يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ ٱعۡبُدُواْ رَبَّكُمُ ٱلَّذِي خَلَقَكُمۡ وَٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِكُمۡ لَعَلَّكُمۡ تَتَّقُونَ
Enyi watu, muabuduni Mola wenu ambaye amekuumbeni na (ameumba) waliokuwepo kabla yenu ili muwe Wacha Mungu
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ عَلَيۡكُمۡ أَنفُسَكُمۡۖ لَا يَضُرُّكُم مَّن ضَلَّ إِذَا ٱهۡتَدَيۡتُمۡۚ إِلَى ٱللَّهِ مَرۡجِعُكُمۡ جَمِيعٗا فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ
Enyi mlioamini, zijalini nafsi zenu. Hawakudhuruni waliopotea ikiwa nyinyi mmeongoka. Kwa Allah tu ndio marejeo yenu nyote; basi atakuambieni yale yote mliyokuwa mnayatenda
قُلۡ أَغَيۡرَ ٱللَّهِ أَبۡغِي رَبّٗا وَهُوَ رَبُّ كُلِّ شَيۡءٖۚ وَلَا تَكۡسِبُ كُلُّ نَفۡسٍ إِلَّا عَلَيۡهَاۚ وَلَا تَزِرُ وَازِرَةٞ وِزۡرَ أُخۡرَىٰۚ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّكُم مَّرۡجِعُكُمۡ فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمۡ فِيهِ تَخۡتَلِفُونَ
Sema: Je nitafute Mola mlezi asiekuwa Allah! na ilhali yeye (Allah) ni Mola Mlezi wa kila kitu? Na kila nafsi haitachuma (jambo la kheri au la shari) isipokuwa litarudi kwake mwenyewe. Na hatabeba mtu yeyote mzigo wa (dhambi za) mwengine. Kisha (nyote) marejeo yenu ni kwa Mola wenu tu, na atakuelezeni yote mliyokuwa mkitofautiana
يَٰبَنِيٓ ءَادَمَ لَا يَفۡتِنَنَّكُمُ ٱلشَّيۡطَٰنُ كَمَآ أَخۡرَجَ أَبَوَيۡكُم مِّنَ ٱلۡجَنَّةِ يَنزِعُ عَنۡهُمَا لِبَاسَهُمَا لِيُرِيَهُمَا سَوۡءَٰتِهِمَآۚ إِنَّهُۥ يَرَىٰكُمۡ هُوَ وَقَبِيلُهُۥ مِنۡ حَيۡثُ لَا تَرَوۡنَهُمۡۗ إِنَّا جَعَلۡنَا ٱلشَّيَٰطِينَ أَوۡلِيَآءَ لِلَّذِينَ لَا يُؤۡمِنُونَ
Enyi Wanadamu, kamwe shetani asikufitinisheni[1] kama alivyowatoa Peponi wazazi wenu, akiwavua nguo zao ili kuwawekea wazi tupu zao. Hakika yeye (shetani) anakuoneni yeye na jeshi lake katika namna ambayo nyinyi hamuwaoni. Hakika, sisi tumewafanya mashetani wandani wa (watu) wasioamini
1- - Shetani asikudanganyeni kwa kukupambieni maasi, kama ambavyo alimhadaa baba yenu Adamu na mkewe kwa kuwashawishi waonje mti. Matokeo yake walitolewa Peponi.
