۞وَإِذۡ نَتَقۡنَا ٱلۡجَبَلَ فَوۡقَهُمۡ كَأَنَّهُۥ ظُلَّةٞ وَظَنُّوٓاْ أَنَّهُۥ وَاقِعُۢ بِهِمۡ خُذُواْ مَآ ءَاتَيۡنَٰكُم بِقُوَّةٖ وَٱذۡكُرُواْ مَا فِيهِ لَعَلَّكُمۡ تَتَّقُونَ
Na (kumbuka) wakati tulipou-nyanyua mlima juu yao ukawa kama kiwingu na wakadhani kuwa utawaangukia (na kuwaambia): Chukueni kwa nguvu yale tuliyo-kupeni, na yakumbukeni yaliomo ndani yake ili muwe wacha Mungu
وَإِذۡ أَخَذَ رَبُّكَ مِنۢ بَنِيٓ ءَادَمَ مِن ظُهُورِهِمۡ ذُرِّيَّتَهُمۡ وَأَشۡهَدَهُمۡ عَلَىٰٓ أَنفُسِهِمۡ أَلَسۡتُ بِرَبِّكُمۡۖ قَالُواْ بَلَىٰ شَهِدۡنَآۚ أَن تَقُولُواْ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ إِنَّا كُنَّا عَنۡ هَٰذَا غَٰفِلِينَ
Na (kumbuka) wakati Mola wako alipochukua kwa wanadamu kizazi chao kutokea migongoni mwao na akawashuhudisha wen-yewe (kwa kuwauliza kwamba): Hivi mimi sio Mola wenu Mlezi? Wakasema: “Kwa nini (isiwe hivyo? Tumeshuhudia (kuwa wewe ni Mola wetu Mlezi”. (Tumefanya hivyo) Ili msije kusema Siku ya Kiyama kuwa: Sisi tulikuwa tumeghafilika na haya (tulikuwa hatuyajui)
أَوۡ تَقُولُوٓاْ إِنَّمَآ أَشۡرَكَ ءَابَآؤُنَا مِن قَبۡلُ وَكُنَّا ذُرِّيَّةٗ مِّنۢ بَعۡدِهِمۡۖ أَفَتُهۡلِكُنَا بِمَا فَعَلَ ٱلۡمُبۡطِلُونَ
Au (msije) mkasema: Hali ilivyo ni kwamba, baba zetu ndio waliofanya ushirikina kabla yetu, na sisi tulikuwa kizazi tu baada yao. Hivi basi unatuangamiza kwa sababu ya waliyoyafanya waharibifu?
وَكَذَٰلِكَ نُفَصِّلُ ٱلۡأٓيَٰتِ وَلَعَلَّهُمۡ يَرۡجِعُونَ
Na hivyo tunazifafanua Aya na huwenda watarejea (kwa Mola wao)
وَٱتۡلُ عَلَيۡهِمۡ نَبَأَ ٱلَّذِيٓ ءَاتَيۡنَٰهُ ءَايَٰتِنَا فَٱنسَلَخَ مِنۡهَا فَأَتۡبَعَهُ ٱلشَّيۡطَٰنُ فَكَانَ مِنَ ٱلۡغَاوِينَ
Na wasomee habari kubwa ya yule ambaye tulimpa Aya zetu na akajivua nazo (akazipuuza) na shetani akamfuatilia akawa miongoni mwa wapotevu
وَلَوۡ شِئۡنَا لَرَفَعۡنَٰهُ بِهَا وَلَٰكِنَّهُۥٓ أَخۡلَدَ إِلَى ٱلۡأَرۡضِ وَٱتَّبَعَ هَوَىٰهُۚ فَمَثَلُهُۥ كَمَثَلِ ٱلۡكَلۡبِ إِن تَحۡمِلۡ عَلَيۡهِ يَلۡهَثۡ أَوۡ تَتۡرُكۡهُ يَلۡهَثۚ ذَّـٰلِكَ مَثَلُ ٱلۡقَوۡمِ ٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَاۚ فَٱقۡصُصِ ٱلۡقَصَصَ لَعَلَّهُمۡ يَتَفَكَّرُونَ
Na kwa hakika kabisa, lau kama tungetaka tungempandisha (daraja la juu kabisa) kwa Aya hizo, lakini yeye aliing’ang’ania dunia na akafuata utashi wa nafsi yake. Basi mfano wake ni kama mfano wa mbwa; ukimkurupusha anatoa ulimi kwa kuhema na ukimuacha anatoa ulimi kwa kuhema. Huo ni mfano wa watu waliozikadhibisha Aya zetu. Basi hadithia visa hivi ili (watu) watafakari
