فَلَنَسۡـَٔلَنَّ ٱلَّذِينَ أُرۡسِلَ إِلَيۡهِمۡ وَلَنَسۡـَٔلَنَّ ٱلۡمُرۡسَلِينَ
Kwa hakika kabisa, tutawauliza wale waliopelekewa (Mitume) na kwa hakika kabisa tutawauliza tuliowapeleka (Mitume)
فَلَنَقُصَّنَّ عَلَيۡهِم بِعِلۡمٖۖ وَمَا كُنَّا غَآئِبِينَ
Tena, kwa yakini kabisa, tutawasimulia (walichokifanya) kwa kujua (kwa hoja), na hatukuwa mbali nao
وَٱلۡوَزۡنُ يَوۡمَئِذٍ ٱلۡحَقُّۚ فَمَن ثَقُلَتۡ مَوَٰزِينُهُۥ فَأُوْلَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡمُفۡلِحُونَ
Na mizani siku hiyo ni haki tu. Basi yeyote ambaye uzani wake (wa matendo yakheri) utakuwa mzito (na kuelemea) basi hao ndio tu wenye kufaulu
وَمَنۡ خَفَّتۡ مَوَٰزِينُهُۥ فَأُوْلَـٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ خَسِرُوٓاْ أَنفُسَهُم بِمَا كَانُواْ بِـَٔايَٰتِنَا يَظۡلِمُونَ
Na yeyote ambaye uzani wake (wa matendo yake ya kheri) utakuwa hafifu, basi hao ndio waliozitia hasara nafsi zao kwa sababu ya walivyokuwa wanazifanyia dhulumu aya zetu (kwa kuzikataa na kuzipinga)
وَلَقَدۡ مَكَّنَّـٰكُمۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَجَعَلۡنَا لَكُمۡ فِيهَا مَعَٰيِشَۗ قَلِيلٗا مَّا تَشۡكُرُونَ
Na kwa hakika kabisa, tulikupeni nafasi ardhini (duniani), na tulikufanyieni humo njia za (kupata) maisha (yenu). Ni uchache mno mnavyoshukuru
وَلَقَدۡ خَلَقۡنَٰكُمۡ ثُمَّ صَوَّرۡنَٰكُمۡ ثُمَّ قُلۡنَا لِلۡمَلَـٰٓئِكَةِ ٱسۡجُدُواْ لِأٓدَمَ فَسَجَدُوٓاْ إِلَّآ إِبۡلِيسَ لَمۡ يَكُن مِّنَ ٱلسَّـٰجِدِينَ
Na kwa hakika kabisa, tulikuumbeni, kisha tulikutieni sura, kisha tuliwaambia Malaika: Msujudieni Adamu. Walisujudu isipokuwa Ibilisi tu, hakuwa miongoni mwa waliosujudu
قَالَ مَا مَنَعَكَ أَلَّا تَسۡجُدَ إِذۡ أَمَرۡتُكَۖ قَالَ أَنَا۠ خَيۡرٞ مِّنۡهُ خَلَقۡتَنِي مِن نَّارٖ وَخَلَقۡتَهُۥ مِن طِينٖ
(Allah) Alisema (akimuuliza Ibilisi): Kipi kilichokuzuia usisujudu pale nilipokuamrisha? (Ibilisi) Alisema: Mimi ni bora zaidi kuliko yeye; umeniumba kwa moto, na yeye umemuumba kwa udongo
قَالَ فَٱهۡبِطۡ مِنۡهَا فَمَا يَكُونُ لَكَ أَن تَتَكَبَّرَ فِيهَا فَٱخۡرُجۡ إِنَّكَ مِنَ ٱلصَّـٰغِرِينَ
(Allah) Akasema: Basi teremka humo. Haikustahiki kwako kufanya kiburi humo. Basi toka. Hakika, wewe ni miongoni mwa walio duni kabisa
قَالَ أَنظِرۡنِيٓ إِلَىٰ يَوۡمِ يُبۡعَثُونَ
(Ibilisi) Alisema: Nibakishe mpaka Siku (waja wako) wataka-pofufuliwa
قَالَ إِنَّكَ مِنَ ٱلۡمُنظَرِينَ
(Allah) Akasema: Hakika, wewe ni miongoni mwa watakaobakishwa
قَالَ فَبِمَآ أَغۡوَيۡتَنِي لَأَقۡعُدَنَّ لَهُمۡ صِرَٰطَكَ ٱلۡمُسۡتَقِيمَ
