Sourate: YUSUF 

Verset : 53

۞وَمَآ أُبَرِّئُ نَفۡسِيٓۚ إِنَّ ٱلنَّفۡسَ لَأَمَّارَةُۢ بِٱلسُّوٓءِ إِلَّا مَا رَحِمَ رَبِّيٓۚ إِنَّ رَبِّي غَفُورٞ رَّحِيمٞ

(Yusuf aliendelea kusema) Nami siisafishi nafsi yangu (sijitoi lawamani). Kwa hakika nafsi inaamrisha mno maovu, isipokuwa ile tu aliyoirehemu Mola wangu Mlezi. Hakika, Mola wangu Mlezi ni Msamehevu, mwingi wa rehema



Sourate: YUSUF 

Verset : 54

وَقَالَ ٱلۡمَلِكُ ٱئۡتُونِي بِهِۦٓ أَسۡتَخۡلِصۡهُ لِنَفۡسِيۖ فَلَمَّا كَلَّمَهُۥ قَالَ إِنَّكَ ٱلۡيَوۡمَ لَدَيۡنَا مَكِينٌ أَمِينٞ

Na mfalme alisema: Nileteeni, awe msaidizi wangu binafsi. Basi (mfalme) alipomsemeza (Yusuf alibaini kipawa chake na) alinena: Hakika wewe leo umemakinika kwetu na umeaminika



Sourate: YUSUF 

Verset : 55

قَالَ ٱجۡعَلۡنِي عَلَىٰ خَزَآئِنِ ٱلۡأَرۡضِۖ إِنِّي حَفِيظٌ عَلِيمٞ

(Yusuf) Alisema: Nifanye mtunza hazina za nchi. Kwani hakika mimi ni (mshika hazina) mlinzi mahiri sana, mjuzi sana



Sourate: YUSUF 

Verset : 56

وَكَذَٰلِكَ مَكَّنَّا لِيُوسُفَ فِي ٱلۡأَرۡضِ يَتَبَوَّأُ مِنۡهَا حَيۡثُ يَشَآءُۚ نُصِيبُ بِرَحۡمَتِنَا مَن نَّشَآءُۖ وَلَا نُضِيعُ أَجۡرَ ٱلۡمُحۡسِنِينَ

Na kama hivyo tulimmakinisha Yusuf (na kumpa cheo katika nchi); akawa anakaa humo popote anapopenda. Tunamfikishia rehema zetu tumtakaye, na hatupotezi malipo ya wafanyao mazuri



Sourate: YUSUF 

Verset : 57

وَلَأَجۡرُ ٱلۡأٓخِرَةِ خَيۡرٞ لِّلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَكَانُواْ يَتَّقُونَ

Na kwa hakika kabisa, malipo ya Akhera ni bora zaidi kwa walioamini na wakawa wanamcha Allah



Sourate: YUSUF 

Verset : 58

وَجَآءَ إِخۡوَةُ يُوسُفَ فَدَخَلُواْ عَلَيۡهِ فَعَرَفَهُمۡ وَهُمۡ لَهُۥ مُنكِرُونَ

Na walikuja (wale) ndugu wa Yusuf na wakaingia kwake; akawajua na wao hawakumjua



Sourate: YUSUF 

Verset : 59

وَلَمَّا جَهَّزَهُم بِجَهَازِهِمۡ قَالَ ٱئۡتُونِي بِأَخٖ لَّكُم مِّنۡ أَبِيكُمۡۚ أَلَا تَرَوۡنَ أَنِّيٓ أُوفِي ٱلۡكَيۡلَ وَأَنَا۠ خَيۡرُ ٱلۡمُنزِلِينَ

Na alipowatimizia mahitaji yao (ya shehena ya chakula) alisema: (mtakapokuja mara nyingine) Nileteeni ndugu yenu kwa (upande wa) Baba yenu. Je, hamuoni ya kwamba mimi ninatimiza kipimo, nami ni mbora wa wakarimu?



