Capítulo: AL-IMRAN 

Verso : 1

الٓمٓ

Alif Laam Miim[1]


1- - Allah ndiye ajuwaye zaidi madhumuni ya herufi hizi.


Capítulo: AL-IMRAN 

Verso : 2

ٱللَّهُ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ ٱلۡحَيُّ ٱلۡقَيُّومُ

Allah, hakuna Mwenye haki ya kuabudiwa isipokuwa Yeye tu, Mwenye uhai wa milele, Mwenye kusimamia mambo yote



Capítulo: AL-IMRAN 

Verso : 3

نَزَّلَ عَلَيۡكَ ٱلۡكِتَٰبَ بِٱلۡحَقِّ مُصَدِّقٗا لِّمَا بَيۡنَ يَدَيۡهِ وَأَنزَلَ ٱلتَّوۡرَىٰةَ وَٱلۡإِنجِيلَ

Amekuteremshia Kitabu kwa haki kikisadikisha yaliyokuwepo kabla yake. Na ameteremshaTaurati na Injili



Capítulo: AL-IMRAN 

Verso : 4

مِن قَبۡلُ هُدٗى لِّلنَّاسِ وَأَنزَلَ ٱلۡفُرۡقَانَۗ إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ لَهُمۡ عَذَابٞ شَدِيدٞۗ وَٱللَّهُ عَزِيزٞ ذُو ٱنتِقَامٍ

(Ameteremsha Taurati na Injili) Kabla (ya Kurani) ili (vitabu vyote hivyo) viwe muongozo kwa watu. Na ameteremsha Alfurqan. Hakika, wale waliokanusha Aya za Allah watapata adhabu kali, na Allah ni Mwenye nguvu kubwa, Mwenye kutesa



Capítulo: AL-IMRAN 

Verso : 5

إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَخۡفَىٰ عَلَيۡهِ شَيۡءٞ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَلَا فِي ٱلسَّمَآءِ

Kwa hakika, Allah hakijifichi kwake chochote; sio ardhini wala mbinguni



Capítulo: AL-IMRAN 

Verso : 6

هُوَ ٱلَّذِي يُصَوِّرُكُمۡ فِي ٱلۡأَرۡحَامِ كَيۡفَ يَشَآءُۚ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡحَكِيمُ

Yeye ndiye anayekutieni maumbo mkiwa katika mifuko ya uzazi kwa namna apendavyo. Hakuna aliye na haki ya kuabudiwa isipokuwa yeye tu, Mwenye nguvu kubwa, Mwingi wa hekima



Capítulo: AL-IMRAN 

Verso : 7

هُوَ ٱلَّذِيٓ أَنزَلَ عَلَيۡكَ ٱلۡكِتَٰبَ مِنۡهُ ءَايَٰتٞ مُّحۡكَمَٰتٌ هُنَّ أُمُّ ٱلۡكِتَٰبِ وَأُخَرُ مُتَشَٰبِهَٰتٞۖ فَأَمَّا ٱلَّذِينَ فِي قُلُوبِهِمۡ زَيۡغٞ فَيَتَّبِعُونَ مَا تَشَٰبَهَ مِنۡهُ ٱبۡتِغَآءَ ٱلۡفِتۡنَةِ وَٱبۡتِغَآءَ تَأۡوِيلِهِۦۖ وَمَا يَعۡلَمُ تَأۡوِيلَهُۥٓ إِلَّا ٱللَّهُۗ وَٱلرَّـٰسِخُونَ فِي ٱلۡعِلۡمِ يَقُولُونَ ءَامَنَّا بِهِۦ كُلّٞ مِّنۡ عِندِ رَبِّنَاۗ وَمَا يَذَّكَّرُ إِلَّآ أُوْلُواْ ٱلۡأَلۡبَٰبِ

Yeye ndiye aliyekuteremshia Kitabu. Baadhi ya Aya zake zinafahamika kwa wepesi (na) ambazo ndio msingi wa kitabu (hiki cha Kurani). Na (Aya) nyingine zinatatiza. Ama wale ambao ndani ya nyoyo zao kuna upotevu, wanafuata (Aya) zinazotatiza, kwa kutaka fitina na kutaka kuzipotosha. Na hakuna anayejua tafsiri yake (halisi) isipokuwa Allah tu. Na wale waliobobea katika elimu husema: Tumeziamini (Aya) zote. Zote (hizo) zinatoka kwa Mola wetu Mlezi. Na hawawaidhiki isipokuwa wenye akili tu



