Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 105

مَّا يَوَدُّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ مِنۡ أَهۡلِ ٱلۡكِتَٰبِ وَلَا ٱلۡمُشۡرِكِينَ أَن يُنَزَّلَ عَلَيۡكُم مِّنۡ خَيۡرٖ مِّن رَّبِّكُمۡۚ وَٱللَّهُ يَخۡتَصُّ بِرَحۡمَتِهِۦ مَن يَشَآءُۚ وَٱللَّهُ ذُو ٱلۡفَضۡلِ ٱلۡعَظِيمِ

Watu wa Kitabu waliokufuru na washirikishaji hawapendi mteremshiwe heri yoyote kutoka kwa Mola wenu. Na Allah humkusudia (kumpa) rehema zake amtakaye, na Allah ni Mwenye fadhila kubwa



Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 106

۞مَا نَنسَخۡ مِنۡ ءَايَةٍ أَوۡ نُنسِهَا نَأۡتِ بِخَيۡرٖ مِّنۡهَآ أَوۡ مِثۡلِهَآۗ أَلَمۡ تَعۡلَمۡ أَنَّ ٱللَّهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٌ

Hakuna Aya yoyote tunayoifuta au kuisahaulisha isipokuwa kwamba tunaleta iliyo bora zaidi kuliko ile au iliyo mfano wake. Je, hujui kwamba Allah ni Muweza wa kila jambo?



Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 107

أَلَمۡ تَعۡلَمۡ أَنَّ ٱللَّهَ لَهُۥ مُلۡكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۗ وَمَا لَكُم مِّن دُونِ ٱللَّهِ مِن وَلِيّٖ وَلَا نَصِيرٍ

Je, hujui kwamba Allah ndiye Mwenye ufalme wa mbinguni na ardhini? Na nyinyi hamna mlinzi wala msaidizi mwingine badala ya Allah



Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 108

أَمۡ تُرِيدُونَ أَن تَسۡـَٔلُواْ رَسُولَكُمۡ كَمَا سُئِلَ مُوسَىٰ مِن قَبۡلُۗ وَمَن يَتَبَدَّلِ ٱلۡكُفۡرَ بِٱلۡإِيمَٰنِ فَقَدۡ ضَلَّ سَوَآءَ ٱلسَّبِيلِ

Au mnataka kumuuliza Mtume wenu kama (Mtume) Musa alivyoulizwa hapo zamani? Na anayebadilisha imani kwa ukafiri, bila shaka ameipotea njia yasawa



Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 109

وَدَّ كَثِيرٞ مِّنۡ أَهۡلِ ٱلۡكِتَٰبِ لَوۡ يَرُدُّونَكُم مِّنۢ بَعۡدِ إِيمَٰنِكُمۡ كُفَّارًا حَسَدٗا مِّنۡ عِندِ أَنفُسِهِم مِّنۢ بَعۡدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمُ ٱلۡحَقُّۖ فَٱعۡفُواْ وَٱصۡفَحُواْ حَتَّىٰ يَأۡتِيَ ٱللَّهُ بِأَمۡرِهِۦٓۗ إِنَّ ٱللَّهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٞ

Watu wa Kitabu wengi wanapenda laiti wakurudisheni muwe makafiri baada ya kuamini kwenu, kwa sababu ya husuda iliyomo nyoyoni mwao baada ya kuwa haki imewapambanukia. Basi sameheni na puuzeni mpaka Allah alete amri yake. Hakika, Allah ni Muweza sana wa kila jambo



Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 110

وَأَقِيمُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتُواْ ٱلزَّكَوٰةَۚ وَمَا تُقَدِّمُواْ لِأَنفُسِكُم مِّنۡ خَيۡرٖ تَجِدُوهُ عِندَ ٱللَّهِۗ إِنَّ ٱللَّهَ بِمَا تَعۡمَلُونَ بَصِيرٞ

Na simamisheni Swala na toeni Zaka, na heri yoyote muitanguliziayo kwa ajili yenu mtaikuta mbele ya Allah. Hakika, Allah anayaona mno mnayoyatenda



Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 111

وَقَالُواْ لَن يَدۡخُلَ ٱلۡجَنَّةَ إِلَّا مَن كَانَ هُودًا أَوۡ نَصَٰرَىٰۗ تِلۡكَ أَمَانِيُّهُمۡۗ قُلۡ هَاتُواْ بُرۡهَٰنَكُمۡ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ

Na wamesema: Katu, hataingia Peponi isipokuwa tu Myahudi au Mnaswara! Hayo ndio matamanio yao. Sema: Leteni ushahidi wenu kama ninyi ni wa kweli



Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 112

بَلَىٰۚ مَنۡ أَسۡلَمَ وَجۡهَهُۥ لِلَّهِ وَهُوَ مُحۡسِنٞ فَلَهُۥٓ أَجۡرُهُۥ عِندَ رَبِّهِۦ وَلَا خَوۡفٌ عَلَيۡهِمۡ وَلَا هُمۡ يَحۡزَنُونَ

Naam, wenye kujisalimisha kwa Allah na ilhali wanatenda yaliyo mazuri, basi watapata malipo yao kwa Mola wao, na hawatakuwa na hofu na hawatahuzunika



Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 113

وَقَالَتِ ٱلۡيَهُودُ لَيۡسَتِ ٱلنَّصَٰرَىٰ عَلَىٰ شَيۡءٖ وَقَالَتِ ٱلنَّصَٰرَىٰ لَيۡسَتِ ٱلۡيَهُودُ عَلَىٰ شَيۡءٖ وَهُمۡ يَتۡلُونَ ٱلۡكِتَٰبَۗ كَذَٰلِكَ قَالَ ٱلَّذِينَ لَا يَعۡلَمُونَ مِثۡلَ قَوۡلِهِمۡۚ فَٱللَّهُ يَحۡكُمُ بَيۡنَهُمۡ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ فِيمَا كَانُواْ فِيهِ يَخۡتَلِفُونَ

Na Wayahudi wamesema: Manaswara hawa na kitu (chochote cha maana). Na Manaswara wame-sema: Wayahudi hawana kitu (chochote cha maana), na wao (wote) wanasoma Kitabu (kitakatifu kitokacho kwa Mola wao). Kama hivyo, wale ambao hawajui kitu wamesema mfano wa maneno yao. Basi Allah atahukumu baina yao Siku ya Kiyama katika yale waliyokuwa wakitafautiana



Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 114

وَمَنۡ أَظۡلَمُ مِمَّن مَّنَعَ مَسَٰجِدَ ٱللَّهِ أَن يُذۡكَرَ فِيهَا ٱسۡمُهُۥ وَسَعَىٰ فِي خَرَابِهَآۚ أُوْلَـٰٓئِكَ مَا كَانَ لَهُمۡ أَن يَدۡخُلُوهَآ إِلَّا خَآئِفِينَۚ لَهُمۡ فِي ٱلدُّنۡيَا خِزۡيٞ وَلَهُمۡ فِي ٱلۡأٓخِرَةِ عَذَابٌ عَظِيمٞ

Na ninani dhalimu zaidi kuliko yule azuiaye Misikitiya Allah kutajwa humo jina lake na kujitahidi kuiharibu? Hao haitawawia kuingia humo ila kwa kuogopa. Watapata fedheha katika dunia, na akhera watapata adhabu kubwa



Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 115

وَلِلَّهِ ٱلۡمَشۡرِقُ وَٱلۡمَغۡرِبُۚ فَأَيۡنَمَا تُوَلُّواْ فَثَمَّ وَجۡهُ ٱللَّهِۚ إِنَّ ٱللَّهَ وَٰسِعٌ عَلِيمٞ

Mashariki na magharibi ni ya Allah. Hakika Allah ni Mwenye ukwasi, Mwenye kujua



Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 116

وَقَالُواْ ٱتَّخَذَ ٱللَّهُ وَلَدٗاۗ سُبۡحَٰنَهُۥۖ بَل لَّهُۥ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۖ كُلّٞ لَّهُۥ قَٰنِتُونَ

Na (Makafiri wote) wamesema: Allah amefanya mtoto. Utakasifu ni wake. Bali ni miliki yake yeye tu vilivyomo mbinguni na ardhini. Vyote vina myenyekea yeye tu



Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 117

بَدِيعُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۖ وَإِذَا قَضَىٰٓ أَمۡرٗا فَإِنَّمَا يَقُولُ لَهُۥ كُن فَيَكُونُ

Muanzilishi wa mbingu na ardhi. Na anapopitisha jambo liwe, basi huliambia tu “kuwa” na linakuwa



Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 118

وَقَالَ ٱلَّذِينَ لَا يَعۡلَمُونَ لَوۡلَا يُكَلِّمُنَا ٱللَّهُ أَوۡ تَأۡتِينَآ ءَايَةٞۗ كَذَٰلِكَ قَالَ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِم مِّثۡلَ قَوۡلِهِمۡۘ تَشَٰبَهَتۡ قُلُوبُهُمۡۗ قَدۡ بَيَّنَّا ٱلۡأٓيَٰتِ لِقَوۡمٖ يُوقِنُونَ

Na walisema wasiojua (kitu kwamba): Kwanini Allah asituambie wenyewe, au usitujie muujiza!? Kama hivyo walisema waliokuwa kabla yao mfano wa kauli yao hiyo. Zimefanana nyoyo zao. Hakika tumebainisha miujiza mbalimbali kwa watu wanaoamini



Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 119

إِنَّآ أَرۡسَلۡنَٰكَ بِٱلۡحَقِّ بَشِيرٗا وَنَذِيرٗاۖ وَلَا تُسۡـَٔلُ عَنۡ أَصۡحَٰبِ ٱلۡجَحِيمِ

Hakika sisi tumekutuma kwa haki ukiwa mwenye kutoa habari njema na kutahadharisha. Na wala hutaulizwa kuhusu watu wa motoni



Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 120

وَلَن تَرۡضَىٰ عَنكَ ٱلۡيَهُودُ وَلَا ٱلنَّصَٰرَىٰ حَتَّىٰ تَتَّبِعَ مِلَّتَهُمۡۗ قُلۡ إِنَّ هُدَى ٱللَّهِ هُوَ ٱلۡهُدَىٰۗ وَلَئِنِ ٱتَّبَعۡتَ أَهۡوَآءَهُم بَعۡدَ ٱلَّذِي جَآءَكَ مِنَ ٱلۡعِلۡمِ مَا لَكَ مِنَ ٱللَّهِ مِن وَلِيّٖ وَلَا نَصِيرٍ

Na kamwe hawatakuridhia Wayahudi na Wanaswara hadi utakapoifuata dini yao. Sema: Muongozo wa Allah ndio muongozo. Na ikiwa utafuata matamanio yao baada ya elimu iliyo kujia, basi hutampata yeyote wa kukutetea wala wa kukunusuru zaidi ya Allah



Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 121

ٱلَّذِينَ ءَاتَيۡنَٰهُمُ ٱلۡكِتَٰبَ يَتۡلُونَهُۥ حَقَّ تِلَاوَتِهِۦٓ أُوْلَـٰٓئِكَ يُؤۡمِنُونَ بِهِۦۗ وَمَن يَكۡفُرۡ بِهِۦ فَأُوْلَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡخَٰسِرُونَ

Wale ambao tumewapa kitabu (wakawa) wanakisoma ipasavyo, basi hao ndio wanaokiamini, na wale watakaokipinga basi hao ndio wenye kupata hasara



Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 122

يَٰبَنِيٓ إِسۡرَـٰٓءِيلَ ٱذۡكُرُواْ نِعۡمَتِيَ ٱلَّتِيٓ أَنۡعَمۡتُ عَلَيۡكُمۡ وَأَنِّي فَضَّلۡتُكُمۡ عَلَى ٱلۡعَٰلَمِينَ

Enyi Wana wa Israili, kum-bukeni neema zangu ambazo nime-kuneemesheni, na nimekufanyeni bora zaidi kuliko walimwengu (wa wakati wenu)



Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 123

وَٱتَّقُواْ يَوۡمٗا لَّا تَجۡزِي نَفۡسٌ عَن نَّفۡسٖ شَيۡـٔٗا وَلَا يُقۡبَلُ مِنۡهَا عَدۡلٞ وَلَا تَنفَعُهَا شَفَٰعَةٞ وَلَا هُمۡ يُنصَرُونَ