Sourate: YUSUF 

Verset : 60

فَإِن لَّمۡ تَأۡتُونِي بِهِۦ فَلَا كَيۡلَ لَكُمۡ عِندِي وَلَا تَقۡرَبُونِ

Na msiponiletea (ndugu yenu wa Baba mmoja) basi (mjue) hampati kipimo chochote kwangu na wala msinisogelee



Sourate: YUSUF 

Verset : 61

قَالُواْ سَنُرَٰوِدُ عَنۡهُ أَبَاهُ وَإِنَّا لَفَٰعِلُونَ

Walisema: Sisi tutamuengaenga (tutamrai) Baba yake na tutahakikisha tunafanya hivyo



Sourate: YUSUF 

Verset : 62

وَقَالَ لِفِتۡيَٰنِهِ ٱجۡعَلُواْ بِضَٰعَتَهُمۡ فِي رِحَالِهِمۡ لَعَلَّهُمۡ يَعۡرِفُونَهَآ إِذَا ٱنقَلَبُوٓاْ إِلَىٰٓ أَهۡلِهِمۡ لَعَلَّهُمۡ يَرۡجِعُونَ

Na (Yusuf) aliwaambia vijana wake: Ziwekeni bidhaa zao katika mizigo yao ili wazione watakaporudi kwa watu wao ili wapate (hamu ya) kurejea tena



Sourate: YUSUF 

Verset : 63

فَلَمَّا رَجَعُوٓاْ إِلَىٰٓ أَبِيهِمۡ قَالُواْ يَـٰٓأَبَانَا مُنِعَ مِنَّا ٱلۡكَيۡلُ فَأَرۡسِلۡ مَعَنَآ أَخَانَا نَكۡتَلۡ وَإِنَّا لَهُۥ لَحَٰفِظُونَ

Basi waliporejea kwa Baba yao, walisema: Ewe Baba yetu, tumezuiwa kupimiwa (tosha yetu siku zijazo tusipoenda na ndugu yetu). Basi (tunaomba tukienda tena) mruhusu ndugu yetu aende nasi ili tukapate kupimiwa (mahitaji yetu) na kwa yakini kabisa sisi (tunaahidi) tutamlinda



Sourate: YUSUF 

Verset : 64

قَالَ هَلۡ ءَامَنُكُمۡ عَلَيۡهِ إِلَّا كَمَآ أَمِنتُكُمۡ عَلَىٰٓ أَخِيهِ مِن قَبۡلُ فَٱللَّهُ خَيۡرٌ حَٰفِظٗاۖ وَهُوَ أَرۡحَمُ ٱلرَّـٰحِمِينَ

(Yakub) Alisema: Je, niwaaminini kwa huyu kama nilivyokuaminini kwa nduguye zamani? Basi Allah ndiye mbora wa kulinda, naye ndiye Mbora wa kuhurumia kuliko wahurumiaji wote



Sourate: YUSUF 

Verset : 65

وَلَمَّا فَتَحُواْ مَتَٰعَهُمۡ وَجَدُواْ بِضَٰعَتَهُمۡ رُدَّتۡ إِلَيۡهِمۡۖ قَالُواْ يَـٰٓأَبَانَا مَا نَبۡغِيۖ هَٰذِهِۦ بِضَٰعَتُنَا رُدَّتۡ إِلَيۡنَاۖ وَنَمِيرُ أَهۡلَنَا وَنَحۡفَظُ أَخَانَا وَنَزۡدَادُ كَيۡلَ بَعِيرٖۖ ذَٰلِكَ كَيۡلٞ يَسِيرٞ

Na walipofungua mizigo yao walikuta wamerudishiwa bidhaa zao. Walisema: Ewe Baba yetu, tutake nini (tena zaidi ya ukarimu huu)? Hizi hapa bidhaa zetu tumerudishiwa. Acha tuwaletee watu wetu chakula na tutamlinda ndugu yetu na tutaongeza shehena ya ngamia. Hicho (tulichopewa) ni kipimo kidogo mno (ukilinganisha na utajiri wa mfalme)



Sourate: YUSUF 

Verset : 66

قَالَ لَنۡ أُرۡسِلَهُۥ مَعَكُمۡ حَتَّىٰ تُؤۡتُونِ مَوۡثِقٗا مِّنَ ٱللَّهِ لَتَأۡتُنَّنِي بِهِۦٓ إِلَّآ أَن يُحَاطَ بِكُمۡۖ فَلَمَّآ ءَاتَوۡهُ مَوۡثِقَهُمۡ قَالَ ٱللَّهُ عَلَىٰ مَا نَقُولُ وَكِيلٞ

