Sourate: AR-RA’D 

Verset : 2

ٱللَّهُ ٱلَّذِي رَفَعَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ بِغَيۡرِ عَمَدٖ تَرَوۡنَهَاۖ ثُمَّ ٱسۡتَوَىٰ عَلَى ٱلۡعَرۡشِۖ وَسَخَّرَ ٱلشَّمۡسَ وَٱلۡقَمَرَۖ كُلّٞ يَجۡرِي لِأَجَلٖ مُّسَمّٗىۚ يُدَبِّرُ ٱلۡأَمۡرَ يُفَصِّلُ ٱلۡأٓيَٰتِ لَعَلَّكُم بِلِقَآءِ رَبِّكُمۡ تُوقِنُونَ

Allah (pekee ndiye) aliyeziinua mbingu bila ya nguzo mnazoziona. Kisha amelingana sawa juu ya Arshi.[1] Na amelitiisha jua na mwezi[2] (kwa manufaa na maslahi ya viumbe). Kila kimoja (kati ya jua na mwezi) kinakwenda (kwenye mhimili wake) kwa muda maalumu. (Yeye Allah ndiye) Anayeendesha mambo (yote), anafafanua Aya ili mpate kuwa na yakini ya kukutana na Mola wenu Mlezi


1- - Amelingana sawa kwa namna inayowiana na Uungu wake bila ya kufananisha, kulinganisha, kukanusha au kupotosha maana.


2- - Amefanya jua na mwezi vitiifu vikifuata utaratibu na mpangilio maalum aliouweka Allah Muumba.


Sourate: AR-RA’D 

Verset : 3

وَهُوَ ٱلَّذِي مَدَّ ٱلۡأَرۡضَ وَجَعَلَ فِيهَا رَوَٰسِيَ وَأَنۡهَٰرٗاۖ وَمِن كُلِّ ٱلثَّمَرَٰتِ جَعَلَ فِيهَا زَوۡجَيۡنِ ٱثۡنَيۡنِۖ يُغۡشِي ٱلَّيۡلَ ٱلنَّهَارَۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَٰتٖ لِّقَوۡمٖ يَتَفَكَّرُونَ

Na yeye ndiye aliyeitandaza ardhi na akaweka humo milima thabiti na mito. Na katika kila matunda ameumba jozi[1]. Anaufunika usiku juu ya mchana. Hakika, katika hayo zimo ishara kwa watu wanaofikiri


1- - Viwili viwili/jike na dume


Sourate: AR-RA’D 

Verset : 4

وَفِي ٱلۡأَرۡضِ قِطَعٞ مُّتَجَٰوِرَٰتٞ وَجَنَّـٰتٞ مِّنۡ أَعۡنَٰبٖ وَزَرۡعٞ وَنَخِيلٞ صِنۡوَانٞ وَغَيۡرُ صِنۡوَانٖ يُسۡقَىٰ بِمَآءٖ وَٰحِدٖ وَنُفَضِّلُ بَعۡضَهَا عَلَىٰ بَعۡضٖ فِي ٱلۡأُكُلِۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَٰتٖ لِّقَوۡمٖ يَعۡقِلُونَ

Na kwenye ardhi kuna vipande vinavyopakana na bustani za mizabibu na mimea (mingine) na mitende inayochipua kwenye shina moja na isiyochipua kwenye shina moja. (Mimea yote hiyo) inamwagiliwa kwa maji ya aina moja (lakini mazao na ladha zake zinatofautiana). Na tunafanya baadhi yake kuwa bora kuliko mingine katika kula (ladha). Hakika, katika hayo zimo ishara kwa watu wanaotia mambo akilini



Sourate: AR-RA’D 

Verset : 5

۞وَإِن تَعۡجَبۡ فَعَجَبٞ قَوۡلُهُمۡ أَءِذَا كُنَّا تُرَٰبًا أَءِنَّا لَفِي خَلۡقٖ جَدِيدٍۗ أُوْلَـٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ بِرَبِّهِمۡۖ وَأُوْلَـٰٓئِكَ ٱلۡأَغۡلَٰلُ فِيٓ أَعۡنَاقِهِمۡۖ وَأُوْلَـٰٓئِكَ أَصۡحَٰبُ ٱلنَّارِۖ هُمۡ فِيهَا خَٰلِدُونَ

