كَمۡ تَرَكُواْ مِن جَنَّـٰتٖ وَعُيُونٖ
Mabustani mangapi, na chemchem ngapi waliziacha!
Compartir :
وَزُرُوعٖ وَمَقَامٖ كَرِيمٖ
Na mimea na vyeo vitukufu!
وَنَعۡمَةٖ كَانُواْ فِيهَا فَٰكِهِينَ
Na neema walizokuwa wakiji-stareheshea!
كَذَٰلِكَۖ وَأَوۡرَثۡنَٰهَا قَوۡمًا ءَاخَرِينَ
Ndio hivyo! Na tukawarithisha haya watu wenginewe
فَمَا بَكَتۡ عَلَيۡهِمُ ٱلسَّمَآءُ وَٱلۡأَرۡضُ وَمَا كَانُواْ مُنظَرِينَ
Hazikuwalilia mbingu wala ardhi, wala hawakupewa muhula
وَلَقَدۡ نَجَّيۡنَا بَنِيٓ إِسۡرَـٰٓءِيلَ مِنَ ٱلۡعَذَابِ ٱلۡمُهِينِ
Na bila ya shaka tuliwaokoa Wana wa Israili katika adhabu ya kuwadhalilisha
مِن فِرۡعَوۡنَۚ إِنَّهُۥ كَانَ عَالِيٗا مِّنَ ٱلۡمُسۡرِفِينَ
Ya Firauni. Hakika yeye alikuwa jeuri katika wenye kupindukia mipaka
وَلَقَدِ ٱخۡتَرۡنَٰهُمۡ عَلَىٰ عِلۡمٍ عَلَى ٱلۡعَٰلَمِينَ
Na tuliwakhiari kwa ujuzi wetu kuliko walimwengu wenginewe
وَءَاتَيۡنَٰهُم مِّنَ ٱلۡأٓيَٰتِ مَا فِيهِ بَلَـٰٓؤٞاْ مُّبِينٌ
Na tukawapa katika ishara zenye majaribio yaliyo wazi
إِنَّ هَـٰٓؤُلَآءِ لَيَقُولُونَ
Hakika hawa wanasema:
إِنۡ هِيَ إِلَّا مَوۡتَتُنَا ٱلۡأُولَىٰ وَمَا نَحۡنُ بِمُنشَرِينَ
Hapana ila kufa kwetu mara ya kwanza tu, wala sisi hatufufuliwi
فَأۡتُواْ بِـَٔابَآئِنَآ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ
Basi warudisheni baba zetu, ikiwa nyinyi mnasema kweli
أَهُمۡ خَيۡرٌ أَمۡ قَوۡمُ تُبَّعٖ وَٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡ أَهۡلَكۡنَٰهُمۡۚ إِنَّهُمۡ كَانُواْ مُجۡرِمِينَ
Je! Ni wao bora au watu wa Tubbaa’ na walio kuwa kabla yao? Tuliwaangamiza. Hakika hao walikuwa wakosefu
وَمَا خَلَقۡنَا ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ وَمَا بَيۡنَهُمَا لَٰعِبِينَ
Na hatukuziumba mbingu na ardhi na vilivyomo baina yake kwa mchezo
مَا خَلَقۡنَٰهُمَآ إِلَّا بِٱلۡحَقِّ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَهُمۡ لَا يَعۡلَمُونَ
Hatukuviumba hivyo ila kwa Haki, lakini wengi wao hawajui
إِنَّ يَوۡمَ ٱلۡفَصۡلِ مِيقَٰتُهُمۡ أَجۡمَعِينَ
Hakika siku ya Uamuzi ni wakati ulio wekwa kwa wao wote
يَوۡمَ لَا يُغۡنِي مَوۡلًى عَن مَّوۡلٗى شَيۡـٔٗا وَلَا هُمۡ يُنصَرُونَ
Siku ambayo rafiki hatamfaa rafiki yake kwa chochote, wala hawatanusuriwa
إِلَّا مَن رَّحِمَ ٱللَّهُۚ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ
Isipo kuwa atakaye mrehemu Allah. Hakika Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu
إِنَّ شَجَرَتَ ٱلزَّقُّومِ
Hakika Mti wa Zaqqum
طَعَامُ ٱلۡأَثِيمِ
Ni chakula cha mwenye dhambi
كَٱلۡمُهۡلِ يَغۡلِي فِي ٱلۡبُطُونِ
Kama shaba iliyo yayushwa, hutokota matumboni
كَغَلۡيِ ٱلۡحَمِيمِ
Kama kutokota kwa maji ya moto
خُذُوهُ فَٱعۡتِلُوهُ إِلَىٰ سَوَآءِ ٱلۡجَحِيمِ
(Itasemwa:) Mkamateni na mtupeni katikati ya Jahannamu!
ثُمَّ صُبُّواْ فَوۡقَ رَأۡسِهِۦ مِنۡ عَذَابِ ٱلۡحَمِيمِ
Kisha mwagieni juu ya kichwa chake adhabu ya maji yanayo chemka
ذُقۡ إِنَّكَ أَنتَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡكَرِيمُ
Onja! Ati wewe ndiye mwenye nguvu, mtukufu!
إِنَّ هَٰذَا مَا كُنتُم بِهِۦ تَمۡتَرُونَ
Hakika haya ndiyo mliyo kuwa mkiyatilia shaka
إِنَّ ٱلۡمُتَّقِينَ فِي مَقَامٍ أَمِينٖ
Hakika wachamngu watakuwa katika mahali pa amani
فِي جَنَّـٰتٖ وَعُيُونٖ
Katika mabustani na chemchem
يَلۡبَسُونَ مِن سُندُسٖ وَإِسۡتَبۡرَقٖ مُّتَقَٰبِلِينَ
Watavaa hariri nyepesi na hariri nzito wakikabiliana
كَذَٰلِكَ وَزَوَّجۡنَٰهُم بِحُورٍ عِينٖ
Hivi ndivyo itakavyo kuwa, na tutawaoza mahurulaini