ٱلَّذِينَ ءَاتَيۡنَٰهُمُ ٱلۡكِتَٰبَ يَتۡلُونَهُۥ حَقَّ تِلَاوَتِهِۦٓ أُوْلَـٰٓئِكَ يُؤۡمِنُونَ بِهِۦۗ وَمَن يَكۡفُرۡ بِهِۦ فَأُوْلَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡخَٰسِرُونَ
Wale ambao tumewapa kitabu (wakawa) wanakisoma ipasavyo, basi hao ndio wanaokiamini, na wale watakaokipinga basi hao ndio wenye kupata hasara
۞لَيۡسُواْ سَوَآءٗۗ مِّنۡ أَهۡلِ ٱلۡكِتَٰبِ أُمَّةٞ قَآئِمَةٞ يَتۡلُونَ ءَايَٰتِ ٱللَّهِ ءَانَآءَ ٱلَّيۡلِ وَهُمۡ يَسۡجُدُونَ
Watu wa Kitabu hawalingani (katika uovu). Miongoni mwa Watu wa Kitabu lipo kundi lililosimama imara (katika haki) wanasoma Aya za Allah nyakati za usiku na wanasujudu
أَفَلَا يَتَدَبَّرُونَ ٱلۡقُرۡءَانَۚ وَلَوۡ كَانَ مِنۡ عِندِ غَيۡرِ ٱللَّهِ لَوَجَدُواْ فِيهِ ٱخۡتِلَٰفٗا كَثِيرٗا
Hivi hawaizingatii hii Kurani? Na lau kama ingetoka kwa asiyekuwa Allah bila shaka wangekuta ndani yake kasoro nyingi
وَإِذَا قُرِئَ ٱلۡقُرۡءَانُ فَٱسۡتَمِعُواْ لَهُۥ وَأَنصِتُواْ لَعَلَّكُمۡ تُرۡحَمُونَ
Na wakati inasomwa Qur’ani isikilizeni na nyamazeni ili mpate kupewa rehema[1]
1- - Aya hii ina mafunzo makubwa kwa Muislamu. 1) Kuiheshimu Qur’ani kwa kuisikiliza na kukaa kimya. 2) Muislamu anapata rehema kwa kutekeleza agizo la kusikiliza na kukaa kimya. 3) Kama kusikiliza tu na kukaa kimya Muislamu anapata rehema, hii inaonesha kwamba kuifanyia kazi Qur’ani na kutekeleza mafunzo yake kuna rehema zaidi. 4) Ni muhimu kwa Muislamu kuangalia mazingira ya kusoma Qur’ani. Kwa muktadha huu, si jambo jema na ni makuruhu kusoma Qur’ani au kuweka sauti ya Qu’ani katika mazingira ambayo sio rafiki kama kwenye mikusanyiko ya sokoni, dukani, ndani ya vyombo vya usafiri n.k.
فَإِذَا قَرَأۡتَ ٱلۡقُرۡءَانَ فَٱسۡتَعِذۡ بِٱللَّهِ مِنَ ٱلشَّيۡطَٰنِ ٱلرَّجِيمِ
Na pindi unapotaka kusoma Qur’ani, basi jikinge kwa Allah (akulinde) na shetani aliyelaaniwa
وَٱتۡلُ مَآ أُوحِيَ إِلَيۡكَ مِن كِتَابِ رَبِّكَۖ لَا مُبَدِّلَ لِكَلِمَٰتِهِۦ وَلَن تَجِدَ مِن دُونِهِۦ مُلۡتَحَدٗا
Na soma uliyo funuliwa katika Kitabu cha Mola wako Mlezi. Hapana wa kubadilisha maneno yake. Wala nawe hutapata makimbilio isipo kuwa kwake
وَقَالَ ٱلرَّسُولُ يَٰرَبِّ إِنَّ قَوۡمِي ٱتَّخَذُواْ هَٰذَا ٱلۡقُرۡءَانَ مَهۡجُورٗا
Na Mtume alikuwa akisema: Ee Mola wangu Mlezi! Hakika watu wangu wameifanya hii Qur’ani ni yenye kuhamwa
وَأَنۡ أَتۡلُوَاْ ٱلۡقُرۡءَانَۖ فَمَنِ ٱهۡتَدَىٰ فَإِنَّمَا يَهۡتَدِي لِنَفۡسِهِۦۖ وَمَن ضَلَّ فَقُلۡ إِنَّمَآ أَنَا۠ مِنَ ٱلۡمُنذِرِينَ
Na niisome Qur’ani. Na mwenye kuongoka, basi ameongoka kwa faida ya nafsi yake; na aliyepotea - basi sema: Hakika mimi ni miongoni mwa waonyaji
ٱتۡلُ مَآ أُوحِيَ إِلَيۡكَ مِنَ ٱلۡكِتَٰبِ وَأَقِمِ ٱلصَّلَوٰةَۖ إِنَّ ٱلصَّلَوٰةَ تَنۡهَىٰ عَنِ ٱلۡفَحۡشَآءِ وَٱلۡمُنكَرِۗ وَلَذِكۡرُ ٱللَّهِ أَكۡبَرُۗ وَٱللَّهُ يَعۡلَمُ مَا تَصۡنَعُونَ
Soma uliyo funuliwa katika Kitabu, na ushike Sala. Hakika Sala inazuilia mambo machafu na maovu. Na kwa yakini kumtaja Allah ndilo jambo kubwa kabisa. Na Allah anayajua mnayo yatenda
