وَٱلَّيۡلِ إِذَا يَغۡشَىٰ
Naapa kwa usiku unapo funika!
Partager :
وَٱلنَّهَارِ إِذَا تَجَلَّىٰ
Na mchana unapo dhihiri!
وَمَا خَلَقَ ٱلذَّكَرَ وَٱلۡأُنثَىٰٓ
Na kwa Aliye umba dume na jike!
إِنَّ سَعۡيَكُمۡ لَشَتَّىٰ
Hakika juhudi zenu bila ya shaka ni tofauti
فَأَمَّا مَنۡ أَعۡطَىٰ وَٱتَّقَىٰ
Ama mwenye kutoa na akamcha Allah
وَصَدَّقَ بِٱلۡحُسۡنَىٰ
Na akalisadikisha lilio jema,
فَسَنُيَسِّرُهُۥ لِلۡيُسۡرَىٰ
Tutamsahilishia yawe mepesi
وَأَمَّا مَنۢ بَخِلَ وَٱسۡتَغۡنَىٰ
Na ama mwenye kufanya ubakhili, na asiwe na haja ya wenzake,
وَكَذَّبَ بِٱلۡحُسۡنَىٰ
Na akakanusha lilio jema,
فَسَنُيَسِّرُهُۥ لِلۡعُسۡرَىٰ
Tutamsahilishia yawe mazito!
وَمَا يُغۡنِي عَنۡهُ مَالُهُۥٓ إِذَا تَرَدَّىٰٓ
Na mali yake yatamfaa nini atakapo kuwa anadidimia?
إِنَّ عَلَيۡنَا لَلۡهُدَىٰ
Hakika ni juu yetu kuonyesha uongofu
وَإِنَّ لَنَا لَلۡأٓخِرَةَ وَٱلۡأُولَىٰ
Na hakika ni yetu Sisi Akhera na dunia
فَأَنذَرۡتُكُمۡ نَارٗا تَلَظَّىٰ
Basi nakuonyeni na Moto unao waka!
لَا يَصۡلَىٰهَآ إِلَّا ٱلۡأَشۡقَى
Hatauingia ila mwovu kabisa!
ٱلَّذِي كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰ
Anaye kadhibisha na kupa mgongo
وَسَيُجَنَّبُهَا ٱلۡأَتۡقَى
Na mcha Mungu ataepushwa nao
ٱلَّذِي يُؤۡتِي مَالَهُۥ يَتَزَكَّىٰ
Ambaye hutoa mali yake kwa ajili ya kujitakasa
وَمَا لِأَحَدٍ عِندَهُۥ مِن نِّعۡمَةٖ تُجۡزَىٰٓ
Na wala si kwa kuwa yupo yeyote aliye mfanyia hisani ndio anamlipa
إِلَّا ٱبۡتِغَآءَ وَجۡهِ رَبِّهِ ٱلۡأَعۡلَىٰ
Ila ni kutaka radhi ya Mola wake Mlezi aliye juu kabisa
وَلَسَوۡفَ يَرۡضَىٰ
Naye atakuja ridhika!