(Ibilisi) Akasema: Basi kwa sababu umenipotosha (umeniacha nipotoke), nina apa kwamba, nitawakalia (nitawawekea vikwazo) katika njia yako ya sawa
ثُمَّ لَأٓتِيَنَّهُم مِّنۢ بَيۡنِ أَيۡدِيهِمۡ وَمِنۡ خَلۡفِهِمۡ وَعَنۡ أَيۡمَٰنِهِمۡ وَعَن شَمَآئِلِهِمۡۖ وَلَا تَجِدُ أَكۡثَرَهُمۡ شَٰكِرِينَ
Kisha, kwa yakini kabisa, nitawaendea mbele yao na nyuma yao na kuliani kwao na kushotoni kwao[1]. Na hutapata wengi wao wenye kushukuru
1- - Hapa Ibilisi anakusudia kwamba, atamfuatilia mwanadamu kila alipo. Hii ni sawa na ule msemo wa Kiswahili wa mtaani usemao “Nitakula naye sahani moja”.
قَالَ ٱخۡرُجۡ مِنۡهَا مَذۡءُومٗا مَّدۡحُورٗاۖ لَّمَن تَبِعَكَ مِنۡهُمۡ لَأَمۡلَأَنَّ جَهَنَّمَ مِنكُمۡ أَجۡمَعِينَ
(Allah) Akasema (kumwambia Ibilisi kwamba): Toka humo (Peponi) ukiwa umechukiwa, umelaaniwa. Kwa yakini kabisa, yeyote atakayekufuata wewe miongoni mwao hakika nitaijaza Jahanamu kwa (kukutumbukizeni humo) nyinyi nyote
وَيَـٰٓـَٔادَمُ ٱسۡكُنۡ أَنتَ وَزَوۡجُكَ ٱلۡجَنَّةَ فَكُلَا مِنۡ حَيۡثُ شِئۡتُمَا وَلَا تَقۡرَبَا هَٰذِهِ ٱلشَّجَرَةَ فَتَكُونَا مِنَ ٱلظَّـٰلِمِينَ
Na ewe Adamu, kaa wewe na mkeo Peponi. Basi kuleni katika mpendavyo na msiusogelee mti huu, mtakuwa miongoni mwa madhalimu
فَوَسۡوَسَ لَهُمَا ٱلشَّيۡطَٰنُ لِيُبۡدِيَ لَهُمَا مَا وُۥرِيَ عَنۡهُمَا مِن سَوۡءَٰتِهِمَا وَقَالَ مَا نَهَىٰكُمَا رَبُّكُمَا عَنۡ هَٰذِهِ ٱلشَّجَرَةِ إِلَّآ أَن تَكُونَا مَلَكَيۡنِ أَوۡ تَكُونَا مِنَ ٱلۡخَٰلِدِينَ
Basi shetani akawashawishi wawili hao ili awafunulie tupu zao zilizohifadhiwa na kusema (akiwaambia): Mola wenu hakukukatazeni mti huu isipokuwa tu msije mkawa Malaika wawili au mkawa miongoni mwa watakaoishi milele
وَقَاسَمَهُمَآ إِنِّي لَكُمَا لَمِنَ ٱلنَّـٰصِحِينَ
Na (shetani) akawaapia (kwamba): Kwa hakika kabisa, mimi kwenu ni miongoni mwa watoaji nasaha
فَدَلَّىٰهُمَا بِغُرُورٖۚ فَلَمَّا ذَاقَا ٱلشَّجَرَةَ بَدَتۡ لَهُمَا سَوۡءَٰتُهُمَا وَطَفِقَا يَخۡصِفَانِ عَلَيۡهِمَا مِن وَرَقِ ٱلۡجَنَّةِۖ وَنَادَىٰهُمَا رَبُّهُمَآ أَلَمۡ أَنۡهَكُمَا عَن تِلۡكُمَا ٱلشَّجَرَةِ وَأَقُل لَّكُمَآ إِنَّ ٱلشَّيۡطَٰنَ لَكُمَا عَدُوّٞ مُّبِينٞ
(Shetani) Akawashusha (Kutoka katika daraja la utiifu na kuwaweka katika uovu wa kukaidi amri ya Allah) kwa njia ya hadaa. Basi walipo uonja mti ule, zilidhihiri tupu zao na wakaanza kujibandika majani ya bustanini (ili kujisitiri). Na Mola wao aliwaita: Hivi sikukukatazeni mti ule na kukuambieni ya kwamba, hakika shetani kwenu ni adui aliye dhahiri sana?
