Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 111

۞وَلَوۡ أَنَّنَا نَزَّلۡنَآ إِلَيۡهِمُ ٱلۡمَلَـٰٓئِكَةَ وَكَلَّمَهُمُ ٱلۡمَوۡتَىٰ وَحَشَرۡنَا عَلَيۡهِمۡ كُلَّ شَيۡءٖ قُبُلٗا مَّا كَانُواْ لِيُؤۡمِنُوٓاْ إِلَّآ أَن يَشَآءَ ٱللَّهُ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَهُمۡ يَجۡهَلُونَ

Na lau kama tungewateremshia Malaika na wafu wakawazungumzisha na tukawakusanyia kila kitu mbele (yao) wasingeamini isipokuwa tu Allah akitaka, na lakini wengi wao wanajitia ujinga



Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 112

وَكَذَٰلِكَ جَعَلۡنَا لِكُلِّ نَبِيٍّ عَدُوّٗا شَيَٰطِينَ ٱلۡإِنسِ وَٱلۡجِنِّ يُوحِي بَعۡضُهُمۡ إِلَىٰ بَعۡضٖ زُخۡرُفَ ٱلۡقَوۡلِ غُرُورٗاۚ وَلَوۡ شَآءَ رَبُّكَ مَا فَعَلُوهُۖ فَذَرۡهُمۡ وَمَا يَفۡتَرُونَ

Na kama hivyo tumemuwekea kila Nabii adui; mashetani watu na (mashetani) majini, wao kwa wao wakipeana maneno ya kupamba pamba kwa kudanganyana. Na lau kama Mola wako angetaka, wasingeyafanya hayo. Basi waache na hayo wayazushayo



Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 113

وَلِتَصۡغَىٰٓ إِلَيۡهِ أَفۡـِٔدَةُ ٱلَّذِينَ لَا يُؤۡمِنُونَ بِٱلۡأٓخِرَةِ وَلِيَرۡضَوۡهُ وَلِيَقۡتَرِفُواْ مَا هُم مُّقۡتَرِفُونَ

Na ili nyoyo za wasioamini Akhera ziyasikilize (maneno hayo ya kupamba) na ili wayaridhie na ili wachume wanayoyachuma



Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 114

أَفَغَيۡرَ ٱللَّهِ أَبۡتَغِي حَكَمٗا وَهُوَ ٱلَّذِيٓ أَنزَلَ إِلَيۡكُمُ ٱلۡكِتَٰبَ مُفَصَّلٗاۚ وَٱلَّذِينَ ءَاتَيۡنَٰهُمُ ٱلۡكِتَٰبَ يَعۡلَمُونَ أَنَّهُۥ مُنَزَّلٞ مِّن رَّبِّكَ بِٱلۡحَقِّۖ فَلَا تَكُونَنَّ مِنَ ٱلۡمُمۡتَرِينَ

Hivi nitake hakimu (muamuzi) asiyekuwa Allah, na ilhali yeye ndiye aliyekuteremshieni kitabu kikiwa kimefafanuliwa? Na wale tuliowapa kitabu wanajua kwamba kimetereshwa kutoka kwa Mola wako kwa haki. Kwa hiyo usiwe miongoni mwa wenye shaka kabisa



Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 115

وَتَمَّتۡ كَلِمَتُ رَبِّكَ صِدۡقٗا وَعَدۡلٗاۚ لَّا مُبَدِّلَ لِكَلِمَٰتِهِۦۚ وَهُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلۡعَلِيمُ

Na neno la Mola wako Mlezi limetimia kwa haki na uadilifu. Hakuna wa kubadilisha maneno yake, na yeye ni Mwenye kusikia, Mjuzi (wa kila kitu)



Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 116

وَإِن تُطِعۡ أَكۡثَرَ مَن فِي ٱلۡأَرۡضِ يُضِلُّوكَ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِۚ إِن يَتَّبِعُونَ إِلَّا ٱلظَّنَّ وَإِنۡ هُمۡ إِلَّا يَخۡرُصُونَ

Na ikiwa utawatii walio wengi humu duniani watakupoteza katika njia ya Allah[1]. Hawafuati isipokuwa dhana tu, na hawakuwa wao isipokuwa tu wanaongopa


1- - Usemi wa Kiswahili wa “Wengi wape” katika Uislamu hauna nafasi. Kinachotakiwa katika Uislamu ni haki na uadilifu. Haki haipimwi kwa wingi au uchache.


Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 117

إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعۡلَمُ مَن يَضِلُّ عَن سَبِيلِهِۦۖ وَهُوَ أَعۡلَمُ بِٱلۡمُهۡتَدِينَ

Kwa hakika, Mola wako Mlezi ndiye tu amjuae zaidi aliyepotea katika njia yake, na yeye ndiye awajuae zaidi wenye kuongoka



Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 118

فَكُلُواْ مِمَّا ذُكِرَ ٱسۡمُ ٱللَّهِ عَلَيۡهِ إِن كُنتُم بِـَٔايَٰتِهِۦ مُؤۡمِنِينَ

Basi kuleni miongoni mwa vilivyotajiwa jina la Allah (wakati wa kuchinjwa) ikiwa nyinyi mnaziamini Aya zake



Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 119

وَمَا لَكُمۡ أَلَّا تَأۡكُلُواْ مِمَّا ذُكِرَ ٱسۡمُ ٱللَّهِ عَلَيۡهِ وَقَدۡ فَصَّلَ لَكُم مَّا حَرَّمَ عَلَيۡكُمۡ إِلَّا مَا ٱضۡطُرِرۡتُمۡ إِلَيۡهِۗ وَإِنَّ كَثِيرٗا لَّيُضِلُّونَ بِأَهۡوَآئِهِم بِغَيۡرِ عِلۡمٍۚ إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعۡلَمُ بِٱلۡمُعۡتَدِينَ

Na mna kikwazo gani nyinyi hamli miongoni mwa vilivyotajiwa jina la Allah na ilhali amekufafanulieni vile alivyokuharamishieni[1], isipokuwa vile mlivyolazimika kwa dharura? Na kwa hakika, wengi wanapotea kwa sababu ya utashi wa nafsi zao bila ya elimu. Kwa hakika, Mola wako Mlezi anawajua zaidi wanaovuka mipaka


1- - Rejea Aya ya 3 ya Sura Almaida (5).


Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 120

وَذَرُواْ ظَٰهِرَ ٱلۡإِثۡمِ وَبَاطِنَهُۥٓۚ إِنَّ ٱلَّذِينَ يَكۡسِبُونَ ٱلۡإِثۡمَ سَيُجۡزَوۡنَ بِمَا كَانُواْ يَقۡتَرِفُونَ

Na acheni dhambi za dhahiri na za siri. Kwa hakika wale ambao wanachuma (wanatenda) dhambi watalipwa yote waliyokuwa wanayatenda



Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 121

وَلَا تَأۡكُلُواْ مِمَّا لَمۡ يُذۡكَرِ ٱسۡمُ ٱللَّهِ عَلَيۡهِ وَإِنَّهُۥ لَفِسۡقٞۗ وَإِنَّ ٱلشَّيَٰطِينَ لَيُوحُونَ إِلَىٰٓ أَوۡلِيَآئِهِمۡ لِيُجَٰدِلُوكُمۡۖ وَإِنۡ أَطَعۡتُمُوهُمۡ إِنَّكُمۡ لَمُشۡرِكُونَ