Na kama unastaajabu, basi ni ajabu sana (ule) usemi wao (kwamba): Ati tutakapokuwa mchanga, kweli kabisa tutakuwa katika umbo jipya? Hao ndio waliomkufuru Mola wao Mlezi na hao ndio wenye makongwa shingoni mwao, na hao ndio watu wa Motoni, humo watadumu



Sourate: AR-RA’D 

Verset : 6

وَيَسۡتَعۡجِلُونَكَ بِٱلسَّيِّئَةِ قَبۡلَ ٱلۡحَسَنَةِ وَقَدۡ خَلَتۡ مِن قَبۡلِهِمُ ٱلۡمَثُلَٰتُۗ وَإِنَّ رَبَّكَ لَذُو مَغۡفِرَةٖ لِّلنَّاسِ عَلَىٰ ظُلۡمِهِمۡۖ وَإِنَّ رَبَّكَ لَشَدِيدُ ٱلۡعِقَابِ

Na (Washirikina makafiri) wanakuhimiza (ulete) mabaya (adhabu) kabla ya mazuri, na wakati zilikwishapita kabla yao adhabu zinazofanana (na dhambi hizi). Na hakika, Mola wako Mlezi ni Mwenye msamaha kwa watu pamoja na udhalimu wao (wa kumkufuru Allah). Na hakika, Mola wako Mlezi ni Mkali wa kuadhibu



Sourate: AR-RA’D 

Verset : 7

وَيَقُولُ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ لَوۡلَآ أُنزِلَ عَلَيۡهِ ءَايَةٞ مِّن رَّبِّهِۦٓۗ إِنَّمَآ أَنتَ مُنذِرٞۖ وَلِكُلِّ قَوۡمٍ هَادٍ

Na waliokufuru wanasema: Mbona hakuteremshiwa muujiza kutoka kwa Mola wake Mlezi? Hakika ilivyo ni kwamba, wewe ni muonyaji tu, na kila watu wana kiongozi



Sourate: AR-RA’D 

Verset : 8

ٱللَّهُ يَعۡلَمُ مَا تَحۡمِلُ كُلُّ أُنثَىٰ وَمَا تَغِيضُ ٱلۡأَرۡحَامُ وَمَا تَزۡدَادُۚ وَكُلُّ شَيۡءٍ عِندَهُۥ بِمِقۡدَارٍ

Allah anajua mimba abebayo kila mwanamke na kinacho pungukana kinachozidi.[1] Na kila kitu kwake ni kwa kipimo (maalum)


1- - Allah pia anakijua kile kitakachozaliwa kabla ya wakati (njiti) au kitakachozaliwa baada ya kupita miezi
ya uzazi au kikiwa hai au kimekufa n.k.


Sourate: AR-RA’D 

Verset : 9

عَٰلِمُ ٱلۡغَيۡبِ وَٱلشَّهَٰدَةِ ٱلۡكَبِيرُ ٱلۡمُتَعَالِ

(Yeye Allah ni) Mjuzi wa yanayoonekana na yasioonekana, Mkubwa, Aliye juu



Sourate: AR-RA’D 

Verset : 10

سَوَآءٞ مِّنكُم مَّنۡ أَسَرَّ ٱلۡقَوۡلَ وَمَن جَهَرَ بِهِۦ وَمَنۡ هُوَ مُسۡتَخۡفِۭ بِٱلَّيۡلِ وَسَارِبُۢ بِٱلنَّهَارِ

Ni sawa (kwake) anayeficha kauli (yake) kati yenu na anayeidhihirisha na anayejibanza (anayejificha) usiku na anayetembea (kwenye mihangaiko yake) kweupe mchana



Sourate: AR-RA’D 

Verset : 11

لَهُۥ مُعَقِّبَٰتٞ مِّنۢ بَيۡنِ يَدَيۡهِ وَمِنۡ خَلۡفِهِۦ يَحۡفَظُونَهُۥ مِنۡ أَمۡرِ ٱللَّهِۗ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُغَيِّرُ مَا بِقَوۡمٍ حَتَّىٰ يُغَيِّرُواْ مَا بِأَنفُسِهِمۡۗ وَإِذَآ أَرَادَ ٱللَّهُ بِقَوۡمٖ سُوٓءٗا فَلَا مَرَدَّ لَهُۥۚ وَمَا لَهُم مِّن دُونِهِۦ مِن وَالٍ

Kila mtu anao (Malaika) wafuatiliaji mbele yake na nyuma yake wanaomhifadhi[1] kwa amri ya Allah. Hakika, Allah habadili yaliyopo kwa watu mpaka (wao wenyewe) wabadili yaliyomo nafsini mwao. Na Allah anapotaka kuwafikishia jambo baya watu hakuna wa kulizuia na (watu) hawana mlinzi yeyote badala yake


1- - Mwanadamu kila alipo ana Malaika wanaomfuatilia kwa maelekezo ya Allah; wanaomhifadhi yeye na pia kuhifadhi na kutunza kumbukumbu za mambo yote anayoyafanya na pia kauli zote anazozitamka kama ilivyotajwa katika Aya ya 18 ya Sura Qaf (50) na Aya ya 10 mpaka 12 za Sura Al-infitaar (82).


Sourate: AR-RA’D 

Verset : 12

هُوَ ٱلَّذِي يُرِيكُمُ ٱلۡبَرۡقَ خَوۡفٗا وَطَمَعٗا وَيُنشِئُ ٱلسَّحَابَ ٱلثِّقَالَ

Yeye (Allah) ndiye anayewaonyesheni umeme (wa radi) ili mhofu (kuunguzwa na umeme huo) na (muwe na) tamaa (ya kunyeshewa mvua) na huanzisha (huyaleta) mawingu mazito (yenye maji)



Sourate: AR-RA’D 

Verset : 13

وَيُسَبِّحُ ٱلرَّعۡدُ بِحَمۡدِهِۦ وَٱلۡمَلَـٰٓئِكَةُ مِنۡ خِيفَتِهِۦ وَيُرۡسِلُ ٱلصَّوَٰعِقَ فَيُصِيبُ بِهَا مَن يَشَآءُ وَهُمۡ يُجَٰدِلُونَ فِي ٱللَّهِ وَهُوَ شَدِيدُ ٱلۡمِحَالِ

Na Radi inamtakasa Allah kwa kumuhimidi na Malaika pia (wanamsabihi Allah) kwa kumuogopa. Na (Allah) anapeleka vimondo (vya umeme wa radi) na kumlengeshea (vimondo hivyo) amtakaye. Nao wanabishana kuhusu Allah hali ya kuwa Yeye ni Mkali wa kuadhibu



Sourate: AR-RA’D 

Verset : 14

لَهُۥ دَعۡوَةُ ٱلۡحَقِّۚ وَٱلَّذِينَ يَدۡعُونَ مِن دُونِهِۦ لَا يَسۡتَجِيبُونَ لَهُم بِشَيۡءٍ إِلَّا كَبَٰسِطِ كَفَّيۡهِ إِلَى ٱلۡمَآءِ لِيَبۡلُغَ فَاهُ وَمَا هُوَ بِبَٰلِغِهِۦۚ وَمَا دُعَآءُ ٱلۡكَٰفِرِينَ إِلَّا فِي ضَلَٰلٖ

Ni wake yeye (Allah) tu ulin-ganiaji (uhubiri) wa haki. Na wale wanaowaomba (Miungu wengine) badala yake hawatawajibu chochote; bali ni kama anaye nyoosha viganja vyake kwenye maji ili yafike kinywani kwake, lakini hayafiki. Na hayakuwa maombi (ulinganizi) wa makafiri ilani katika upotevu



Sourate: AR-RA’D 

Verset : 15

وَلِلَّهِۤ يَسۡجُدُۤ مَن فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ طَوۡعٗا وَكَرۡهٗا وَظِلَٰلُهُم بِٱلۡغُدُوِّ وَٱلۡأٓصَالِ۩

Na vinamsujudia Allah (viumbe vyote) viliyomo mbinguni na ardhini asubuhi na jioni vikitaka (kwa hiari)[1] na visitake (kwa lazima)[2] na (pia) vivuli vyao (vinamsujudia Allah na kumnyenyekea)


1- - Hawa ikiwa ni pamoja na waumini wanao mnyenyekea Allah wakati wa shida na raha.


2- - Hawa ikiwa ni pamoja na makafiri wanao mnyenyekea Allah wanapokuwa na shida tu.


