إِنَّ ٱلۡمُنَٰفِقِينَ فِي ٱلدَّرۡكِ ٱلۡأَسۡفَلِ مِنَ ٱلنَّارِ وَلَن تَجِدَ لَهُمۡ نَصِيرًا
Hakika, wanafiki watakuwa katika tabaka la chini kabisa la Moto, na hutampata yeyote wa kuwanusuru
يَحۡذَرُ ٱلۡمُنَٰفِقُونَ أَن تُنَزَّلَ عَلَيۡهِمۡ سُورَةٞ تُنَبِّئُهُم بِمَا فِي قُلُوبِهِمۡۚ قُلِ ٱسۡتَهۡزِءُوٓاْ إِنَّ ٱللَّهَ مُخۡرِجٞ مَّا تَحۡذَرُونَ
Wanafiki wanaogopa kute-remshiwa Sura itakayowafichulia yaliyomo katika nyoyo zao. Sema (uwaambie na kwa kuwaonya kwamba): Fanyeni mzaha, hakika Allah atayadhidirisha hayo mnayoogopa (yasijulikane)
وَلَئِن سَأَلۡتَهُمۡ لَيَقُولُنَّ إِنَّمَا كُنَّا نَخُوضُ وَنَلۡعَبُۚ قُلۡ أَبِٱللَّهِ وَءَايَٰتِهِۦ وَرَسُولِهِۦ كُنتُمۡ تَسۡتَهۡزِءُونَ
Na kwa yakini kabisa, ukiwauliza (wanafiki kuhusu unafiki na dhihaka zao) watasema: Sisi tulikuwa tukipiga porojo na kucheza tu. Sema: Je, mlikuwa mkimfanyia masihara Allah na Aya zake (Qur’an) na Mtume wake?
لَا تَعۡتَذِرُواْ قَدۡ كَفَرۡتُم بَعۡدَ إِيمَٰنِكُمۡۚ إِن نَّعۡفُ عَن طَآئِفَةٖ مِّنكُمۡ نُعَذِّبۡ طَآئِفَةَۢ بِأَنَّهُمۡ كَانُواْ مُجۡرِمِينَ
(Enyi wanafiki) Msitoe udhuru; hakika mmekwisha kufuru baada ya kuamini kwenu. Ikiwa tutalisamehe kundi katika nyinyi, tunaliadhibu kundi jingine kwa sababu walikuwa wakosefu
ٱلۡمُنَٰفِقُونَ وَٱلۡمُنَٰفِقَٰتُ بَعۡضُهُم مِّنۢ بَعۡضٖۚ يَأۡمُرُونَ بِٱلۡمُنكَرِ وَيَنۡهَوۡنَ عَنِ ٱلۡمَعۡرُوفِ وَيَقۡبِضُونَ أَيۡدِيَهُمۡۚ نَسُواْ ٱللَّهَ فَنَسِيَهُمۡۚ إِنَّ ٱلۡمُنَٰفِقِينَ هُمُ ٱلۡفَٰسِقُونَ
Wanafiki wanaume na wanafiki wanawake; wote ni hali moja (wanafanana katika unafiki na kutoamini). Wanaamrisha maovu na wanakataza mema na wanakunja mikono yao (kwa kukataa kutoa katika njia za heri). Wamemsahau Allah, basi naye amejifanya amewasahau (amewaacha na unafiki wao). Hakika, wanafiki ndio waovu hasa
وَعَدَ ٱللَّهُ ٱلۡمُنَٰفِقِينَ وَٱلۡمُنَٰفِقَٰتِ وَٱلۡكُفَّارَ نَارَ جَهَنَّمَ خَٰلِدِينَ فِيهَاۚ هِيَ حَسۡبُهُمۡۚ وَلَعَنَهُمُ ٱللَّهُۖ وَلَهُمۡ عَذَابٞ مُّقِيمٞ
Allah amewaahidi wanafiki wanaume na wanafiki wanawake na makafiri Moto wa Jahanamu wakidumu humo milele. Hilo ndilo linalowatosha, na Allah amewalaani na watapata adhabu ya kudumu
كَٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِكُمۡ كَانُوٓاْ أَشَدَّ مِنكُمۡ قُوَّةٗ وَأَكۡثَرَ أَمۡوَٰلٗا وَأَوۡلَٰدٗا فَٱسۡتَمۡتَعُواْ بِخَلَٰقِهِمۡ فَٱسۡتَمۡتَعۡتُم بِخَلَٰقِكُمۡ كَمَا ٱسۡتَمۡتَعَ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِكُم بِخَلَٰقِهِمۡ وَخُضۡتُمۡ كَٱلَّذِي خَاضُوٓاْۚ أُوْلَـٰٓئِكَ حَبِطَتۡ أَعۡمَٰلُهُمۡ فِي ٱلدُّنۡيَا وَٱلۡأٓخِرَةِۖ وَأُوْلَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡخَٰسِرُونَ
(Enyi wanafiki vitendo vyenu vya dhihaka) Ni kama (vya) wale (wanafiki) waliokuwepo kabla yenu. Walikuwa na nguvu mno na mali na watoto zaidi kuliko nyinyi. Basi walistarehe na fungu lao, na nyinyi mstarehe na fungu lenu, kama waliokuwepo kabla yenu walivyostarehe na fungu lao. Na nyinyi mmezama (katika maovu) kama wao walivyozama. Hao ndio ambao vitendo vyao vimeharibika katika dunia na Akhera; na hao ndio waliokula hasara hasa
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّبِيُّ جَٰهِدِ ٱلۡكُفَّارَ وَٱلۡمُنَٰفِقِينَ وَٱغۡلُظۡ عَلَيۡهِمۡۚ وَمَأۡوَىٰهُمۡ جَهَنَّمُۖ وَبِئۡسَ ٱلۡمَصِيرُ
Ewe Nabii, pambana na makafiri na wanafiki (kwa mbinu za aina zote) na uwe mkali kwao. Na makazi yao ni Jahanamu, na huo ni mwisho mbaya sana
يَحۡلِفُونَ بِٱللَّهِ مَا قَالُواْ وَلَقَدۡ قَالُواْ كَلِمَةَ ٱلۡكُفۡرِ وَكَفَرُواْ بَعۡدَ إِسۡلَٰمِهِمۡ وَهَمُّواْ بِمَا لَمۡ يَنَالُواْۚ وَمَا نَقَمُوٓاْ إِلَّآ أَنۡ أَغۡنَىٰهُمُ ٱللَّهُ وَرَسُولُهُۥ مِن فَضۡلِهِۦۚ فَإِن يَتُوبُواْ يَكُ خَيۡرٗا لَّهُمۡۖ وَإِن يَتَوَلَّوۡاْ يُعَذِّبۡهُمُ ٱللَّهُ عَذَابًا أَلِيمٗا فِي ٱلدُّنۡيَا وَٱلۡأٓخِرَةِۚ وَمَا لَهُمۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ مِن وَلِيّٖ وَلَا نَصِيرٖ
(Wanafiki) Wanaapa kwa (jina la) Allah kuwa hawakusema (hayo maneno yaliyokufikia). Na kwa hakika kabisa, walisema neno la ukafiri na wamekufuru baada ya kusilimu kwao na walikusudia kufanya ambayo hawakuyapata (ya kutaka kumuua Mtume na kuwafukuza Waislamu) na hawakuchukia ila tu kwa sababu Allah na Mtume wake wamewatajirisha (Waislamu kwa kuwapa neema mbali mbali) kutokana na fadhila zake. Basi iwapo watatubu itakuwa heri kwao na wakikengeuka, Allah atawaadhibu adhabu inayoumiza mno (hapa) duniani na (kesho) Akhera, na hawana katika ardhi yeyote wa kuwalinda wala wa kuwanusuru
۞وَمِنۡهُم مَّنۡ عَٰهَدَ ٱللَّهَ لَئِنۡ ءَاتَىٰنَا مِن فَضۡلِهِۦ لَنَصَّدَّقَنَّ وَلَنَكُونَنَّ مِنَ ٱلصَّـٰلِحِينَ
Na miongoni mwao (hao wanafiki) wapo waliomuahidi Allah kwamba: Iwapo (Allah) atatupa katika fadhila zake basi kwa yakini kabisa tutatoa sadaka sana na tutakuwa katika watendao mema
فَلَمَّآ ءَاتَىٰهُم مِّن فَضۡلِهِۦ بَخِلُواْ بِهِۦ وَتَوَلَّواْ وَّهُم مُّعۡرِضُونَ
Basi (Allah) alipowapa katika fadhila zake walizifanyia ubahili na wakakengeuka na huku wakipuuza (walichokiahidi)
فَأَعۡقَبَهُمۡ نِفَاقٗا فِي قُلُوبِهِمۡ إِلَىٰ يَوۡمِ يَلۡقَوۡنَهُۥ بِمَآ أَخۡلَفُواْ ٱللَّهَ مَا وَعَدُوهُ وَبِمَا كَانُواْ يَكۡذِبُونَ
Basi (Allah) akawapa hatima ya unafiki nyoyoni mwao mpaka Siku watapokutana naye, kwa sababu ya kuwa walimhalifu Allah katika yale waliyomuahidi, na kwa sababu ya kusema kwao uwongo
أَلَمۡ يَعۡلَمُوٓاْ أَنَّ ٱللَّهَ يَعۡلَمُ سِرَّهُمۡ وَنَجۡوَىٰهُمۡ وَأَنَّ ٱللَّهَ عَلَّـٰمُ ٱلۡغُيُوبِ
Hivi, (wanafiki) hawakujua kwamba Allah anajua siri zao na minong’ono yao na kwamba Allah ni Mwenye kuyajua mno (mambo) ya Ghaibu?