Capítulo: AL-IMRAN 

Verso : 8

رَبَّنَا لَا تُزِغۡ قُلُوبَنَا بَعۡدَ إِذۡ هَدَيۡتَنَا وَهَبۡ لَنَا مِن لَّدُنكَ رَحۡمَةًۚ إِنَّكَ أَنتَ ٱلۡوَهَّابُ

Ewe Mola wetu, usiziache nyoyo zetu zipotee baada ya kuwa umetuongoza, na tunaomba rehema kwako. Hakika, wewe ni Mtoaji sana



Capítulo: AL-IMRAN 

Verso : 9

رَبَّنَآ إِنَّكَ جَامِعُ ٱلنَّاسِ لِيَوۡمٖ لَّا رَيۡبَ فِيهِۚ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُخۡلِفُ ٱلۡمِيعَادَ

Ewe Mola wetu, hakika wewe ni mwenye kuwakusanya watu katika siku isiyokuwa na shaka. Hakika, Allah havunji ahadi



Capítulo: AL-IMRAN 

Verso : 10

إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ لَن تُغۡنِيَ عَنۡهُمۡ أَمۡوَٰلُهُمۡ وَلَآ أَوۡلَٰدُهُم مِّنَ ٱللَّهِ شَيۡـٔٗاۖ وَأُوْلَـٰٓئِكَ هُمۡ وَقُودُ ٱلنَّارِ

Hakika, waliokufuru, katu hazitawasaidia chochote mali zao wala watoto wao kwa Allah, na hao ndio kuniza Motoni



Capítulo: AL-IMRAN 

Verso : 11

كَدَأۡبِ ءَالِ فِرۡعَوۡنَ وَٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡۚ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَا فَأَخَذَهُمُ ٱللَّهُ بِذُنُوبِهِمۡۗ وَٱللَّهُ شَدِيدُ ٱلۡعِقَابِ

Sawa na mwenendo wa watu wa Firauni na wale waliokuwepo kabla yao; walizipinga Aya zetu, basi Allah akawaadhibu kwa sababu ya madhambi yao na Allah ni Mkali sana wa kuadhibu



Capítulo: AL-IMRAN 

Verso : 12

قُل لِّلَّذِينَ كَفَرُواْ سَتُغۡلَبُونَ وَتُحۡشَرُونَ إِلَىٰ جَهَنَّمَۖ وَبِئۡسَ ٱلۡمِهَادُ

Waambie waliokufuru kwamba: Mtashindwa na mtakusanywa mpelekwe Jahanamu, na hayo ni makazi mabaya sana



Capítulo: AL-IMRAN 

Verso : 13

قَدۡ كَانَ لَكُمۡ ءَايَةٞ فِي فِئَتَيۡنِ ٱلۡتَقَتَاۖ فِئَةٞ تُقَٰتِلُ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ وَأُخۡرَىٰ كَافِرَةٞ يَرَوۡنَهُم مِّثۡلَيۡهِمۡ رَأۡيَ ٱلۡعَيۡنِۚ وَٱللَّهُ يُؤَيِّدُ بِنَصۡرِهِۦ مَن يَشَآءُۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَعِبۡرَةٗ لِّأُوْلِي ٱلۡأَبۡصَٰرِ

Hakika, ilikuwepo kwenu alama katika makundi mawili yaliyokutana (katika vita). Kundi moja likipigana katika njia ya Allah, na jingine la makafiri wanawaona (Waislamu) kwa mtazamo wa macho mara mbili yao. Na Allah anamtia nguvu amtakaye kwa (kumpa) ushindi wake. Hakika, katika hilo kuna mazingatio kwa wenye kuona mbali



Capítulo: AL-IMRAN 

Verso : 14

زُيِّنَ لِلنَّاسِ حُبُّ ٱلشَّهَوَٰتِ مِنَ ٱلنِّسَآءِ وَٱلۡبَنِينَ وَٱلۡقَنَٰطِيرِ ٱلۡمُقَنطَرَةِ مِنَ ٱلذَّهَبِ وَٱلۡفِضَّةِ وَٱلۡخَيۡلِ ٱلۡمُسَوَّمَةِ وَٱلۡأَنۡعَٰمِ وَٱلۡحَرۡثِۗ ذَٰلِكَ مَتَٰعُ ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَاۖ وَٱللَّهُ عِندَهُۥ حُسۡنُ ٱلۡمَـَٔابِ

Watu wamepambiwa kupenda kutamani wanawake na watoto wanaume na marundo mengi ya dhahabu na fedha na farasi wanaofunzwa na wanyama wafugwao na mashamba. Hizo ni starehe za maisha ya duniani, na mafikio mazuri yapo kwa Allah tu



