فَإِن لَّمۡ تَفۡعَلُواْ وَلَن تَفۡعَلُواْ فَٱتَّقُواْ ٱلنَّارَ ٱلَّتِي وَقُودُهَا ٱلنَّاسُ وَٱلۡحِجَارَةُۖ أُعِدَّتۡ لِلۡكَٰفِرِينَ
Na msipofanya (hivyo) na kamwe hamtaweza kufanya (hivyo), basi uogopeni Moto ambao nishati yake ni watu na mawe, ulioandaliwa kwa ajili ya makafiri
وَبَشِّرِ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّـٰلِحَٰتِ أَنَّ لَهُمۡ جَنَّـٰتٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُۖ كُلَّمَا رُزِقُواْ مِنۡهَا مِن ثَمَرَةٖ رِّزۡقٗا قَالُواْ هَٰذَا ٱلَّذِي رُزِقۡنَا مِن قَبۡلُۖ وَأُتُواْ بِهِۦ مُتَشَٰبِهٗاۖ وَلَهُمۡ فِيهَآ أَزۡوَٰجٞ مُّطَهَّرَةٞۖ وَهُمۡ فِيهَا خَٰلِدُونَ
Na wape bishara wale walioamini na kufanya matendo mema kuwa, watapata bustani zitiririkazo mito chini yake. Kila wanapopewa riziki ya matunda humo wanasema: Hii ndio ile riziki tuliyopewa kabla. Na wamepewa riziki hiyo ikiwa inafanana. Na watapata humo wake waliotwaharishwa, na watabaki humo daima
۞إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَسۡتَحۡيِۦٓ أَن يَضۡرِبَ مَثَلٗا مَّا بَعُوضَةٗ فَمَا فَوۡقَهَاۚ فَأَمَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ فَيَعۡلَمُونَ أَنَّهُ ٱلۡحَقُّ مِن رَّبِّهِمۡۖ وَأَمَّا ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ فَيَقُولُونَ مَاذَآ أَرَادَ ٱللَّهُ بِهَٰذَا مَثَلٗاۘ يُضِلُّ بِهِۦ كَثِيرٗا وَيَهۡدِي بِهِۦ كَثِيرٗاۚ وَمَا يُضِلُّ بِهِۦٓ إِلَّا ٱلۡفَٰسِقِينَ
Hakika, Allah haoni aibu kutoa mfano wowote; wa mbu na (mfano) zaidi (ya mbu). Ama walioamini wanajua kuwa mfano huo ni haki kutoka kwa Mola wao. Na ama waliokufuru, wanasema kuwa: Allah amekusudia nini kwa mfano huu? Allah, kwa mfano huu, anawaacha wengi wapotee na anawaongoza wengi. Na (Allah) hawaachi kupotea kwa mfano huu isipokuwa waovu tu
ٱلَّذِينَ يَنقُضُونَ عَهۡدَ ٱللَّهِ مِنۢ بَعۡدِ مِيثَٰقِهِۦ وَيَقۡطَعُونَ مَآ أَمَرَ ٱللَّهُ بِهِۦٓ أَن يُوصَلَ وَيُفۡسِدُونَ فِي ٱلۡأَرۡضِۚ أُوْلَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡخَٰسِرُونَ
Ambao wana vunja ahadi za Allah baada ya kuwekwa, na wanakataa alichoamuru Allah kiungwe, na wanafanya uharibifu ardhini. Hao tu ndio wenye hasara
كَيۡفَ تَكۡفُرُونَ بِٱللَّهِ وَكُنتُمۡ أَمۡوَٰتٗا فَأَحۡيَٰكُمۡۖ ثُمَّ يُمِيتُكُمۡ ثُمَّ يُحۡيِيكُمۡ ثُمَّ إِلَيۡهِ تُرۡجَعُونَ
Vipi mnamkufuru Allah, na ilhali mlikuwa wafu akakupeni uhai? Kisha atakufisheni, kisha atakupeni uhai. Na kisha ni kwake tu ndiko mtakakorejeshwa