سَآءَ مَثَلًا ٱلۡقَوۡمُ ٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَا وَأَنفُسَهُمۡ كَانُواْ يَظۡلِمُونَ
(Huo) Ni mfano mbaya kabisa (wa) watu waliokadhibisha Aya zetu na nafsi zao wakawa wanazidhulumu (kwa kutoamini)
مَن يَهۡدِ ٱللَّهُ فَهُوَ ٱلۡمُهۡتَدِيۖ وَمَن يُضۡلِلۡ فَأُوْلَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡخَٰسِرُونَ
Yeyote ambaye Allah amemuongoza, basi huyo tu ndiye aliyeongoka, na wale ambao amewaacha wapotee basi hao tu ndio waliopata hasara
وَلَقَدۡ ذَرَأۡنَا لِجَهَنَّمَ كَثِيرٗا مِّنَ ٱلۡجِنِّ وَٱلۡإِنسِۖ لَهُمۡ قُلُوبٞ لَّا يَفۡقَهُونَ بِهَا وَلَهُمۡ أَعۡيُنٞ لَّا يُبۡصِرُونَ بِهَا وَلَهُمۡ ءَاذَانٞ لَّا يَسۡمَعُونَ بِهَآۚ أُوْلَـٰٓئِكَ كَٱلۡأَنۡعَٰمِ بَلۡ هُمۡ أَضَلُّۚ أُوْلَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡغَٰفِلُونَ
Na kwa hakika kabisa, tum-eiumbia Jahanamu majini na watu wengi. Wana nyoyo lakini hawafahamu kwa nyoyo hizo, na wana macho lakini hawaoni kwa macho hayo, na wana masikio lakini hawasikii kwa masikio hayo. Hao ni kama wanyama wafugwao, bali wao ni wapotevu zaidi (kuliko mifugo). Hao ndio hasa walioghafilika
وَلِلَّهِ ٱلۡأَسۡمَآءُ ٱلۡحُسۡنَىٰ فَٱدۡعُوهُ بِهَاۖ وَذَرُواْ ٱلَّذِينَ يُلۡحِدُونَ فِيٓ أَسۡمَـٰٓئِهِۦۚ سَيُجۡزَوۡنَ مَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ
Na Allah ana majina mazuri kabisa, basi muombeni kwa majina hayo. Na waacheni wale wanaoya-potosha majina yake; watalipwa yale waliyokuwa wakiyatenda
وَمِمَّنۡ خَلَقۡنَآ أُمَّةٞ يَهۡدُونَ بِٱلۡحَقِّ وَبِهِۦ يَعۡدِلُونَ
Na katika tuliowaumba upo umma unao ongoza kwa kutumia haki na kwa (haki) hiyo wanafanya uadilifu
وَٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَا سَنَسۡتَدۡرِجُهُم مِّنۡ حَيۡثُ لَا يَعۡلَمُونَ
Na wale waliozikadhibisha Aya zetu, tutakwenda nao pole pole kwa namna ambayo (wenyewe) hawaijui
وَأُمۡلِي لَهُمۡۚ إِنَّ كَيۡدِي مَتِينٌ
Na ninawapa muda. Hakika, mkakati wangu ni madhubuti sana
أَوَلَمۡ يَتَفَكَّرُواْۗ مَا بِصَاحِبِهِم مِّن جِنَّةٍۚ إِنۡ هُوَ إِلَّا نَذِيرٞ مُّبِينٌ
Hivi hawatafakari? Huyu mwen-zao (Mtume Muhammad) hana chembe ya wazimu! Hakuwa yeye isipokuwa tu ni Muonyaji dhahiri
أَوَلَمۡ يَنظُرُواْ فِي مَلَكُوتِ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَمَا خَلَقَ ٱللَّهُ مِن شَيۡءٖ وَأَنۡ عَسَىٰٓ أَن يَكُونَ قَدِ ٱقۡتَرَبَ أَجَلُهُمۡۖ فَبِأَيِّ حَدِيثِۭ بَعۡدَهُۥ يُؤۡمِنُونَ
Hivi hawautafakari ufalme (mkubwa) wa mbinguni na ardhini na vitu vyote (vingine) ambavyo Allah ameviumba na kwamba inawezekana kuwa muda wao utakuwa umekaribia? Basi ni mazungumzo gani tena baada ya haya watayaamini?
