Sourate: AL-AARAAF 

Verset : 66

قَالَ ٱلۡمَلَأُ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ مِن قَوۡمِهِۦٓ إِنَّا لَنَرَىٰكَ فِي سَفَاهَةٖ وَإِنَّا لَنَظُنُّكَ مِنَ ٱلۡكَٰذِبِينَ

Mamwinyi ambao wamekufuru katika watu wake wakasema: Kwa hakika, sisi tunakuona umo katika upumbavu na kwa hakika kabisa tunakudhania (tuna wasiwasi nawe) kuwa wewe ni miongoni mwa waongo



Sourate: AL-AARAAF 

Verset : 67

قَالَ يَٰقَوۡمِ لَيۡسَ بِي سَفَاهَةٞ وَلَٰكِنِّي رَسُولٞ مِّن رَّبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ

(Mtume Nuhu) Akasema: Enyi watu wangu, mimi sina upumbavu wowote, lakini mimi ni Mtume niliyetoka kwa Mola wa walimwengu



Sourate: AL-AARAAF 

Verset : 68

أُبَلِّغُكُمۡ رِسَٰلَٰتِ رَبِّي وَأَنَا۠ لَكُمۡ نَاصِحٌ أَمِينٌ

Ninakufikishieni ujumbe wa Mola wangu, na mimi kwenu ni mtoaji nasaha, muaminifu sana



Sourate: AL-AARAAF 

Verset : 69

أَوَعَجِبۡتُمۡ أَن جَآءَكُمۡ ذِكۡرٞ مِّن رَّبِّكُمۡ عَلَىٰ رَجُلٖ مِّنكُمۡ لِيُنذِرَكُمۡۚ وَٱذۡكُرُوٓاْ إِذۡ جَعَلَكُمۡ خُلَفَآءَ مِنۢ بَعۡدِ قَوۡمِ نُوحٖ وَزَادَكُمۡ فِي ٱلۡخَلۡقِ بَصۜۡطَةٗۖ فَٱذۡكُرُوٓاْ ءَالَآءَ ٱللَّهِ لَعَلَّكُمۡ تُفۡلِحُونَ

Hivi mmestaajabu kwa kukufikieni ukumbusho kutoka kwa Mola wenu Mlezi kupitia kwa mtu miongoni mwenu ili akuonyeni? Na kumbukeni alivyokufanyeni makhalifa (warithi) baada ya watu wa Nuhu, na akakuongezeeni umbo kubwa. Basi zikumbukeni neema za Allah ili mfaulu



Sourate: AL-AARAAF 

Verset : 70

قَالُوٓاْ أَجِئۡتَنَا لِنَعۡبُدَ ٱللَّهَ وَحۡدَهُۥ وَنَذَرَ مَا كَانَ يَعۡبُدُ ءَابَآؤُنَا فَأۡتِنَا بِمَا تَعِدُنَآ إِن كُنتَ مِنَ ٱلصَّـٰدِقِينَ

Wakasema: Hivi umetujia kwa ajili ya kuwa tumuabudu Allah peke yake na tuache (Miungu) wote ambao baba zetu walikuwa wanawaabudu? Basi tuletee (hayo) unayotuahidi ukiwa unasema kweli



Sourate: AL-AARAAF 

Verset : 71

قَالَ قَدۡ وَقَعَ عَلَيۡكُم مِّن رَّبِّكُمۡ رِجۡسٞ وَغَضَبٌۖ أَتُجَٰدِلُونَنِي فِيٓ أَسۡمَآءٖ سَمَّيۡتُمُوهَآ أَنتُمۡ وَءَابَآؤُكُم مَّا نَزَّلَ ٱللَّهُ بِهَا مِن سُلۡطَٰنٖۚ فَٱنتَظِرُوٓاْ إِنِّي مَعَكُم مِّنَ ٱلۡمُنتَظِرِينَ

