ذَٰلِكَ بِأَنَّ ٱللَّهَ نَزَّلَ ٱلۡكِتَٰبَ بِٱلۡحَقِّۗ وَإِنَّ ٱلَّذِينَ ٱخۡتَلَفُواْ فِي ٱلۡكِتَٰبِ لَفِي شِقَاقِۭ بَعِيدٖ
Hayo ni kwa sababu Allah ameteremsha kitabu kwa haki, na wale waliotafautiana katika kitabu wamo katika mpasuko ulio mbali
تِلۡكَ ءَايَٰتُ ٱللَّهِ نَتۡلُوهَا عَلَيۡكَ بِٱلۡحَقِّۚ وَإِنَّكَ لَمِنَ ٱلۡمُرۡسَلِينَ
Hizi ni Aya za Allah tunazokusomea kwa haki na bila shaka wewe ni miongoni mwa Mitume
نَزَّلَ عَلَيۡكَ ٱلۡكِتَٰبَ بِٱلۡحَقِّ مُصَدِّقٗا لِّمَا بَيۡنَ يَدَيۡهِ وَأَنزَلَ ٱلتَّوۡرَىٰةَ وَٱلۡإِنجِيلَ
Amekuteremshia Kitabu kwa haki kikisadikisha yaliyokuwepo kabla yake. Na ameteremshaTaurati na Injili
هُوَ ٱلَّذِيٓ أَنزَلَ عَلَيۡكَ ٱلۡكِتَٰبَ مِنۡهُ ءَايَٰتٞ مُّحۡكَمَٰتٌ هُنَّ أُمُّ ٱلۡكِتَٰبِ وَأُخَرُ مُتَشَٰبِهَٰتٞۖ فَأَمَّا ٱلَّذِينَ فِي قُلُوبِهِمۡ زَيۡغٞ فَيَتَّبِعُونَ مَا تَشَٰبَهَ مِنۡهُ ٱبۡتِغَآءَ ٱلۡفِتۡنَةِ وَٱبۡتِغَآءَ تَأۡوِيلِهِۦۖ وَمَا يَعۡلَمُ تَأۡوِيلَهُۥٓ إِلَّا ٱللَّهُۗ وَٱلرَّـٰسِخُونَ فِي ٱلۡعِلۡمِ يَقُولُونَ ءَامَنَّا بِهِۦ كُلّٞ مِّنۡ عِندِ رَبِّنَاۗ وَمَا يَذَّكَّرُ إِلَّآ أُوْلُواْ ٱلۡأَلۡبَٰبِ
Yeye ndiye aliyekuteremshia Kitabu. Baadhi ya Aya zake zinafahamika kwa wepesi (na) ambazo ndio msingi wa kitabu (hiki cha Kurani). Na (Aya) nyingine zinatatiza. Ama wale ambao ndani ya nyoyo zao kuna upotevu, wanafuata (Aya) zinazotatiza, kwa kutaka fitina na kutaka kuzipotosha. Na hakuna anayejua tafsiri yake (halisi) isipokuwa Allah tu. Na wale waliobobea katika elimu husema: Tumeziamini (Aya) zote. Zote (hizo) zinatoka kwa Mola wetu Mlezi. Na hawawaidhiki isipokuwa wenye akili tu
تِلۡكَ ءَايَٰتُ ٱللَّهِ نَتۡلُوهَا عَلَيۡكَ بِٱلۡحَقِّۗ وَمَا ٱللَّهُ يُرِيدُ ظُلۡمٗا لِّلۡعَٰلَمِينَ
Hizo ni Aya za Allah tunakusomea kwa haki, na Allah hataki kuwadhulumu walimwengu
إِنَّآ أَنزَلۡنَآ إِلَيۡكَ ٱلۡكِتَٰبَ بِٱلۡحَقِّ لِتَحۡكُمَ بَيۡنَ ٱلنَّاسِ بِمَآ أَرَىٰكَ ٱللَّهُۚ وَلَا تَكُن لِّلۡخَآئِنِينَ خَصِيمٗا
Hakika, sisi tumekuteremshia kitabu kwa haki ili uhukumu baina ya watu kwa kile ambacho Allah amekuonyesha (amekuelimisha). Na usiwe mtetezi wa wanaofanya khiana
وَلَوۡلَا فَضۡلُ ٱللَّهِ عَلَيۡكَ وَرَحۡمَتُهُۥ لَهَمَّت طَّآئِفَةٞ مِّنۡهُمۡ أَن يُضِلُّوكَ وَمَا يُضِلُّونَ إِلَّآ أَنفُسَهُمۡۖ وَمَا يَضُرُّونَكَ مِن شَيۡءٖۚ وَأَنزَلَ ٱللَّهُ عَلَيۡكَ ٱلۡكِتَٰبَ وَٱلۡحِكۡمَةَ وَعَلَّمَكَ مَا لَمۡ تَكُن تَعۡلَمُۚ وَكَانَ فَضۡلُ ٱللَّهِ عَلَيۡكَ عَظِيمٗا
Na lau kama si hisani ya Allah na rehema zake kwako basi kwa yakini kabisa kundi miongoni mwao lilikusudia kukupotosha. Na hawapotoshi ispokuwa nafsi zao tu na hawatakudhuru chochote. Na Allah amekuteremshia kitabu (Qur’an) na hekima, na amekufundisha uliyokuwa huyajui. Na hisani ya Allah kwako ni kubwa sana
