فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Basi ni zipi neema za Mola wenu mnazikanusha?
Partager :
وَمِن دُونِهِمَا جَنَّتَانِ
Na zaidi ya hizo mbili, ziko bustani mbili zingine
مُدۡهَآمَّتَانِ
Za rangi ya kijani iliyokoza
فِيهِمَا عَيۡنَانِ نَضَّاخَتَانِ
Mna humo chemchemu mbili zenye kububujika kwa nguvu mfululizo
فِيهِمَا فَٰكِهَةٞ وَنَخۡلٞ وَرُمَّانٞ
Mna humo matunda na mitende na makomamanga
فِيهِنَّ خَيۡرَٰتٌ حِسَانٞ
Mna humo wanawake wema wazuri
حُورٞ مَّقۡصُورَٰتٞ فِي ٱلۡخِيَامِ
weupe wakiwa na macho mapana waliotawishwa kwenye mahema
لَمۡ يَطۡمِثۡهُنَّ إِنسٞ قَبۡلَهُمۡ وَلَا جَآنّٞ
hawajaguswa na Mtu kabla yao wala Jini
مُتَّكِـِٔينَ عَلَىٰ رَفۡرَفٍ خُضۡرٖ وَعَبۡقَرِيٍّ حِسَانٖ
Wakiegemea kwenye matakia ya kijani na mazulia ya rangi mbalimbali ya hariri mazuri mno yasiyo na kifani
تَبَٰرَكَ ٱسۡمُ رَبِّكَ ذِي ٱلۡجَلَٰلِ وَٱلۡإِكۡرَامِ
Limetukuka jina la Mola wako mwenye utukufu na ukarimu
إِذَا وَقَعَتِ ٱلۡوَاقِعَةُ
Wakati kitakapotokea Kiyama
لَيۡسَ لِوَقۡعَتِهَا كَاذِبَةٌ
Hakuna mpingaji wa kutokea kwake
خَافِضَةٞ رَّافِعَةٌ
Ni chenye kuwashusha hadhi (makafiri) na kuwanyanyua hadhi (waumini)
إِذَا رُجَّتِ ٱلۡأَرۡضُ رَجّٗا
Wakati ardhi itakapotikiswa mtikiso mkubwa
وَبُسَّتِ ٱلۡجِبَالُ بَسّٗا
Na milima ikapondwa pondwa upondwaji mkubwa
فَكَانَتۡ هَبَآءٗ مُّنۢبَثّٗا
(Kwa sababu ya kupondwa pondwa huko, milima) ikawa vumbi lenye kutawanyika
وَكُنتُمۡ أَزۡوَٰجٗا ثَلَٰثَةٗ
Na nyinyi (watu) mtakuwa namna tatu
فَأَصۡحَٰبُ ٱلۡمَيۡمَنَةِ مَآ أَصۡحَٰبُ ٱلۡمَيۡمَنَةِ
Basi watakuwepo watu wa kuliani. Je, ni kina nani watu wa kuliani?
وَأَصۡحَٰبُ ٱلۡمَشۡـَٔمَةِ مَآ أَصۡحَٰبُ ٱلۡمَشۡـَٔمَةِ
Na (watakuwepo) watu wa kushotoni. Je, ni kina nani watu wa kushotoni?
وَٱلسَّـٰبِقُونَ ٱلسَّـٰبِقُونَ
Na (watakuwepo) waliotangulia mbele, (basi) watakua mbele.[1]
1- - Hawa ni wale ambao walitangulia mbele katika mambo ya kheri duniani ndio watakuwa mbele katika vyeo vya akhera.
أُوْلَـٰٓئِكَ ٱلۡمُقَرَّبُونَ
Hao ndio watakao kurubishwa
فِي جَنَّـٰتِ ٱلنَّعِيمِ
katika pepo zenye neema