(Yakubu) Alisema: Katu sitamruhusu (aende) nanyi mpaka mnipe ahadi nzito kwa Allah kwamba lazima mtanirudishia (mtarudi naye), ila ikiwa mmezungukwa (mmezidiwa nguvu kwa jambo lililo nje ya uwezo wenu). Basi walipompa ahadi yao alisema: Allah kwa tuyasemayo ndiye Mtegemewa



Sourate: YUSUF 

Verset : 67

وَقَالَ يَٰبَنِيَّ لَا تَدۡخُلُواْ مِنۢ بَابٖ وَٰحِدٖ وَٱدۡخُلُواْ مِنۡ أَبۡوَٰبٖ مُّتَفَرِّقَةٖۖ وَمَآ أُغۡنِي عَنكُم مِّنَ ٱللَّهِ مِن شَيۡءٍۖ إِنِ ٱلۡحُكۡمُ إِلَّا لِلَّهِۖ عَلَيۡهِ تَوَكَّلۡتُۖ وَعَلَيۡهِ فَلۡيَتَوَكَّلِ ٱلۡمُتَوَكِّلُونَ

Na alisema: Enyi wanangu, msiingie (Misri) kupitia mlango mmoja, bali ingieni kwa kupitia milango mbali mbali. Na mimi sikufaeni kitu chochote mbele ya Allah. Hakuna hukumu isipokuwa ya Allah tu, yeye tu nimemtegemea na yeye tu wamtegemee wenye kutegemea



Sourate: YUSUF 

Verset : 68

وَلَمَّا دَخَلُواْ مِنۡ حَيۡثُ أَمَرَهُمۡ أَبُوهُم مَّا كَانَ يُغۡنِي عَنۡهُم مِّنَ ٱللَّهِ مِن شَيۡءٍ إِلَّا حَاجَةٗ فِي نَفۡسِ يَعۡقُوبَ قَضَىٰهَاۚ وَإِنَّهُۥ لَذُو عِلۡمٖ لِّمَا عَلَّمۡنَٰهُ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يَعۡلَمُونَ

Na walipoingia (kwa tahadhari) kama Baba yao alivyowaamrisha hakuna kitu chochote kilichowafaa kwa Allah, isipokuwa tu haja (huruma) iliyokuwemo katika nafsi ya Yakubu aliyoitimiza (kwa kuwaambia wanawe wawe na tahadhari). Na hakika kabisa yeye (Yakubu) ni mwenye kuyajua tuliyomfundisha lakini watu wengi hawajui[1]


1- - Watu wengi sana hawajui siri ya kadari na kwamba, kuchukua tahadhari hakupingani na kutawakali na kumtegemea Allah.


Sourate: YUSUF 

Verset : 69

وَلَمَّا دَخَلُواْ عَلَىٰ يُوسُفَ ءَاوَىٰٓ إِلَيۡهِ أَخَاهُۖ قَالَ إِنِّيٓ أَنَا۠ أَخُوكَ فَلَا تَبۡتَئِسۡ بِمَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ

Na walipoingia kwa Yusuf alimvuta (alimchukua) ndugu yake (huku) akisema (naye kwa siri): “Hakika, mimi ni ndugu yako. Kwa hiyo, usihuzunike kwa yale waliyokuwa wanayafanya”



Sourate: YUSUF 

Verset : 70

فَلَمَّا جَهَّزَهُم بِجَهَازِهِمۡ جَعَلَ ٱلسِّقَايَةَ فِي رَحۡلِ أَخِيهِ ثُمَّ أَذَّنَ مُؤَذِّنٌ أَيَّتُهَا ٱلۡعِيرُ إِنَّكُمۡ لَسَٰرِقُونَ

Basi alipowaandalia mahitaji yao aliliweka (kwa siri) bakuli katika mzigo wa ndugu yake, kisha mtangazaji akatangaza: Enyi wasafiri, kwa hakika kabisa, nyinyi ni wezi!