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ ءَامِنُواْ بِٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦ وَٱلۡكِتَٰبِ ٱلَّذِي نَزَّلَ عَلَىٰ رَسُولِهِۦ وَٱلۡكِتَٰبِ ٱلَّذِيٓ أَنزَلَ مِن قَبۡلُۚ وَمَن يَكۡفُرۡ بِٱللَّهِ وَمَلَـٰٓئِكَتِهِۦ وَكُتُبِهِۦ وَرُسُلِهِۦ وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِ فَقَدۡ ضَلَّ ضَلَٰلَۢا بَعِيدًا
Enyi mlioamini, endeleeni kumuaminini Allah na Mtume wake na kitabu (Qur’ani) alichokiteremsha kwa Mtume wake na vitabu alivyoviteremsha kabla yake (kabla ya Qur’ani). Na yeyote anayempinga Allah na Malaika wake na Vitabu vyake na Mitume wake na Siku ya Mwisho, basi amepotea upotevu wa mbali kabisa
لَّـٰكِنِ ٱللَّهُ يَشۡهَدُ بِمَآ أَنزَلَ إِلَيۡكَۖ أَنزَلَهُۥ بِعِلۡمِهِۦۖ وَٱلۡمَلَـٰٓئِكَةُ يَشۡهَدُونَۚ وَكَفَىٰ بِٱللَّهِ شَهِيدًا
Lakini Allah anashuhudia aliyokuteremshia. Ameyateremsha kwa ujuzi wake, na Malaika (pia) wanashuhudia. Na inatosha kwamba Allah ni Shahidi
أَفَغَيۡرَ ٱللَّهِ أَبۡتَغِي حَكَمٗا وَهُوَ ٱلَّذِيٓ أَنزَلَ إِلَيۡكُمُ ٱلۡكِتَٰبَ مُفَصَّلٗاۚ وَٱلَّذِينَ ءَاتَيۡنَٰهُمُ ٱلۡكِتَٰبَ يَعۡلَمُونَ أَنَّهُۥ مُنَزَّلٞ مِّن رَّبِّكَ بِٱلۡحَقِّۖ فَلَا تَكُونَنَّ مِنَ ٱلۡمُمۡتَرِينَ
Hivi nitake hakimu (muamuzi) asiyekuwa Allah, na ilhali yeye ndiye aliyekuteremshieni kitabu kikiwa kimefafanuliwa? Na wale tuliowapa kitabu wanajua kwamba kimetereshwa kutoka kwa Mola wako kwa haki. Kwa hiyo usiwe miongoni mwa wenye shaka kabisa
وَهَٰذَا كِتَٰبٌ أَنزَلۡنَٰهُ مُبَارَكٞ فَٱتَّبِعُوهُ وَٱتَّقُواْ لَعَلَّكُمۡ تُرۡحَمُونَ
Na hii (Qur’ani) ni kitabu tulichokiteremsha, chenye baraka. Basi kifuateni na mcheni Allah ili mpate kushushiwa rehema
كِتَٰبٌ أُنزِلَ إِلَيۡكَ فَلَا يَكُن فِي صَدۡرِكَ حَرَجٞ مِّنۡهُ لِتُنذِرَ بِهِۦ وَذِكۡرَىٰ لِلۡمُؤۡمِنِينَ
(Hii Qur’ani ni) Kitabu ulichoteremshiwa. Basi kusiwe na uzito wowote ndani ya kifua chako juu yake (usikose raha katika kukiamini na kukitangaza). (Umeteremshiwa kitabu hiki) Ili kwacho uwaonye (watu) na (ili kiwe) ukumbusho kwa waumini
إِنَّ وَلِـِّۧيَ ٱللَّهُ ٱلَّذِي نَزَّلَ ٱلۡكِتَٰبَۖ وَهُوَ يَتَوَلَّى ٱلصَّـٰلِحِينَ
Hakika, mlinzi wangu ni Allah ambaye ameteremsha kitabu (Qur’ani), naye ndiye anawalinda waja wema
قُل لَّوۡ شَآءَ ٱللَّهُ مَا تَلَوۡتُهُۥ عَلَيۡكُمۡ وَلَآ أَدۡرَىٰكُم بِهِۦۖ فَقَدۡ لَبِثۡتُ فِيكُمۡ عُمُرٗا مِّن قَبۡلِهِۦٓۚ أَفَلَا تَعۡقِلُونَ
Sema: Lau kama Allah angetaka nisingekusomeeni (hii Qur’ani), na (Allah) asingekujulisheni (kuwa hiyo Qur’ani ni haki), kwa sababu bila ya shaka yoyote nimekaa nanyi umri mwingi kabla yake (kabla ya kuletewa hii Qur’ani na wala sikukuambieni kuwa mimi nimeleta Qur’ani). Je, hamtumii akili?