Capítulo: AL-IMRAN 

Verso : 15

۞قُلۡ أَؤُنَبِّئُكُم بِخَيۡرٖ مِّن ذَٰلِكُمۡۖ لِلَّذِينَ ٱتَّقَوۡاْ عِندَ رَبِّهِمۡ جَنَّـٰتٞ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ خَٰلِدِينَ فِيهَا وَأَزۡوَٰجٞ مُّطَهَّرَةٞ وَرِضۡوَٰنٞ مِّنَ ٱللَّهِۗ وَٱللَّهُ بَصِيرُۢ بِٱلۡعِبَادِ

Sema: Je, nikupeni habari ya vilivyo bora zaidi kuliko hivyo? Wenye ucha Mungu tu watapata kwa Mola wao bustani zipitazo mito chini yake, watakaa humo milele na (pia watapata) wake waliotakaswa na radhi za Allah, na Allah ni Mwenye kuwaona sana waja



Capítulo: AL-IMRAN 

Verso : 16

ٱلَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَآ إِنَّنَآ ءَامَنَّا فَٱغۡفِرۡ لَنَا ذُنُوبَنَا وَقِنَا عَذَابَ ٱلنَّارِ

Ambao wanasema: Ewe Mola wetu, hakika sisi tumeamini, hivyo tusamehe dhambi zetu na tukinge na adhabu ya Moto



Capítulo: AL-IMRAN 

Verso : 17

ٱلصَّـٰبِرِينَ وَٱلصَّـٰدِقِينَ وَٱلۡقَٰنِتِينَ وَٱلۡمُنفِقِينَ وَٱلۡمُسۡتَغۡفِرِينَ بِٱلۡأَسۡحَارِ

Na wafanyao subira na wasemao kweli na wanaotii na wanaotoa (walivyojaaliwa na kuwapa wengine) na wanaoomba msamaha usiku wa manane



Capítulo: AL-IMRAN 

Verso : 18

شَهِدَ ٱللَّهُ أَنَّهُۥ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ وَٱلۡمَلَـٰٓئِكَةُ وَأُوْلُواْ ٱلۡعِلۡمِ قَآئِمَۢا بِٱلۡقِسۡطِۚ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡحَكِيمُ

Allah Ameshuhudia kwamba, hakuna mwenye haki ya kuabudiwa isipokuwa yeye tu, na Malaika (pia wameshudia hivyo) na wenye elimu, akisimamia uadilifu. Hakuna mwenye haki ya kuabudiwa isipokuwa yeye tu, Mwenye nguvu kubwa, Mwenye hekima nyingi



Capítulo: AL-IMRAN 

Verso : 19

إِنَّ ٱلدِّينَ عِندَ ٱللَّهِ ٱلۡإِسۡلَٰمُۗ وَمَا ٱخۡتَلَفَ ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡكِتَٰبَ إِلَّا مِنۢ بَعۡدِ مَا جَآءَهُمُ ٱلۡعِلۡمُ بَغۡيَۢا بَيۡنَهُمۡۗ وَمَن يَكۡفُرۡ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ فَإِنَّ ٱللَّهَ سَرِيعُ ٱلۡحِسَابِ

Hakika, dini (inayokubalika) kwa Allah ni Uislamu tu. Na wale waliopewa Kitabu hawakutofautiana isipokuwa tu baada ya kuwa elimu imewafikia kwa sababu ya uovu uliokuwepo kati yao. Na yeyote anayezikataa Aya za Allah, basi hakika Allah ni Mwepesi mno wa kuhesabu



Capítulo: AL-IMRAN 

Verso : 20

فَإِنۡ حَآجُّوكَ فَقُلۡ أَسۡلَمۡتُ وَجۡهِيَ لِلَّهِ وَمَنِ ٱتَّبَعَنِۗ وَقُل لِّلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡكِتَٰبَ وَٱلۡأُمِّيِّـۧنَ ءَأَسۡلَمۡتُمۡۚ فَإِنۡ أَسۡلَمُواْ فَقَدِ ٱهۡتَدَواْۖ وَّإِن تَوَلَّوۡاْ فَإِنَّمَا عَلَيۡكَ ٱلۡبَلَٰغُۗ وَٱللَّهُ بَصِيرُۢ بِٱلۡعِبَادِ

Na kama watakuletea hoja (yoyote), basi sema: Nimeukabidhi uso wangu (nimejisalimisha) kwa Allah; mimi na wale walionifuata. Na waambie waliopewa kitabu na wasio na elimu kwamba: Je, mmesilimu (Mmejisalimisha kwa Allah)? Kama wamesilimu basi hakika wameongoka, na kama wakikataa, basi wajibu wako ni kufikisha tu. Na Allah anawaona mno waja