هُوَ ٱلَّذِي خَلَقَ لَكُم مَّا فِي ٱلۡأَرۡضِ جَمِيعٗا ثُمَّ ٱسۡتَوَىٰٓ إِلَى ٱلسَّمَآءِ فَسَوَّىٰهُنَّ سَبۡعَ سَمَٰوَٰتٖۚ وَهُوَ بِكُلِّ شَيۡءٍ عَلِيمٞ
Ni yeye tu aliye kuumbieni vyote vilivyomo ardhini. Kisha akakusudia mbingu na kuziumba zikiwa mbingu saba zilizo sawa. Na yeye ni mjuzi wa kila kitu
وَإِذۡ قَالَ رَبُّكَ لِلۡمَلَـٰٓئِكَةِ إِنِّي جَاعِلٞ فِي ٱلۡأَرۡضِ خَلِيفَةٗۖ قَالُوٓاْ أَتَجۡعَلُ فِيهَا مَن يُفۡسِدُ فِيهَا وَيَسۡفِكُ ٱلدِّمَآءَ وَنَحۡنُ نُسَبِّحُ بِحَمۡدِكَ وَنُقَدِّسُ لَكَۖ قَالَ إِنِّيٓ أَعۡلَمُ مَا لَا تَعۡلَمُونَ
Na (kumbuka) Mola wako alipowaambia Malaika kuwa: Kwa yakini, mimi nitamuweka Khalifa ardhini. Wakasema: Hivi unamuweka humo atakayefanya uharibifu humo na kumwaga damu, na wakati sisi tunakutakasa kwa kukusifu? (Allah) Akasema: Mimi ninajua msichokijua
وَعَلَّمَ ءَادَمَ ٱلۡأَسۡمَآءَ كُلَّهَا ثُمَّ عَرَضَهُمۡ عَلَى ٱلۡمَلَـٰٓئِكَةِ فَقَالَ أَنۢبِـُٔونِي بِأَسۡمَآءِ هَـٰٓؤُلَآءِ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ
Na akamfundisha Adamu majina yote, kisha akawaleta wenye majina hayo mbele ya malaika. Akawaambia: Nitajieni majina ya hawa kama ninyi ni wa kweli
قَالُواْ سُبۡحَٰنَكَ لَا عِلۡمَ لَنَآ إِلَّا مَا عَلَّمۡتَنَآۖ إِنَّكَ أَنتَ ٱلۡعَلِيمُ ٱلۡحَكِيمُ
Wakasema: Utakatifu ni wako. Hakuna tunachokijua ila tu ulichotujulisha. Hakika, wewe tu ndiye Mjuzi, Mwenye hekima
قَالَ يَـٰٓـَٔادَمُ أَنۢبِئۡهُم بِأَسۡمَآئِهِمۡۖ فَلَمَّآ أَنۢبَأَهُم بِأَسۡمَآئِهِمۡ قَالَ أَلَمۡ أَقُل لَّكُمۡ إِنِّيٓ أَعۡلَمُ غَيۡبَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَأَعۡلَمُ مَا تُبۡدُونَ وَمَا كُنتُمۡ تَكۡتُمُونَ
Akasema: Ewe Adamu, waambie majina yao. Basi alipowaambia majina yao, (Allah) akasema: Je, si nilikuambieni kuwa mimi ninajua visivyoonekana mbinguni na ardhini? Na ninayajua mno mnayo yadhihirisha na mnayoyaficha
وَإِذۡ قُلۡنَا لِلۡمَلَـٰٓئِكَةِ ٱسۡجُدُواْ لِأٓدَمَ فَسَجَدُوٓاْ إِلَّآ إِبۡلِيسَ أَبَىٰ وَٱسۡتَكۡبَرَ وَكَانَ مِنَ ٱلۡكَٰفِرِينَ
Na (kumbuka) tulipowaambia Malaika (kuwa): Msujudieni Adamu. Wakasujudu, isipokuwa Ibilisi alikataa na kuleta kiburi na akawa miongoni mwa makafiri
وَقُلۡنَا يَـٰٓـَٔادَمُ ٱسۡكُنۡ أَنتَ وَزَوۡجُكَ ٱلۡجَنَّةَ وَكُلَا مِنۡهَا رَغَدًا حَيۡثُ شِئۡتُمَا وَلَا تَقۡرَبَا هَٰذِهِ ٱلشَّجَرَةَ فَتَكُونَا مِنَ ٱلظَّـٰلِمِينَ
Na tulisema: Ewe Adamu, ishi wewe na mkeo Peponi na kuleni humo kwa uhuru popote mtakapo na msiusogelee mti huu ili msije mkawa miongoni mwa madhalimu
