لَّا ظَلِيلٖ وَلَا يُغۡنِي مِنَ ٱللَّهَبِ
Hakiwafuniki, na wala hakiwa-kingi na muwako wa moto
Compartir :
إِنَّهَا تَرۡمِي بِشَرَرٖ كَٱلۡقَصۡرِ
Hakika Moto huo hurusha macheche Kama majumba!
كَأَنَّهُۥ جِمَٰلَتٞ صُفۡرٞ
Kana kwamba ni ngamia waku-bwa wa rangi ya manjano!
وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ
Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
هَٰذَا يَوۡمُ لَا يَنطِقُونَ
Hii ni siku ambayo hawatatamka kitu,
وَلَا يُؤۡذَنُ لَهُمۡ فَيَعۡتَذِرُونَ
Wala hawataruhusiwa kutoa udhuru
هَٰذَا يَوۡمُ ٱلۡفَصۡلِۖ جَمَعۡنَٰكُمۡ وَٱلۡأَوَّلِينَ
Hii ndiyo siku ya kupambanua. Tumekukusanyeni nyinyi na walio tangulia
فَإِن كَانَ لَكُمۡ كَيۡدٞ فَكِيدُونِ
Ikiwa mnayo hila yoyote ile basi Nifanyieni mimi
إِنَّ ٱلۡمُتَّقِينَ فِي ظِلَٰلٖ وَعُيُونٖ
Hakika wacha Mungu watakuwa katika vivuli na chemchem
وَفَوَٰكِهَ مِمَّا يَشۡتَهُونَ
Na matunda katika yale wanayoyatamani
كُلُواْ وَٱشۡرَبُواْ هَنِيٓـَٔۢا بِمَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ
(Wataabiwa): Kuleni na kunyweni kwa furaha kwasababu ya yale mliyokuwa mkiyatenda
إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجۡزِي ٱلۡمُحۡسِنِينَ
Hakika sisi ndio kama hivyo tunavyo walipa watendao mema
كُلُواْ وَتَمَتَّعُواْ قَلِيلًا إِنَّكُم مُّجۡرِمُونَ
Kuleni na mjifurahishe kidogo tu. Hakika nyinyi ni wakosefu!
وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ ٱرۡكَعُواْ لَا يَرۡكَعُونَ
Na walipokuwa wakiambiwa Rukuuni (mswali), hawakuwa wakirukuu
فَبِأَيِّ حَدِيثِۭ بَعۡدَهُۥ يُؤۡمِنُونَ
Basi maneno gani baada ya hii (Qurani) watayaamini?