Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 96

فَالِقُ ٱلۡإِصۡبَاحِ وَجَعَلَ ٱلَّيۡلَ سَكَنٗا وَٱلشَّمۡسَ وَٱلۡقَمَرَ حُسۡبَانٗاۚ ذَٰلِكَ تَقۡدِيرُ ٱلۡعَزِيزِ ٱلۡعَلِيمِ

(Allah) Ni Mpasuaji wa mapam-bazuko ya asubuhi na ameufanya usiku mapumziko na utulivu, na (amefanya) jua na mwezi kwenda kwa hesabu. Huo ndio mpangilio wa (Allah) Mwenye nguvu nyingi, Mjuzi sana



Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 97

وَهُوَ ٱلَّذِي جَعَلَ لَكُمُ ٱلنُّجُومَ لِتَهۡتَدُواْ بِهَا فِي ظُلُمَٰتِ ٱلۡبَرِّ وَٱلۡبَحۡرِۗ قَدۡ فَصَّلۡنَا ٱلۡأٓيَٰتِ لِقَوۡمٖ يَعۡلَمُونَ

Na yeye (Allah) ndiye aliye-kuwekeeni nyota ili zikuongozeni katika giza la bara na baharini. Hakika, tumezifafanua Aya (hizi) kwa watu wanaojua (wenye elimu)



Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 98

وَهُوَ ٱلَّذِيٓ أَنشَأَكُم مِّن نَّفۡسٖ وَٰحِدَةٖ فَمُسۡتَقَرّٞ وَمُسۡتَوۡدَعٞۗ قَدۡ فَصَّلۡنَا ٱلۡأٓيَٰتِ لِقَوۡمٖ يَفۡقَهُونَ

Na yeye (Allah) ndiye aliye-kuumbeni kwa mara ya kwanza kutoka katika nafsi moja[1]. Basi pakomahali pa kutulizana (kwa ajili yenukatika matumbo ya mama zenu) na pako mahali pa hifadhi (makaburini). Hakika tumezifafanua Aya (hizi) kwa watu wanaofahamu


1- - (ambae ni Adamu, Allah amshushie amani)


Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 99

وَهُوَ ٱلَّذِيٓ أَنزَلَ مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءٗ فَأَخۡرَجۡنَا بِهِۦ نَبَاتَ كُلِّ شَيۡءٖ فَأَخۡرَجۡنَا مِنۡهُ خَضِرٗا نُّخۡرِجُ مِنۡهُ حَبّٗا مُّتَرَاكِبٗا وَمِنَ ٱلنَّخۡلِ مِن طَلۡعِهَا قِنۡوَانٞ دَانِيَةٞ وَجَنَّـٰتٖ مِّنۡ أَعۡنَابٖ وَٱلزَّيۡتُونَ وَٱلرُّمَّانَ مُشۡتَبِهٗا وَغَيۡرَ مُتَشَٰبِهٍۗ ٱنظُرُوٓاْ إِلَىٰ ثَمَرِهِۦٓ إِذَآ أَثۡمَرَ وَيَنۡعِهِۦٓۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكُمۡ لَأٓيَٰتٖ لِّقَوۡمٖ يُؤۡمِنُونَ

Na yeye ndiye aliyeteremsha maji (mvua) kutoka mawinguni, basi kwa maji hayo tukatoa (tukaotesha) mimea ya kila kitu (aina). Tumetoa humo mimea ya kijani (ambapo) tunatoa kutokana na hiyo (mimea ya kijani) punje zilizopandana. Na katika mitende katika makole yake yapo yaliyoinama, na bustani za mizabibu na mizaituni na makomamanga yaliyofanana na yasiyofanana. Angalieni matunda yake yanapozaa na yanapoiva. Hakika, katika hayo kuna alama (mazingatio) kwa wanaoamini



Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 100

وَجَعَلُواْ لِلَّهِ شُرَكَآءَ ٱلۡجِنَّ وَخَلَقَهُمۡۖ وَخَرَقُواْ لَهُۥ بَنِينَ وَبَنَٰتِۭ بِغَيۡرِ عِلۡمٖۚ سُبۡحَٰنَهُۥ وَتَعَٰلَىٰ عَمَّا يَصِفُونَ

Na wamewafanya Majini kuwa ni washirika wa Allah, na (ilhali yeye ndiye) amewaumba, na bila ya elimu yoyote wamemzushia yeye (uongo) kuwa ana watoto wanaume na watoto wanawake. Utakatifu ni wake na ameepukana na yote wanayomuhusisha nayo



Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 101

بَدِيعُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۖ أَنَّىٰ يَكُونُ لَهُۥ وَلَدٞ وَلَمۡ تَكُن لَّهُۥ صَٰحِبَةٞۖ وَخَلَقَ كُلَّ شَيۡءٖۖ وَهُوَ بِكُلِّ شَيۡءٍ عَلِيمٞ

(Allah) Ni Muumbaji wa mbingu na ardhi. Iweje awe na mwana na (ilhali) hakuwa na mke? Na ameumba kila kitu, naye ni Mjuzi wa kila kitu



Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 102

ذَٰلِكُمُ ٱللَّهُ رَبُّكُمۡۖ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَۖ خَٰلِقُ كُلِّ شَيۡءٖ فَٱعۡبُدُوهُۚ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ وَكِيلٞ

Huyo Ndiye Allah, Mola wenu Mlezi. Hakuna mwenye haki ya kuabudiwa ila yeye tu, Muumba wa kila kitu. Basi muabudini. Na yeye ni Msimamizi mzuri sana wa kila kitu



Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 103

لَّا تُدۡرِكُهُ ٱلۡأَبۡصَٰرُ وَهُوَ يُدۡرِكُ ٱلۡأَبۡصَٰرَۖ وَهُوَ ٱللَّطِيفُ ٱلۡخَبِيرُ

Macho hayamuoni (hapa duniani) na yeye anayaona macho[1]. Na yeye ni Mpole sana, Mwenye habari (za kila kitu)


1- - Itikadi ya Watu wa Suna na Jamaa (Suni) ni kwamba, Allah haonekani hapa duniani kwa mujibu wa Aya hii na pia kwa mujibu wa: 1) Nukuu ya Mama Aisha mke wa Mtume aliyenukuliwa akisema kuwa: “Anayedai kuwa Muhammad alimuona Mola wake hakika amesema uongo”. 2) Aya ya 143 ya Sura Al-aaraaf (7) ambapo Mtume Musa alimuomba Mola wake amuwezeshe kumuona na ikashindikana. Ama Akhera Allah ataonekana kwa mujibu wa: 1) Aya ya 23 ya Sura Alqiyama (75). 2) Aya ya 15 ya Sura Almutwaffifiin (83) inayoeleza kuwa makafiri Siku ya Kiama watazuiwa kumuona Mola wao. Amesema Imamu Shaafii katika kuitafsiri Aya hii kwamba, hii inaonesha kuwa Waumini hawatazuiwa kumuona Mola wao.


Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 104

قَدۡ جَآءَكُم بَصَآئِرُ مِن رَّبِّكُمۡۖ فَمَنۡ أَبۡصَرَ فَلِنَفۡسِهِۦۖ وَمَنۡ عَمِيَ فَعَلَيۡهَاۚ وَمَآ أَنَا۠ عَلَيۡكُم بِحَفِيظٖ

Hakika, zimekujieni (hoja) zifunguazo macho kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Basi atakaeziona ni kwa faida yake na atakaejifanya kipofu basi ni hasara yake, na mimi si mlinzi wenu (sikuamrishwa kuwa mlinzi wenu)



Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 105

وَكَذَٰلِكَ نُصَرِّفُ ٱلۡأٓيَٰتِ وَلِيَقُولُواْ دَرَسۡتَ وَلِنُبَيِّنَهُۥ لِقَوۡمٖ يَعۡلَمُونَ

