نَحۡنُ خَلَقۡنَٰكُمۡ فَلَوۡلَا تُصَدِّقُونَ
Sisi Tumekuumbeni, basi kwa nini hamsadikishi hilo?
Partager :
أَفَرَءَيۡتُم مَّا تُمۡنُونَ
Je, mnaona mbegu ya uzazi mnayo imwagia kwa nguvu?
ءَأَنتُمۡ تَخۡلُقُونَهُۥٓ أَمۡ نَحۡنُ ٱلۡخَٰلِقُونَ
Je, nyinyi ndio mnaiumba au sisi ndio Waumbaji?
نَحۡنُ قَدَّرۡنَا بَيۡنَكُمُ ٱلۡمَوۡتَ وَمَا نَحۡنُ بِمَسۡبُوقِينَ
Sisi tumekadiria kati yenu umauti na haikua sisi wenye kukimbiwa
عَلَىٰٓ أَن نُّبَدِّلَ أَمۡثَٰلَكُمۡ وَنُنشِئَكُمۡ فِي مَا لَا تَعۡلَمُونَ
Kwamba Tuwabadilishe wengine mfano wenu, na Tukuumbeni katika umbo msilolijua
وَلَقَدۡ عَلِمۡتُمُ ٱلنَّشۡأَةَ ٱلۡأُولَىٰ فَلَوۡلَا تَذَكَّرُونَ
Na bila shaka mmejua umbo la kwanza, basi kwanini hamkumbuki?
أَفَرَءَيۡتُم مَّا تَحۡرُثُونَ
Je, mnaona mbegu mnazo-zipanda?
ءَأَنتُمۡ تَزۡرَعُونَهُۥٓ أَمۡ نَحۡنُ ٱلزَّـٰرِعُونَ
Je, ni nyinyi ndio mnaziotesha, au Sisi ndio Wenye kuotesha mimea?
لَوۡ نَشَآءُ لَجَعَلۡنَٰهُ حُطَٰمٗا فَظَلۡتُمۡ تَفَكَّهُونَ
Lau Tungelitaka, Tungelifanya mabua yaliyonyauka na mkabaki mnashangaa na kusikitika
إِنَّا لَمُغۡرَمُونَ
(Mkisema): Hakika sisi tumegharimika
بَلۡ نَحۡنُ مَحۡرُومُونَ
Bali sisi tumenyimwa
أَفَرَءَيۡتُمُ ٱلۡمَآءَ ٱلَّذِي تَشۡرَبُونَ
Je, mnaona maji ambayo mnakunywa?
ءَأَنتُمۡ أَنزَلۡتُمُوهُ مِنَ ٱلۡمُزۡنِ أَمۡ نَحۡنُ ٱلۡمُنزِلُونَ
Je, ni nyinyi ndio mliyoyateremsha kutoka katika mawingu ya mvua au Sisi ndio Wateremshaji?
لَوۡ نَشَآءُ جَعَلۡنَٰهُ أُجَاجٗا فَلَوۡلَا تَشۡكُرُونَ
Lau Tungelitaka, Tungeliyafanya ya chumvi kali chungu basi kwa nini hamshukuru?
أَفَرَءَيۡتُمُ ٱلنَّارَ ٱلَّتِي تُورُونَ
Je, mnaona moto ambao mnauwasha?
ءَأَنتُمۡ أَنشَأۡتُمۡ شَجَرَتَهَآ أَمۡ نَحۡنُ ٱلۡمُنشِـُٔونَ
Je, ni nyinyi ndio mliouumba mti wake, au Sisi ndio Waumbaji wa mti huo?
نَحۡنُ جَعَلۡنَٰهَا تَذۡكِرَةٗ وَمَتَٰعٗا لِّلۡمُقۡوِينَ
Sisi Tumeufanya kuwa ni ukumbusho na manufaa kwa wasafiri
فَسَبِّحۡ بِٱسۡمِ رَبِّكَ ٱلۡعَظِيمِ
Basi litakase jina la Mola wako aliyetukuka
۞فَلَآ أُقۡسِمُ بِمَوَٰقِعِ ٱلنُّجُومِ
Basi Naapa kwa maangukio ya nyota
وَإِنَّهُۥ لَقَسَمٞ لَّوۡ تَعۡلَمُونَ عَظِيمٌ
Hakika hicho ni kiapo kikubwa lau mnaelewa
إِنَّهُۥ لَقُرۡءَانٞ كَرِيمٞ
Hakika ya hiyo ni Kurani tukufu
فِي كِتَٰبٖ مَّكۡنُونٖ
Katika Kitabu kilichohifadhiwa
لَّا يَمَسُّهُۥٓ إِلَّا ٱلۡمُطَهَّرُونَ
Haigusi isipokuwa waliotakaswa kabisa (Walio twahara)
تَنزِيلٞ مِّن رَّبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ
Ni uteremsho kutoka kwa Mola wa walimwengu wote
أَفَبِهَٰذَا ٱلۡحَدِيثِ أَنتُم مُّدۡهِنُونَ
Hivi kwa maneno haya nyinyi mnapuuza na kuikanusha?
وَتَجۡعَلُونَ رِزۡقَكُمۡ أَنَّكُمۡ تُكَذِّبُونَ
Na mnafanya (badala ya kushu-kuru) kwa riziki mnayopata, nyinyi ndio mnakad hibisha
فَلَوۡلَآ إِذَا بَلَغَتِ ٱلۡحُلۡقُومَ
Itakuaje basi pale roho itaka-pofika kwenye koo
وَأَنتُمۡ حِينَئِذٖ تَنظُرُونَ
Na nyinyi wakati huo mnatazama tu
وَنَحۡنُ أَقۡرَبُ إِلَيۡهِ مِنكُمۡ وَلَٰكِن لَّا تُبۡصِرُونَ
Nasi Tuko karibu naye zaidi kuliko nyinyi, lakini nyinyi hamuoni
فَلَوۡلَآ إِن كُنتُمۡ غَيۡرَ مَدِينِينَ
Na lau kuwa nyinyi hammo katika mamlaka yangu.[1]
1- - Basi kama lau kusingekua na kufufuliwa.