قُلۡ يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ إِنِّي رَسُولُ ٱللَّهِ إِلَيۡكُمۡ جَمِيعًا ٱلَّذِي لَهُۥ مُلۡكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۖ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ يُحۡيِۦ وَيُمِيتُۖ فَـَٔامِنُواْ بِٱللَّهِ وَرَسُولِهِ ٱلنَّبِيِّ ٱلۡأُمِّيِّ ٱلَّذِي يُؤۡمِنُ بِٱللَّهِ وَكَلِمَٰتِهِۦ وَٱتَّبِعُوهُ لَعَلَّكُمۡ تَهۡتَدُونَ
Sema: Enyi watu, hakika mimi ni Mtume wa Allah kwenu nyote[1]. (Allah) Ambaye ni wake pekee ufalme wa mbinguni na ardhini. Hapana mwenye haki ya kuabudiwa isipokuwa yeye tu. Anahuisha na anafisha. Basi muaminini Allah na Mtume wake, Nabii ambaye hasomi kilichoandikwa, ambaye anamuamini Allah na maneno yake, na mfuateni ili mpate kuongoka
1- - Aya hii ni tangazo rasmi kwamba, Uislamu ni dini ya ulimwengu wote na sio ya taifa fulani, kabila fulani au jamii fulani.
ذَٰلِكَ بِأَنَّ ٱللَّهَ لَمۡ يَكُ مُغَيِّرٗا نِّعۡمَةً أَنۡعَمَهَا عَلَىٰ قَوۡمٍ حَتَّىٰ يُغَيِّرُواْ مَا بِأَنفُسِهِمۡ وَأَنَّ ٱللَّهَ سَمِيعٌ عَلِيمٞ
Hiyo (ada ya kuwaadhibu makafiri au kuchukua neema zake) ni kwasababu Allah habadilishi neema zozote alizo waneemesha watu, mpaka wao wabadilishe yaliyomo nafsini mwao. Na hakika Allah ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua
قُلۡ يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ قَدۡ جَآءَكُمُ ٱلۡحَقُّ مِن رَّبِّكُمۡۖ فَمَنِ ٱهۡتَدَىٰ فَإِنَّمَا يَهۡتَدِي لِنَفۡسِهِۦۖ وَمَن ضَلَّ فَإِنَّمَا يَضِلُّ عَلَيۡهَاۖ وَمَآ أَنَا۠ عَلَيۡكُم بِوَكِيلٖ
Sema: Enyi watu, hakika imekujieni haki kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Basi yeyote anayeongoka, anaongoka kwa faida ya nafsi yake, na anayepotea, basi kwa hakika anapotea kwa hasara ya nafsi yake. Na mimi si msaidizi kwenu
لَهُۥ مُعَقِّبَٰتٞ مِّنۢ بَيۡنِ يَدَيۡهِ وَمِنۡ خَلۡفِهِۦ يَحۡفَظُونَهُۥ مِنۡ أَمۡرِ ٱللَّهِۗ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُغَيِّرُ مَا بِقَوۡمٍ حَتَّىٰ يُغَيِّرُواْ مَا بِأَنفُسِهِمۡۗ وَإِذَآ أَرَادَ ٱللَّهُ بِقَوۡمٖ سُوٓءٗا فَلَا مَرَدَّ لَهُۥۚ وَمَا لَهُم مِّن دُونِهِۦ مِن وَالٍ
Kila mtu anao (Malaika) wafuatiliaji mbele yake na nyuma yake wanaomhifadhi[1] kwa amri ya Allah. Hakika, Allah habadili yaliyopo kwa watu mpaka (wao wenyewe) wabadili yaliyomo nafsini mwao. Na Allah anapotaka kuwafikishia jambo baya watu hakuna wa kulizuia na (watu) hawana mlinzi yeyote badala yake
1- - Mwanadamu kila alipo ana Malaika wanaomfuatilia kwa maelekezo ya Allah; wanaomhifadhi yeye na pia kuhifadhi na kutunza kumbukumbu za mambo yote anayoyafanya na pia kauli zote anazozitamka kama ilivyotajwa katika Aya ya 18 ya Sura Qaf (50) na Aya ya 10 mpaka 12 za Sura Al-infitaar (82).