وَٱذۡكُرۡنَ مَا يُتۡلَىٰ فِي بُيُوتِكُنَّ مِنۡ ءَايَٰتِ ٱللَّهِ وَٱلۡحِكۡمَةِۚ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ لَطِيفًا خَبِيرًا
Na kumbukeni yasomwayo majumbani mwenu katika Aya za Allah na hekima. Kwa hakika Allah ni Mjuzi wa mambo ya siri, na Mwenye khabari
إِنَّ ٱلَّذِينَ يَتۡلُونَ كِتَٰبَ ٱللَّهِ وَأَقَامُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَأَنفَقُواْ مِمَّا رَزَقۡنَٰهُمۡ سِرّٗا وَعَلَانِيَةٗ يَرۡجُونَ تِجَٰرَةٗ لَّن تَبُورَ
Hakika wale wanao soma Kitabu cha Allah, na wakashika Sala, na wakatoa kwa siri na kwa dhaahiri katika tulivyo waruzuku, hao hutaraji biashara isiyo bwaga. (isiyokatika)
كِتَٰبٌ أَنزَلۡنَٰهُ إِلَيۡكَ مُبَٰرَكٞ لِّيَدَّبَّرُوٓاْ ءَايَٰتِهِۦ وَلِيَتَذَكَّرَ أُوْلُواْ ٱلۡأَلۡبَٰبِ
Na hiki Kitabu, tumekuteremshia wewe, chenye baraka, ili wazizingatie Aya zake, na wawaidhike wenye akili
أَفَلَا يَتَدَبَّرُونَ ٱلۡقُرۡءَانَ أَمۡ عَلَىٰ قُلُوبٍ أَقۡفَالُهَآ
Je! Hawaizingatii hii Qur’ani? Au kwenye nyoyo (zao) zipo kufuli?
أَوۡ زِدۡ عَلَيۡهِ وَرَتِّلِ ٱلۡقُرۡءَانَ تَرۡتِيلًا
Au izidishe, na soma Qurani vizuri (kwa kufuata kanuni, sheria na taratibu zake)
۞إِنَّ رَبَّكَ يَعۡلَمُ أَنَّكَ تَقُومُ أَدۡنَىٰ مِن ثُلُثَيِ ٱلَّيۡلِ وَنِصۡفَهُۥ وَثُلُثَهُۥ وَطَآئِفَةٞ مِّنَ ٱلَّذِينَ مَعَكَۚ وَٱللَّهُ يُقَدِّرُ ٱلَّيۡلَ وَٱلنَّهَارَۚ عَلِمَ أَن لَّن تُحۡصُوهُ فَتَابَ عَلَيۡكُمۡۖ فَٱقۡرَءُواْ مَا تَيَسَّرَ مِنَ ٱلۡقُرۡءَانِۚ عَلِمَ أَن سَيَكُونُ مِنكُم مَّرۡضَىٰ وَءَاخَرُونَ يَضۡرِبُونَ فِي ٱلۡأَرۡضِ يَبۡتَغُونَ مِن فَضۡلِ ٱللَّهِ وَءَاخَرُونَ يُقَٰتِلُونَ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِۖ فَٱقۡرَءُواْ مَا تَيَسَّرَ مِنۡهُۚ وَأَقِيمُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتُواْ ٱلزَّكَوٰةَ وَأَقۡرِضُواْ ٱللَّهَ قَرۡضًا حَسَنٗاۚ وَمَا تُقَدِّمُواْ لِأَنفُسِكُم مِّنۡ خَيۡرٖ تَجِدُوهُ عِندَ ٱللَّهِ هُوَ خَيۡرٗا وَأَعۡظَمَ أَجۡرٗاۚ وَٱسۡتَغۡفِرُواْ ٱللَّهَۖ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمُۢ
Hakika Mola wako anajua ya kuwa hakika wewe unakesha karibu na thuluthi mbili za usiku, na nusu yake, na thuluthi yake. Na baadhi ya watu walio pamoja nawe kadhaalika. Na Allah ndiye anaye ukadiria usiku na mchana. Anajua kuwa hamuwezi kuweka hesabu, basi amekusameheni. Basi someni kilicho chepesi katika Qurani. Anajua ya kuwa baadhi yenu watakuwa wagonjwa, na wengine wanasafiri katika ardhi wakitafuta fadhila za Allah, na wengine wanapigana katika Njia ya Allah. Kwa hivyo someni kilicho chepesi humo, na simamisheni Sala, na toeni Zaka, na mkopesheni Allah mkopo ulio mwema. Na kheri yoyote mnayo itanguliza kwa ajili ya nafsi zenu mtaikuta kwa Allah, nayo imekuwa bora zaidi, na ina thawabu kubwa sana. Na mtakeni msamaha Allah. Hakika Allah ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu
ٱقۡرَأۡ بِٱسۡمِ رَبِّكَ ٱلَّذِي خَلَقَ
Soma kwa jina la Mola wako Mlezi ambaye ameumba
ٱقۡرَأۡ وَرَبُّكَ ٱلۡأَكۡرَمُ
Soma! Na Mola wako Mlezi ni Mkarimu kushinda wote!