لَآ أُقۡسِمُ بِهَٰذَا ٱلۡبَلَدِ
Naapa kwa Mji huu!
Compartir :
وَأَنتَ حِلُّۢ بِهَٰذَا ٱلۡبَلَدِ
Nawe unakaa Mji huu
وَوَالِدٖ وَمَا وَلَدَ
Na naapa kwa mzazi na alicho kizaa
لَقَدۡ خَلَقۡنَا ٱلۡإِنسَٰنَ فِي كَبَدٍ
Hakika tumemuumba mtu katika taabu
أَيَحۡسَبُ أَن لَّن يَقۡدِرَ عَلَيۡهِ أَحَدٞ
Ati anadhani hapana yeyote atakaye muweza?
يَقُولُ أَهۡلَكۡتُ مَالٗا لُّبَدًا
Anasema: Nimeteketeza mali chungu nzima
أَيَحۡسَبُ أَن لَّمۡ يَرَهُۥٓ أَحَدٌ
Ati anadhani ya kuwa hapana yeyote anaye mwona?
أَلَمۡ نَجۡعَل لَّهُۥ عَيۡنَيۡنِ
Kwani hatukumpa macho mawili?
وَلِسَانٗا وَشَفَتَيۡنِ
Na ulimi, na midomo miwili?
وَهَدَيۡنَٰهُ ٱلنَّجۡدَيۡنِ
Na tukambainishia njia zote mbili?
فَلَا ٱقۡتَحَمَ ٱلۡعَقَبَةَ
Lakini hakujitoma (hakuingia) kwenye njia ya vikwazo vya milimani
وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا ٱلۡعَقَبَةُ
Na nini kitakujulisha ni nini njia ya vikwazo vya milimani?
فَكُّ رَقَبَةٍ
Kumkomboa mtumwa;
أَوۡ إِطۡعَٰمٞ فِي يَوۡمٖ ذِي مَسۡغَبَةٖ
Au kumlisha siku ya njaa
يَتِيمٗا ذَا مَقۡرَبَةٍ
Yatima aliye katika jamaa wa karibu (ndugu)
أَوۡ مِسۡكِينٗا ذَا مَتۡرَبَةٖ
Au masikini aliye vumbini
ثُمَّ كَانَ مِنَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَتَوَاصَوۡاْ بِٱلصَّبۡرِ وَتَوَاصَوۡاْ بِٱلۡمَرۡحَمَةِ
Tena awe miongoni mwa walio amini na wakausiana kusubiri na wakausiana kuhurumiana
أُوْلَـٰٓئِكَ أَصۡحَٰبُ ٱلۡمَيۡمَنَةِ
Hao ndio watu wa kheri wa kuliani
وَٱلَّذِينَ كَفَرُواْ بِـَٔايَٰتِنَا هُمۡ أَصۡحَٰبُ ٱلۡمَشۡـَٔمَةِ
Lakini walio zikataa Ishara zetu, hao ndio watu wa shari wa kushotoni
عَلَيۡهِمۡ نَارٞ مُّؤۡصَدَةُۢ
Juu yao utakuwa Moto ulio fungiwa kila upande