ibada zangu, na uhai wangu, na kufa kwangu, ni kwa ajili ya Allah, Mola Mlezi wa viumbe vyote”. Surat Al-An’aam: 162.
Yafanye maisha yako yote ni kwa ajili ya Allah, katika Sala zako na matendo yako, na kila harakati zako za kila siku. Kwani kumtakasia Allah katika ibada zako ndiyo njia ya utukufu wako.
Tunajifunza kuwa:
Kumtakasia Allah ni njia bora ya kurekebisha maisha yasiyo na mipaka.
Sala zako, ibada zako na maisha yako yote yanapo kuwa ni kwa ajili ya Allah, utapata nguvu na utulivu.
Ishi kwa ajili ya Allah, hiyo ndiyo maana ya maisha ya kweli.
Tunajifunza kuwa:
Maisha kwa ajili ya Allah ndiyo sababu ya kupata radhi za Allah.