مَن يُضۡلِلِ ٱللَّهُ فَلَا هَادِيَ لَهُۥۚ وَيَذَرُهُمۡ فِي طُغۡيَٰنِهِمۡ يَعۡمَهُونَ
Wote ambao Allah amewaacha wapotee hakuna wa kuwaongoza, na anawaacha katika upotevu wao wakitangatanga
يَسۡـَٔلُونَكَ عَنِ ٱلسَّاعَةِ أَيَّانَ مُرۡسَىٰهَاۖ قُلۡ إِنَّمَا عِلۡمُهَا عِندَ رَبِّيۖ لَا يُجَلِّيهَا لِوَقۡتِهَآ إِلَّا هُوَۚ ثَقُلَتۡ فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۚ لَا تَأۡتِيكُمۡ إِلَّا بَغۡتَةٗۗ يَسۡـَٔلُونَكَ كَأَنَّكَ حَفِيٌّ عَنۡهَاۖ قُلۡ إِنَّمَا عِلۡمُهَا عِندَ ٱللَّهِ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يَعۡلَمُونَ
Wanakuuliza kuhusu Kiyama; ni lini? Sema: Ilivyo ni kwamba ujuzi wake upo kwa Mola wangu Mlezi. Hakuna wa kuuweka wazi wakati wake isipokuwa yeye tu. Limekuwa jambo zito mno mbinguni na ardhini. Hakitakujieni isipokuwa tu kwa ghafla. Wanakuuliza kuhusu hicho (Kiyama) kama vile wewe umekitafiti (na ukakijua bara bara). Sema (uwaambie): Ujuzi wake uko kwa Allah na lakini watu wengi hawajui
قُل لَّآ أَمۡلِكُ لِنَفۡسِي نَفۡعٗا وَلَا ضَرًّا إِلَّا مَا شَآءَ ٱللَّهُۚ وَلَوۡ كُنتُ أَعۡلَمُ ٱلۡغَيۡبَ لَٱسۡتَكۡثَرۡتُ مِنَ ٱلۡخَيۡرِ وَمَا مَسَّنِيَ ٱلسُّوٓءُۚ إِنۡ أَنَا۠ إِلَّا نَذِيرٞ وَبَشِيرٞ لِّقَوۡمٖ يُؤۡمِنُونَ
Sema: Similiki manufaa wala madhara kuiletea nafsi yangu, isipokuwa tu alitakalo Allah (ndilo linaloweza kunifika; liwe jema au baya). Na lau kama ningekuwa najua Ghaibu (yaliyojificha) ningefanya sana (mambo ya) kheri na lisingenigusa jambo baya (lolote). Mimi sio chochote isipokwa tu ni Muonyaji na Mbashiri (Mtoaji habari njema) kwa watu wanaoamini
۞هُوَ ٱلَّذِي خَلَقَكُم مِّن نَّفۡسٖ وَٰحِدَةٖ وَجَعَلَ مِنۡهَا زَوۡجَهَا لِيَسۡكُنَ إِلَيۡهَاۖ فَلَمَّا تَغَشَّىٰهَا حَمَلَتۡ حَمۡلًا خَفِيفٗا فَمَرَّتۡ بِهِۦۖ فَلَمَّآ أَثۡقَلَت دَّعَوَا ٱللَّهَ رَبَّهُمَا لَئِنۡ ءَاتَيۡتَنَا صَٰلِحٗا لَّنَكُونَنَّ مِنَ ٱلشَّـٰكِرِينَ
Yeye (Allah) Ndiye aliyeku-umbeni kutokana na nafsi moja (Adamu), na akajaalia kutoka katika nafsi hiyo mkewe ili apate utulivu kwake. Na (Adamu) alipomuingilia (mkewe) tu alibeba mimba nyepesi (kwa sababu ndio kwanza ilitunga) na aliweza kutembea nayo. Basi alipopata uzito (wa mimba kwa sababu ilikuwa kubwa) wote wawili (Adamu na mkewe) walimuomba Allah Mola wao Mlezi (na kusema): Kwa yakini kabisa (ewe Mola wetu), kama utatupa (mtoto) mwema bila shaka tutakuwa miongoni mwa wenye kushukuru
فَلَمَّآ ءَاتَىٰهُمَا صَٰلِحٗا جَعَلَا لَهُۥ شُرَكَآءَ فِيمَآ ءَاتَىٰهُمَاۚ فَتَعَٰلَى ٱللَّهُ عَمَّا يُشۡرِكُونَ
Basi (Allah) alipowapa wawili hao (mtoto) mwema, walimfanyia yeye (Allah) washirika katika kile alichowapa.[1] Basi Allah ametakasika na vyote wanavyovishirikisha naye
1- - Wanazuoni wa Kisunna (Ahlus Sunna Wal Jamaa) wanaamini kwamba, Adamu kama Nabii wa Allah hawezi kumfanyia ushirika Allah katika kumuomba na kumuabudu. Neno ushirikishaji ulikousudiwa hapa ni msamiati wa lugha tu na hauna maana ile ya kisheria inayomtoa muumini katika Imani yake.
