فَكُبۡكِبُواْ فِيهَا هُمۡ وَٱلۡغَاوُۥنَ
Basi watavurumizwa humo wao na hao wakosefu,
Compartir :
وَجُنُودُ إِبۡلِيسَ أَجۡمَعُونَ
Na majeshi ya Ibilisi yote
قَالُواْ وَهُمۡ فِيهَا يَخۡتَصِمُونَ
Watasema, na hali ya kuwa wanazozana humo:
تَٱللَّهِ إِن كُنَّا لَفِي ضَلَٰلٖ مُّبِينٍ
Wallahi! Kwa yakini tulikuwa katika upotovu ulio dhaahiri
إِذۡ نُسَوِّيكُم بِرَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ
Tulipo kufanyeni ni sawa na Mola Mlezi wa walimwengu wote
وَمَآ أَضَلَّنَآ إِلَّا ٱلۡمُجۡرِمُونَ
Na hawakupoteza ila wale wakosefu
فَمَا لَنَا مِن شَٰفِعِينَ
Basi hatuna waombezi
وَلَا صَدِيقٍ حَمِيمٖ
Wala rafiki wa dhati
فَلَوۡ أَنَّ لَنَا كَرَّةٗ فَنَكُونَ مِنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ
Laiti tungelipata kurejea tena tungeli kuwa katika Waumini
إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةٗۖ وَمَا كَانَ أَكۡثَرُهُم مُّؤۡمِنِينَ
Hakika katika haya ipo Ishara, lakini wengi wao hawakuwa wenye kuamini
وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ
Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu
كَذَّبَتۡ قَوۡمُ نُوحٍ ٱلۡمُرۡسَلِينَ
Kaumu ya Nuhu waliwakadhibisha Mitume
إِذۡ قَالَ لَهُمۡ أَخُوهُمۡ نُوحٌ أَلَا تَتَّقُونَ
Alipowaambia ndugu yao, Nuhu: Je! Hamumuogopi Allah?
إِنِّي لَكُمۡ رَسُولٌ أَمِينٞ
Hakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu
فَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَأَطِيعُونِ
Basi Mcheni Allah, na nitiini mimi
وَمَآ أَسۡـَٔلُكُمۡ عَلَيۡهِ مِنۡ أَجۡرٍۖ إِنۡ أَجۡرِيَ إِلَّا عَلَىٰ رَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ
Na sikutakini juu yake ujira, kwani ujira wangu hauko ila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote