Sourate: HUUD 

Verset : 66

فَلَمَّا جَآءَ أَمۡرُنَا نَجَّيۡنَا صَٰلِحٗا وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مَعَهُۥ بِرَحۡمَةٖ مِّنَّا وَمِنۡ خِزۡيِ يَوۡمِئِذٍۚ إِنَّ رَبَّكَ هُوَ ٱلۡقَوِيُّ ٱلۡعَزِيزُ

Basi ilipokuja amri yetu tulimuokoa Swaleh na wale walio amini pamoja naye kwa rehema kutoka kwetu na kutokana na fedheha ya siku hiyo. Hakika Mola wako mlezi ndiye mwenye nguvu zaidi mwenye ushindi



Sourate: HUUD 

Verset : 67

وَأَخَذَ ٱلَّذِينَ ظَلَمُواْ ٱلصَّيۡحَةُ فَأَصۡبَحُواْ فِي دِيَٰرِهِمۡ جَٰثِمِينَ

Na ukelele ukawaangamiza wale waliodhulumu, na wakapambazukiwa wakiwa maiti ndani ya majumba yao



Sourate: HUUD 

Verset : 68

كَأَن لَّمۡ يَغۡنَوۡاْ فِيهَآۗ أَلَآ إِنَّ ثَمُودَاْ كَفَرُواْ رَبَّهُمۡۗ أَلَا بُعۡدٗا لِّثَمُودَ

Kana kwamba hawakuwepo humo. Elewa! Hakika Thamud walimkufuru Mola wao mlezi. Eleweni! Maangamizi yawafike watu wa Thamudi



Sourate: HUUD 

Verset : 69

وَلَقَدۡ جَآءَتۡ رُسُلُنَآ إِبۡرَٰهِيمَ بِٱلۡبُشۡرَىٰ قَالُواْ سَلَٰمٗاۖ قَالَ سَلَٰمٞۖ فَمَا لَبِثَ أَن جَآءَ بِعِجۡلٍ حَنِيذٖ

Na hakika walikuja wajumbe wetu kwa Ibrahimu kwa bishara njema, wakasema: Salama! Naye akasema: salama! Haukupita muda akaleta ndama wa kuchoma



Sourate: HUUD 

Verset : 70

فَلَمَّا رَءَآ أَيۡدِيَهُمۡ لَا تَصِلُ إِلَيۡهِ نَكِرَهُمۡ وَأَوۡجَسَ مِنۡهُمۡ خِيفَةٗۚ قَالُواْ لَا تَخَفۡ إِنَّآ أُرۡسِلۡنَآ إِلَىٰ قَوۡمِ لُوطٖ

Na pindi alipoona mikono yao haimfikii (ndama-hawali) aliwatilia shaka, na woga ukamuingia. (Malaika) Wakamwambia: Usiogope! Hakika sisi tumetumwa kwa watu wa Lutwi’



Sourate: HUUD 

Verset : 71

وَٱمۡرَأَتُهُۥ قَآئِمَةٞ فَضَحِكَتۡ فَبَشَّرۡنَٰهَا بِإِسۡحَٰقَ وَمِن وَرَآءِ إِسۡحَٰقَ يَعۡقُوبَ

Na mkewe alikuwa kasimama, na akacheka. Basi tukambashiria (kuzaliwa mtoto) Is-haq, na baada ya Is-haq Yakubu



Sourate: HUUD 

Verset : 72

قَالَتۡ يَٰوَيۡلَتَىٰٓ ءَأَلِدُ وَأَنَا۠ عَجُوزٞ وَهَٰذَا بَعۡلِي شَيۡخًاۖ إِنَّ هَٰذَا لَشَيۡءٌ عَجِيبٞ

(Mke wa Ibrahimu) akasema: Ee, hivi nitazaa kweli ilhali mimi ni kikongwe! Na mume wangu huyu ni kizee? Hakika hili ni jambo la ajabu sana!



Sourate: HUUD 

Verset : 73

قَالُوٓاْ أَتَعۡجَبِينَ مِنۡ أَمۡرِ ٱللَّهِۖ رَحۡمَتُ ٱللَّهِ وَبَرَكَٰتُهُۥ عَلَيۡكُمۡ أَهۡلَ ٱلۡبَيۡتِۚ إِنَّهُۥ حَمِيدٞ مَّجِيدٞ

(Malaika) wakasema: hivi, unastaajabu amri ya Allah? Rehema ya Allah na baraka zake ziko kwenu, watu wa nyumba hii! Hakika Yeye ni Mwenye kusifiwaMwenye kutukuzwa



Sourate: HUUD 

Verset : 74

فَلَمَّا ذَهَبَ عَنۡ إِبۡرَٰهِيمَ ٱلرَّوۡعُ وَجَآءَتۡهُ ٱلۡبُشۡرَىٰ يُجَٰدِلُنَا فِي قَوۡمِ لُوطٍ

Na pindi hofu ilipomuondoka Ibrahimu, na ikamjia ile bishara (ya kupata mtoto), alianza kujadiliana nasi kuhusu watu wa Lutwi’



