Sourate: AR-RA’D 

Verset : 19

۞أَفَمَن يَعۡلَمُ أَنَّمَآ أُنزِلَ إِلَيۡكَ مِن رَّبِّكَ ٱلۡحَقُّ كَمَنۡ هُوَ أَعۡمَىٰٓۚ إِنَّمَا يَتَذَكَّرُ أُوْلُواْ ٱلۡأَلۡبَٰبِ

Je, anayejua ya kwamba yaliyo teremshwa kwako kutoka kwa Mola wako Mlezi ni haki ni sawa na aliye kipofu? Kwa hakika kabisa, wenye akili ndio wanaozingatia



Sourate: AR-RA’D 

Verset : 20

ٱلَّذِينَ يُوفُونَ بِعَهۡدِ ٱللَّهِ وَلَا يَنقُضُونَ ٱلۡمِيثَٰقَ

Wale (wenye akili ndio) wana-otimiza ahadi za Allah, wala hawa-vunji maagano



Sourate: AR-RA’D 

Verset : 21

وَٱلَّذِينَ يَصِلُونَ مَآ أَمَرَ ٱللَّهُ بِهِۦٓ أَن يُوصَلَ وَيَخۡشَوۡنَ رَبَّهُمۡ وَيَخَافُونَ سُوٓءَ ٱلۡحِسَابِ

Na wale (wenye akili ndio) ambao huyaunga aliyoamrisha Allah yaungwe, na wanaihofu hesabu mbaya



Sourate: AR-RA’D 

Verset : 22

وَٱلَّذِينَ صَبَرُواْ ٱبۡتِغَآءَ وَجۡهِ رَبِّهِمۡ وَأَقَامُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَأَنفَقُواْ مِمَّا رَزَقۡنَٰهُمۡ سِرّٗا وَعَلَانِيَةٗ وَيَدۡرَءُونَ بِٱلۡحَسَنَةِ ٱلسَّيِّئَةَ أُوْلَـٰٓئِكَ لَهُمۡ عُقۡبَى ٱلدَّارِ

Na ambao husubiri kwa kutaka radhi za Mola wao Mlezi, na wakasimamisha Swala, na wakatoa katika tulivyowaruzuku kwa siri na kwa uwazi, na wakayaondoa maovu kwa mema. Hao ndio watakaopata malipo ya nyumba ya Akhera



Sourate: AR-RA’D 

Verset : 23

جَنَّـٰتُ عَدۡنٖ يَدۡخُلُونَهَا وَمَن صَلَحَ مِنۡ ءَابَآئِهِمۡ وَأَزۡوَٰجِهِمۡ وَذُرِّيَّـٰتِهِمۡۖ وَٱلۡمَلَـٰٓئِكَةُ يَدۡخُلُونَ عَلَيۡهِم مِّن كُلِّ بَابٖ

Nazo ni Bustani za milele, wataingia wao na waliyo wema miongoni mwa Baba zao, na wake zao, na vizazi vyao (hata kama hawakufikia daraja za ucha Mungu). Na Malaika wanaingia kwao wao katika kila mlango



Sourate: AR-RA’D 

Verset : 24

سَلَٰمٌ عَلَيۡكُم بِمَا صَبَرۡتُمۡۚ فَنِعۡمَ عُقۡبَى ٱلدَّارِ

(Wakiwaambia) Assalamu Alaikum, Amani iwe kwenu, kwasababu ya mlivyo subiri, basi ni mema mno malipo ya nyumba ya Akhera



Sourate: AR-RA’D 

Verset : 25

وَٱلَّذِينَ يَنقُضُونَ عَهۡدَ ٱللَّهِ مِنۢ بَعۡدِ مِيثَٰقِهِۦ وَيَقۡطَعُونَ مَآ أَمَرَ ٱللَّهُ بِهِۦٓ أَن يُوصَلَ وَيُفۡسِدُونَ فِي ٱلۡأَرۡضِ أُوْلَـٰٓئِكَ لَهُمُ ٱللَّعۡنَةُ وَلَهُمۡ سُوٓءُ ٱلدَّارِ

Na wale wanaovunja ahadi za Allah baada ya kuzifunga, na wanakata aliyoamrisha Allah yaungwe, na wanafanya uharibifu katika nchi: hao ndio watakaopata laana, na watapata nyumba mbaya



Sourate: AR-RA’D 

Verset : 26

ٱللَّهُ يَبۡسُطُ ٱلرِّزۡقَ لِمَن يَشَآءُ وَيَقۡدِرُۚ وَفَرِحُواْ بِٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا وَمَا ٱلۡحَيَوٰةُ ٱلدُّنۡيَا فِي ٱلۡأٓخِرَةِ إِلَّا مَتَٰعٞ