وَمَا كَانَ هَٰذَا ٱلۡقُرۡءَانُ أَن يُفۡتَرَىٰ مِن دُونِ ٱللَّهِ وَلَٰكِن تَصۡدِيقَ ٱلَّذِي بَيۡنَ يَدَيۡهِ وَتَفۡصِيلَ ٱلۡكِتَٰبِ لَا رَيۡبَ فِيهِ مِن رَّبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ
Na haiwezekani Qur’ani hii kutungwa na yeyote kinyume na Allah, lakini (Qur’ani) ni usadikisho wa yote yaliyotangulia (katika vitabu na sheria za Manabii waliotangulia), na ni ufafanuzi wa kitabu (sheria za umma wa Muhammad) kisichokuwa na shaka kutoka kwa Mola mlezi wa walimwengu wote
فَإِن كُنتَ فِي شَكّٖ مِّمَّآ أَنزَلۡنَآ إِلَيۡكَ فَسۡـَٔلِ ٱلَّذِينَ يَقۡرَءُونَ ٱلۡكِتَٰبَ مِن قَبۡلِكَۚ لَقَدۡ جَآءَكَ ٱلۡحَقُّ مِن رَّبِّكَ فَلَا تَكُونَنَّ مِنَ ٱلۡمُمۡتَرِينَ
Basi kama una shaka katika yale tuliyokuteremshia, basi waulize wale wanaosoma kitabu (Taurati) kabla yako. Kwa yakini kabisa, haki imekwisha kukufikia kutoka kwa Mola wako Mlezi. Kwa hiyo, katu usiwe miongoni mwa watiao shaka
الٓرۚ كِتَٰبٌ أُحۡكِمَتۡ ءَايَٰتُهُۥ ثُمَّ فُصِّلَتۡ مِن لَّدُنۡ حَكِيمٍ خَبِيرٍ
Alif, laam, raa (hizi ni herufi za mkato na Allah ndiye anayejua maana yake). Hiki ni kitabu (ambacho) zimetengenezwa vyema Aya zake kisha zimefafanuliwa kutoka kwa aliye na Hekima, Mwenye habari nyingi
إِنَّآ أَنزَلۡنَٰهُ قُرۡءَٰنًا عَرَبِيّٗا لَّعَلَّكُمۡ تَعۡقِلُونَ
Hakika, sisi tumeiteremsha Qur’ani kwa Kiarabu ili mpate kuelewa
نَحۡنُ نَقُصُّ عَلَيۡكَ أَحۡسَنَ ٱلۡقَصَصِ بِمَآ أَوۡحَيۡنَآ إِلَيۡكَ هَٰذَا ٱلۡقُرۡءَانَ وَإِن كُنتَ مِن قَبۡلِهِۦ لَمِنَ ٱلۡغَٰفِلِينَ
Sisi tunakusimulia simulizi nzuri sana kwa (huu) Wahyi tuliokufunulia wa hii Qur’ani, na ingawa kabla yake ulikuwa miongoni mwa wasiojua
الٓمٓرۚ تِلۡكَ ءَايَٰتُ ٱلۡكِتَٰبِۗ وَٱلَّذِيٓ أُنزِلَ إِلَيۡكَ مِن رَّبِّكَ ٱلۡحَقُّ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يُؤۡمِنُونَ
Alif Laam Miim Raa[1]. Hizo ni Aya za Kitabu. Na (hii Qur’an ni wahyi) ambayo umeteremshiwa kutoka kwa Mola wako Mlezi ni haki lakini watu wengi hawaamini
1- - Allah pekee ndiye anayejua maana ya herufi hizi mkato.