۞إِنَّ ٱللَّهَ يَأۡمُرُ بِٱلۡعَدۡلِ وَٱلۡإِحۡسَٰنِ وَإِيتَآيِٕ ذِي ٱلۡقُرۡبَىٰ وَيَنۡهَىٰ عَنِ ٱلۡفَحۡشَآءِ وَٱلۡمُنكَرِ وَٱلۡبَغۡيِۚ يَعِظُكُمۡ لَعَلَّكُمۡ تَذَكَّرُونَ
Kwa hakika Allah anaamuru uadilifu, na ihsani, na kuwapa (sadaka) ndugu wa karibu na anakataza uchafu, na uovu, na uasi. Anawanasihini ili mpate kukumbuka
۞وَقَضَىٰ رَبُّكَ أَلَّا تَعۡبُدُوٓاْ إِلَّآ إِيَّاهُ وَبِٱلۡوَٰلِدَيۡنِ إِحۡسَٰنًاۚ إِمَّا يَبۡلُغَنَّ عِندَكَ ٱلۡكِبَرَ أَحَدُهُمَآ أَوۡ كِلَاهُمَا فَلَا تَقُل لَّهُمَآ أُفّٖ وَلَا تَنۡهَرۡهُمَا وَقُل لَّهُمَا قَوۡلٗا كَرِيمٗا
Na Mola wako Mlezi ameam-risha kuwa msimuabudu yeyote ila Yeye tu, na wazazi wawili muwa-tendee wema. Mmoja wao akifikia uzee, naye yuko kwako, au wote wawili, basi usimwambie hata: Ah! Wala usiwakemee. Na sema nao kwa msemo wa heshima
وَلَا تَقۡرَبُواْ مَالَ ٱلۡيَتِيمِ إِلَّا بِٱلَّتِي هِيَ أَحۡسَنُ حَتَّىٰ يَبۡلُغَ أَشُدَّهُۥۚ وَأَوۡفُواْ بِٱلۡعَهۡدِۖ إِنَّ ٱلۡعَهۡدَ كَانَ مَسۡـُٔولٗا
Wala msiyakaribie mali ya yatima, isipokuwa kwa njia iliyo bora, mpaka afike utuuzimani. Na timizeni ahadi. Kwa hakika ahadi ni yenye kuulizwa
وَأَوۡفُواْ ٱلۡكَيۡلَ إِذَا كِلۡتُمۡ وَزِنُواْ بِٱلۡقِسۡطَاسِ ٱلۡمُسۡتَقِيمِۚ ذَٰلِكَ خَيۡرٞ وَأَحۡسَنُ تَأۡوِيلٗا
Na timizeni kipimo mpimapo. Na pimeni kwa mizani zilizo sawa. Hayo ni wema kwenu na hatimaye ndio bora
وَلَا تَقۡفُ مَا لَيۡسَ لَكَ بِهِۦ عِلۡمٌۚ إِنَّ ٱلسَّمۡعَ وَٱلۡبَصَرَ وَٱلۡفُؤَادَ كُلُّ أُوْلَـٰٓئِكَ كَانَ عَنۡهُ مَسۡـُٔولٗا
Wala usiyafuate usiyo na ujuzi nayo. Hakika masikio, na macho, na moyo - hivyo vyote vitasailiwa (vitaulizwa)
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ ٱتَّقُواْ رَبَّكُمۡۚ إِنَّ زَلۡزَلَةَ ٱلسَّاعَةِ شَيۡءٌ عَظِيمٞ
Enyi watu, mcheni Mola wenu Mlezi. Hakika tetemeko la Kiyama ni jambo kubwa mno
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ ٱتَّقُواْ رَبَّكُمۡ وَٱخۡشَوۡاْ يَوۡمٗا لَّا يَجۡزِي وَالِدٌ عَن وَلَدِهِۦ وَلَا مَوۡلُودٌ هُوَ جَازٍ عَن وَالِدِهِۦ شَيۡـًٔاۚ إِنَّ وَعۡدَ ٱللَّهِ حَقّٞۖ فَلَا تَغُرَّنَّكُمُ ٱلۡحَيَوٰةُ ٱلدُّنۡيَا وَلَا يَغُرَّنَّكُم بِٱللَّهِ ٱلۡغَرُورُ