Allah humkunjulia riziki amtakaye, na huibana. Na (watu wa Makkah) wamefurahia maisha ya dunia. Na uhai wa dunia kwa kulinganisha na Akhera si kitu ila ni starehe ndogo



Sourate: AR-RA’D 

Verset : 27

وَيَقُولُ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ لَوۡلَآ أُنزِلَ عَلَيۡهِ ءَايَةٞ مِّن رَّبِّهِۦۚ قُلۡ إِنَّ ٱللَّهَ يُضِلُّ مَن يَشَآءُ وَيَهۡدِيٓ إِلَيۡهِ مَنۡ أَنَابَ

Na wanasema waliokufuru: Kwa nini hakuteremshiwa muujiza kutoka kwa Mola wake Mlezi. Sema: Hakika Allah humpoteza amtakaye, na humuongoza atakaye kuelekea kwake



Sourate: AR-RA’D 

Verset : 28

ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَتَطۡمَئِنُّ قُلُوبُهُم بِذِكۡرِ ٱللَّهِۗ أَلَا بِذِكۡرِ ٱللَّهِ تَطۡمَئِنُّ ٱلۡقُلُوبُ

Wale walioamini na zikatua nyoyo zao kwa kumkumbuka Allah. Hakika kwa kumkumbuka Allah ndio nyoyo hutulia



Sourate: AR-RA’D 

Verset : 29

ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّـٰلِحَٰتِ طُوبَىٰ لَهُمۡ وَحُسۡنُ مَـَٔابٖ

Wale walioamini na wakatenda mema watakuwa na raha na marejeo mazuri



Sourate: AR-RA’D 

Verset : 30

كَذَٰلِكَ أَرۡسَلۡنَٰكَ فِيٓ أُمَّةٖ قَدۡ خَلَتۡ مِن قَبۡلِهَآ أُمَمٞ لِّتَتۡلُوَاْ عَلَيۡهِمُ ٱلَّذِيٓ أَوۡحَيۡنَآ إِلَيۡكَ وَهُمۡ يَكۡفُرُونَ بِٱلرَّحۡمَٰنِۚ قُلۡ هُوَ رَبِّي لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ عَلَيۡهِ تَوَكَّلۡتُ وَإِلَيۡهِ مَتَابِ

(Kama tulivyowatuma Mitume waliotangulia) kama hivyo tulikutuma kwa umma ambao ulikwishapita kabla yao nyumati nyingine, ili uwasomee tunayokufunulia, na wao wanamkufuru Rahmani, Sema: Yeye ndiye Mola wangu Mlezi. Hapana muabudiwa wa haki isipokuwa Yeye tu. Kwake tu nimetegemea, na kwake tu ndio marejeo



Sourate: AR-RA’D 

Verset : 31

وَلَوۡ أَنَّ قُرۡءَانٗا سُيِّرَتۡ بِهِ ٱلۡجِبَالُ أَوۡ قُطِّعَتۡ بِهِ ٱلۡأَرۡضُ أَوۡ كُلِّمَ بِهِ ٱلۡمَوۡتَىٰۗ بَل لِّلَّهِ ٱلۡأَمۡرُ جَمِيعًاۗ أَفَلَمۡ يَاْيۡـَٔسِ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ أَن لَّوۡ يَشَآءُ ٱللَّهُ لَهَدَى ٱلنَّاسَ جَمِيعٗاۗ وَلَا يَزَالُ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ تُصِيبُهُم بِمَا صَنَعُواْ قَارِعَةٌ أَوۡ تَحُلُّ قَرِيبٗا مِّن دَارِهِمۡ حَتَّىٰ يَأۡتِيَ وَعۡدُ ٱللَّهِۚ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُخۡلِفُ ٱلۡمِيعَادَ

(Hii Qur’an ilitosha kabisa kuwa muujiza, lau wangekuwa na akili) Na kama ingelikuwa (hii) Qur’ani ndiyo itumikayo kung’olea milima (kwa kule kuteremka na kusomwa kwake), au kupasuliwa ardhi (ili iwe mito, n.k) na kusemeshewa wafu (kusomewa ili wawe hai), (basi ingelikuwa hii Qur’ani! Na pia wasingeamini). Bali mambo yote ni ya Allah. Je, hawajajua walioamini kwamba lau Allah angependa bila ya shaka angewaongoa watu wote (wawe waumini)? Wala wale waliokufuru hawaachi kusibiwa na majanga kwa waliyoyatenda, au ikawateremkia (adhabu) karibu na nyumbani kwao, mpaka ifike ahadi ya Allah. Hakika Allah havunji miadi yake