Capítulo: AL-IMRAN 

Verso : 21

إِنَّ ٱلَّذِينَ يَكۡفُرُونَ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ وَيَقۡتُلُونَ ٱلنَّبِيِّـۧنَ بِغَيۡرِ حَقّٖ وَيَقۡتُلُونَ ٱلَّذِينَ يَأۡمُرُونَ بِٱلۡقِسۡطِ مِنَ ٱلنَّاسِ فَبَشِّرۡهُم بِعَذَابٍ أَلِيمٍ

Hakika, wanaozikataa Aya za Allah na wanaua Mitume bila ya hakina (pia wanaua) watu ambao wanaamrisha uadilifu, wape habari njema[1] ya adhabu iumizayo sana


1- - “…wape habari njema ya adhabu iumizayo sana”. Hapa Kurani imetumia muundo wa fasihi ya lugha ya
Kiarabu unaoitwa “Muundo wa Kudhihaki”. Kumuahidi mtu kuwa utamuadhibu si habari njema na ya
kumfurahisha. Lakini kurani inasema “…wape habari njema ya adhabu iumizayo sana”. Ni aina fulani tu
ya kuwakebehi makafiri na kuwadhihaki. Muundo huu umetumika katika maeneo mengi ya Kurani
ikiwemo Aya ya 49 ya Sura Addukhaan (44) ambapo kafiri wakati atakapoadhibiwa motoni ataambiwa:
“… Onja (adhabu, kwa sababu) wewe ndiye hasa mwenye ukubwa, mheshimiwa! ”Vipi tena mheshimiwa
anaadhibiwa? Huku ni kumdhihaki tu!


Capítulo: AL-IMRAN 

Verso : 22

أُوْلَـٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ حَبِطَتۡ أَعۡمَٰلُهُمۡ فِي ٱلدُّنۡيَا وَٱلۡأٓخِرَةِ وَمَا لَهُم مِّن نَّـٰصِرِينَ

Hao ndio ambao amali zao zimepomoka (zimepotea bure) duniani na Akhera na hawana yeyote wa kuwanusuru”



Capítulo: AL-IMRAN 

Verso : 23

أَلَمۡ تَرَ إِلَى ٱلَّذِينَ أُوتُواْ نَصِيبٗا مِّنَ ٱلۡكِتَٰبِ يُدۡعَوۡنَ إِلَىٰ كِتَٰبِ ٱللَّهِ لِيَحۡكُمَ بَيۡنَهُمۡ ثُمَّ يَتَوَلَّىٰ فَرِيقٞ مِّنۡهُمۡ وَهُم مُّعۡرِضُونَ

Hivi hukuwaona ambao wamepewa sehemu ya kitabu; wanaitwa kukiendea kitabu cha Allah ili kihukumu baina yao, kisha kundi miongoni mwao linakengeuka na wao wakipuuza?



Capítulo: AL-IMRAN 

Verso : 24

ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمۡ قَالُواْ لَن تَمَسَّنَا ٱلنَّارُ إِلَّآ أَيَّامٗا مَّعۡدُودَٰتٖۖ وَغَرَّهُمۡ فِي دِينِهِم مَّا كَانُواْ يَفۡتَرُونَ

Hiyo ni kwa sababu walisema: Moto (wa Jahanamu) hautatugusa[1] isipokuwa kwa siku chache tu, na yaliwadanganya katika dini yao yale waliyokuwa wakiyazua


1- - Hautatuunguza


Capítulo: AL-IMRAN 

Verso : 25

فَكَيۡفَ إِذَا جَمَعۡنَٰهُمۡ لِيَوۡمٖ لَّا رَيۡبَ فِيهِ وَوُفِّيَتۡ كُلُّ نَفۡسٖ مَّا كَسَبَتۡ وَهُمۡ لَا يُظۡلَمُونَ

Basi itakuwaje tutakapo-wakusanya kwa ajili ya siku ambayo haina shaka, na kila nafsi italipwa kwa ukamilifu kutokana na ilichokichuma na wao hawatadhulumiwa?



