قَدۡ سَمِعَ ٱللَّهُ قَوۡلَ ٱلَّتِي تُجَٰدِلُكَ فِي زَوۡجِهَا وَتَشۡتَكِيٓ إِلَى ٱللَّهِ وَٱللَّهُ يَسۡمَعُ تَحَاوُرَكُمَآۚ إِنَّ ٱللَّهَ سَمِيعُۢ بَصِيرٌ
Hakika, Allah amekwishasikia kauli ya yule mwanamke anayejadiliana nawe (ewe Muhammad) kuhusu mumewe, na anamshitakia Allah, na Allah anayasikia majibizano yenu. Hakika, Allah ni Mwenye kusikia yote, Mwenye kuona yote
ٱلَّذِينَ يُظَٰهِرُونَ مِنكُم مِّن نِّسَآئِهِم مَّا هُنَّ أُمَّهَٰتِهِمۡۖ إِنۡ أُمَّهَٰتُهُمۡ إِلَّا ٱلَّـٰٓـِٔي وَلَدۡنَهُمۡۚ وَإِنَّهُمۡ لَيَقُولُونَ مُنكَرٗا مِّنَ ٱلۡقَوۡلِ وَزُورٗاۚ وَإِنَّ ٱللَّهَ لَعَفُوٌّ غَفُورٞ
Wale miongoni mwenu ambao wanawatamkia wake zao Dhwihari[1], (Nyinyi kwetu kama migongo ya mama zetu). Hao wake zao si mama zao. Hawakuwa mama zao isipokuwa wale waliowazaa. Na hakika wao bila shaka wanasema kauli ya kuchukiza na uongo. Na hakika Allah bila shaka ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa Maghfira
1- - Dhwihari ni mume kumfananisha mkewe na mwanamke mwengine ambae kwake ni haramu kumuoa.
وَٱلَّذِينَ يُظَٰهِرُونَ مِن نِّسَآئِهِمۡ ثُمَّ يَعُودُونَ لِمَا قَالُواْ فَتَحۡرِيرُ رَقَبَةٖ مِّن قَبۡلِ أَن يَتَمَآسَّاۚ ذَٰلِكُمۡ تُوعَظُونَ بِهِۦۚ وَٱللَّهُ بِمَا تَعۡمَلُونَ خَبِيرٞ
Na wale ambao wanaowatamkia wake zao dhwihaar, kisha wakarudi katika waliyoyasema (kuitengua dhwihaar), basi ni kuacha huru mtumwa kabla ya kugusana. Hayo mnawaidhiwa kwayo. Na Allah kwa yale myatendayo ni Mwenye khabari kwa yale mnayo yatenda
فَمَن لَّمۡ يَجِدۡ فَصِيَامُ شَهۡرَيۡنِ مُتَتَابِعَيۡنِ مِن قَبۡلِ أَن يَتَمَآسَّاۖ فَمَن لَّمۡ يَسۡتَطِعۡ فَإِطۡعَامُ سِتِّينَ مِسۡكِينٗاۚ ذَٰلِكَ لِتُؤۡمِنُواْ بِٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦۚ وَتِلۡكَ حُدُودُ ٱللَّهِۗ وَلِلۡكَٰفِرِينَ عَذَابٌ أَلِيمٌ
Na yule asiyepata uwezo, basi afunge Swiyaam miezi miwili mfululuzo kabla ya kugusana. Na yule asiyeweza, basi alishe chakula masikini sitini. Hivyo ili mumuamini Allah na Rasuli Wake. Na hiyo ni mipaka ya Allah. Na makafiri watapata adhabu iumizayo
إِنَّ ٱلَّذِينَ يُحَآدُّونَ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ كُبِتُواْ كَمَا كُبِتَ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡۚ وَقَدۡ أَنزَلۡنَآ ءَايَٰتِۭ بَيِّنَٰتٖۚ وَلِلۡكَٰفِرِينَ عَذَابٞ مُّهِينٞ
Hakika wale wanao pinzana na Allah na Mtume Wake watadhalilishwa kama walivyo dhalilishwa wale wa kabla yao. Na Tumekwishateremsha Ishara zilizo wazi na makafiri watapata adhabu ya kudhalilisha