قَالَا رَبَّنَا ظَلَمۡنَآ أَنفُسَنَا وَإِن لَّمۡ تَغۡفِرۡ لَنَا وَتَرۡحَمۡنَا لَنَكُونَنَّ مِنَ ٱلۡخَٰسِرِينَ
(Adamu na mkewe) Wakasema: Ewe Mola wetu Mlezi, sisi tumezidhulumu nafsi zetu, na kama hutatusamehe na kutuhurumia kwa hakika kabisa tutakuwa miongoni mwa wenye hasara
قَالَ ٱهۡبِطُواْ بَعۡضُكُمۡ لِبَعۡضٍ عَدُوّٞۖ وَلَكُمۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ مُسۡتَقَرّٞ وَمَتَٰعٌ إِلَىٰ حِينٖ
(Allah) Akasema: Teremkeni, nyinyi kwa nyinyi ni maadui, na nyinyi katika ardhi (duniani) mtakuwa na makazi na starehe (burudani) mpaka muda (maalumu)
قَالَ فِيهَا تَحۡيَوۡنَ وَفِيهَا تَمُوتُونَ وَمِنۡهَا تُخۡرَجُونَ
(Allah) Akasema: Humo (duniani) mtaishi na humo mtakufa na humo mtatolewa (mtafufuliwa)
يَٰبَنِيٓ ءَادَمَ قَدۡ أَنزَلۡنَا عَلَيۡكُمۡ لِبَاسٗا يُوَٰرِي سَوۡءَٰتِكُمۡ وَرِيشٗاۖ وَلِبَاسُ ٱلتَّقۡوَىٰ ذَٰلِكَ خَيۡرٞۚ ذَٰلِكَ مِنۡ ءَايَٰتِ ٱللَّهِ لَعَلَّهُمۡ يَذَّكَّرُونَ
Enyi wanadamu, hakika tumekuteremshieni vazi linaloficha tupu zenu na pambo. Na vazi la kumcha Allah ndio bora zaidi. Hizo ni baadhi ya ishara za Allah ili (wanadamu) wapate kukumbuka (neema za Mola wao Mlezi na kumshukuru)
يَٰبَنِيٓ ءَادَمَ لَا يَفۡتِنَنَّكُمُ ٱلشَّيۡطَٰنُ كَمَآ أَخۡرَجَ أَبَوَيۡكُم مِّنَ ٱلۡجَنَّةِ يَنزِعُ عَنۡهُمَا لِبَاسَهُمَا لِيُرِيَهُمَا سَوۡءَٰتِهِمَآۚ إِنَّهُۥ يَرَىٰكُمۡ هُوَ وَقَبِيلُهُۥ مِنۡ حَيۡثُ لَا تَرَوۡنَهُمۡۗ إِنَّا جَعَلۡنَا ٱلشَّيَٰطِينَ أَوۡلِيَآءَ لِلَّذِينَ لَا يُؤۡمِنُونَ
Enyi Wanadamu, kamwe shetani asikufitinisheni[1] kama alivyowatoa Peponi wazazi wenu, akiwavua nguo zao ili kuwawekea wazi tupu zao. Hakika yeye (shetani) anakuoneni yeye na jeshi lake katika namna ambayo nyinyi hamuwaoni. Hakika, sisi tumewafanya mashetani wandani wa (watu) wasioamini
1- - Shetani asikudanganyeni kwa kukupambieni maasi, kama ambavyo alimhadaa baba yenu Adamu na mkewe kwa kuwashawishi waonje mti. Matokeo yake walitolewa Peponi.