Capítulo: AL-IMRAN 

Verso : 26

قُلِ ٱللَّهُمَّ مَٰلِكَ ٱلۡمُلۡكِ تُؤۡتِي ٱلۡمُلۡكَ مَن تَشَآءُ وَتَنزِعُ ٱلۡمُلۡكَ مِمَّن تَشَآءُ وَتُعِزُّ مَن تَشَآءُ وَتُذِلُّ مَن تَشَآءُۖ بِيَدِكَ ٱلۡخَيۡرُۖ إِنَّكَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٞ

Sema: Ewe Mola wangu, Mmiliki wa ufalme, unampa ufalme umtakaye, na unamuondolea ufalme umtakaye, na unamtukuza umtakaye, na unamfanya dhalili umtakaye. Kheri zote zipo mkononi mwako tu. Hakika, wewe ni Muweza sana wa kila kitu



Capítulo: AL-IMRAN 

Verso : 27

تُولِجُ ٱلَّيۡلَ فِي ٱلنَّهَارِ وَتُولِجُ ٱلنَّهَارَ فِي ٱلَّيۡلِۖ وَتُخۡرِجُ ٱلۡحَيَّ مِنَ ٱلۡمَيِّتِ وَتُخۡرِجُ ٱلۡمَيِّتَ مِنَ ٱلۡحَيِّۖ وَتَرۡزُقُ مَن تَشَآءُ بِغَيۡرِ حِسَابٖ

Unauingiza usiku ndani ya mchana[1], na unauingiza mchana ndani ya usiku, na unatoa (kiumbe) hai kutoka katika (kiumbe) mfu, na unatoa (kiumbe) mfu kutoka katika (kiumbe) hai. Na unampa riziki umtakaye bila ya hesabu


1- - Allah anauingiza usiku katika mchana na unakuwa mrefu katika kipindi fulani na pia anauingiza mchana
katika usiku na unakuwa mrefu katika kipindi kingine. Allah anaelezea uweza wake mkubwa unaotoa
kiumbe hai kutoka katika kinachoonekana kama kiumbe mfu, na anatoa kiumbe mfu katika kiumbe hai!
Hapa Allah anelezea uwezo wake mkubwa katika kinachoitwa “Mfuatano na muendelezo wa maisha ya
viumbe hai”.


Capítulo: AL-IMRAN 

Verso : 28

لَّا يَتَّخِذِ ٱلۡمُؤۡمِنُونَ ٱلۡكَٰفِرِينَ أَوۡلِيَآءَ مِن دُونِ ٱلۡمُؤۡمِنِينَۖ وَمَن يَفۡعَلۡ ذَٰلِكَ فَلَيۡسَ مِنَ ٱللَّهِ فِي شَيۡءٍ إِلَّآ أَن تَتَّقُواْ مِنۡهُمۡ تُقَىٰةٗۗ وَيُحَذِّرُكُمُ ٱللَّهُ نَفۡسَهُۥۗ وَإِلَى ٱللَّهِ ٱلۡمَصِيرُ

Waumini wasiwafanye makafiri kuwa vipenzi vyao badala ya Waumini (wenzao). Na atakayefanya hilo, basi hana chochote mbele ya Allah, isipokuwa kwa kujikinga dhidi ya shari zao. Na Allah anakutahadharisheni nafsi yake. Na kwa Allah tu ndio marejeo



Capítulo: AL-IMRAN 

Verso : 29

قُلۡ إِن تُخۡفُواْ مَا فِي صُدُورِكُمۡ أَوۡ تُبۡدُوهُ يَعۡلَمۡهُ ٱللَّهُۗ وَيَعۡلَمُ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِۗ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٞ

Sema: Mkiyaficha yaliyomo vifuani mwenu au mkiyadhihirisha Allah anayajua, na anayajua yaliyomo mbinguni na yaliyomo ardhini, na Allah ni Mwenye uweza mkubwa wa kila kitu



Capítulo: AL-IMRAN 

Verso : 30

يَوۡمَ تَجِدُ كُلُّ نَفۡسٖ مَّا عَمِلَتۡ مِنۡ خَيۡرٖ مُّحۡضَرٗا وَمَا عَمِلَتۡ مِن سُوٓءٖ تَوَدُّ لَوۡ أَنَّ بَيۡنَهَا وَبَيۡنَهُۥٓ أَمَدَۢا بَعِيدٗاۗ وَيُحَذِّرُكُمُ ٱللَّهُ نَفۡسَهُۥۗ وَٱللَّهُ رَءُوفُۢ بِٱلۡعِبَادِ

Siku ambayo kila nafsi itakuta kheri iliyoitenda ikiwa imehudhurishwa, na pia ubaya iliyoutenda. Itapenda lau kungekuwepo masafa marefu kati yake na ubaya huo. Na Allah anakutahadharisheni nafsi yake. Na Allah ni Mpole mno kwa waja (wake)