Sourate: AR-RA’D 

Verset : 16

قُلۡ مَن رَّبُّ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ قُلِ ٱللَّهُۚ قُلۡ أَفَٱتَّخَذۡتُم مِّن دُونِهِۦٓ أَوۡلِيَآءَ لَا يَمۡلِكُونَ لِأَنفُسِهِمۡ نَفۡعٗا وَلَا ضَرّٗاۚ قُلۡ هَلۡ يَسۡتَوِي ٱلۡأَعۡمَىٰ وَٱلۡبَصِيرُ أَمۡ هَلۡ تَسۡتَوِي ٱلظُّلُمَٰتُ وَٱلنُّورُۗ أَمۡ جَعَلُواْ لِلَّهِ شُرَكَآءَ خَلَقُواْ كَخَلۡقِهِۦ فَتَشَٰبَهَ ٱلۡخَلۡقُ عَلَيۡهِمۡۚ قُلِ ٱللَّهُ خَٰلِقُ كُلِّ شَيۡءٖ وَهُوَ ٱلۡوَٰحِدُ ٱلۡقَهَّـٰرُ

Sema: Ni nani Mola Mlezi wa mbingu na ardhi? Sema: Ni Allah tu. Sema: Basi je, ilikuwaje mnawafanya wengine badala yake kuwa ni walinzi, nao hawamiliki kwa nafsi zao jema wala baya? Sema: je, anaweza kulingana kipofu na anayeona? Au linaweza kuwa sawa giza na nuru? Au wamemfanyia Allah washirika (kwamba, nao wana uwezo wa) kuumba kama aumbavyo Yeye, na (kwamba kwa washirikina) viumbe (hivyo walivyovitengeneza) kwao vina haki ya kuabudiwa kama Allah)? Sema: Allah ndiye Muumba wa kila kitu. Na Yeye ni Mmoja Mwenye kushinda



Sourate: AR-RA’D 

Verset : 17

أَنزَلَ مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءٗ فَسَالَتۡ أَوۡدِيَةُۢ بِقَدَرِهَا فَٱحۡتَمَلَ ٱلسَّيۡلُ زَبَدٗا رَّابِيٗاۖ وَمِمَّا يُوقِدُونَ عَلَيۡهِ فِي ٱلنَّارِ ٱبۡتِغَآءَ حِلۡيَةٍ أَوۡ مَتَٰعٖ زَبَدٞ مِّثۡلُهُۥۚ كَذَٰلِكَ يَضۡرِبُ ٱللَّهُ ٱلۡحَقَّ وَٱلۡبَٰطِلَۚ فَأَمَّا ٱلزَّبَدُ فَيَذۡهَبُ جُفَآءٗۖ وَأَمَّا مَا يَنفَعُ ٱلنَّاسَ فَيَمۡكُثُ فِي ٱلۡأَرۡضِۚ كَذَٰلِكَ يَضۡرِبُ ٱللَّهُ ٱلۡأَمۡثَالَ

(Allah) Ameteremsha maji kutoka mawinguni. Na mabonde yakatiririsha maji kwa kadiri yake. Na mafuriko yakachukua mapovu yaliyokusanyika juu yake. Na baadhi ya (madini) wanayo yayeyusha katika moto kwa kutaka mapambo au vyombo hutokea povu vile vile (wakati wa kuyayusha). Namna hiyo ndivyo Allah anavyopiga mifano ya haki na batili. Basi lile povu linapita kama takataka tu. Ama kinachowafaa watu hubakia kwenye ardhi. Hivi ndivyo Allah anavyopiga mifano



Sourate: AR-RA’D 

Verset : 18

لِلَّذِينَ ٱسۡتَجَابُواْ لِرَبِّهِمُ ٱلۡحُسۡنَىٰۚ وَٱلَّذِينَ لَمۡ يَسۡتَجِيبُواْ لَهُۥ لَوۡ أَنَّ لَهُم مَّا فِي ٱلۡأَرۡضِ جَمِيعٗا وَمِثۡلَهُۥ مَعَهُۥ لَٱفۡتَدَوۡاْ بِهِۦٓۚ أُوْلَـٰٓئِكَ لَهُمۡ سُوٓءُ ٱلۡحِسَابِ وَمَأۡوَىٰهُمۡ جَهَنَّمُۖ وَبِئۡسَ ٱلۡمِهَادُ

Wale waliomuitikia Mola wao Mlezi watapata wema (Pepo). Na wale wasiomuitikia, hata wangelikuwa na vyote vilivyomo katika ardhi na mfano wa hivyo, bila ya shaka wangevitoa kujikomboa. Hao watakuwa na hesabu mbaya, na makao yao ni Jahanamu. Napo ni mahala pabaya mno