فَأَزَلَّهُمَا ٱلشَّيۡطَٰنُ عَنۡهَا فَأَخۡرَجَهُمَا مِمَّا كَانَا فِيهِۖ وَقُلۡنَا ٱهۡبِطُواْ بَعۡضُكُمۡ لِبَعۡضٍ عَدُوّٞۖ وَلَكُمۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ مُسۡتَقَرّٞ وَمَتَٰعٌ إِلَىٰ حِينٖ
Shetani akawatelezesha kwenye Pepo hiyo, hivyo akawatoa katika hali waliyokuwa nayo. Na tukasema: Teremkeni. Nyinyi kwa nyinyi mtakuwa maadui. Na mtakuwa na makazi na starehe ardhini mpaka muda maalumu
فَتَلَقَّىٰٓ ءَادَمُ مِن رَّبِّهِۦ كَلِمَٰتٖ فَتَابَ عَلَيۡهِۚ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلتَّوَّابُ ٱلرَّحِيمُ
Adamu akapokea maneno (ya toba) kutoka kwa Mola wake (akatubu) na (Allah) akamkubalia toba yake. Hakika yeye (Allah) ni Mwingi wa kupokea toba, Mwingi wa rehema
قُلۡنَا ٱهۡبِطُواْ مِنۡهَا جَمِيعٗاۖ فَإِمَّا يَأۡتِيَنَّكُم مِّنِّي هُدٗى فَمَن تَبِعَ هُدَايَ فَلَا خَوۡفٌ عَلَيۡهِمۡ وَلَا هُمۡ يَحۡزَنُونَ
Tukasema: Teremkeni humo nyote. Basi utakapokujieni muongozo kutoka kwangu, watakaoufuata muongozo wangu hawatakuwa na hofu yoyote na wao hawatahuzunika
وَٱلَّذِينَ كَفَرُواْ وَكَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَآ أُوْلَـٰٓئِكَ أَصۡحَٰبُ ٱلنَّارِۖ هُمۡ فِيهَا خَٰلِدُونَ
Na ambao wamekufuru na wakazikadhibisha Aya zetu, hao ni watu wa motoni, wataishi humo milele
يَٰبَنِيٓ إِسۡرَـٰٓءِيلَ ٱذۡكُرُواْ نِعۡمَتِيَ ٱلَّتِيٓ أَنۡعَمۡتُ عَلَيۡكُمۡ وَأَوۡفُواْ بِعَهۡدِيٓ أُوفِ بِعَهۡدِكُمۡ وَإِيَّـٰيَ فَٱرۡهَبُونِ
Enyi Wana wa Israeli, kumbukeni neema zangu ambazo nimekuneemesheni, na tekelezeni ahadi zangu, nami nitekeleze ahadi zenu, naniogopeni mimi tu
وَءَامِنُواْ بِمَآ أَنزَلۡتُ مُصَدِّقٗا لِّمَا مَعَكُمۡ وَلَا تَكُونُوٓاْ أَوَّلَ كَافِرِۭ بِهِۦۖ وَلَا تَشۡتَرُواْ بِـَٔايَٰتِي ثَمَنٗا قَلِيلٗا وَإِيَّـٰيَ فَٱتَّقُونِ
Na yaaminini yale niliyo-yateremsha yakiwa yanasadikisha hayo mliyonayo, na msiwe wa kwanza kuyakufuru, na msizi-badilishe Aya zangu kwa thamani ndogo, na mniogope mimi tu
وَلَا تَلۡبِسُواْ ٱلۡحَقَّ بِٱلۡبَٰطِلِ وَتَكۡتُمُواْ ٱلۡحَقَّ وَأَنتُمۡ تَعۡلَمُونَ
Na msichanganye haki na batili na msifiche haki na ilhali mnajua
وَأَقِيمُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتُواْ ٱلزَّكَوٰةَ وَٱرۡكَعُواْ مَعَ ٱلرَّـٰكِعِينَ
Na simamisheni Swala na toeni Zaka na rukuuni pamoja na wanaorukuu
۞أَتَأۡمُرُونَ ٱلنَّاسَ بِٱلۡبِرِّ وَتَنسَوۡنَ أَنفُسَكُمۡ وَأَنتُمۡ تَتۡلُونَ ٱلۡكِتَٰبَۚ أَفَلَا تَعۡقِلُونَ
Je, mnaamrisha watu kutenda wema na mnajisahau, na ilhali nyinyi mnakisoma kitabu? Je, hamtumii akili?