يَوۡمَ يَبۡعَثُهُمُ ٱللَّهُ جَمِيعٗا فَيُنَبِّئُهُم بِمَا عَمِلُوٓاْۚ أَحۡصَىٰهُ ٱللَّهُ وَنَسُوهُۚ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ شَهِيدٌ
Siku Atakayowafufua Allah wote, Awajulishe yale waliyoyatenda, Allah Ameyadhibiti na wao wameyasahau; na Allah ni Shahidi juu ya kila kitu
أَلَمۡ تَرَ أَنَّ ٱللَّهَ يَعۡلَمُ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِۖ مَا يَكُونُ مِن نَّجۡوَىٰ ثَلَٰثَةٍ إِلَّا هُوَ رَابِعُهُمۡ وَلَا خَمۡسَةٍ إِلَّا هُوَ سَادِسُهُمۡ وَلَآ أَدۡنَىٰ مِن ذَٰلِكَ وَلَآ أَكۡثَرَ إِلَّا هُوَ مَعَهُمۡ أَيۡنَ مَا كَانُواْۖ ثُمَّ يُنَبِّئُهُم بِمَا عَمِلُواْ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِۚ إِنَّ ٱللَّهَ بِكُلِّ شَيۡءٍ عَلِيمٌ
Je, huoni kwamba Allah Anajua yaliyomo mbinguni na yaliyomo ardhini? Hauwi mnong’ono wa watatu isipokuwa Yeye ni wa nne wao (kwa ujuzi Wake), na wala watano isipokuwa Yeye ni wa sita wao (kwa ujuzi Wake), na wala chini kuliko ya hivyo, na wala wengi zaidi isipokuwa Yeye Yu pamoja nao (kwa ujuzi Wake) popote watakapokuwa; kisha Siku ya Kiyama Atawajulisha yale waliyoyatenda. Hakika Allah kwa kila kitu ni mjuzi
أَلَمۡ تَرَ إِلَى ٱلَّذِينَ نُهُواْ عَنِ ٱلنَّجۡوَىٰ ثُمَّ يَعُودُونَ لِمَا نُهُواْ عَنۡهُ وَيَتَنَٰجَوۡنَ بِٱلۡإِثۡمِ وَٱلۡعُدۡوَٰنِ وَمَعۡصِيَتِ ٱلرَّسُولِۖ وَإِذَا جَآءُوكَ حَيَّوۡكَ بِمَا لَمۡ يُحَيِّكَ بِهِ ٱللَّهُ وَيَقُولُونَ فِيٓ أَنفُسِهِمۡ لَوۡلَا يُعَذِّبُنَا ٱللَّهُ بِمَا نَقُولُۚ حَسۡبُهُمۡ جَهَنَّمُ يَصۡلَوۡنَهَاۖ فَبِئۡسَ ٱلۡمَصِيرُ
Je, huwaoni wale waliokatazwa kunong’ona, kisha wanarudia yale waliyokatazwa nayo, na wananong’onezana kuhusu dhambi na uadui na kumuasi Mtume. Na wanapokujia wanakuamkia kwa maamkizi Asiyokuamkia kwayo Allah; na wanasema katika nafsi zao: Mbona Allah Hatuadhibu kwa yale tunayoyasema? Jahannam inawatosheleza, wataingia waungue, basi ubaya ulioje mahali pa kuishia
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِذَا تَنَٰجَيۡتُمۡ فَلَا تَتَنَٰجَوۡاْ بِٱلۡإِثۡمِ وَٱلۡعُدۡوَٰنِ وَمَعۡصِيَتِ ٱلرَّسُولِ وَتَنَٰجَوۡاْ بِٱلۡبِرِّ وَٱلتَّقۡوَىٰۖ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ ٱلَّذِيٓ إِلَيۡهِ تُحۡشَرُونَ
Enyi walioamini! Mna-ponong’onezana, basi msinon-g’onezane kuhusu dhambi na uadui na kumuasi Mtume, bali nong’onezaneni kuhusu wema na taqwa; na mcheni Allah Ambaye Kwake Pekee mtakusanywa
إِنَّمَا ٱلنَّجۡوَىٰ مِنَ ٱلشَّيۡطَٰنِ لِيَحۡزُنَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَلَيۡسَ بِضَآرِّهِمۡ شَيۡـًٔا إِلَّا بِإِذۡنِ ٱللَّهِۚ وَعَلَى ٱللَّهِ فَلۡيَتَوَكَّلِ ٱلۡمُؤۡمِنُونَ
