Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 36

۞إِنَّمَا يَسۡتَجِيبُ ٱلَّذِينَ يَسۡمَعُونَۘ وَٱلۡمَوۡتَىٰ يَبۡعَثُهُمُ ٱللَّهُ ثُمَّ إِلَيۡهِ يُرۡجَعُونَ

Ilivyo ni kwamba, wanaoitika (wito) ni wale tu wanaosikia (usikivu wa mazingatio). Na wafu (wa nyoyo ambao ni makafiri) Allah atawafufua, kisha kwake tu watarudishwa



Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 37

وَقَالُواْ لَوۡلَا نُزِّلَ عَلَيۡهِ ءَايَةٞ مِّن رَّبِّهِۦۚ قُلۡ إِنَّ ٱللَّهَ قَادِرٌ عَلَىٰٓ أَن يُنَزِّلَ ءَايَةٗ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَهُمۡ لَا يَعۡلَمُونَ

Na walisema: (ingekuwa vizuri) lau kama (Mtume Muhammad) angeteremshiwa Aya (Muujiza) kutoka kwa Mola wake. Sema: Hakika, Allah ni mwenye uwezo wa kuteremsha Aya (Muujiza wanaoutaka) lakini wengi wao hawajui (kitakachowakuta kama wakiteremshiwa muujiza na wasiamini)



Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 38

وَمَا مِن دَآبَّةٖ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَلَا طَـٰٓئِرٖ يَطِيرُ بِجَنَاحَيۡهِ إِلَّآ أُمَمٌ أَمۡثَالُكُمۚ مَّا فَرَّطۡنَا فِي ٱلۡكِتَٰبِ مِن شَيۡءٖۚ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّهِمۡ يُحۡشَرُونَ

Na hakuna kiumbe yeyote anayetembea ardhini wala ndege anayeruka kwa mbawa zake, isipokuwa tu ni mataifa mfano wenu. Hatukuzembea (hatukuacha) kitu chochote katika (hiki) Kitabu (cha Qur’ani). Kisha watakusanywa kwa Mola wao tu (Siku ya Kiyama)



Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 39

وَٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَا صُمّٞ وَبُكۡمٞ فِي ٱلظُّلُمَٰتِۗ مَن يَشَإِ ٱللَّهُ يُضۡلِلۡهُ وَمَن يَشَأۡ يَجۡعَلۡهُ عَلَىٰ صِرَٰطٖ مُّسۡتَقِيمٖ

Na wale waliozipinga Aya zetu ni viziwi na mabubu (wamo) katika giza. Allah akitaka yeyote (apotee) atampoteza, na mwenye kumtaka (aongoke) anamuweka katika njia iliyonyooka (Uislamu)



Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 40

قُلۡ أَرَءَيۡتَكُمۡ إِنۡ أَتَىٰكُمۡ عَذَابُ ٱللَّهِ أَوۡ أَتَتۡكُمُ ٱلسَّاعَةُ أَغَيۡرَ ٱللَّهِ تَدۡعُونَ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ

Sema: Hivi mnaonaje itakapokujieni adhabu ya Allah (hapa duniani) au kitakapokujieni Kiyama, hivi mtawaomba (Miungu wengine) badala ya Allah kama kweli nyinyi ni wakweli?



Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 41

بَلۡ إِيَّاهُ تَدۡعُونَ فَيَكۡشِفُ مَا تَدۡعُونَ إِلَيۡهِ إِن شَآءَ وَتَنسَوۡنَ مَا تُشۡرِكُونَ

Bali ni yeye tu ndiye mnayemuomba na (kwa sababu ya maombi yenu) anatatua matatizo mnayo omba (yatatuliwe) akitaka, na (wakati huo) mnawasahau wale (Miungu) mnaowashirikisha (na Allah)



Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 42

وَلَقَدۡ أَرۡسَلۡنَآ إِلَىٰٓ أُمَمٖ مِّن قَبۡلِكَ فَأَخَذۡنَٰهُم بِٱلۡبَأۡسَآءِ وَٱلضَّرَّآءِ لَعَلَّهُمۡ يَتَضَرَّعُونَ