Sourate: HUUD 

Verset : 75

إِنَّ إِبۡرَٰهِيمَ لَحَلِيمٌ أَوَّـٰهٞ مُّنِيبٞ

Hakika Ibrahimu alikuwa mpole, ana huruma, na mwepesi wa kurejea kwa Allah



Sourate: HUUD 

Verset : 76

يَـٰٓإِبۡرَٰهِيمُ أَعۡرِضۡ عَنۡ هَٰذَآۖ إِنَّهُۥ قَدۡ جَآءَ أَمۡرُ رَبِّكَۖ وَإِنَّهُمۡ ءَاتِيهِمۡ عَذَابٌ غَيۡرُ مَرۡدُودٖ

(Malaika walimwambia): Ewe Ibrahimu! Hili liache! Kwa hakika kabisa amri ya Mola wako mlezi imeshafika, na hakika hao itawafika adhabu isiyo rudi nyuma



Sourate: HUUD 

Verset : 77

وَلَمَّا جَآءَتۡ رُسُلُنَا لُوطٗا سِيٓءَ بِهِمۡ وَضَاقَ بِهِمۡ ذَرۡعٗا وَقَالَ هَٰذَا يَوۡمٌ عَصِيبٞ

Na pindi wajumbe wetu walipo kuja kwa Lutwi’ alijihisi huzuni na akawaonea dhiki. Na akasema: Hii leo ni siku ngumu sana!



Sourate: HUUD 

Verset : 78

وَجَآءَهُۥ قَوۡمُهُۥ يُهۡرَعُونَ إِلَيۡهِ وَمِن قَبۡلُ كَانُواْ يَعۡمَلُونَ ٱلسَّيِّـَٔاتِۚ قَالَ يَٰقَوۡمِ هَـٰٓؤُلَآءِ بَنَاتِي هُنَّ أَطۡهَرُ لَكُمۡۖ فَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَلَا تُخۡزُونِ فِي ضَيۡفِيٓۖ أَلَيۡسَ مِنكُمۡ رَجُلٞ رَّشِيدٞ

Watu wake wakamjia mbio mbio. Na kabla ya hapo walikuwa wakitenda maovu. (Lutwi) akawaambia: Enyi watu wangu! Hawa hapa binti zangu, ndio wametakasika zaidi kwenu. Basi mcheni Allah, na msinifedheheshe mbele ya wageni wangu. Hivi, miongoni mwenu hakuna hata mmoja aliye na akili?



Sourate: HUUD 

Verset : 79

قَالُواْ لَقَدۡ عَلِمۡتَ مَا لَنَا فِي بَنَاتِكَ مِنۡ حَقّٖ وَإِنَّكَ لَتَعۡلَمُ مَا نُرِيدُ

Wakasema: Bila shaka unajua hatuna haki juu ya binti zako, na hakika unajua tunayoyataka



Sourate: HUUD 

Verset : 80

قَالَ لَوۡ أَنَّ لِي بِكُمۡ قُوَّةً أَوۡ ءَاوِيٓ إِلَىٰ رُكۡنٖ شَدِيدٖ

(Lutwi) akasema: Laiti mimi ningekuwa na nguvu ya kuwazuia, au ningekuwa na kabila na jamaa wenye nguvu tungepambana nanyi!



Sourate: HUUD 

Verset : 81

قَالُواْ يَٰلُوطُ إِنَّا رُسُلُ رَبِّكَ لَن يَصِلُوٓاْ إِلَيۡكَۖ فَأَسۡرِ بِأَهۡلِكَ بِقِطۡعٖ مِّنَ ٱلَّيۡلِ وَلَا يَلۡتَفِتۡ مِنكُمۡ أَحَدٌ إِلَّا ٱمۡرَأَتَكَۖ إِنَّهُۥ مُصِيبُهَا مَآ أَصَابَهُمۡۚ إِنَّ مَوۡعِدَهُمُ ٱلصُّبۡحُۚ أَلَيۡسَ ٱلصُّبۡحُ بِقَرِيبٖ

(Malaika) wakasema: Ewe Lutwi›! Sisi ni wajumbe wa Mola wako mlezi, hawatakufikia. Na ondoka pamoja na watu wako katika kipande cha usiku uliobaki. Na yeyote miongoni mwenu asigeuke kutazama nyuma, isipokuwa mkeo itamfika adhabu (itakayowafika wengine). Hakika miadi yao ni asubuhi. Hivi, asubuhi si karibu?



Sourate: HUUD 

Verset : 82

فَلَمَّا جَآءَ أَمۡرُنَا جَعَلۡنَا عَٰلِيَهَا سَافِلَهَا وَأَمۡطَرۡنَا عَلَيۡهَا حِجَارَةٗ مِّن سِجِّيلٖ مَّنضُودٖ

Basi ilipofika amri yetu tulikigeza (kijiji kile) juu chini, na tukawateremshia mvua ya mawe kutoka Motoni



Sourate: HUUD 

Verset : 83

مُّسَوَّمَةً عِندَ رَبِّكَۖ وَمَا هِيَ مِنَ ٱلظَّـٰلِمِينَ بِبَعِيدٖ

(Mawe) yaliyotiwa alama maalumu kwa Mola wako mlezi. Na (mawe) hayo hayawakosi madhalimu