Na iogopeni siku ambayo nafsi haitaifaa nafsi nyingine (kwa) chochote, na haitakubaliwa nafsi hiyo fidia wala kuombewa msamaha na kamwe hawatanusuriwa



Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 124

۞وَإِذِ ٱبۡتَلَىٰٓ إِبۡرَٰهِـۧمَ رَبُّهُۥ بِكَلِمَٰتٖ فَأَتَمَّهُنَّۖ قَالَ إِنِّي جَاعِلُكَ لِلنَّاسِ إِمَامٗاۖ قَالَ وَمِن ذُرِّيَّتِيۖ قَالَ لَا يَنَالُ عَهۡدِي ٱلظَّـٰلِمِينَ

Na (Kumbuka) Allah alipompa mtihani Ibrahimu wa maneno akayatimiza. Akasema: Hakika mimi nimekufanya kiongozi kwa watu. Akasema (Ibrahimu huku akiomba): Na katika kizazi changu? (Allah) Akasema: Ahadi yangu (hii) hawataipata madhalimu



Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 125

وَإِذۡ جَعَلۡنَا ٱلۡبَيۡتَ مَثَابَةٗ لِّلنَّاسِ وَأَمۡنٗا وَٱتَّخِذُواْ مِن مَّقَامِ إِبۡرَٰهِـۧمَ مُصَلّٗىۖ وَعَهِدۡنَآ إِلَىٰٓ إِبۡرَٰهِـۧمَ وَإِسۡمَٰعِيلَ أَن طَهِّرَا بَيۡتِيَ لِلطَّآئِفِينَ وَٱلۡعَٰكِفِينَ وَٱلرُّكَّعِ ٱلسُّجُودِ

Na (kumbuka) tulipoifanya Kaaba sehemu ya watu kurejea na mahali pa amani, nafanyeni mahali aliposimama Ibrahimu mahali pakuswali. Na tukawaagiza Ibrahimu na Ismaili, (kuwa) itwaharisheni Nyumba yangu kwa ajili ya wanaofanya twawafu na wanaokaa itikafu na wanaorukuu na kusujudu



Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 126

وَإِذۡ قَالَ إِبۡرَٰهِـۧمُ رَبِّ ٱجۡعَلۡ هَٰذَا بَلَدًا ءَامِنٗا وَٱرۡزُقۡ أَهۡلَهُۥ مِنَ ٱلثَّمَرَٰتِ مَنۡ ءَامَنَ مِنۡهُم بِٱللَّهِ وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِۚ قَالَ وَمَن كَفَرَ فَأُمَتِّعُهُۥ قَلِيلٗا ثُمَّ أَضۡطَرُّهُۥٓ إِلَىٰ عَذَابِ ٱلنَّارِۖ وَبِئۡسَ ٱلۡمَصِيرُ

Na (kumbuka) aliposema Ibrahimu: “Ewe Mola wangu, ufanye mji huu (wa Makkah) uwe wa amani, na waruzuku watu wake katika matunda; yule aliye muamini Allah miongoni mwao na kuamini Siku ya Mwisho. (Allah) akasema: Na mwenye kukufuru nitamstarehesha kidogo kisha nitamswaga kwenda kwenye adhabu ya moto, na hatima mbaya mno ni hiyo



Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 127

وَإِذۡ يَرۡفَعُ إِبۡرَٰهِـۧمُ ٱلۡقَوَاعِدَ مِنَ ٱلۡبَيۡتِ وَإِسۡمَٰعِيلُ رَبَّنَا تَقَبَّلۡ مِنَّآۖ إِنَّكَ أَنتَ ٱلسَّمِيعُ ٱلۡعَلِيمُ

Na (kumbuka wakati) Ibrahimu na Ismaili wanainua misingi ya Kaaba (wakisema): “Ewe Mola wetu, tukubalie. Hakika, wewe ndiye msikivu, mjuzi sana



Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 128

رَبَّنَا وَٱجۡعَلۡنَا مُسۡلِمَيۡنِ لَكَ وَمِن ذُرِّيَّتِنَآ أُمَّةٗ مُّسۡلِمَةٗ لَّكَ وَأَرِنَا مَنَاسِكَنَا وَتُبۡ عَلَيۡنَآۖ إِنَّكَ أَنتَ ٱلتَّوَّابُ ٱلرَّحِيمُ

