۞فَنَبَذۡنَٰهُ بِٱلۡعَرَآءِ وَهُوَ سَقِيمٞ
Lakini tulimtupa ufukweni patupu, hali yu mgonjwa
Partager :
وَأَنۢبَتۡنَا عَلَيۡهِ شَجَرَةٗ مِّن يَقۡطِينٖ
Na tukauotesha juu yake mmea wa kabila ya mung’unye
وَأَرۡسَلۡنَٰهُ إِلَىٰ مِاْئَةِ أَلۡفٍ أَوۡ يَزِيدُونَ
Na tulimtuma kwa watu laki moja au zaidi
فَـَٔامَنُواْ فَمَتَّعۡنَٰهُمۡ إِلَىٰ حِينٖ
Basi wakaamini, na tukawastarehesha kwa muda
فَٱسۡتَفۡتِهِمۡ أَلِرَبِّكَ ٱلۡبَنَاتُ وَلَهُمُ ٱلۡبَنُونَ
Basi waulize: Ati Mola wako Mlezi ndiye mwenye watoto wa kike, na wao wanao watoto wa kiume?
أَمۡ خَلَقۡنَا ٱلۡمَلَـٰٓئِكَةَ إِنَٰثٗا وَهُمۡ شَٰهِدُونَ
Au tumewaumba Malaika kuwa ni wanawake, na wao wakashuhudia?
أَلَآ إِنَّهُم مِّنۡ إِفۡكِهِمۡ لَيَقُولُونَ
Ati ni kwa uzushi wao ndio wanasema:
وَلَدَ ٱللَّهُ وَإِنَّهُمۡ لَكَٰذِبُونَ
Allah amezaa! Ama hakika bila ya shaka hao ni waongo!
أَصۡطَفَى ٱلۡبَنَاتِ عَلَى ٱلۡبَنِينَ
Ati amekhiari watoto wa kike kuliko wanaume?
مَا لَكُمۡ كَيۡفَ تَحۡكُمُونَ
Mna nini? Mnahukumu vipi nyinyi?
أَفَلَا تَذَكَّرُونَ
Hamkumbuki?
أَمۡ لَكُمۡ سُلۡطَٰنٞ مُّبِينٞ
Au mnayo hoja iliyo wazi?
فَأۡتُواْ بِكِتَٰبِكُمۡ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ
Basi leteni Kitabu chenu kama mnasema kweli
وَجَعَلُواْ بَيۡنَهُۥ وَبَيۡنَ ٱلۡجِنَّةِ نَسَبٗاۚ وَلَقَدۡ عَلِمَتِ ٱلۡجِنَّةُ إِنَّهُمۡ لَمُحۡضَرُونَ
Na wameweka mahusiano ya nasaba baina yake na majini; na majini wamekwisha jua bila ya shaka kuwa wao watahudhurishwa
سُبۡحَٰنَ ٱللَّهِ عَمَّا يَصِفُونَ
Subhana ‘Llah Ametakasika Allah na hayo wanayo msingizia
إِلَّا عِبَادَ ٱللَّهِ ٱلۡمُخۡلَصِينَ
Isipo kuwa waja wa Allah walio safishwa
فَإِنَّكُمۡ وَمَا تَعۡبُدُونَ
Basi hakika nyinyi na mnao waabudu
مَآ أَنتُمۡ عَلَيۡهِ بِفَٰتِنِينَ
Hamwezi kuwapoteza
إِلَّا مَنۡ هُوَ صَالِ ٱلۡجَحِيمِ
Isipo kuwa yule atakaye ingia Motoni
وَمَامِنَّآ إِلَّا لَهُۥ مَقَامٞ مَّعۡلُومٞ
Na hapana katika sisi ila anapo mahali pake maalumu
وَإِنَّا لَنَحۡنُ ٱلصَّآفُّونَ
Na hakika bila ya shaka sisi ndio wajipangao safu
وَإِنَّا لَنَحۡنُ ٱلۡمُسَبِّحُونَ
Na hakika sisi ndio wenye kusabihi kutakasa
وَإِن كَانُواْ لَيَقُولُونَ
Na walikuwapo walio kuwa wakisema:
لَوۡ أَنَّ عِندَنَا ذِكۡرٗا مِّنَ ٱلۡأَوَّلِينَ
Tungelikuwa na Ukumbusho kama wa watu wa zamani,
لَكُنَّا عِبَادَ ٱللَّهِ ٱلۡمُخۡلَصِينَ
Bila ya shaka tungeli kuwa ni waja wa Allah wenye ikhlasi
فَكَفَرُواْ بِهِۦۖ فَسَوۡفَ يَعۡلَمُونَ
Lakini waliukataa. Basi watakuja jua
وَلَقَدۡ سَبَقَتۡ كَلِمَتُنَا لِعِبَادِنَا ٱلۡمُرۡسَلِينَ
Na bila ya shaka neno letu lilikwisha tangulia kwa waja wetu walio tumwa
إِنَّهُمۡ لَهُمُ ٱلۡمَنصُورُونَ
Ya kuwa wao bila ya shaka ndio watakao nusuriwa
وَإِنَّ جُندَنَا لَهُمُ ٱلۡغَٰلِبُونَ
Na kwamba jeshi letu ndilo litakalo shinda
فَتَوَلَّ عَنۡهُمۡ حَتَّىٰ حِينٖ
Basi waachilie mbali kwa muda