أَيُشۡرِكُونَ مَا لَا يَخۡلُقُ شَيۡـٔٗا وَهُمۡ يُخۡلَقُونَ
Hivi wanafanya ushirikina (wa kuvishirikisha na Allah na kuvifanya Miungu) visivyokuwa na uwezo wa kuumba chochote, na ilhali Miungu hao (wanaoshirikishwa ndio) wanaumbwa?
وَلَا يَسۡتَطِيعُونَ لَهُمۡ نَصۡرٗا وَلَآ أَنفُسَهُمۡ يَنصُرُونَ
Na hawana uwezo wa kuwanusuru wao, wala wao wenyewe hawawezi kujinusuru
وَإِن تَدۡعُوهُمۡ إِلَى ٱلۡهُدَىٰ لَا يَتَّبِعُوكُمۡۚ سَوَآءٌ عَلَيۡكُمۡ أَدَعَوۡتُمُوهُمۡ أَمۡ أَنتُمۡ صَٰمِتُونَ
Na mkiwaita wafuate muongozo (wa Allah) hawakufuateni. Ni sawa kwenu; mmewaita au mmekaa kimya
إِنَّ ٱلَّذِينَ تَدۡعُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ عِبَادٌ أَمۡثَالُكُمۡۖ فَٱدۡعُوهُمۡ فَلۡيَسۡتَجِيبُواْ لَكُمۡ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ
Hakika, wale mnaowaomba (na kuwaabudu) badala ya Allah ni waja mfano wenu (ni waja kama nyinyi). Basi waombeni wakuitikieni, ikiwa nyinyi ni wakweli
أَلَهُمۡ أَرۡجُلٞ يَمۡشُونَ بِهَآۖ أَمۡ لَهُمۡ أَيۡدٖ يَبۡطِشُونَ بِهَآۖ أَمۡ لَهُمۡ أَعۡيُنٞ يُبۡصِرُونَ بِهَآۖ أَمۡ لَهُمۡ ءَاذَانٞ يَسۡمَعُونَ بِهَاۗ قُلِ ٱدۡعُواْ شُرَكَآءَكُمۡ ثُمَّ كِيدُونِ فَلَا تُنظِرُونِ
Hivi wana miguu wanayotembelea? au wana mikono wanayokamatia? au wana macho wanayo onea? au wana masikio wanayosikilizia? Sema (uwaambie): Waiteni hao washirika wenu kisha nifanyieni vitimbi vyenu wala msinicheleweshe
إِنَّ وَلِـِّۧيَ ٱللَّهُ ٱلَّذِي نَزَّلَ ٱلۡكِتَٰبَۖ وَهُوَ يَتَوَلَّى ٱلصَّـٰلِحِينَ
Hakika, mlinzi wangu ni Allah ambaye ameteremsha kitabu (Qur’ani), naye ndiye anawalinda waja wema
وَٱلَّذِينَ تَدۡعُونَ مِن دُونِهِۦ لَا يَسۡتَطِيعُونَ نَصۡرَكُمۡ وَلَآ أَنفُسَهُمۡ يَنصُرُونَ
Na wale mnaowaomba badala yake hawawezi kukunusuruni wala wao wenyewe hawawezi kujinusuru
وَإِن تَدۡعُوهُمۡ إِلَى ٱلۡهُدَىٰ لَا يَسۡمَعُواْۖ وَتَرَىٰهُمۡ يَنظُرُونَ إِلَيۡكَ وَهُمۡ لَا يُبۡصِرُونَ
Na kama mtawaita wafuate muongozo (wa Allah) hawasikii, na utawaona wanakukodolea macho na ilhali hawaoni
خُذِ ٱلۡعَفۡوَ وَأۡمُرۡ بِٱلۡعُرۡفِ وَأَعۡرِضۡ عَنِ ٱلۡجَٰهِلِينَ
Samehe na amrisha mema, na wapuuze wajinga
وَإِمَّا يَنزَغَنَّكَ مِنَ ٱلشَّيۡطَٰنِ نَزۡغٞ فَٱسۡتَعِذۡ بِٱللَّهِۚ إِنَّهُۥ سَمِيعٌ عَلِيمٌ
Na iwapo utahisi ushawishi wowote wa shetani basi omba kinga kwa Allah. Hakika, yeye (Allah) ni Msikivu sana, Mjuzi mno