وَأُمِّهِۦ وَأَبِيهِ
Na mama yake na baba yake
Partager :
وَصَٰحِبَتِهِۦ وَبَنِيهِ
Na mkewe na wanae
لِكُلِّ ٱمۡرِيٕٖ مِّنۡهُمۡ يَوۡمَئِذٖ شَأۡنٞ يُغۡنِيهِ
(Kwasababu) Kila mtu miongoni mwao siku hiyo atakuwa na lake la kumtosha yeye mwenyewe
وُجُوهٞ يَوۡمَئِذٖ مُّسۡفِرَةٞ
Siku hiyo ziko nyuso zitakazo nawiri
ضَاحِكَةٞ مُّسۡتَبۡشِرَةٞ
Zikicheka na kufurahika, (na zitachangamka)
وَوُجُوهٞ يَوۡمَئِذٍ عَلَيۡهَا غَبَرَةٞ
Na ziko nyuso siku hiyo zitakuwa na vumbi juu yake
تَرۡهَقُهَا قَتَرَةٌ
Zitafunikwa na giza zito
أُوْلَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡكَفَرَةُ ٱلۡفَجَرَةُ
Hao ndio makafiri watenda maovu
إِذَا ٱلشَّمۡسُ كُوِّرَتۡ
Jua litakapokunjwa kunjwa (na kupotea mwanga wake)
وَإِذَا ٱلنُّجُومُ ٱنكَدَرَتۡ
Na nyota zitikapotiwa giza (zitakapozimwa nuru yake)
وَإِذَا ٱلۡجِبَالُ سُيِّرَتۡ
Na milima itakapoendeshwa (itakapondolewa)
وَإِذَا ٱلۡعِشَارُ عُطِّلَتۡ
Na ngamia wenye mimba pevu watakapotelekezwa
وَإِذَا ٱلۡوُحُوشُ حُشِرَتۡ
Na wanyama wa mwituni watakapokusanywa
وَإِذَا ٱلۡبِحَارُ سُجِّرَتۡ
Na bahari zitakapowashwa moto
وَإِذَا ٱلنُّفُوسُ زُوِّجَتۡ
Na roho zitakapounganishwa na viwiliwili vyao
وَإِذَا ٱلۡمَوۡءُۥدَةُ سُئِلَتۡ
Na mtoto wa kike aliyezikwa akiwa hai atakapoulizwa
بِأَيِّ ذَنۢبٖ قُتِلَتۡ
Ameuawa kosa gani?
وَإِذَا ٱلصُّحُفُ نُشِرَتۡ
Na sahifa (kurasa) za kurekodi (matendo ya waja) zitakapo kunjuliwa, [wakati wa kuhesabiwa watu]
وَإِذَا ٱلسَّمَآءُ كُشِطَتۡ
Na mbingu itapo ondoshwa pahala pake
وَإِذَا ٱلۡجَحِيمُ سُعِّرَتۡ
Na Jahannamu itakapo chochewa
وَإِذَا ٱلۡجَنَّةُ أُزۡلِفَتۡ
Na Pepo ikasogezwa karibu
عَلِمَتۡ نَفۡسٞ مَّآ أَحۡضَرَتۡ
Kila nafsi itajua ilicho kihudhurisha
فَلَآ أُقۡسِمُ بِٱلۡخُنَّسِ
Basi Naapa kwa sayari zinapo rejea nyuma, zinazotoweka (mchana na zinadhihirika usiku)
ٱلۡجَوَارِ ٱلۡكُنَّسِ
Zinazotembea na kujificha
وَٱلَّيۡلِ إِذَا عَسۡعَسَ
Na naapa kwa usiku unapo pungua giza lake
وَٱلصُّبۡحِ إِذَا تَنَفَّسَ
Na Naapa kwa asubuhi inapo pambazuka
إِنَّهُۥ لَقَوۡلُ رَسُولٖ كَرِيمٖ
Hakika hii (Qurani) bila shaka ni kauli (ameifikisha) Mjumbe mtukufu (Jibrili)
ذِي قُوَّةٍ عِندَ ذِي ٱلۡعَرۡشِ مَكِينٖ
Mwenye nguvu na cheo kitukufu kwa (Allah) Anayemiliki ‘Arsh. [Kiti cha Enzi]
مُّطَاعٖ ثَمَّ أَمِينٖ
Anayetiiwa (na Malaika), mwaminifu huko (mbinguni)
وَمَا صَاحِبُكُم بِمَجۡنُونٖ
Na wala huyu mwenzenu hana wazimu