Sourate: YUSUF 

Verset : 71

قَالُواْ وَأَقۡبَلُواْ عَلَيۡهِم مَّاذَا تَفۡقِدُونَ

Walisema na huku wakiwaelekea (waliokuwa wakitangaza kwamba): Kwani mmepotelewa na nini?



Sourate: YUSUF 

Verset : 72

قَالُواْ نَفۡقِدُ صُوَاعَ ٱلۡمَلِكِ وَلِمَن جَآءَ بِهِۦ حِمۡلُ بَعِيرٖ وَأَنَا۠ بِهِۦ زَعِيمٞ

Walisema: Tumepoteza bakuli la mfalme. Na atakayelileta atapewa shehena nzima ya ngamia na mimi ni mdhamini wa hilo



Sourate: YUSUF 

Verset : 73

قَالُواْ تَٱللَّهِ لَقَدۡ عَلِمۡتُم مَّا جِئۡنَا لِنُفۡسِدَ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَمَا كُنَّا سَٰرِقِينَ

Walisema: Tuna apa kwa Allah kwamba, kwa hakika kabisa, nyinyi mmejua fika kwamba sisi hatukuja kufanya uharibifu katika nchi (hii) na sisi sio wezi



Sourate: YUSUF 

Verset : 74

قَالُواْ فَمَا جَزَـٰٓؤُهُۥٓ إِن كُنتُمۡ كَٰذِبِينَ

Walisema: Basi malipo (adhabu) yake (huyo mwizi) ni nini ikiwa nyinyi ni waongo?



Sourate: YUSUF 

Verset : 75

قَالُواْ جَزَـٰٓؤُهُۥ مَن وُجِدَ فِي رَحۡلِهِۦ فَهُوَ جَزَـٰٓؤُهُۥۚ كَذَٰلِكَ نَجۡزِي ٱلظَّـٰلِمِينَ

Walisema: Malipo (adhabu) yake (ni kufanywa mtumwa wa aliyeibiwa) yule ambaye bakuli limekutwa katika mizigo yake. Hiyo ndio adhabu yake. Hivi ndivyo tunavyowalipa madhalimu



Sourate: YUSUF 

Verset : 76

فَبَدَأَ بِأَوۡعِيَتِهِمۡ قَبۡلَ وِعَآءِ أَخِيهِ ثُمَّ ٱسۡتَخۡرَجَهَا مِن وِعَآءِ أَخِيهِۚ كَذَٰلِكَ كِدۡنَا لِيُوسُفَۖ مَا كَانَ لِيَأۡخُذَ أَخَاهُ فِي دِينِ ٱلۡمَلِكِ إِلَّآ أَن يَشَآءَ ٱللَّهُۚ نَرۡفَعُ دَرَجَٰتٖ مَّن نَّشَآءُۗ وَفَوۡقَ كُلِّ ذِي عِلۡمٍ عَلِيمٞ

Basi (Yule mpekuzi) alianza kwenye mizigo yao kabla ya mzigo wa ndugu yake. Kisha alilitoa (bakuli lililoibwa) kutoka katika mzigo wa ndugu yake. Hivi ndivyo tulivyomfunza Yusuf mbinu (ya kubaki na nduguye). Asingeweza kumchukua ndugu yake kwa sharia ya mfalme isipokuwa kwa matakwa ya Allah. Tunawainua daraja nyingi tuwatakao na juu ya kila anayejua yupo anayejua zaidi



Sourate: YUSUF 

Verset : 77

۞قَالُوٓاْ إِن يَسۡرِقۡ فَقَدۡ سَرَقَ أَخٞ لَّهُۥ مِن قَبۡلُۚ فَأَسَرَّهَا يُوسُفُ فِي نَفۡسِهِۦ وَلَمۡ يُبۡدِهَا لَهُمۡۚ قَالَ أَنتُمۡ شَرّٞ مَّكَانٗاۖ وَٱللَّهُ أَعۡلَمُ بِمَا تَصِفُونَ

Walisema (ndugu wa Yusuf): Ikiwa (huyu ndiye) ameeiba, basi nduguye vile vile aliiba zamani. Basi Yusuf aliyaweka siri moyoni mwake (maneno ya ndugu zake) na wala hakuwadhihirishia. Aliwaambia: Nyinyi mpo katika hali mbaya zaidi, na Allah anayajua zaidi hayo mnayosingizia