Enyi watu! Mcheni Mola wenu Mlezi, na iogopeni siku ambayo mzazi hatamfaa mwana, wala mwana hatamfaa mzazi kwa lolote. Hakika ahadi ya Allah ni ya kweli. Basi yasikudanganyeni maisha ya dunia, wala asikudanganyeni juu ya Allah mdanganyifu
وَلَا تَزِرُ وَازِرَةٞ وِزۡرَ أُخۡرَىٰۚ وَإِن تَدۡعُ مُثۡقَلَةٌ إِلَىٰ حِمۡلِهَا لَا يُحۡمَلۡ مِنۡهُ شَيۡءٞ وَلَوۡ كَانَ ذَا قُرۡبَىٰٓۗ إِنَّمَا تُنذِرُ ٱلَّذِينَ يَخۡشَوۡنَ رَبَّهُم بِٱلۡغَيۡبِ وَأَقَامُواْ ٱلصَّلَوٰةَۚ وَمَن تَزَكَّىٰ فَإِنَّمَا يَتَزَكَّىٰ لِنَفۡسِهِۦۚ وَإِلَى ٱللَّهِ ٱلۡمَصِيرُ
Na mbebaji habebi mzigo wa mwingine. Na aliyetopewa na mzigo wake akiomba uchukuliwe hautachukuliwa hata kidogo, na angemuomba jamaa yake. Hakika wewe unawaonya wale wanao mcha Mola wao Mlezi kwa ghaibu, na wanashika Sala. Na anaye jitakasa, basi anajitakasa kwa ajili ya nafsi yake. Na marejeo ni kwa Allah
إِن تَكۡفُرُواْ فَإِنَّ ٱللَّهَ غَنِيٌّ عَنكُمۡۖ وَلَا يَرۡضَىٰ لِعِبَادِهِ ٱلۡكُفۡرَۖ وَإِن تَشۡكُرُواْ يَرۡضَهُ لَكُمۡۗ وَلَا تَزِرُ وَازِرَةٞ وِزۡرَ أُخۡرَىٰۚ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّكُم مَّرۡجِعُكُمۡ فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَۚ إِنَّهُۥ عَلِيمُۢ بِذَاتِ ٱلصُّدُورِ
Mkikufuru basi Allah si mwenye haja nanyi, lakini hafurahii kufuru kwa waja wake. Na mkishukuru Yeye hufurahika nanyi. Wala mbebaji habebi mzigo wa mwingine. Kisha marejeo yenu ni kwa Mola wenu Mlezi. Hapo atakwambieni mliyo kuwa mkiyafanya. Hakika Yeye ni Mwenye kuyajua vyema yaliyomo vifuani
وَمَا خَلَقۡتُ ٱلۡجِنَّ وَٱلۡإِنسَ إِلَّا لِيَعۡبُدُونِ
Na sikuwaumba majini na wanadamu ila kwa ajili ya kuniabudu
أَلَّا تَزِرُ وَازِرَةٞ وِزۡرَ أُخۡرَىٰ
Na kwamba mbebaji dhambi hatobeba mzigo wa mwengine
وَأَن لَّيۡسَ لِلۡإِنسَٰنِ إِلَّا مَا سَعَىٰ
Na kwamba Mtu hatopata malipo isipokuwa yale aliyoyafanyia juhudi
وَأَنَّ سَعۡيَهُۥ سَوۡفَ يُرَىٰ
Na kwamba juhudi yake itakuja kuonekana
ثُمَّ يُجۡزَىٰهُ ٱلۡجَزَآءَ ٱلۡأَوۡفَىٰ
Kisha atalipwa malipo yake kamilifu