Akasema: Hakika, imekwisha kufikeni adhabu na ghadhabu kutoka kwa Mola wenu. Hivi mnajadiliana nami katika majina mliyoyataja (mliyoyazusha) nyinyi na baba zenu na Allah hakuteremsha dalili kuhusiana nayo? Basi ngojeeni na mimi pamoja nanyi ni miongoni mwa wenye kungojea



Sourate: AL-AARAAF 

Verset : 72

فَأَنجَيۡنَٰهُ وَٱلَّذِينَ مَعَهُۥ بِرَحۡمَةٖ مِّنَّا وَقَطَعۡنَا دَابِرَ ٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَاۖ وَمَا كَانُواْ مُؤۡمِنِينَ

Basi tukamuokoa yeye na wale waliokuwa pamoja naye kwa rehema zetu, na tukakata mzizi wa wale waliozikadhibisha Aya zetu na hawakuwa waumini



Sourate: AL-AARAAF 

Verset : 73

وَإِلَىٰ ثَمُودَ أَخَاهُمۡ صَٰلِحٗاۚ قَالَ يَٰقَوۡمِ ٱعۡبُدُواْ ٱللَّهَ مَا لَكُم مِّنۡ إِلَٰهٍ غَيۡرُهُۥۖ قَدۡ جَآءَتۡكُم بَيِّنَةٞ مِّن رَّبِّكُمۡۖ هَٰذِهِۦ نَاقَةُ ٱللَّهِ لَكُمۡ ءَايَةٗۖ فَذَرُوهَا تَأۡكُلۡ فِيٓ أَرۡضِ ٱللَّهِۖ وَلَا تَمَسُّوهَا بِسُوٓءٖ فَيَأۡخُذَكُمۡ عَذَابٌ أَلِيمٞ

Na (tulimtuma) kwa (kabila la) Thamudi ndugu yao Swalehe akasema: Enyi watu wangu, muabuduni Allah, hamna nyinyi Mola mwingine Mlezi zaidi yake. Hakika, umekufikieni ushahidi (muujiza unaothibitisha ukweli wangu) kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Huyu ni ngamia wa Allah akiwa ushahidi kwenu. Basi mwacheni ale katika ardhi ya Allah, na msimguse kwa ubaya wowote ikawa sababu ya kukuchukueni (kukupateni) adhabu iumizayo sana



Sourate: AL-AARAAF 

Verset : 74

وَٱذۡكُرُوٓاْ إِذۡ جَعَلَكُمۡ خُلَفَآءَ مِنۢ بَعۡدِ عَادٖ وَبَوَّأَكُمۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ تَتَّخِذُونَ مِن سُهُولِهَا قُصُورٗا وَتَنۡحِتُونَ ٱلۡجِبَالَ بُيُوتٗاۖ فَٱذۡكُرُوٓاْ ءَالَآءَ ٱللَّهِ وَلَا تَعۡثَوۡاْ فِي ٱلۡأَرۡضِ مُفۡسِدِينَ

Na kumbukeni wakati (Allah) alipokufanyeni makhalifa (warithi) baada ya (watu wa) Adi na akakuwekeni vizuri ardhini; mnajenga makasri (majumba ya kifahari) katika eneo lake la tambarare, na mnachonga majabali na kuyafanya majumba. Basi kumbukeni neema za Allah, na msifanye uovu ardhini (duniani)



Sourate: AL-AARAAF 

Verset : 75

قَالَ ٱلۡمَلَأُ ٱلَّذِينَ ٱسۡتَكۡبَرُواْ مِن قَوۡمِهِۦ لِلَّذِينَ ٱسۡتُضۡعِفُواْ لِمَنۡ ءَامَنَ مِنۡهُمۡ أَتَعۡلَمُونَ أَنَّ صَٰلِحٗا مُّرۡسَلٞ مِّن رَّبِّهِۦۚ قَالُوٓاْ إِنَّا بِمَآ أُرۡسِلَ بِهِۦ مُؤۡمِنُونَ