Sourate: AR-RA’D 

Verset : 32

وَلَقَدِ ٱسۡتُهۡزِئَ بِرُسُلٖ مِّن قَبۡلِكَ فَأَمۡلَيۡتُ لِلَّذِينَ كَفَرُواْ ثُمَّ أَخَذۡتُهُمۡۖ فَكَيۡفَ كَانَ عِقَابِ

Na hakika walifanyiwa kejeli Mitume waliokuwa kabla yako. Na nikawapa muda (wa kujitafakari na kutubu) wale waliokufuru, kisha nikawashika (kwa adhabu kali), Basi ilikuwaje adhabu yangu (itokanayo na shere na kufuru zao)!?



Sourate: AR-RA’D 

Verset : 33

أَفَمَنۡ هُوَ قَآئِمٌ عَلَىٰ كُلِّ نَفۡسِۭ بِمَا كَسَبَتۡۗ وَجَعَلُواْ لِلَّهِ شُرَكَآءَ قُلۡ سَمُّوهُمۡۚ أَمۡ تُنَبِّـُٔونَهُۥ بِمَا لَا يَعۡلَمُ فِي ٱلۡأَرۡضِ أَم بِظَٰهِرٖ مِّنَ ٱلۡقَوۡلِۗ بَلۡ زُيِّنَ لِلَّذِينَ كَفَرُواْ مَكۡرُهُمۡ وَصُدُّواْ عَنِ ٱلسَّبِيلِۗ وَمَن يُضۡلِلِ ٱللَّهُ فَمَا لَهُۥ مِنۡ هَادٖ

Je, (analingana sawa yule) Msimamizi wa kila nafsi (na Mjuzi) wa wachumayo, na wakamfanyia Allah washirika! Sema watajeni. Au ndio mnampa (Allah) habari ya (washirika) asio na habari nao katika (mbingu na) ardhi; au (ndio mnawasifu hao washirika) kwa maneno matupu? Bali waliokufuru wamepambiwa vitimbi vyao na wamezuiliwa njia (ya haki). Na ambaye Allah amemuacha apotee basi hana wa kumuongoa



Sourate: AR-RA’D 

Verset : 34

لَّهُمۡ عَذَابٞ فِي ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَاۖ وَلَعَذَابُ ٱلۡأٓخِرَةِ أَشَقُّۖ وَمَا لَهُم مِّنَ ٱللَّهِ مِن وَاقٖ

(Hao makafiri) Wana adhabu katika maisha ya dunia, na adhabu ya Akhera ni nzito mno. Na wala hawatakuwa na wa kuwahami na (adhabu ya) Allah



Sourate: AR-RA’D 

Verset : 35

۞مَّثَلُ ٱلۡجَنَّةِ ٱلَّتِي وُعِدَ ٱلۡمُتَّقُونَۖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُۖ أُكُلُهَا دَآئِمٞ وَظِلُّهَاۚ تِلۡكَ عُقۡبَى ٱلَّذِينَ ٱتَّقَواْۚ وَّعُقۡبَى ٱلۡكَٰفِرِينَ ٱلنَّارُ

Mfano wa Pepo waliyoahidiwa wacha Mungu, inapita mbele yake mito, matunda yake hayana msimu, na pia kivuli chake. Huu ndio mwisho wa wale waliojilinda. Na mwisho wa makafiri ni Moto



Sourate: AR-RA’D 

Verset : 36

وَٱلَّذِينَ ءَاتَيۡنَٰهُمُ ٱلۡكِتَٰبَ يَفۡرَحُونَ بِمَآ أُنزِلَ إِلَيۡكَۖ وَمِنَ ٱلۡأَحۡزَابِ مَن يُنكِرُ بَعۡضَهُۥۚ قُلۡ إِنَّمَآ أُمِرۡتُ أَنۡ أَعۡبُدَ ٱللَّهَ وَلَآ أُشۡرِكَ بِهِۦٓۚ إِلَيۡهِ أَدۡعُواْ وَإِلَيۡهِ مَـَٔابِ

Na wale tuliowapa Kitabu wanafurahia yale uliyoteremshiwa[1]. Na katika makundi mengine wapo wanaoyakataa baadhi yake[2]. Sema: Nimeamrishwa nimuabudu Allah, na wala nisimshirikishe. Kuelekea kwake Yeye tu ndiyo ninaita (watu), na kwake Yeye tu ndio marejeo yangu


1- - Wanaolengwa kuifurahikia Qura’n hapa ni wale wa Yahudi waliosilimu katika enzi za Mtume akiwemo
Abdallah bin Salam na wenzake.