Sourate: YUSUF 

Verset : 78

قَالُواْ يَـٰٓأَيُّهَا ٱلۡعَزِيزُ إِنَّ لَهُۥٓ أَبٗا شَيۡخٗا كَبِيرٗا فَخُذۡ أَحَدَنَا مَكَانَهُۥٓۖ إِنَّا نَرَىٰكَ مِنَ ٱلۡمُحۡسِنِينَ

Walisema (kwa kubembeleza): Ewe Mheshimiwa, huyu ana Baba mzee sana (na anampenda mno mwanawe). Kwa hivyo (tunakuomba) mchukue mmoja wetu badala yake. Hakika sisi tunakuona wewe ni katika wanaotenda mazuri



Sourate: YUSUF 

Verset : 79

قَالَ مَعَاذَ ٱللَّهِ أَن نَّأۡخُذَ إِلَّا مَن وَجَدۡنَا مَتَٰعَنَا عِندَهُۥٓ إِنَّآ إِذٗا لَّظَٰلِمُونَ

(Yusuf) Alisema: Allah apishe mbali (hatuwezi) kumshika yeyote yule isipokuwa tuliyemkuta na kitu chetu. Sisi tukifanya hivyo (mtakavyo) kwa yakini kabisa tutakuwa madhalimu (kwa kufanya uonevu)



Sourate: YUSUF 

Verset : 80

فَلَمَّا ٱسۡتَيۡـَٔسُواْ مِنۡهُ خَلَصُواْ نَجِيّٗاۖ قَالَ كَبِيرُهُمۡ أَلَمۡ تَعۡلَمُوٓاْ أَنَّ أَبَاكُمۡ قَدۡ أَخَذَ عَلَيۡكُم مَّوۡثِقٗا مِّنَ ٱللَّهِ وَمِن قَبۡلُ مَا فَرَّطتُمۡ فِي يُوسُفَۖ فَلَنۡ أَبۡرَحَ ٱلۡأَرۡضَ حَتَّىٰ يَأۡذَنَ لِيٓ أَبِيٓ أَوۡ يَحۡكُمَ ٱللَّهُ لِيۖ وَهُوَ خَيۡرُ ٱلۡحَٰكِمِينَ

Basi walipomkatia tamaa (ndugu yao) walikwenda kando kunong’ona. Mkubwa wao alisema: Je, hamjui (hamkumbuki) kwamba Baba yenu alichukua kwenu ahadi nzito (kiapo cha kumlinda ndugu yenu) kwa Allah, na kabla ya hapo mlifanya uzembe kwa Yusuf? Basi mimi siondoki nchi hii mpaka Baba yangu anipe ruhusa au Allah anihukumie na Yeye (Allah) ndiye Mbora wa mahakimu



Sourate: YUSUF 

Verset : 81

ٱرۡجِعُوٓاْ إِلَىٰٓ أَبِيكُمۡ فَقُولُواْ يَـٰٓأَبَانَآ إِنَّ ٱبۡنَكَ سَرَقَ وَمَا شَهِدۡنَآ إِلَّا بِمَا عَلِمۡنَا وَمَا كُنَّا لِلۡغَيۡبِ حَٰفِظِينَ

Rudini kwa Baba yenu, na mwambieni: Ewe Baba yetu, kwa hakika mwanao ameiba (bakuli la mfalme) na sisi hatukushuhudia (wizi huo) ila kwa tulichokijua (kwa kuona kwa macho yetu bakuli likitolewa kwenye mzigo wake) na sisi hatukuwa watunzaji wa (mambo) ya Ghaibu (hata tujue kuwa ndugu yetu ataiba)



Sourate: YUSUF 

Verset : 82

وَسۡـَٔلِ ٱلۡقَرۡيَةَ ٱلَّتِي كُنَّا فِيهَا وَٱلۡعِيرَ ٱلَّتِيٓ أَقۡبَلۡنَا فِيهَاۖ وَإِنَّا لَصَٰدِقُونَ

Na waulize (watu wa) mji tuliokuwepo na msafara tuliokuja nao, na kwa hakika kabisa sisi ni wasema kweli