Ewe Mola wetu, tufanye sisi tuwe watiifu kwako, na katika kizazi chetu wawe umma mtiifu kwako. Na tuelekeze ibada zetu na pokea toba zetu. Hakika wewe tu ndiye mwingi wa kupokea toba mwingi wa rehema



Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 129

رَبَّنَا وَٱبۡعَثۡ فِيهِمۡ رَسُولٗا مِّنۡهُمۡ يَتۡلُواْ عَلَيۡهِمۡ ءَايَٰتِكَ وَيُعَلِّمُهُمُ ٱلۡكِتَٰبَ وَٱلۡحِكۡمَةَ وَيُزَكِّيهِمۡۖ إِنَّكَ أَنتَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡحَكِيمُ

Ewe Mola wetu, na wapelekee Mtume miongoni mwao, atakayewasomea Aya zako na kuwafundisha kitabu na hekima na kuwatakasa. Hakika wewe tu ndiye mwenye nguvu kubwa mwingi wa hekima



Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 130

وَمَن يَرۡغَبُ عَن مِّلَّةِ إِبۡرَٰهِـۧمَ إِلَّا مَن سَفِهَ نَفۡسَهُۥۚ وَلَقَدِ ٱصۡطَفَيۡنَٰهُ فِي ٱلدُّنۡيَاۖ وَإِنَّهُۥ فِي ٱلۡأٓخِرَةِ لَمِنَ ٱلصَّـٰلِحِينَ

Na hakuna anayeichukia dini ya Ibrahimu isipokuwa yule anayejitia upumbavu. Na bila shaka tumemteua duniani, na hakika akhera atakuwa miongoni mwa watu wema



Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 131

إِذۡ قَالَ لَهُۥ رَبُّهُۥٓ أَسۡلِمۡۖ قَالَ أَسۡلَمۡتُ لِرَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ

Na (kumbuka) Mola wake alipomwambia: Jisalimishe. Akasema: Nimejisalimisha kwa Mola wa walimwengu wote



Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 132

وَوَصَّىٰ بِهَآ إِبۡرَٰهِـۧمُ بَنِيهِ وَيَعۡقُوبُ يَٰبَنِيَّ إِنَّ ٱللَّهَ ٱصۡطَفَىٰ لَكُمُ ٱلدِّينَ فَلَا تَمُوتُنَّ إِلَّا وَأَنتُم مُّسۡلِمُونَ

Na Ibrahimu aliwausia hayo watoto wake na Yakubu (kwa kuwaambia): “Enyi watoto wangu, hakika Allah amekuteulieni dini, basi msife isipokuwa mkiwa Waisilamu



Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 133

أَمۡ كُنتُمۡ شُهَدَآءَ إِذۡ حَضَرَ يَعۡقُوبَ ٱلۡمَوۡتُ إِذۡ قَالَ لِبَنِيهِ مَا تَعۡبُدُونَ مِنۢ بَعۡدِيۖ قَالُواْ نَعۡبُدُ إِلَٰهَكَ وَإِلَٰهَ ءَابَآئِكَ إِبۡرَٰهِـۧمَ وَإِسۡمَٰعِيلَ وَإِسۡحَٰقَ إِلَٰهٗا وَٰحِدٗا وَنَحۡنُ لَهُۥ مُسۡلِمُونَ

Je, mlikuwepo wakati Yakubu yalipomfika mauti, pale alipowaambia watoto wake: Mtaabudu nini baada yangu? Wakasema: Tutamuabudu Mola wako na (ambaye ndiye) Mola wa baba zako Ibrahimu na Ismaili na Is-haka, Mola Mmoja, na sisi tumejisalimisha kwake tu



Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 134

تِلۡكَ أُمَّةٞ قَدۡ خَلَتۡۖ لَهَا مَا كَسَبَتۡ وَلَكُم مَّا كَسَبۡتُمۡۖ وَلَا تُسۡـَٔلُونَ عَمَّا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ

Huo ni umma umeshapita. Utapata ulicho kichuma na nyinyi mtapata mlicho kichuma. Na hamtaulizwa kuhusu waliyokuwa wakiyafanya