Na kwa hakika kabisa, tulituma (Mitume) katika mataifa mengi kabla yako (wakawapinga) tukawachukulia hatua (ya kuwaadhibu) kwa shida na madhara ili wawe wanyenyekevu



Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 43

فَلَوۡلَآ إِذۡ جَآءَهُم بَأۡسُنَا تَضَرَّعُواْ وَلَٰكِن قَسَتۡ قُلُوبُهُمۡ وَزَيَّنَ لَهُمُ ٱلشَّيۡطَٰنُ مَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ

Basi walau ilipowajia adhabu yetu wangekuwa wanyenyekevu, lakini nyoyo zao zilikuwa ngumu, na shetani aliwapambia yale waliyokuwa wanayatenda



Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 44

فَلَمَّا نَسُواْ مَا ذُكِّرُواْ بِهِۦ فَتَحۡنَا عَلَيۡهِمۡ أَبۡوَٰبَ كُلِّ شَيۡءٍ حَتَّىٰٓ إِذَا فَرِحُواْ بِمَآ أُوتُوٓاْ أَخَذۡنَٰهُم بَغۡتَةٗ فَإِذَا هُم مُّبۡلِسُونَ

Basi walipoyasahau (na kuacha kuyafanyia kazi) yale waliyokumbushwa, tuliwafungulia milango ya kila kitu, hadi walipofurahia yale waliyopewa tuliwachukulia hatua (na kuwaadhibu) ghafla, mara moja wakawa wamekata tamaa (ya kuokoka)



Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 45

فَقُطِعَ دَابِرُ ٱلۡقَوۡمِ ٱلَّذِينَ ظَلَمُواْۚ وَٱلۡحَمۡدُ لِلَّهِ رَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ

Basi mzizi wa watu walio-dhulumu (waliomfanyia ushirika Allah) ukakatwa (wakaangamizwa wote), na kila sifa njema anaistahiki Allah Mola Mlezi wa viumbe wote



Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 46

قُلۡ أَرَءَيۡتُمۡ إِنۡ أَخَذَ ٱللَّهُ سَمۡعَكُمۡ وَأَبۡصَٰرَكُمۡ وَخَتَمَ عَلَىٰ قُلُوبِكُم مَّنۡ إِلَٰهٌ غَيۡرُ ٱللَّهِ يَأۡتِيكُم بِهِۗ ٱنظُرۡ كَيۡفَ نُصَرِّفُ ٱلۡأٓيَٰتِ ثُمَّ هُمۡ يَصۡدِفُونَ

Sema: Je, mnaonaje kama Allah atachukua usikivu wenu na macho yenu na akaziziba nyoyo zenu, ni Mungu gani asiyekuwa Allah atakayewaletea hayo? Angalia namna tunavyobainisha Aya (hoja) kisha wao wanapinga!



Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 47

قُلۡ أَرَءَيۡتَكُمۡ إِنۡ أَتَىٰكُمۡ عَذَابُ ٱللَّهِ بَغۡتَةً أَوۡ جَهۡرَةً هَلۡ يُهۡلَكُ إِلَّا ٱلۡقَوۡمُ ٱلظَّـٰلِمُونَ

Sema: Hivi mwaonaje kama itakujieni adhabu ya Allah ghafla au (ikikujieni) wazi wazi (ilhali mnaiona), si hawataangamizwa isipokuwa tu watu madhalimu (wanaomfanyia ushirika Allah)?



Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 48

وَمَا نُرۡسِلُ ٱلۡمُرۡسَلِينَ إِلَّا مُبَشِّرِينَ وَمُنذِرِينَۖ فَمَنۡ ءَامَنَ وَأَصۡلَحَ فَلَا خَوۡفٌ عَلَيۡهِمۡ وَلَا هُمۡ يَحۡزَنُونَ

Na hatutumi Mitume isipokuwa (kazi yao ni) kutoa bishara (habari njema kwa wenye kutenda mema) na kutoa maonyo (kwa watendao maovu). Basi watakaoamini na wakatenda mema, hawatakuwa na hofu na hawatahuzunika



Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 49

وَٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَا يَمَسُّهُمُ ٱلۡعَذَابُ بِمَا كَانُواْ يَفۡسُقُونَ

Na wale waliozipinga Aya zetu itawashika (itawapata) adhabu kwasababu ya uovu waliokuwa wanaufanya



Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 50

قُل لَّآ أَقُولُ لَكُمۡ عِندِي خَزَآئِنُ ٱللَّهِ وَلَآ أَعۡلَمُ ٱلۡغَيۡبَ وَلَآ أَقُولُ لَكُمۡ إِنِّي مَلَكٌۖ إِنۡ أَتَّبِعُ إِلَّا مَا يُوحَىٰٓ إِلَيَّۚ قُلۡ هَلۡ يَسۡتَوِي ٱلۡأَعۡمَىٰ وَٱلۡبَصِيرُۚ أَفَلَا تَتَفَكَّرُونَ

Sema (uwaambie): Mimi sikuambieni kuwa ninamiliki hazina za Allah, na wala sijui Ghaibu na wala sikuambieni kuwa mimi ni Malaika. Mimi sifuati isipokuwa tu wahyi (ufunuo) ninaoletewa. Sema: Hivi yuko sawa kipofu na anayeona? Hivi hamtafakari?



Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 51

وَأَنذِرۡ بِهِ ٱلَّذِينَ يَخَافُونَ أَن يُحۡشَرُوٓاْ إِلَىٰ رَبِّهِمۡ لَيۡسَ لَهُم مِّن دُونِهِۦ وَلِيّٞ وَلَا شَفِيعٞ لَّعَلَّهُمۡ يَتَّقُونَ

Na waonye kwayo (Qur’ani) wale wanao ogopa kukusanywa kwa Mola wao wakiwa hawana msimamizi wala muombezi isipokuwa yeye (Allah), ili wamche Allah



Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 52

وَلَا تَطۡرُدِ ٱلَّذِينَ يَدۡعُونَ رَبَّهُم بِٱلۡغَدَوٰةِ وَٱلۡعَشِيِّ يُرِيدُونَ وَجۡهَهُۥۖ مَا عَلَيۡكَ مِنۡ حِسَابِهِم مِّن شَيۡءٖ وَمَا مِنۡ حِسَابِكَ عَلَيۡهِم مِّن شَيۡءٖ فَتَطۡرُدَهُمۡ فَتَكُونَ مِنَ ٱلظَّـٰلِمِينَ

Na usiwafukuze wale wanaomuabudu Mola wao asubuhi na jioni, wakitaka radhi za Allah (kwa ibada zao hizo). Si jukumu lako kuwalipa chochote, na wao hawana jukumu la kukulipa chochote hadi iwe sababu ya kuwafukuza. Basi (ukifanya hivyo) utakuwa miongoni mwa madhalimu (wanaodhulumu nafsi zao kwa kufanya yasiyomridhisha Allah)



Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 53

وَكَذَٰلِكَ فَتَنَّا بَعۡضَهُم بِبَعۡضٖ لِّيَقُولُوٓاْ أَهَـٰٓؤُلَآءِ مَنَّ ٱللَّهُ عَلَيۡهِم مِّنۢ بَيۡنِنَآۗ أَلَيۡسَ ٱللَّهُ بِأَعۡلَمَ بِٱلشَّـٰكِرِينَ

Na kama hivyo tuliwatia majaribuni baadhi yao kwa wengine ili waseme: Hivi hawa ndio Allah amewaneemesha kati yetu? Hivi Allah hawajui wenye kushukuru?



Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 54

وَإِذَا جَآءَكَ ٱلَّذِينَ يُؤۡمِنُونَ بِـَٔايَٰتِنَا فَقُلۡ سَلَٰمٌ عَلَيۡكُمۡۖ كَتَبَ رَبُّكُمۡ عَلَىٰ نَفۡسِهِ ٱلرَّحۡمَةَ أَنَّهُۥ مَنۡ عَمِلَ مِنكُمۡ سُوٓءَۢا بِجَهَٰلَةٖ ثُمَّ تَابَ مِنۢ بَعۡدِهِۦ وَأَصۡلَحَ فَأَنَّهُۥ غَفُورٞ رَّحِيمٞ

Na watakapokujia wale wanao-ziamini Aya zetu sema (uwaambie): Amani iwe kwenu. Mola wenu mwenyewe rehema amejithibitishia kwamba, yeyote miongoni mwenu atakayefanya jambo ovu kwa kutojua, kisha baada yake akatubu na kurekebisha (tabia yake) basi hakika yeye (Allah) ni Msamehevu sana, Mwenye kurehemu



Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 55

وَكَذَٰلِكَ نُفَصِّلُ ٱلۡأٓيَٰتِ وَلِتَسۡتَبِينَ سَبِيلُ ٱلۡمُجۡرِمِينَ

Na kama hivyo tunazichambua Aya ili ibainike njia ya waovu



Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 56

قُلۡ إِنِّي نُهِيتُ أَنۡ أَعۡبُدَ ٱلَّذِينَ تَدۡعُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِۚ قُل لَّآ أَتَّبِعُ أَهۡوَآءَكُمۡ قَدۡ ضَلَلۡتُ إِذٗا وَمَآ أَنَا۠ مِنَ ٱلۡمُهۡتَدِينَ

Sema: Hakika, mimi nimeka-tazwa kuabudu wale (Miungu) mnaowaomba badala ya Allah. Sema: Hakika, mimi sifuati utashi wa nafsi zenu. (Nikifanya hivyo) Hakika nitakuwa nimepotea, na sitakuwa miongoni mwa watu walio ongoka



Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 57

قُلۡ إِنِّي عَلَىٰ بَيِّنَةٖ مِّن رَّبِّي وَكَذَّبۡتُم بِهِۦۚ مَا عِندِي مَا تَسۡتَعۡجِلُونَ بِهِۦٓۚ إِنِ ٱلۡحُكۡمُ إِلَّا لِلَّهِۖ يَقُصُّ ٱلۡحَقَّۖ وَهُوَ خَيۡرُ ٱلۡفَٰصِلِينَ

Sema: Hakika, mimi nipo katika hoja ya wazi itokayo kwa Mola wangu Mlezi, na nyinyi mmempinga. Mimi sina kile mnachokiharakisha. Hakuna hukumu isipokuwa ya Allah tu. Yeye anaeleza haki, na yeye ni mbora zaidi ya wakatao shauri



Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 58

قُل لَّوۡ أَنَّ عِندِي مَا تَسۡتَعۡجِلُونَ بِهِۦ لَقُضِيَ ٱلۡأَمۡرُ بَيۡنِي وَبَيۡنَكُمۡۗ وَٱللَّهُ أَعۡلَمُ بِٱلظَّـٰلِمِينَ

Sema: Lau kama ningekuwa na kile mnachokiharakisha, basi lingekwishahukumiwa jambo kati yangu na kati yenu. Na Allah anawajua zaidi madhalimu



Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 59

۞وَعِندَهُۥ مَفَاتِحُ ٱلۡغَيۡبِ لَا يَعۡلَمُهَآ إِلَّا هُوَۚ وَيَعۡلَمُ مَا فِي ٱلۡبَرِّ وَٱلۡبَحۡرِۚ وَمَا تَسۡقُطُ مِن وَرَقَةٍ إِلَّا يَعۡلَمُهَا وَلَا حَبَّةٖ فِي ظُلُمَٰتِ ٱلۡأَرۡضِ وَلَا رَطۡبٖ وَلَا يَابِسٍ إِلَّا فِي كِتَٰبٖ مُّبِينٖ

Na ziko kwake yeye (Allah) tu funguo (hazina) za Ghaibu; hakuna azijuaye isipokuwa yeye tu. Na anajua kilichopo nchi kavu na baharini. Na halidondoki jani lolote ila analijua. Na (haidondoka) punje yoyote katika giza la ardhini na kibichi na kikavu isipokuwa kipo katika kitabu kinachobainisha (kila kitu)



Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 60

وَهُوَ ٱلَّذِي يَتَوَفَّىٰكُم بِٱلَّيۡلِ وَيَعۡلَمُ مَا جَرَحۡتُم بِٱلنَّهَارِ ثُمَّ يَبۡعَثُكُمۡ فِيهِ لِيُقۡضَىٰٓ أَجَلٞ مُّسَمّٗىۖ ثُمَّ إِلَيۡهِ مَرۡجِعُكُمۡ ثُمَّ يُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ

Na yeye (Allah) ndiye ambaye anakufisheni usiku (anakutieni katika usingizi) na anajua mliyoyafanya mchana. Kisha atakufufueni humo (katika mchana) ili utimizwe muda uliowekwa. Kisha kwake tu ndio marejeo yenu, kisha atakupeni habari ya yote mliyokuwa mnayafanya



Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 61

وَهُوَ ٱلۡقَاهِرُ فَوۡقَ عِبَادِهِۦۖ وَيُرۡسِلُ عَلَيۡكُمۡ حَفَظَةً حَتَّىٰٓ إِذَا جَآءَ أَحَدَكُمُ ٱلۡمَوۡتُ تَوَفَّتۡهُ رُسُلُنَا وَهُمۡ لَا يُفَرِّطُونَ

Na yeye tu ndiye Mwenye nguvu kubwa juu ya waja wake, na anatuma kwenu (Malaika) waangalizi (wanaowalinda binadamu na kutunza kumbukumbu za matendo yao)[1], mpaka kinapomfikia mmoja wenu kifo wajumbe wetu wanamfisha, na hawafanyi uzembe


1- - Rejea Aya ya 11, Sura Arraad (13).


Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 62

ثُمَّ رُدُّوٓاْ إِلَى ٱللَّهِ مَوۡلَىٰهُمُ ٱلۡحَقِّۚ أَلَا لَهُ ٱلۡحُكۡمُ وَهُوَ أَسۡرَعُ ٱلۡحَٰسِبِينَ

Kisha watarudishwa kwa Allah, Mola wao wa haki. Ehee, elewa kwamba, hukumu ni yake yeye (Allah) tu, na yeye ni Mwepesi sana wa wanaohesabu



Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 63

قُلۡ مَن يُنَجِّيكُم مِّن ظُلُمَٰتِ ٱلۡبَرِّ وَٱلۡبَحۡرِ تَدۡعُونَهُۥ تَضَرُّعٗا وَخُفۡيَةٗ لَّئِنۡ أَنجَىٰنَا مِنۡ هَٰذِهِۦ لَنَكُونَنَّ مِنَ ٱلشَّـٰكِرِينَ

Sema: Ni nani anayekuokoeni katika giza la bara na baharini? Mnamuomba kwa unyenyekevu na kwa siri, (mkisema kwamba:) Endapo (Allah) atatuokoa kwenye haya kwa hakika kabisa tutakuwa miongoni mwa wenye kushukuru



Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 64

قُلِ ٱللَّهُ يُنَجِّيكُم مِّنۡهَا وَمِن كُلِّ كَرۡبٖ ثُمَّ أَنتُمۡ تُشۡرِكُونَ

Sema: Allah anakuokoeni kwenye hayo na kwenye kila janga, kisha nyinyi mnafanya ushirikina!



Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 65

قُلۡ هُوَ ٱلۡقَادِرُ عَلَىٰٓ أَن يَبۡعَثَ عَلَيۡكُمۡ عَذَابٗا مِّن فَوۡقِكُمۡ أَوۡ مِن تَحۡتِ أَرۡجُلِكُمۡ أَوۡ يَلۡبِسَكُمۡ شِيَعٗا وَيُذِيقَ بَعۡضَكُم بَأۡسَ بَعۡضٍۗ ٱنظُرۡ كَيۡفَ نُصَرِّفُ ٱلۡأٓيَٰتِ لَعَلَّهُمۡ يَفۡقَهُونَ

Sema: Yeye tu ndiye Muweza wa kuleta kwenu adhabu itokayo juu yenu au chini ya miguu yenu, au kukuvalisheni nguo ya mfarakano wa makundi na kukuonjesheni mkong’oto wa (nguvu za) wengine. Ona, namna tunavyozifafanua Aya (hoja) ili wapate kufahamu