الٓرۚ كِتَٰبٌ أَنزَلۡنَٰهُ إِلَيۡكَ لِتُخۡرِجَ ٱلنَّاسَ مِنَ ٱلظُّلُمَٰتِ إِلَى ٱلنُّورِ بِإِذۡنِ رَبِّهِمۡ إِلَىٰ صِرَٰطِ ٱلۡعَزِيزِ ٱلۡحَمِيدِ
Alif Lam Raa[1]. Hiki ni Kitabu tulichokiteremsha kwako ili kwacho uwatowe watu kwenye giza uwapeleke kwenye muangaza, kwa idhini ya Mola wao Mlezi, uwafikishe kwenye Njia ya Mwenye nguvu, Msifiwa
1- - Allah ndiye ajuaye maana halisi ya herufi hizi.
إِنَّا نَحۡنُ نَزَّلۡنَا ٱلذِّكۡرَ وَإِنَّا لَهُۥ لَحَٰفِظُونَ
Hakika Sisi ndio tuliouteremsha Ukumbusho huu, na hakika Sisi ndio tutakaoulinda
وَلَقَدۡ ءَاتَيۡنَٰكَ سَبۡعٗا مِّنَ ٱلۡمَثَانِي وَٱلۡقُرۡءَانَ ٱلۡعَظِيمَ
Na tumekupa Aya saba (za Sura Al-fatiha) zisomwazo mara kwa mara, na Qur’ani Tukufu
بِٱلۡبَيِّنَٰتِ وَٱلزُّبُرِۗ وَأَنزَلۡنَآ إِلَيۡكَ ٱلذِّكۡرَ لِتُبَيِّنَ لِلنَّاسِ مَا نُزِّلَ إِلَيۡهِمۡ وَلَعَلَّهُمۡ يَتَفَكَّرُونَ
(Tuliwatuma) wakiwa na dalili za wazi. Na tumekuteremshia (ewe Muhammad) ukumbusho (Qur’ani) ili uwabainishie watu (kilichojificha katika maana na hukumu zake), na ili wapate kutafakari
وَإِذَا بَدَّلۡنَآ ءَايَةٗ مَّكَانَ ءَايَةٖ وَٱللَّهُ أَعۡلَمُ بِمَا يُنَزِّلُ قَالُوٓاْ إِنَّمَآ أَنتَ مُفۡتَرِۭۚ بَلۡ أَكۡثَرُهُمۡ لَا يَعۡلَمُونَ
Na pindi tunapobadilisha Aya mahali pa Aya (nyingine), Allah ndiye mjuzi zaidi kwa anachoteremsha (na alichokiondoa), walisema: Hakika wewe ni mzushi tu. Bali wengi wao hawajui
قُلۡ نَزَّلَهُۥ رُوحُ ٱلۡقُدُسِ مِن رَّبِّكَ بِٱلۡحَقِّ لِيُثَبِّتَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَهُدٗى وَبُشۡرَىٰ لِلۡمُسۡلِمِينَ
Sema: Ameiteremsha Roho mtakatifu (Jibrili) kutoka kwa Mola wako mlezi kwa haki kabisa, ili kuwaimarisha wale walioamini, na kuwa mwongozo na habari njema kwa Waislamu
وَبِٱلۡحَقِّ أَنزَلۡنَٰهُ وَبِٱلۡحَقِّ نَزَلَۗ وَمَآ أَرۡسَلۡنَٰكَ إِلَّا مُبَشِّرٗا وَنَذِيرٗا
Na kwa Haki tumeiteremsha, na kwa Haki imeteremka. Na hatukukutuma ila uwe mbashiri na muonyaji
وَقُرۡءَانٗا فَرَقۡنَٰهُ لِتَقۡرَأَهُۥ عَلَى ٱلنَّاسِ عَلَىٰ مُكۡثٖ وَنَزَّلۡنَٰهُ تَنزِيلٗا
Na Qur’ani tumeigawanya sehemu mbali mbali ili uwasomee watu kwa kituo, na tumeiteremsha kidogo kidogo
ٱلۡحَمۡدُ لِلَّهِ ٱلَّذِيٓ أَنزَلَ عَلَىٰ عَبۡدِهِ ٱلۡكِتَٰبَ وَلَمۡ يَجۡعَل لَّهُۥ عِوَجَاۜ
Kuhimidiwa ni kwa Allah ambaye amemteremshia mja wake Kitabu, wala hakukifanya kina upogo
قَيِّمٗا لِّيُنذِرَ بَأۡسٗا شَدِيدٗا مِّن لَّدُنۡهُ وَيُبَشِّرَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ ٱلَّذِينَ يَعۡمَلُونَ ٱلصَّـٰلِحَٰتِ أَنَّ لَهُمۡ أَجۡرًا حَسَنٗا
Kimenyooka sawa, ili kitoe onyo kali kutoka kwake, na kiwabashirie Waumini watendao mema kwamba watapata ujira mzuri