Mamwinyi walio onesha kiburi katika watuwake wali-sema kuwaambia waumini walionyanyaswa: Hivi mnajua kweli kuwa Swaleh ametumwa na Mola wake? Wakasema: Hakika, sisi tunayaamini yale aliyotumwa



Sourate: AL-AARAAF 

Verset : 76

قَالَ ٱلَّذِينَ ٱسۡتَكۡبَرُوٓاْ إِنَّا بِٱلَّذِيٓ ءَامَنتُم بِهِۦ كَٰفِرُونَ

Wale waliotakabari wakasema: Hakika, sisi ni wenye kuyapinga (hayo) mliyoyaamini



Sourate: AL-AARAAF 

Verset : 77

فَعَقَرُواْ ٱلنَّاقَةَ وَعَتَوۡاْ عَنۡ أَمۡرِ رَبِّهِمۡ وَقَالُواْ يَٰصَٰلِحُ ٱئۡتِنَا بِمَا تَعِدُنَآ إِن كُنتَ مِنَ ٱلۡمُرۡسَلِينَ

Wakamchinja ngamia na wakaasi amri ya Mola wao na wakasema: Ewe Swaleh, haya tuletee (hayo) unayotuahidi kama wewe ni mion-goni mwa Mitume



Sourate: AL-AARAAF 

Verset : 78

فَأَخَذَتۡهُمُ ٱلرَّجۡفَةُ فَأَصۡبَحُواْ فِي دَارِهِمۡ جَٰثِمِينَ

Basi likawachukua tetemeko (la ardhi) na wakawa wameangamia majumbani mwao huku wamepiga magoti



Sourate: AL-AARAAF 

Verset : 79

فَتَوَلَّىٰ عَنۡهُمۡ وَقَالَ يَٰقَوۡمِ لَقَدۡ أَبۡلَغۡتُكُمۡ رِسَالَةَ رَبِّي وَنَصَحۡتُ لَكُمۡ وَلَٰكِن لَّا تُحِبُّونَ ٱلنَّـٰصِحِينَ

Basi akaachana nao na kusema: Enyi watu zangu, kwa Yakini kabisa nimekufikishieni ujumbe wa Mola wangu Mlezi na nimekupeni nasaha na lakini hamuwapendi wenye kunasihi



Sourate: AL-AARAAF 

Verset : 80

وَلُوطًا إِذۡ قَالَ لِقَوۡمِهِۦٓ أَتَأۡتُونَ ٱلۡفَٰحِشَةَ مَا سَبَقَكُم بِهَا مِنۡ أَحَدٖ مِّنَ ٱلۡعَٰلَمِينَ

Na (kumbuka Mtume) Lutwi wakati alipowaambia watu wake (kwamba): Hivi mnafanya uchafu ambao hajakutangulieni yeyote miongoni mwa walimwengu kuufanya?



Sourate: AL-AARAAF 

Verset : 81

إِنَّكُمۡ لَتَأۡتُونَ ٱلرِّجَالَ شَهۡوَةٗ مِّن دُونِ ٱلنِّسَآءِۚ بَلۡ أَنتُمۡ قَوۡمٞ مُّسۡرِفُونَ

Hakika, nyinyi mnawaendea (mnawatamani) wanaume kimatamanio badala ya wanawake? Ama kweli ninyi ni watu mliokiuka mipaka (katika uovu)



Sourate: AL-AARAAF 

Verset : 82

وَمَا كَانَ جَوَابَ قَوۡمِهِۦٓ إِلَّآ أَن قَالُوٓاْ أَخۡرِجُوهُم مِّن قَرۡيَتِكُمۡۖ إِنَّهُمۡ أُنَاسٞ يَتَطَهَّرُونَ

Na halikuwa jibu la watu wake isipokuwa tu walisema (kwamba): Watoeni (wafukuzeni) katika mji wenu, maana wao ni watu wanaojifanya wasafi



