كَلَّاۖ لَيُنۢبَذَنَّ فِي ٱلۡحُطَمَةِ
la hasha! Atavurumishwa katika moto hutama
Partager :
وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا ٱلۡحُطَمَةُ
Na nani atakujuvya ni nini moto wa hutama?
نَارُ ٱللَّهِ ٱلۡمُوقَدَةُ
Moto wa Mwenyezi Mungu ulio washwa
ٱلَّتِي تَطَّلِعُ عَلَى ٱلۡأَفۡـِٔدَةِ
Ambao unapanda nyoyoni
إِنَّهَا عَلَيۡهِم مُّؤۡصَدَةٞ
Hakika huo utafungiwa nao
فِي عَمَدٖ مُّمَدَّدَةِۭ
Kwenye nguzo zilio nyooshwa
أَلَمۡ تَرَ كَيۡفَ فَعَلَ رَبُّكَ بِأَصۡحَٰبِ ٱلۡفِيلِ
Je, hukuona jinsi Mola wako Mlezi alivyo watenda wale wenye tembo?
أَلَمۡ يَجۡعَلۡ كَيۡدَهُمۡ فِي تَضۡلِيلٖ
Je, hakujaalia vitimbi vyao kuharibika?
وَأَرۡسَلَ عَلَيۡهِمۡ طَيۡرًا أَبَابِيلَ
Na akawapelekea ndege makundi kwa makundi?
تَرۡمِيهِم بِحِجَارَةٖ مِّن سِجِّيلٖ
(Ndege) Wanaowatupia mawe ya Motoni?
فَجَعَلَهُمۡ كَعَصۡفٖ مَّأۡكُولِۭ
(Mawe hayo) Yakawafanya kama majani yaliyoliwa (yaliyotafunwa)!
لِإِيلَٰفِ قُرَيۡشٍ
Kwasababu ya kuzoea kwa Waqureshi
إِۦلَٰفِهِمۡ رِحۡلَةَ ٱلشِّتَآءِ وَٱلصَّيۡفِ
Kuzoea kwao safari za Kusi na Kaskazi
فَلۡيَعۡبُدُواْ رَبَّ هَٰذَا ٱلۡبَيۡتِ
Kwasababu ya hayo, wamuabudu Mola Mlezi wa Nyumba hii (Tukufu ya Makka)
ٱلَّذِيٓ أَطۡعَمَهُم مِّن جُوعٖ وَءَامَنَهُم مِّنۡ خَوۡفِۭ
Ambaye amewalisha wasipate njaa, na amewasalimisha wasipate hofu
أَرَءَيۡتَ ٱلَّذِي يُكَذِّبُ بِٱلدِّينِ
Je, umemuona anayekadhibisha (anayekataa) dini?
فَذَٰلِكَ ٱلَّذِي يَدُعُّ ٱلۡيَتِيمَ
Basi huyo ni anayemsukuma (na kumtelekeza) yatima
وَلَا يَحُضُّ عَلَىٰ طَعَامِ ٱلۡمِسۡكِينِ
Wala hahimizi kumlisha (kumpa chakula) maskini
فَوَيۡلٞ لِّلۡمُصَلِّينَ
Basi, ole wao wanaoswali
ٱلَّذِينَ هُمۡ عَن صَلَاتِهِمۡ سَاهُونَ
Ambao wanapuuza Swala zao
ٱلَّذِينَ هُمۡ يُرَآءُونَ
Ambao wanaonyesha (matendo yao kwa watu ili wasifiwe)
وَيَمۡنَعُونَ ٱلۡمَاعُونَ
Na wanazuia msaada
إِنَّآ أَعۡطَيۡنَٰكَ ٱلۡكَوۡثَرَ
Hakika tumekupa Kauthar (kheri nyingi ikiwemo mto wa Peponi)
فَصَلِّ لِرَبِّكَ وَٱنۡحَرۡ
Basi Swali na uchinje kwa ajili ya Mola wako Mlezi
إِنَّ شَانِئَكَ هُوَ ٱلۡأَبۡتَرُ
Hakika anayekuchukia (wewe Muhammad) ndiye hasa aliyepungukiwa (na kheri zote)
قُلۡ يَـٰٓأَيُّهَا ٱلۡكَٰفِرُونَ
Sema: Enyi makafiri
لَآ أَعۡبُدُ مَا تَعۡبُدُونَ
Siabudu mnacho kiabudu
وَلَآ أَنتُمۡ عَٰبِدُونَ مَآ أَعۡبُدُ
Na nyinyi hamuabudu ninaye muabudu
وَلَآ أَنَا۠ عَابِدٞ مَّا عَبَدتُّمۡ
Na mimi si mwenye kuviabudu mlivyo viabudu
Na nyinyi si wenye kuabudu ninayemuabudu