ٱلَّذِينَ يَلۡمِزُونَ ٱلۡمُطَّوِّعِينَ مِنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ فِي ٱلصَّدَقَٰتِ وَٱلَّذِينَ لَا يَجِدُونَ إِلَّا جُهۡدَهُمۡ فَيَسۡخَرُونَ مِنۡهُمۡ سَخِرَ ٱللَّهُ مِنۡهُمۡ وَلَهُمۡ عَذَابٌ أَلِيمٌ
Wale wanaowabeua (wanaowabeza) Waumini wanaotoa sadaka (wanapotoa kidogo huwalaumu kwamba hakitoshi, na wanapotoa kingi huwasema wanajionesha), na wasio na cha kutoa ila kadiri ya uwezo wao (wanapotoa), basi wanawakejeli (kwamba Allah hahitaji sadaka za aina hii). Allah atawalipa kwa kejeli zao, na watapata adhabu inayoumiza sana
ٱسۡتَغۡفِرۡ لَهُمۡ أَوۡ لَا تَسۡتَغۡفِرۡ لَهُمۡ إِن تَسۡتَغۡفِرۡ لَهُمۡ سَبۡعِينَ مَرَّةٗ فَلَن يَغۡفِرَ ٱللَّهُ لَهُمۡۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمۡ كَفَرُواْ بِٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦۗ وَٱللَّهُ لَا يَهۡدِي ٱلۡقَوۡمَ ٱلۡفَٰسِقِينَ
Waombee msamaha au usiwaombee (yote ni sawa). Hata ukiwaombea msamaha mara sabini (au zaidi), katu Allah hatawasamehe. Hayo ni kwa sababu wamemkufuru Allah na Mtume wake. Na Allah hawaongoi watu waovu
فَرِحَ ٱلۡمُخَلَّفُونَ بِمَقۡعَدِهِمۡ خِلَٰفَ رَسُولِ ٱللَّهِ وَكَرِهُوٓاْ أَن يُجَٰهِدُواْ بِأَمۡوَٰلِهِمۡ وَأَنفُسِهِمۡ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ وَقَالُواْ لَا تَنفِرُواْ فِي ٱلۡحَرِّۗ قُلۡ نَارُ جَهَنَّمَ أَشَدُّ حَرّٗاۚ لَّوۡ كَانُواْ يَفۡقَهُونَ
Walioachwa nyuma walifurahia kwa kule kubakia kwao nyuma na kumuacha Mtume wa Allah na walichukia (kwenda) kupigana Jihadi kwa mali zao na nafsi zao katika Njia ya Allah na wakasema: Msiende katika (Jihadi kipindi) cha joto. Sema: Moto wa Jahanamu una joto kali zaidi, laiti kama wangekuwa wanafahamu
فَلۡيَضۡحَكُواْ قَلِيلٗا وَلۡيَبۡكُواْ كَثِيرٗا جَزَآءَۢ بِمَا كَانُواْ يَكۡسِبُونَ
Basi wacheke kidogo (hapa duniani) na walie sana (huko Akhera) ikiwa ni malipo ya yale waliyokuwa wakiyachuma
فَإِن رَّجَعَكَ ٱللَّهُ إِلَىٰ طَآئِفَةٖ مِّنۡهُمۡ فَٱسۡتَـٔۡذَنُوكَ لِلۡخُرُوجِ فَقُل لَّن تَخۡرُجُواْ مَعِيَ أَبَدٗا وَلَن تُقَٰتِلُواْ مَعِيَ عَدُوًّاۖ إِنَّكُمۡ رَضِيتُم بِٱلۡقُعُودِ أَوَّلَ مَرَّةٖ فَٱقۡعُدُواْ مَعَ ٱلۡخَٰلِفِينَ
Basi (Ewe Mtume Muhammad) Allah akikurudisha (salama) kwenye kundi moja miongoni mwao (hao wanafiki) na wakakuomba idhini ya kutoka (nawe kwenda vitani) sema: Nyinyi katu hamuwezi kutoka pamoja nami, na asilani hamuwezi kupigana na adui pamoja nami. Hakika, nyinyi mmeridhia kukaa nyuma mara ya kwanza, basi kaeni pamoja na hao wabakiao nyuma (wanawake, watoto na wasiojiweza)
