إِنَّهُمۡ كَانُوٓاْ إِذَا قِيلَ لَهُمۡ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا ٱللَّهُ يَسۡتَكۡبِرُونَ
Wao walipo kuwa wakiambiwa La ilaha illa ‘LLahu Hapana mungu ila Allah tu, wanafanya kiburi
Partager :
وَيَقُولُونَ أَئِنَّا لَتَارِكُوٓاْ ءَالِهَتِنَا لِشَاعِرٖ مَّجۡنُونِۭ
Na wakisema: Hivyo sisi tuiache miungu yetu kwa ajili ya huyu mtunga mashairi mwendawazimu?
بَلۡ جَآءَ بِٱلۡحَقِّ وَصَدَّقَ ٱلۡمُرۡسَلِينَ
Bali huyu amekuja kwa Haki, na amewasadikisha Mitume
إِنَّكُمۡ لَذَآئِقُواْ ٱلۡعَذَابِ ٱلۡأَلِيمِ
Hakika nyinyi bila ya shaka mtaionja adhabu chungu
وَمَا تُجۡزَوۡنَ إِلَّا مَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ
Wala hamlipwi ila hayo mliyo kuwa mkiyafanya
إِلَّا عِبَادَ ٱللَّهِ ٱلۡمُخۡلَصِينَ
Isipo kuwa waja wa Allah walio chaguliwa
أُوْلَـٰٓئِكَ لَهُمۡ رِزۡقٞ مَّعۡلُومٞ
Hao ndio watakao pata riziki maalumu,
فَوَٰكِهُ وَهُم مُّكۡرَمُونَ
Matunda, nao wataheshimiwa
فِي جَنَّـٰتِ ٱلنَّعِيمِ
Katika Bustani za neema
عَلَىٰ سُرُرٖ مُّتَقَٰبِلِينَ
Wako juu ya viti wanatazamana
يُطَافُ عَلَيۡهِم بِكَأۡسٖ مِّن مَّعِينِۭ
Wanazungushiwa kikombe chenye kinywaji cha chemchem
بَيۡضَآءَ لَذَّةٖ لِّلشَّـٰرِبِينَ
Kinywaji cheupe, kitamu kwa wanywao
لَا فِيهَا غَوۡلٞ وَلَا هُمۡ عَنۡهَا يُنزَفُونَ
Hakina madhara, wala hakiwaleweshi
وَعِندَهُمۡ قَٰصِرَٰتُ ٱلطَّرۡفِ عِينٞ
Na watakuwa nao wanawake wenye macho ya staha mazuri
كَأَنَّهُنَّ بَيۡضٞ مَّكۡنُونٞ
Hao wanawake kama mayai yaliyo hifadhika
فَأَقۡبَلَ بَعۡضُهُمۡ عَلَىٰ بَعۡضٖ يَتَسَآءَلُونَ
Waingie kuulizana wenyewe kwa wenyewe
قَالَ قَآئِلٞ مِّنۡهُمۡ إِنِّي كَانَ لِي قَرِينٞ
Aseme msemaji mmoja miongoni mwao: Hakika mimi nalikuwa na rafiki
يَقُولُ أَءِنَّكَ لَمِنَ ٱلۡمُصَدِّقِينَ
Aliye kuwa akinambia: Hivyo wewe ni katika wanao sadiki
أَءِذَا مِتۡنَا وَكُنَّا تُرَابٗا وَعِظَٰمًا أَءِنَّا لَمَدِينُونَ
Ati tukisha kufa tukawa udongo na mifupa, ndio tutalipwa na kuhesabiwa?
قَالَ هَلۡ أَنتُم مُّطَّلِعُونَ
Atasema: Je! Nyie mnawaona?
فَٱطَّلَعَ فَرَءَاهُ فِي سَوَآءِ ٱلۡجَحِيمِ
Basi atachungulia amwone katikati ya Jahannamu
قَالَ تَٱللَّهِ إِن كِدتَّ لَتُرۡدِينِ
Atasema: Wallahi! Ulikaribia kunipoteza
وَلَوۡلَا نِعۡمَةُ رَبِّي لَكُنتُ مِنَ ٱلۡمُحۡضَرِينَ
Na lau kuwa si neema ya Mola wangu Mlezi bila ya shaka ningelikuwa miongoni mwa walio hudhurishwa
أَفَمَا نَحۡنُ بِمَيِّتِينَ
Je! Sisi hatutakufa,
إِلَّا مَوۡتَتَنَا ٱلۡأُولَىٰ وَمَا نَحۡنُ بِمُعَذَّبِينَ
Isipo kuwa kifo chetu cha kwanza? Wala sisi hatutaadhibiwa
إِنَّ هَٰذَا لَهُوَ ٱلۡفَوۡزُ ٱلۡعَظِيمُ
Hakika huku bila ya shaka ndiko kufuzu kukubwa
لِمِثۡلِ هَٰذَا فَلۡيَعۡمَلِ ٱلۡعَٰمِلُونَ
Kwa mfano wa haya nawatende watendao
أَذَٰلِكَ خَيۡرٞ نُّزُلًا أَمۡ شَجَرَةُ ٱلزَّقُّومِ
Je! Kukaribishwa hivi si ndio bora, au mti wa Zaqqum?
إِنَّا جَعَلۡنَٰهَا فِتۡنَةٗ لِّلظَّـٰلِمِينَ
Hakika Sisi tumeufanya huo kuwa ni mateso kwa walio dhulumu
إِنَّهَا شَجَرَةٞ تَخۡرُجُ فِيٓ أَصۡلِ ٱلۡجَحِيمِ
Hakika huo ni mti unao toka katikati ya Jahannamu