Na msile (nyama ya mnyama) ambaye halikutajwa jina la Allah juu yake (wakati wa kuchinjwa), na hakika hilo (la kula nyama ya mnyama ambaye hakuchinjwa kwa taratibu za Kiislamu) ni uasi. Na hakika, mashetani wanatia ushawishi kwa marafiki zao (wa kibinadamu) ili wajadiliane nanyi (katika ulaji wa nyama ya mnyama asiyechinjwa kwa taratibu za Kiislamu). Na kama mkiwatii (katika kuhalalisha nyama ya mnyama asiyechinjwa kwa taratibu za Kiislamu) kwa hakika kabisa nyinyi ni washirikina (makafiri)



Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 122

أَوَمَن كَانَ مَيۡتٗا فَأَحۡيَيۡنَٰهُ وَجَعَلۡنَا لَهُۥ نُورٗا يَمۡشِي بِهِۦ فِي ٱلنَّاسِ كَمَن مَّثَلُهُۥ فِي ٱلظُّلُمَٰتِ لَيۡسَ بِخَارِجٖ مِّنۡهَاۚ كَذَٰلِكَ زُيِّنَ لِلۡكَٰفِرِينَ مَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ

Hivi aliyekuwa maiti, kisha tukampa uhai na tukamjaalia nuru ambayo anatembea nayo kati ya watu; (hivi) mfano wake atakuwa sawa na aliye gizani (ambaye) si mwenye kutoka humo? Kama hivyo tumewapambia makafiri yale waliyokuwa wanayatenda



Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 123

وَكَذَٰلِكَ جَعَلۡنَا فِي كُلِّ قَرۡيَةٍ أَكَٰبِرَ مُجۡرِمِيهَا لِيَمۡكُرُواْ فِيهَاۖ وَمَا يَمۡكُرُونَ إِلَّا بِأَنفُسِهِمۡ وَمَا يَشۡعُرُونَ

Na kama hivyo tumejaalia katika kila mji wauovu wake wakubwa ili wafanye vitimbi humo. Na hawafanyi vitimbi isipokuwa tu wanajifanyia wao wenyewe na hawatambui



Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 124

وَإِذَا جَآءَتۡهُمۡ ءَايَةٞ قَالُواْ لَن نُّؤۡمِنَ حَتَّىٰ نُؤۡتَىٰ مِثۡلَ مَآ أُوتِيَ رُسُلُ ٱللَّهِۘ ٱللَّهُ أَعۡلَمُ حَيۡثُ يَجۡعَلُ رِسَالَتَهُۥۗ سَيُصِيبُ ٱلَّذِينَ أَجۡرَمُواْ صَغَارٌ عِندَ ٱللَّهِ وَعَذَابٞ شَدِيدُۢ بِمَا كَانُواْ يَمۡكُرُونَ

Na inapowajia Aya yoyote, wanasema: Hatutaamini mpaka tupewe mfano wa yale waliyoopewa Mitume wa Allah. Allah ndiye ajuae zaidi mahali anapoweka Ujumbe wake. Wale waliotenda maovu utawapata udhalili na adhabu kali mbele ya Allah kwa sababu ya vitimbi walivyokuwa wakivifanya



Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 125

فَمَن يُرِدِ ٱللَّهُ أَن يَهۡدِيَهُۥ يَشۡرَحۡ صَدۡرَهُۥ لِلۡإِسۡلَٰمِۖ وَمَن يُرِدۡ أَن يُضِلَّهُۥ يَجۡعَلۡ صَدۡرَهُۥ ضَيِّقًا حَرَجٗا كَأَنَّمَا يَصَّعَّدُ فِي ٱلسَّمَآءِۚ كَذَٰلِكَ يَجۡعَلُ ٱللَّهُ ٱلرِّجۡسَ عَلَى ٱلَّذِينَ لَا يُؤۡمِنُونَ

Basi yeyote ambaye Allah anataka kumuongoa anakunjua moyo wake kwa ajili ya (kuukubali) Uislamu. Na yeyote ambaye (Allah) anataka apotoke, anaufanya moyo wake finyu, uliokosa raha kana kwamba anakwea angani. Kama hivyo Allah anawawekea adhabu wasioamini



Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 126

وَهَٰذَا صِرَٰطُ رَبِّكَ مُسۡتَقِيمٗاۗ قَدۡ فَصَّلۡنَا ٱلۡأٓيَٰتِ لِقَوۡمٖ يَذَّكَّرُونَ

Na hii ni njia ya Mola wako Mlezi ikiwa imenyooka. Hakika, tumezifafanua Aya (hoja mbalimbali) kwa watu wanaokumbuka



Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 127

۞لَهُمۡ دَارُ ٱلسَّلَٰمِ عِندَ رَبِّهِمۡۖ وَهُوَ وَلِيُّهُم بِمَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ

Wana nyumba ya amani kwa Mola wao Mlezi, na yeye ndiye Mlinzi wao kwa sababu ya yote waliyokuwa wanayafanya



Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 128

وَيَوۡمَ يَحۡشُرُهُمۡ جَمِيعٗا يَٰمَعۡشَرَ ٱلۡجِنِّ قَدِ ٱسۡتَكۡثَرۡتُم مِّنَ ٱلۡإِنسِۖ وَقَالَ أَوۡلِيَآؤُهُم مِّنَ ٱلۡإِنسِ رَبَّنَا ٱسۡتَمۡتَعَ بَعۡضُنَا بِبَعۡضٖ وَبَلَغۡنَآ أَجَلَنَا ٱلَّذِيٓ أَجَّلۡتَ لَنَاۚ قَالَ ٱلنَّارُ مَثۡوَىٰكُمۡ خَٰلِدِينَ فِيهَآ إِلَّا مَا شَآءَ ٱللَّهُۚ إِنَّ رَبَّكَ حَكِيمٌ عَلِيمٞ

Na (kumbuka) Siku Allah atakapowakusanya wote (na kuwaambia): Enyi jamii ya majini, mmewapotosha sana wanadamu wengi. Na watasema marafiki zao wa kibinadamu kwamba: Ewe Mola wetu Mlezi, walistarehe (walifaidika)[1] baadhi yetu kwa wengine, na tumeufikia muda wetu ambao umetupangia. (Allah) Atasema: Moto ndio mafikio yenu, mtaishi humo milele isipokuwa tu Allah akipenda (mtoke). Hakika, Mola wako Mlezi ni Mwenye hekima, Mjuzi sana


1- - Maana hapa ni kwamba, majini na binadamu kila mmoja amefaidika kwa mwenzake kwa namna mbali mbali, kama hali ilivyo kwa wanaojihusisha na ulimwengu wa uchawi.


Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 129

وَكَذَٰلِكَ نُوَلِّي بَعۡضَ ٱلظَّـٰلِمِينَ بَعۡضَۢا بِمَا كَانُواْ يَكۡسِبُونَ

Na kama hivyo tunawafanya baadhi ya madhalimu wawapende madhalimu wenzao kwa sababu ya yale waliyokuwa wakiyachuma (wakiyafanya)



Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 130

يَٰمَعۡشَرَ ٱلۡجِنِّ وَٱلۡإِنسِ أَلَمۡ يَأۡتِكُمۡ رُسُلٞ مِّنكُمۡ يَقُصُّونَ عَلَيۡكُمۡ ءَايَٰتِي وَيُنذِرُونَكُمۡ لِقَآءَ يَوۡمِكُمۡ هَٰذَاۚ قَالُواْ شَهِدۡنَا عَلَىٰٓ أَنفُسِنَاۖ وَغَرَّتۡهُمُ ٱلۡحَيَوٰةُ ٱلدُّنۡيَا وَشَهِدُواْ عَلَىٰٓ أَنفُسِهِمۡ أَنَّهُمۡ كَانُواْ كَٰفِرِينَ

Enyi jamii ya majini na watu, hivi hawakukujieni Mitume watokanao na nyinyi wakikusomeeni Aya zangu na kukuonyeni (kuhusu) kukutana na siku yenu hii? Watasema: Tumejishuhudia wenyewe. Na maisha ya dunia yamewadanganya na wamejishuhudia wenyewe kwamba walikuwa makafiri



Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 131

ذَٰلِكَ أَن لَّمۡ يَكُن رَّبُّكَ مُهۡلِكَ ٱلۡقُرَىٰ بِظُلۡمٖ وَأَهۡلُهَا غَٰفِلُونَ

Hilo (la kuwapelekea watu Mitume) ni kwa sababu Mola wako si Mwenye kuangamiza miji kwa dhuluma na ilhali watu wake wakiwa wameghafilika (hawajui chochote)



Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 132

وَلِكُلّٖ دَرَجَٰتٞ مِّمَّا عَمِلُواْۚ وَمَا رَبُّكَ بِغَٰفِلٍ عَمَّا يَعۡمَلُونَ

Na wote miongoni mwao (majini na binadamu) wana madaraja kutokana na waliyoyatenda, na Mola wako si Mwenye kughafilika na yote wanayotenda



Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 133

وَرَبُّكَ ٱلۡغَنِيُّ ذُو ٱلرَّحۡمَةِۚ إِن يَشَأۡ يُذۡهِبۡكُمۡ وَيَسۡتَخۡلِفۡ مِنۢ بَعۡدِكُم مَّا يَشَآءُ كَمَآ أَنشَأَكُم مِّن ذُرِّيَّةِ قَوۡمٍ ءَاخَرِينَ

Na Mola wako Mlezi ni Mkwasi, Mwenye rehema. Akitaka atakuondoeni na kuwaweka wengine awatakao kuwa badala yenu baada yenu kama vile alivyokuumbeni nyinyi kutoka katika kizazi cha watu wengine



Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 134

إِنَّ مَا تُوعَدُونَ لَأٓتٖۖ وَمَآ أَنتُم بِمُعۡجِزِينَ

Hakika kabisa, mnayo ahidiwa (na Mola wenu) yanakuja, na nyinyi hamtashinda



Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 135

قُلۡ يَٰقَوۡمِ ٱعۡمَلُواْ عَلَىٰ مَكَانَتِكُمۡ إِنِّي عَامِلٞۖ فَسَوۡفَ تَعۡلَمُونَ مَن تَكُونُ لَهُۥ عَٰقِبَةُ ٱلدَّارِۚ إِنَّهُۥ لَا يُفۡلِحُ ٱلظَّـٰلِمُونَ

Sema: Enyi watu wangu, tendeni kwa kadri ya uwezo wenu. Hakika, mimi ninatenda. Punde tu mtajua ni nani atakuwa na makazi bora mwishoni. Hakika, ilivyo ni kwamba madhalimu hawatafaulu



Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 136

وَجَعَلُواْ لِلَّهِ مِمَّا ذَرَأَ مِنَ ٱلۡحَرۡثِ وَٱلۡأَنۡعَٰمِ نَصِيبٗا فَقَالُواْ هَٰذَا لِلَّهِ بِزَعۡمِهِمۡ وَهَٰذَا لِشُرَكَآئِنَاۖ فَمَا كَانَ لِشُرَكَآئِهِمۡ فَلَا يَصِلُ إِلَى ٱللَّهِۖ وَمَا كَانَ لِلَّهِ فَهُوَ يَصِلُ إِلَىٰ شُرَكَآئِهِمۡۗ سَآءَ مَا يَحۡكُمُونَ

Na wamemfanyia Allah fungu katika mimea na wanyama aliowaumba, na kusema: Hiki ni kwa ajili ya Allah, kwa madai yao tu, na hiki ni kwa ajili ya washirika wetu. Basi kilichokuwa cha washirika wao hakifiki kwa Allah na kilichokuwa cha Allah kinafika kwa washirika wao. Ni mabaya mno (haya) wanayoyahukumu



Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 137

وَكَذَٰلِكَ زَيَّنَ لِكَثِيرٖ مِّنَ ٱلۡمُشۡرِكِينَ قَتۡلَ أَوۡلَٰدِهِمۡ شُرَكَآؤُهُمۡ لِيُرۡدُوهُمۡ وَلِيَلۡبِسُواْ عَلَيۡهِمۡ دِينَهُمۡۖ وَلَوۡ شَآءَ ٱللَّهُ مَا فَعَلُوهُۖ فَذَرۡهُمۡ وَمَا يَفۡتَرُونَ

Na kama hivyo washirikina wengi wa wamepambiwa na washirika wao kuua watoto wao ili wawaangamize na ili wawavurugie dini yao. Na lau kama Allah angetaka wasingefanya hayo. Basi waache na hayo wanayoyazua



Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 138

وَقَالُواْ هَٰذِهِۦٓ أَنۡعَٰمٞ وَحَرۡثٌ حِجۡرٞ لَّا يَطۡعَمُهَآ إِلَّا مَن نَّشَآءُ بِزَعۡمِهِمۡ وَأَنۡعَٰمٌ حُرِّمَتۡ ظُهُورُهَا وَأَنۡعَٰمٞ لَّا يَذۡكُرُونَ ٱسۡمَ ٱللَّهِ عَلَيۡهَا ٱفۡتِرَآءً عَلَيۡهِۚ سَيَجۡزِيهِم بِمَا كَانُواْ يَفۡتَرُونَ

Na wamesema: Wanyama hawa na mimea hii ni marufuku; hawavili (hivyo) isipokuwa tu tuwapendao, kwa madai yao. Na wanyama wengine wameharamishiwa migongo yao (kuwapanda na kuwabebesha mizigo), na wanyama wengine hawawasomei jina la Allah (wakati wa kuwachinja) kwa kumzulia uongo (Allah). (Allah) Atawalipa kwa yote waliyokuwa wakiyazusha



Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 139

وَقَالُواْ مَا فِي بُطُونِ هَٰذِهِ ٱلۡأَنۡعَٰمِ خَالِصَةٞ لِّذُكُورِنَا وَمُحَرَّمٌ عَلَىٰٓ أَزۡوَٰجِنَاۖ وَإِن يَكُن مَّيۡتَةٗ فَهُمۡ فِيهِ شُرَكَآءُۚ سَيَجۡزِيهِمۡ وَصۡفَهُمۡۚ إِنَّهُۥ حَكِيمٌ عَلِيمٞ

Na (Washirikina) wamesema: Vilivyomo ndani ya matumbo ya wanyama hawa (mimba zao) ni mahususi (halali) kwa wanaume wetu na ni haramu kwa wake zetu. Na kama (Wanyama hao) wakiwa wamekufa (nyamafu) basi wao ni washirika kwenye hilo (ni halali kwa wake na waume). (Allah) Atawalipa wasifu wao (wanaoustahiki). Hakika yeye (Allah) ni Mwenye hekima, Mjuzi mno



Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 140

قَدۡ خَسِرَ ٱلَّذِينَ قَتَلُوٓاْ أَوۡلَٰدَهُمۡ سَفَهَۢا بِغَيۡرِ عِلۡمٖ وَحَرَّمُواْ مَا رَزَقَهُمُ ٱللَّهُ ٱفۡتِرَآءً عَلَى ٱللَّهِۚ قَدۡ ضَلُّواْ وَمَا كَانُواْ مُهۡتَدِينَ

Hakika, wamepata hasara wale waliowaua watoto wao kwa upumbavu bila ya kujua na wameharamisha alichowaruzuku Allah kwa kumzushia Allah uongo. Kwa hakika, wamepotea na hawakuwa wenye kuongoka