وَلَا تُصَلِّ عَلَىٰٓ أَحَدٖ مِّنۡهُم مَّاتَ أَبَدٗا وَلَا تَقُمۡ عَلَىٰ قَبۡرِهِۦٓۖ إِنَّهُمۡ كَفَرُواْ بِٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦ وَمَاتُواْ وَهُمۡ فَٰسِقُونَ
Na kamwe usimswalie yeyote katika wao (wanafiki) akifa wala usisimame kaburini kwake (na kumuombea dua). Hakika, hao wamemkufuru Allah na Mtume wake na wamekufa ilhali ni waovu
وَلَا تُعۡجِبۡكَ أَمۡوَٰلُهُمۡ وَأَوۡلَٰدُهُمۡۚ إِنَّمَا يُرِيدُ ٱللَّهُ أَن يُعَذِّبَهُم بِهَا فِي ٱلدُّنۡيَا وَتَزۡهَقَ أَنفُسُهُمۡ وَهُمۡ كَٰفِرُونَ
Na zisikushangaze mali zao na watoto wao (hapa duniani). Ilivyo ni kwamba, Allah anataka kuwaadhibu kwazo duniani[1] na zitoke kwa nguvu roho zao na ilhali wao ni makafiri
1- - Rejea dokezo katika Aya ya 55 ya Sura hii.
وَإِذَآ أُنزِلَتۡ سُورَةٌ أَنۡ ءَامِنُواْ بِٱللَّهِ وَجَٰهِدُواْ مَعَ رَسُولِهِ ٱسۡتَـٔۡذَنَكَ أُوْلُواْ ٱلطَّوۡلِ مِنۡهُمۡ وَقَالُواْ ذَرۡنَا نَكُن مَّعَ ٱلۡقَٰعِدِينَ
Na inapoteremshwa Sura (inayowaamrisha) kwamba: Muaminini Allah na piganeni Jihadi pamoja na Mtume wake, wale wenye uwezo (wa mali na nguvu) miongoni mwao wanakuomba ruhusa na kusema: Tuache tuwe pamoja na wanaokaa nyuma
رَضُواْ بِأَن يَكُونُواْ مَعَ ٱلۡخَوَالِفِ وَطُبِعَ عَلَىٰ قُلُوبِهِمۡ فَهُمۡ لَا يَفۡقَهُونَ
Wameridhia kuwa pamoja na wabakiao nyuma (wenye nyudhuru), na nyoyo zao zikapigwa chapa kwa hivyo hawafahamu
وَمِمَّنۡ حَوۡلَكُم مِّنَ ٱلۡأَعۡرَابِ مُنَٰفِقُونَۖ وَمِنۡ أَهۡلِ ٱلۡمَدِينَةِ مَرَدُواْ عَلَى ٱلنِّفَاقِ لَا تَعۡلَمُهُمۡۖ نَحۡنُ نَعۡلَمُهُمۡۚ سَنُعَذِّبُهُم مَّرَّتَيۡنِ ثُمَّ يُرَدُّونَ إِلَىٰ عَذَابٍ عَظِيمٖ
Na miongoni mwa Mabedui waliopo pembezoni mwenu (pembezoni mwa mji wa Madina) ni wanafiki. Na katika wenyeji wa Madina pia wapo (watu) waliobobea katika unafiki. Wewe huwajui, (lakini) sisi tunawajua. Tutawaadhibu mara mbili, kisha watarudishwa kwenye adhabu kubwa mno
لِّيُعَذِّبَ ٱللَّهُ ٱلۡمُنَٰفِقِينَ وَٱلۡمُنَٰفِقَٰتِ وَٱلۡمُشۡرِكِينَ وَٱلۡمُشۡرِكَٰتِ وَيَتُوبَ ٱللَّهُ عَلَى ٱلۡمُؤۡمِنِينَ وَٱلۡمُؤۡمِنَٰتِۗ وَكَانَ ٱللَّهُ غَفُورٗا رَّحِيمَۢا
Kwa hivyo Allah anawaadhibu wanafiki wanaume, na wanafiki wanawake, na washirikina wanaume, na washirikina wanawake; na anawapokelea toba Waumini wanaume, na Waumini wanawake. Na Allah ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu
وَيُعَذِّبَ ٱلۡمُنَٰفِقِينَ وَٱلۡمُنَٰفِقَٰتِ وَٱلۡمُشۡرِكِينَ وَٱلۡمُشۡرِكَٰتِ ٱلظَّآنِّينَ بِٱللَّهِ ظَنَّ ٱلسَّوۡءِۚ عَلَيۡهِمۡ دَآئِرَةُ ٱلسَّوۡءِۖ وَغَضِبَ ٱللَّهُ عَلَيۡهِمۡ وَلَعَنَهُمۡ وَأَعَدَّ لَهُمۡ جَهَنَّمَۖ وَسَآءَتۡ مَصِيرٗا
Na awape adhabu wanafiki wanaume na wanaafiki wanawake, na washirikina wanaume na washirikina wanawake, wanao mdhania Allah dhana mbaya. Utawafikia mgeuko mbaya, na Allah awakasirikie, na awalaani, na awaandalie Jahannamu. Na hayo ni marudio maovu kabisa
يَوۡمَ يَقُولُ ٱلۡمُنَٰفِقُونَ وَٱلۡمُنَٰفِقَٰتُ لِلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱنظُرُونَا نَقۡتَبِسۡ مِن نُّورِكُمۡ قِيلَ ٱرۡجِعُواْ وَرَآءَكُمۡ فَٱلۡتَمِسُواْ نُورٗاۖ فَضُرِبَ بَيۡنَهُم بِسُورٖ لَّهُۥ بَابُۢ بَاطِنُهُۥ فِيهِ ٱلرَّحۡمَةُ وَظَٰهِرُهُۥ مِن قِبَلِهِ ٱلۡعَذَابُ
Siku wanafiki wa kiume na wanafiki wa kike watakapowaambia wale walioamini: Tungojeeni, tupate mwangaza kutokana na nuru yenu! (Wataambiwa): Rudini nyuma yenu, na mtafute huko nuru (yenu)! Kisha utawekwa ukuta baina yao wenye mlango, ndani mna rahma na nje kwa upande wake wa mbele mna adhabu
يُنَادُونَهُمۡ أَلَمۡ نَكُن مَّعَكُمۡۖ قَالُواْ بَلَىٰ وَلَٰكِنَّكُمۡ فَتَنتُمۡ أَنفُسَكُمۡ وَتَرَبَّصۡتُمۡ وَٱرۡتَبۡتُمۡ وَغَرَّتۡكُمُ ٱلۡأَمَانِيُّ حَتَّىٰ جَآءَ أَمۡرُ ٱللَّهِ وَغَرَّكُم بِٱللَّهِ ٱلۡغَرُورُ
(Wanafiki) Watawaita Waumini wawambie: Je, kwani hatukuwa pamoja nanyi? Watasema: Ndio! Lakini nyinyi mmezifitini nafsi zenu, na mkasitasita; na mkatia shaka, na yakakudanganyeni matamanio ya nafsi zenu, mpaka ikawajieni amri ya Allah (umauti) na akawadanganya kwa Allah mdanganyifu.(msimfuate Allah)
فَٱلۡيَوۡمَ لَا يُؤۡخَذُ مِنكُمۡ فِدۡيَةٞ وَلَا مِنَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْۚ مَأۡوَىٰكُمُ ٱلنَّارُۖ هِيَ مَوۡلَىٰكُمۡۖ وَبِئۡسَ ٱلۡمَصِيرُ
Basi leo haitochukuliwa kutoka kwenu fidia na wala kutoka kwa waliokufuru. Makazi yenu ni moto, hayo ndio yanayostahiki kwenu, na ni marejeo mabaya yalioje
۞أَلَمۡ تَرَ إِلَى ٱلَّذِينَ تَوَلَّوۡاْ قَوۡمًا غَضِبَ ٱللَّهُ عَلَيۡهِم مَّا هُم مِّنكُمۡ وَلَا مِنۡهُمۡ وَيَحۡلِفُونَ عَلَى ٱلۡكَذِبِ وَهُمۡ يَعۡلَمُونَ
Je, hukuona wale waliofanya urafiki na watu ambao Allah Amewakasirikia?, wao si katika nyinyi, na wala si katika wao, na wanaapia uongo hali yakuwa wanajua
أَعَدَّ ٱللَّهُ لَهُمۡ عَذَابٗا شَدِيدًاۖ إِنَّهُمۡ سَآءَ مَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ
Allah Amewaandalia adhabu kali, hakika ni uovu ulioje waliokuwa wakiutenda