Na kama hivyo tunazibainisha Aya ili waseme: Umesoma (kwa mtu fulani) na ili tuzibainishe kwa watu wanaojua (wenye elimu)



Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 106

ٱتَّبِعۡ مَآ أُوحِيَ إِلَيۡكَ مِن رَّبِّكَۖ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَۖ وَأَعۡرِضۡ عَنِ ٱلۡمُشۡرِكِينَ

Fuata yale yote uliyoletewa Wahyi kutoka kwa Mola wako. Hakuna mwenye haki ya kuabudiwa isipokuwa yeye tu, na wapuuze washirikina[1]


1- - Hukumu ya Aya hii imefutwa na Aya 5 ya Sura Attauba (9).


Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 107

وَلَوۡ شَآءَ ٱللَّهُ مَآ أَشۡرَكُواْۗ وَمَا جَعَلۡنَٰكَ عَلَيۡهِمۡ حَفِيظٗاۖ وَمَآ أَنتَ عَلَيۡهِم بِوَكِيلٖ

Na lau kama Allah angetaka wasingeshirikisha. Na hatukukufanya Mlinzi wao, na wewe sio msimamizi wao



Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 108

وَلَا تَسُبُّواْ ٱلَّذِينَ يَدۡعُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ فَيَسُبُّواْ ٱللَّهَ عَدۡوَۢا بِغَيۡرِ عِلۡمٖۗ كَذَٰلِكَ زَيَّنَّا لِكُلِّ أُمَّةٍ عَمَلَهُمۡ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّهِم مَّرۡجِعُهُمۡ فَيُنَبِّئُهُم بِمَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ

Na msiwatukane wale wanao omba (wanaoabudu vitu vingine) badala ya Allah, ikawa sababu ya wao kumtukana Allah bila ya elimu yoyote (kwa ufedhuli)[1]. Kama hivyo tumefanyia kila watu waone mazuri matendo yao. Kisha ni kwa Mola wao tu marejeo yao na atawaambia yote waliyokuwa wakiyatenda


1- - Hapa Waislamu wanakatazwa kutukana wafuasi wa dini nyingine, jambo linaloweza kusababisha wanaotukanwa kujibu mapigo na hatimae nao kumtukana Allah au Mtume na kupelekea kuvunjika kwa amani na utulivu. Ama kuhubiri kwa hekima na mawaidha mazuri, kujadiliana kwa namna nzuri ni jambo linalotakiwa kufanywa.


Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 109

وَأَقۡسَمُواْ بِٱللَّهِ جَهۡدَ أَيۡمَٰنِهِمۡ لَئِن جَآءَتۡهُمۡ ءَايَةٞ لَّيُؤۡمِنُنَّ بِهَاۚ قُلۡ إِنَّمَا ٱلۡأٓيَٰتُ عِندَ ٱللَّهِۖ وَمَا يُشۡعِرُكُمۡ أَنَّهَآ إِذَا جَآءَتۡ لَا يُؤۡمِنُونَ

Na wameapa kwa Allah kwa Imani yao yote kwamba: Kwa yakini kabisa, endapo itawajia Aya yoyote (muujiza) wataiamini. Waambie: Hakika, Aya zote zipo kwa Allah. Na ni kipi kitakachokutambulisheni kuwa zitakapokuja (hizo Aya) hawataamini?



Sourate: AL-AN’AAM 

Verset : 110

وَنُقَلِّبُ أَفۡـِٔدَتَهُمۡ وَأَبۡصَٰرَهُمۡ كَمَا لَمۡ يُؤۡمِنُواْ بِهِۦٓ أَوَّلَ مَرَّةٖ وَنَذَرُهُمۡ فِي طُغۡيَٰنِهِمۡ يَعۡمَهُونَ

Na tunazigeuza nyoyo zao na macho yao kama vile ambavyo hawakumuamini (Mtume) mara ya kwanza, na tutawaacha wakitangatanga katika uovu wao