وَإِذَا فَعَلُواْ فَٰحِشَةٗ قَالُواْ وَجَدۡنَا عَلَيۡهَآ ءَابَآءَنَا وَٱللَّهُ أَمَرَنَا بِهَاۗ قُلۡ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَأۡمُرُ بِٱلۡفَحۡشَآءِۖ أَتَقُولُونَ عَلَى ٱللَّهِ مَا لَا تَعۡلَمُونَ
Na wafanyapo mambo machafu wanasema: (Haya tuyafanyayo) Tumewakuta nayo baba zetu na Allah ametuamuru hayo. Sema: Hakika, Allah haamrishi machafu. Hivi mnamzushia Allah msiyoyajua?
قُلۡ أَمَرَ رَبِّي بِٱلۡقِسۡطِۖ وَأَقِيمُواْ وُجُوهَكُمۡ عِندَ كُلِّ مَسۡجِدٖ وَٱدۡعُوهُ مُخۡلِصِينَ لَهُ ٱلدِّينَۚ كَمَا بَدَأَكُمۡ تَعُودُونَ
Sema: Mola wangu Mlezi ameamrisha (kufanya) uadilifu. Na elekezeni nyuso zenu kila mnaposwali (mkusudieni Allah kila mfanyapo ibada) na muabuduni yeye tu mkimtakasia dini. Kama (Allah) ambavyo amekuumbeni mwanzo ndivyo mtakavyorudi
فَرِيقًا هَدَىٰ وَفَرِيقًا حَقَّ عَلَيۡهِمُ ٱلضَّلَٰلَةُۚ إِنَّهُمُ ٱتَّخَذُواْ ٱلشَّيَٰطِينَ أَوۡلِيَآءَ مِن دُونِ ٱللَّهِ وَيَحۡسَبُونَ أَنَّهُم مُّهۡتَدُونَ
Kundi moja (Allah) ameliongoa na kundi (lingine) limestahiki kupotea. Hakika, wao wamewafanya mashetani wandani (wao) badala ya Allah na wanadhani kwamba wameongoka
۞يَٰبَنِيٓ ءَادَمَ خُذُواْ زِينَتَكُمۡ عِندَ كُلِّ مَسۡجِدٖ وَكُلُواْ وَٱشۡرَبُواْ وَلَا تُسۡرِفُوٓاْۚ إِنَّهُۥ لَا يُحِبُّ ٱلۡمُسۡرِفِينَ
Enyi wanadamu, chukueni mapambo yenu kila muendapo msikitini (kila mnaposwali)[1] na kuleni na kunyweni na msifanye ubadhirifu. Hakika, yeye (Allah) hawapendi wabadhirifu
1- - Aya hii ndio iliyoweka sharti la Muislamu kujisitiri kwa kuvaa nguo za heshima na sitara katika Swala. Na sio kuvaa nguo tu, lakini kuvaa nguo ya sitara, safi na inayopendeza. Kwa msingi huu, sio vyema kwa Muislamu kuswali akiwa amevaa nguo chafu au zenye michoro, picha na mandishi yasiyokuwa na lazima.