Hakika mnong’ono unatokana na shaytwaan ili awahuzunishe wale walioamini, na wala hawezi kuwadhuru chochote isipokuwa kwa idhini ya Allah. Na kwa Allah wategemee wenye kuaumini
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِذَا قِيلَ لَكُمۡ تَفَسَّحُواْ فِي ٱلۡمَجَٰلِسِ فَٱفۡسَحُواْ يَفۡسَحِ ٱللَّهُ لَكُمۡۖ وَإِذَا قِيلَ ٱنشُزُواْ فَٱنشُزُواْ يَرۡفَعِ ٱللَّهُ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مِنكُمۡ وَٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡعِلۡمَ دَرَجَٰتٖۚ وَٱللَّهُ بِمَا تَعۡمَلُونَ خَبِيرٞ
Enyi walioamini! Mnapoambiwa: Fanyeni nafasi katika mabaraza, basi fanyeni nafasi; Allah Atakufanyieni nafasi. Na mnapoambiwa: Inukeni, basi inukeni; Allah Atawainua wale walioamini miongoni mwenu na waliopewa elimu daraja za juu. Na Allah kwa yale myatendayo ni Mwenye khabari nayo
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِذَا نَٰجَيۡتُمُ ٱلرَّسُولَ فَقَدِّمُواْ بَيۡنَ يَدَيۡ نَجۡوَىٰكُمۡ صَدَقَةٗۚ ذَٰلِكَ خَيۡرٞ لَّكُمۡ وَأَطۡهَرُۚ فَإِن لَّمۡ تَجِدُواْ فَإِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٌ
Enyi walioamini! Mnapotaka kushauriana siri na Mtume basi tangulizeni kwanza swadaka kabla ya kusemezana kwenu na Mtume. Hivyo ni kheri kwenu na utakaso zaidi. Na msipopata, basi hakika Allah ni Mwingi wa msamaha na Mwenye kurehemu
ءَأَشۡفَقۡتُمۡ أَن تُقَدِّمُواْ بَيۡنَ يَدَيۡ نَجۡوَىٰكُمۡ صَدَقَٰتٖۚ فَإِذۡ لَمۡ تَفۡعَلُواْ وَتَابَ ٱللَّهُ عَلَيۡكُمۡ فَأَقِيمُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتُواْ ٱلزَّكَوٰةَ وَأَطِيعُواْ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥۚ وَٱللَّهُ خَبِيرُۢ بِمَا تَعۡمَلُونَ
Je, mnakhofu kutanguliza hiyo swadaka kabla ya kusemezana kwenu? Ikiwa hamjafanya hayo, na Allah Akapokea toba yenu; basi simamisheni Sala, na toeni Zaka, na mtiini Allah na Mtume Wake; na Allah ni Mwenye khabari kwa yale myatendayo
۞أَلَمۡ تَرَ إِلَى ٱلَّذِينَ تَوَلَّوۡاْ قَوۡمًا غَضِبَ ٱللَّهُ عَلَيۡهِم مَّا هُم مِّنكُمۡ وَلَا مِنۡهُمۡ وَيَحۡلِفُونَ عَلَى ٱلۡكَذِبِ وَهُمۡ يَعۡلَمُونَ
Je, hukuona wale waliofanya urafiki na watu ambao Allah Amewakasirikia?, wao si katika nyinyi, na wala si katika wao, na wanaapia uongo hali yakuwa wanajua
أَعَدَّ ٱللَّهُ لَهُمۡ عَذَابٗا شَدِيدًاۖ إِنَّهُمۡ سَآءَ مَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ
Allah Amewaandalia adhabu kali, hakika ni uovu ulioje waliokuwa wakiutenda
ٱتَّخَذُوٓاْ أَيۡمَٰنَهُمۡ جُنَّةٗ فَصَدُّواْ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ فَلَهُمۡ عَذَابٞ مُّهِينٞ