وَٱسۡتَعِينُواْ بِٱلصَّبۡرِ وَٱلصَّلَوٰةِۚ وَإِنَّهَا لَكَبِيرَةٌ إِلَّا عَلَى ٱلۡخَٰشِعِينَ
Na ombeni msaada kwa kusubiri na kuswali. Na kwa hakika kabisa, hiyo Swala ni nzito mno isipokuwa kwa wanyenyekevu tu
ٱلَّذِينَ يَظُنُّونَ أَنَّهُم مُّلَٰقُواْ رَبِّهِمۡ وَأَنَّهُمۡ إِلَيۡهِ رَٰجِعُونَ
Ambao wana yakini kwamba watakutana na Mola wao, na kwamba kwake tu watarejea
يَٰبَنِيٓ إِسۡرَـٰٓءِيلَ ٱذۡكُرُواْ نِعۡمَتِيَ ٱلَّتِيٓ أَنۡعَمۡتُ عَلَيۡكُمۡ وَأَنِّي فَضَّلۡتُكُمۡ عَلَى ٱلۡعَٰلَمِينَ
Enyi Wana wa Israeli, kumbukeni neema zangu nilizo kuneemesheni, na kwamba mimi nimekufanyeni bora kuliko walimwengu (wa zama zenu)
وَٱتَّقُواْ يَوۡمٗا لَّا تَجۡزِي نَفۡسٌ عَن نَّفۡسٖ شَيۡـٔٗا وَلَا يُقۡبَلُ مِنۡهَا شَفَٰعَةٞ وَلَا يُؤۡخَذُ مِنۡهَا عَدۡلٞ وَلَا هُمۡ يُنصَرُونَ
Na iogopeni siku ambayo nafsi haitaisaidia chochote nafsi nyingine, na wala hautakubaliwa uombezi wowote kwa nafsi hiyo (kumuombea mwengine), na wala haitachukuliwa fidia yoyote kwa nafsi hiyo, nao hawatanusuriwa
وَإِذۡ نَجَّيۡنَٰكُم مِّنۡ ءَالِ فِرۡعَوۡنَ يَسُومُونَكُمۡ سُوٓءَ ٱلۡعَذَابِ يُذَبِّحُونَ أَبۡنَآءَكُمۡ وَيَسۡتَحۡيُونَ نِسَآءَكُمۡۚ وَفِي ذَٰلِكُم بَلَآءٞ مِّن رَّبِّكُمۡ عَظِيمٞ
Na (kumbukeni) tulipokuokoeni kutoka kwenye mateso ya Firauni na watu wake waliokupeni adhabu mbaya kabisa; wakiwauwa watoto wenu wanaume kwa kuwachinjachinja na wakiwaacha hai watoto wenu wanawake. Na katika hayo kuna mtihani mkubwa sana kwenu kutoka kwa Mola wenu
وَإِذۡ فَرَقۡنَا بِكُمُ ٱلۡبَحۡرَ فَأَنجَيۡنَٰكُمۡ وَأَغۡرَقۡنَآ ءَالَ فِرۡعَوۡنَ وَأَنتُمۡ تَنظُرُونَ
Na (kumbukeni) tulipokut-enganishieni bahari tukakuokoeni na tukawazamisha watu wa Firauni na nyinyi mkitazama
وَإِذۡ وَٰعَدۡنَا مُوسَىٰٓ أَرۡبَعِينَ لَيۡلَةٗ ثُمَّ ٱتَّخَذۡتُمُ ٱلۡعِجۡلَ مِنۢ بَعۡدِهِۦ وَأَنتُمۡ ظَٰلِمُونَ
Na (kumbukeni) tulipoahidiana na Musa siku arobaini, kisha nyinyi mkamfanya ndama (kuwa Mungu) baada ya hapo, na ilhali nyinyi ni wenye kudhulumu (nafsi zenu)”
ثُمَّ عَفَوۡنَا عَنكُم مِّنۢ بَعۡدِ ذَٰلِكَ لَعَلَّكُمۡ تَشۡكُرُونَ
Kisha tukakusameheni baada ya hapo ili mpate kushukuru
وَإِذۡ ءَاتَيۡنَا مُوسَى ٱلۡكِتَٰبَ وَٱلۡفُرۡقَانَ لَعَلَّكُمۡ تَهۡتَدُونَ
Na (kumbukeni) tulipompa Musa kitabu na upambanuzi ili mpate kuongoka