2- - Na wapo baadhi ya Wayahudi kama vile Ka’b bin Al-ashraf na wenzake walikuwa wanayapinga wazi wazi
baadhi ya yale yaliyoteremshwa kwa Mtume.


Sourate: AR-RA’D 

Verset : 37

وَكَذَٰلِكَ أَنزَلۡنَٰهُ حُكۡمًا عَرَبِيّٗاۚ وَلَئِنِ ٱتَّبَعۡتَ أَهۡوَآءَهُم بَعۡدَ مَا جَآءَكَ مِنَ ٱلۡعِلۡمِ مَا لَكَ مِنَ ٱللَّهِ مِن وَلِيّٖ وَلَا وَاقٖ

Na kama hivi (tulivyoiteremsha hii Qur’an ikiwa imesheheni misingi ya dini) tumeiteremsha (pia hii) Qur’ani kuwa ni hukumu (kwa lugha ya) Kiarabu (ili ifahamike na kuhifadhiwa kwa wepesi). Na ukifuata matamanio yao baada ya kukujia elimu, hutakuwa na rafiki wala mlinzi wa kukukinga (na adhabu ya Allah



Sourate: AR-RA’D 

Verset : 38

وَلَقَدۡ أَرۡسَلۡنَا رُسُلٗا مِّن قَبۡلِكَ وَجَعَلۡنَا لَهُمۡ أَزۡوَٰجٗا وَذُرِّيَّةٗۚ وَمَا كَانَ لِرَسُولٍ أَن يَأۡتِيَ بِـَٔايَةٍ إِلَّا بِإِذۡنِ ٱللَّهِۗ لِكُلِّ أَجَلٖ كِتَابٞ

Na hakika Sisi tuliwatuma Mitume kabla yako, na tukawajaalia wawe na wake na watoto dhuriya (kama ulivyo wewe). Na haiwi kwa Mtume kuleta miujiza isipokuwa kwa idhini ya Allah. Kila kipindi kina hukumu yake



Sourate: AR-RA’D 

Verset : 39

يَمۡحُواْ ٱللَّهُ مَا يَشَآءُ وَيُثۡبِتُۖ وَعِندَهُۥٓ أُمُّ ٱلۡكِتَٰبِ

Allah hufuta na huthibitisha ayatakayo (katika hukumu zake). Na asili ya hukumu zote ipo kwake



Sourate: AR-RA’D 

Verset : 40

وَإِن مَّا نُرِيَنَّكَ بَعۡضَ ٱلَّذِي نَعِدُهُمۡ أَوۡ نَتَوَفَّيَنَّكَ فَإِنَّمَا عَلَيۡكَ ٱلۡبَلَٰغُ وَعَلَيۡنَا ٱلۡحِسَابُ

Na iwapo tutakuonesha baadhi ya (adhabu) tulizowaahidi au tukakufisha kabla yake (kabla ya kuwaadhibu), haikuwa jukumu lako wewe isipokuwa ni kufikisha ujumbe na juu yetu ni hesabu



Sourate: AR-RA’D 

Verset : 41

أَوَلَمۡ يَرَوۡاْ أَنَّا نَأۡتِي ٱلۡأَرۡضَ نَنقُصُهَا مِنۡ أَطۡرَافِهَاۚ وَٱللَّهُ يَحۡكُمُ لَا مُعَقِّبَ لِحُكۡمِهِۦۚ وَهُوَ سَرِيعُ ٱلۡحِسَابِ

Je, (watu wa Makkah na wengine) hawaoni tunavyo ipunguza ardhi (wanayoishi) nchani mwake?[1] Na Allah anahukumu, na hapana wa kupinga hukumu yake, naye ni Mwepesi wa kuhesabu


1- - Kusudio la kupunguzwa kwa ardhi hapa, ni pamoja na kuangamizwa na kutawaliwa na Waislamu baadhi
ya mipaka au maeneo yake.