Sourate: AL-AARAAF 

Verset : 83

فَأَنجَيۡنَٰهُ وَأَهۡلَهُۥٓ إِلَّا ٱمۡرَأَتَهُۥ كَانَتۡ مِنَ ٱلۡغَٰبِرِينَ

Basi tulimuokoa yeye na familia yake isipokuwa mkewe tu; alikuwa miongoni mwa waliobaki (katika adhabu)



Sourate: AL-AARAAF 

Verset : 84

وَأَمۡطَرۡنَا عَلَيۡهِم مَّطَرٗاۖ فَٱنظُرۡ كَيۡفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلۡمُجۡرِمِينَ

Na tukawamiminia mvua (ya mawe). Basi tazama; ni namna gani ulikuwa mwisho wa waovu?



Sourate: AL-AARAAF 

Verset : 85

وَإِلَىٰ مَدۡيَنَ أَخَاهُمۡ شُعَيۡبٗاۚ قَالَ يَٰقَوۡمِ ٱعۡبُدُواْ ٱللَّهَ مَا لَكُم مِّنۡ إِلَٰهٍ غَيۡرُهُۥۖ قَدۡ جَآءَتۡكُم بَيِّنَةٞ مِّن رَّبِّكُمۡۖ فَأَوۡفُواْ ٱلۡكَيۡلَ وَٱلۡمِيزَانَ وَلَا تَبۡخَسُواْ ٱلنَّاسَ أَشۡيَآءَهُمۡ وَلَا تُفۡسِدُواْ فِي ٱلۡأَرۡضِ بَعۡدَ إِصۡلَٰحِهَاۚ ذَٰلِكُمۡ خَيۡرٞ لَّكُمۡ إِن كُنتُم مُّؤۡمِنِينَ

Na (tulimpeleka kwa watu wa) Madiyan ndugu yao Shuaibu, akasema: Enyi watu wangu, muabuduni Allah, hamna nyiyi Mungu mwingine isipokuwa yeye (Allah) tu. Hakika, zimekujieni hoja dhahiri kutoka kwa Mola wenu. Basi kamilisheni vipimo vya ujazo na mizani (vipimo vya uzito) na msiwapunje watu vitu vyao na msifanye uharibifu katika Ardhi baada ya kutengenezwa kwake. Hayo ni bora kwenu ikiwa tu nyinyi ni waumini



Sourate: AL-AARAAF 

Verset : 86

وَلَا تَقۡعُدُواْ بِكُلِّ صِرَٰطٖ تُوعِدُونَ وَتَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ مَنۡ ءَامَنَ بِهِۦ وَتَبۡغُونَهَا عِوَجٗاۚ وَٱذۡكُرُوٓاْ إِذۡ كُنتُمۡ قَلِيلٗا فَكَثَّرَكُمۡۖ وَٱنظُرُواْ كَيۡفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلۡمُفۡسِدِينَ

Na msikae kwenye kila njia (msiwe kikwazo) mkitisha (watu) na kuwazuia wale walioiamini njia ya Allah wasiifuate, na mkitaka njia hiyo ipinde. Na kumbukeni mlipokuwa wachache, basi (Allah) akakufanyeni wengi, na tazameni; ulikuwaje mwisho wa waharibifu?



Sourate: AL-AARAAF 

Verset : 87

وَإِن كَانَ طَآئِفَةٞ مِّنكُمۡ ءَامَنُواْ بِٱلَّذِيٓ أُرۡسِلۡتُ بِهِۦ وَطَآئِفَةٞ لَّمۡ يُؤۡمِنُواْ فَٱصۡبِرُواْ حَتَّىٰ يَحۡكُمَ ٱللَّهُ بَيۡنَنَاۚ وَهُوَ خَيۡرُ ٱلۡحَٰكِمِينَ

Na japokuwa kundi miongoni mwenu limeamini yale niliyotumwa na kundi (jingine) halikuyaamini, basi subirini, mpaka Allah atakapohukumu kati yetu. Na yeye (Allah) ni Mbora wa Mahakimu