Wamefanya viapo vyao kuwa ni kinga hivyo wakazuia njia ya Allah, basi hao watapata adhabu idhalilishayo
لَّن تُغۡنِيَ عَنۡهُمۡ أَمۡوَٰلُهُمۡ وَلَآ أَوۡلَٰدُهُم مِّنَ ٱللَّهِ شَيۡـًٔاۚ أُوْلَـٰٓئِكَ أَصۡحَٰبُ ٱلنَّارِۖ هُمۡ فِيهَا خَٰلِدُونَ
Hazitowafaa kitu chochote mali zao na wala watoto wao mbele ya Allah, hao ni watu wa motoni, wao humo ni wenye kudumu milele
يَوۡمَ يَبۡعَثُهُمُ ٱللَّهُ جَمِيعٗا فَيَحۡلِفُونَ لَهُۥ كَمَا يَحۡلِفُونَ لَكُمۡ وَيَحۡسَبُونَ أَنَّهُمۡ عَلَىٰ شَيۡءٍۚ أَلَآ إِنَّهُمۡ هُمُ ٱلۡكَٰذِبُونَ
Siku Atakayowafufua Allah wote, watamwapia kama wanavyokuapieni nyinyi, na wanadhania kwamba wamepata kitu, Tanabahi! Hakika wao ni waongo
ٱسۡتَحۡوَذَ عَلَيۡهِمُ ٱلشَّيۡطَٰنُ فَأَنسَىٰهُمۡ ذِكۡرَ ٱللَّهِۚ أُوْلَـٰٓئِكَ حِزۡبُ ٱلشَّيۡطَٰنِۚ أَلَآ إِنَّ حِزۡبَ ٱلشَّيۡطَٰنِ هُمُ ٱلۡخَٰسِرُونَ
Shetani amewatawala, akawasahaulisha kumkumbuka Allah, hao ndio kundi la shetani. Zindukeni! Hakika kundi la shetani ndio lenye kukhasirika. (lenye kupata khasara)
إِنَّ ٱلَّذِينَ يُحَآدُّونَ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥٓ أُوْلَـٰٓئِكَ فِي ٱلۡأَذَلِّينَ
Hakika wale wanaompinga Allah na Mtume Wake hao ndio miongoni mwa madhalili
كَتَبَ ٱللَّهُ لَأَغۡلِبَنَّ أَنَا۠ وَرُسُلِيٓۚ إِنَّ ٱللَّهَ قَوِيٌّ عَزِيزٞ
Allah Amekwishaandika kwamba: Bila shaka Nitashinda Mimi na Mitume Wangu. Hakika Allah ni Mwenye nguvu zote, Mwenye kushinda
لَّا تَجِدُ قَوۡمٗا يُؤۡمِنُونَ بِٱللَّهِ وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِ يُوَآدُّونَ مَنۡ حَآدَّ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ وَلَوۡ كَانُوٓاْ ءَابَآءَهُمۡ أَوۡ أَبۡنَآءَهُمۡ أَوۡ إِخۡوَٰنَهُمۡ أَوۡ عَشِيرَتَهُمۡۚ أُوْلَـٰٓئِكَ كَتَبَ فِي قُلُوبِهِمُ ٱلۡإِيمَٰنَ وَأَيَّدَهُم بِرُوحٖ مِّنۡهُۖ وَيُدۡخِلُهُمۡ جَنَّـٰتٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ خَٰلِدِينَ فِيهَاۚ رَضِيَ ٱللَّهُ عَنۡهُمۡ وَرَضُواْ عَنۡهُۚ أُوْلَـٰٓئِكَ حِزۡبُ ٱللَّهِۚ أَلَآ إِنَّ حِزۡبَ ٱللَّهِ هُمُ ٱلۡمُفۡلِحُونَ
Hutokuta watu wanaomuamini Allah na Siku ya Mwisho kuwa wanafanya urafiki na kuwapenda wanaompinga Allah na Mtume Wake, japo wakiwa ni baba zao, au watoto wao, au ndugu zao, au jamaa zao. Hao (Allah) Ameandika katika nyoyo zao Imani, na Akawatia nguvu kwa Roho (Wahyi) kutoka Kwake, na Atawaingiza kwenye Mabustani yapitayo chini yake mito humo watakaa milele. Allah Ameridhika nao, nao wameridhika Naye. Hao ndio kundi la Allah. Zindukeni! Hakika kundi la Allah ndio lenye kufaulu