Sourate: AR-RA’D 

Verset : 42

وَقَدۡ مَكَرَ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡ فَلِلَّهِ ٱلۡمَكۡرُ جَمِيعٗاۖ يَعۡلَمُ مَا تَكۡسِبُ كُلُّ نَفۡسٖۗ وَسَيَعۡلَمُ ٱلۡكُفَّـٰرُ لِمَنۡ عُقۡبَى ٱلدَّارِ

Na (hawa makafiri) walishafanya vitimbi (kwa Manabii) waliokuwa kabla yao, lakini Allah ndiye Mwenye mipango yote. Yeye anajua inayo chuma kila nafsi. Na makafiri watajua ni ya nani nyumba ya mwisho Akhera



Sourate: AR-RA’D 

Verset : 43

وَيَقُولُ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ لَسۡتَ مُرۡسَلٗاۚ قُلۡ كَفَىٰ بِٱللَّهِ شَهِيدَۢا بَيۡنِي وَبَيۡنَكُمۡ وَمَنۡ عِندَهُۥ عِلۡمُ ٱلۡكِتَٰبِ

Na wanasema waliokufuru: Wewe hukutumwa (si Mtume wa Allah). Sema: Allah anatosha kuwa shahidi baina yangu na nyinyi (kuhusu usahihi wa Utume wangu), na pia yule mwenye elimu ya Kitabu (kama anakiamini kitabu chake)



Sourate: IBRAHIM 

Verset : 1

الٓرۚ كِتَٰبٌ أَنزَلۡنَٰهُ إِلَيۡكَ لِتُخۡرِجَ ٱلنَّاسَ مِنَ ٱلظُّلُمَٰتِ إِلَى ٱلنُّورِ بِإِذۡنِ رَبِّهِمۡ إِلَىٰ صِرَٰطِ ٱلۡعَزِيزِ ٱلۡحَمِيدِ

Alif Lam Raa[1]. Hiki ni Kitabu tulichokiteremsha kwako ili kwacho uwatowe watu kwenye giza uwapeleke kwenye muangaza, kwa idhini ya Mola wao Mlezi, uwafikishe kwenye Njia ya Mwenye nguvu, Msifiwa


1- - Allah ndiye ajuaye maana halisi ya herufi hizi.


Sourate: IBRAHIM 

Verset : 2

ٱللَّهِ ٱلَّذِي لَهُۥ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِۗ وَوَيۡلٞ لِّلۡكَٰفِرِينَ مِنۡ عَذَابٖ شَدِيدٍ

Allah ambaye ni vyake yeye tu vyote vilivyomo mbinguni na ardhini. Na ole wao makafiri kwa adhabu kali mno



Sourate: IBRAHIM 

Verset : 3

ٱلَّذِينَ يَسۡتَحِبُّونَ ٱلۡحَيَوٰةَ ٱلدُّنۡيَا عَلَى ٱلۡأٓخِرَةِ وَيَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ وَيَبۡغُونَهَا عِوَجًاۚ أُوْلَـٰٓئِكَ فِي ضَلَٰلِۭ بَعِيدٖ

Ambao wanafadhilisha maisha ya dunia kuliko Akhera, na wanazuia (watu wasifuate) Njia ya Allah, na wanataka kuipotosha. Hao wapo kwenye upotevu wa mbali



Sourate: IBRAHIM 

Verset : 4

وَمَآ أَرۡسَلۡنَا مِن رَّسُولٍ إِلَّا بِلِسَانِ قَوۡمِهِۦ لِيُبَيِّنَ لَهُمۡۖ فَيُضِلُّ ٱللَّهُ مَن يَشَآءُ وَيَهۡدِي مَن يَشَآءُۚ وَهُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡحَكِيمُ

Na hatukumtuma Mtume yoyote ila kwa lugha ya kaumu yake ili apate kuwabainishia. Basi Allah humuacha akapotea amtakaye, na akamuongoa amtakaye. Naye ni Mtukufu Mwenye nguvu na Mwenye hekima



Sourate: IBRAHIM 

Verset : 5

وَلَقَدۡ أَرۡسَلۡنَا مُوسَىٰ بِـَٔايَٰتِنَآ أَنۡ أَخۡرِجۡ قَوۡمَكَ مِنَ ٱلظُّلُمَٰتِ إِلَى ٱلنُّورِ وَذَكِّرۡهُم بِأَيَّىٰمِ ٱللَّهِۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَٰتٖ لِّكُلِّ صَبَّارٖ شَكُورٖ

Na kwa hakika kabisa tulimtuma Mussa pamoja na miujiza yetu, (na tulimwambia): Watoe watu wako kwenye giza uwapeleke kwenye mwangaza. Na uwakumbushe siku za Allah. Hakika katika hayo zipo ishara kwa kila mwenye kusubiri (na) kushukuru