قُلۡ مَنۡ حَرَّمَ زِينَةَ ٱللَّهِ ٱلَّتِيٓ أَخۡرَجَ لِعِبَادِهِۦ وَٱلطَّيِّبَٰتِ مِنَ ٱلرِّزۡقِۚ قُلۡ هِيَ لِلَّذِينَ ءَامَنُواْ فِي ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا خَالِصَةٗ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِۗ كَذَٰلِكَ نُفَصِّلُ ٱلۡأٓيَٰتِ لِقَوۡمٖ يَعۡلَمُونَ
Sema: Hivi ni nani aliyeharamisha mapambo ya Allah ambayo ameyatoa kwa waja wake na riziki nzuri? Sema: Hayo (mapambo na riziki nzuri) ni kwa ajili ya wale walioamini katika maisha (yao) ya dunia, yakiwa halisi (ya peke yao) Siku ya Kiyama. Kama hivyo tunazifafanua Aya (zetu) kwa watu wanaojua
قُلۡ إِنَّمَا حَرَّمَ رَبِّيَ ٱلۡفَوَٰحِشَ مَا ظَهَرَ مِنۡهَا وَمَا بَطَنَ وَٱلۡإِثۡمَ وَٱلۡبَغۡيَ بِغَيۡرِ ٱلۡحَقِّ وَأَن تُشۡرِكُواْ بِٱللَّهِ مَا لَمۡ يُنَزِّلۡ بِهِۦ سُلۡطَٰنٗا وَأَن تَقُولُواْ عَلَى ٱللَّهِ مَا لَا تَعۡلَمُونَ
Sema: Hakika, ilivyo ni kwamba, Mola wangu Mlezi ameharamisha (mambo) machafu; ya dhahiri katika hayo na ya siri na dhambi na dhuluma bila ya haki yoyote,[1] na kuvishirikisha na Allah vitu ambavyo hakuviteremshia dalili (hoja) yoyote na (pia Allah ameharamisha) kumsemea Allah msiyoyajua
1- - Dhuluma bila ya haki ni dhuluma isiyokuwa na msingi wa kisheria. Ama kutekeleza haki kwa msingi wa sheria sio dhuluma wala ukandamizaji, ila tu limetumika neno dhuluma kwa ulinganifu wa lugha. Inayo onekana kama ni dhuluma kwenye macho ya wapingaji wa sheria za Allah ni kama kuuawa kwa mtu aliyethibitika kuua, kukatwa mkono mtu aliyethibitika kuiba n.k. Lakini hii sio dhuluma ila ni haki kwa sababu ni utekelezaji wa sheria.
وَلِكُلِّ أُمَّةٍ أَجَلٞۖ فَإِذَا جَآءَ أَجَلُهُمۡ لَا يَسۡتَأۡخِرُونَ سَاعَةٗ وَلَا يَسۡتَقۡدِمُونَ
Na kila umma una muda (wake); basi utakapofika muda wao hawatachelewesha hata saa moja wala hawatasogeza
يَٰبَنِيٓ ءَادَمَ إِمَّا يَأۡتِيَنَّكُمۡ رُسُلٞ مِّنكُمۡ يَقُصُّونَ عَلَيۡكُمۡ ءَايَٰتِي فَمَنِ ٱتَّقَىٰ وَأَصۡلَحَ فَلَا خَوۡفٌ عَلَيۡهِمۡ وَلَا هُمۡ يَحۡزَنُونَ
Enyi wanadamu, watakapo kufikieni Mitume watokanao na nyinyi wakikuhadithieni Aya zangu[1], basi yeyote atakayekuwa na uchaMungu na akafanya mema basi hawatakuwa na hofu yoyote, na hawatahuzunika
1- - Aya hii wanaitumia baadhi ya watu ili kupotosha. Wanadai kwamba, utume bado unaendelea. Itikadi ya Watu wa Sun ana Jama a ni kwamba, utume umekoma kwa Mtume Muhammad. Hakuna Mtume mwingine baada yake. Tujiulize swali la msingi. Aya hapa kama inasema kuwa Mitume wanaendelea kuja je, hizo Aya za Allah wanazotakiwa kutusomea ziko wapi? Rejea Aya ya 40, Sura Al-ahzab (33). Pia rejea Aya ya 158 ya Sura Al-aaraf (7).