الٓمٓ
Alif Laam Miim[1]
1- - Allah ndiye ajuwaye zaidi madhumuni ya herufi hizi.
ذَٰلِكَ ٱلۡكِتَٰبُ لَا رَيۡبَۛ فِيهِۛ هُدٗى لِّلۡمُتَّقِينَ
Kitabu hiki hakina shaka. Ni muongozo kwa Wacha Mungu
ٱلَّذِينَ يُؤۡمِنُونَ بِٱلۡغَيۡبِ وَيُقِيمُونَ ٱلصَّلَوٰةَ وَمِمَّا رَزَقۡنَٰهُمۡ يُنفِقُونَ
Ambao wanaamini Ghaibu na wanasimamisha swala na baadhi ya tulivyowapa wanatoa
وَٱلَّذِينَ يُؤۡمِنُونَ بِمَآ أُنزِلَ إِلَيۡكَ وَمَآ أُنزِلَ مِن قَبۡلِكَ وَبِٱلۡأٓخِرَةِ هُمۡ يُوقِنُونَ
Na ambao wanaamini yale tuliyoyateremsha kwako na yale tuliyoyateremsha kabla yako, na ambao wanaamini Akhera
أُوْلَـٰٓئِكَ عَلَىٰ هُدٗى مِّن رَّبِّهِمۡۖ وَأُوْلَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡمُفۡلِحُونَ
Hao wako juu ya muongozo utokao kwa Mola wao, na hao tu ndio waliofaulu
إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ سَوَآءٌ عَلَيۡهِمۡ ءَأَنذَرۡتَهُمۡ أَمۡ لَمۡ تُنذِرۡهُمۡ لَا يُؤۡمِنُونَ
Hakika, waliokufuru, ni sawa kwao umewahadharisha au hukuwahadharisha; hawaamini
خَتَمَ ٱللَّهُ عَلَىٰ قُلُوبِهِمۡ وَعَلَىٰ سَمۡعِهِمۡۖ وَعَلَىٰٓ أَبۡصَٰرِهِمۡ غِشَٰوَةٞۖ وَلَهُمۡ عَذَابٌ عَظِيمٞ
Allah amefunga nyoyo zao na usikivu wao, na katika uonaji wao kuna kifuniko, na watastahiki adhabu kubwa
وَمِنَ ٱلنَّاسِ مَن يَقُولُ ءَامَنَّا بِٱللَّهِ وَبِٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِ وَمَا هُم بِمُؤۡمِنِينَ
Na miongoni mwa watu wapo wanaosema[1] kuwa: “Tumemuamini Allah na Siku ya Mwisho” na[2] sio waumini (wa kweli)
1- - Kwa maneno tu.
2- - Ukweli ni kwamba…
يُخَٰدِعُونَ ٱللَّهَ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَمَا يَخۡدَعُونَ إِلَّآ أَنفُسَهُمۡ وَمَا يَشۡعُرُونَ
Wanamhadaa Allah na wale walioamini. Na hawahadai isipokuwa nafsi zao tu na wao hawatambui
فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٞ فَزَادَهُمُ ٱللَّهُ مَرَضٗاۖ وَلَهُمۡ عَذَابٌ أَلِيمُۢ بِمَا كَانُواْ يَكۡذِبُونَ
Ndani ya nyoyo zao kuna ugonjwa, na Allah akawaongezea ugonjwa. Na wanastahiki adhabu kali kwa uongo waliokuwa wanaufanya
وَإِذَا قِيلَ لَهُمۡ لَا تُفۡسِدُواْ فِي ٱلۡأَرۡضِ قَالُوٓاْ إِنَّمَا نَحۡنُ مُصۡلِحُونَ
Na wanapoambiwa msifanye uharibifu ardhini wanasema: Hapana, bali sisi niwafanyaji mazuri
أَلَآ إِنَّهُمۡ هُمُ ٱلۡمُفۡسِدُونَ وَلَٰكِن لَّا يَشۡعُرُونَ
Elewa! Kwa yakini, wao ndio waharibifu hasa na lakini hawatambui
وَإِذَا قِيلَ لَهُمۡ ءَامِنُواْ كَمَآ ءَامَنَ ٱلنَّاسُ قَالُوٓاْ أَنُؤۡمِنُ كَمَآ ءَامَنَ ٱلسُّفَهَآءُۗ أَلَآ إِنَّهُمۡ هُمُ ٱلسُّفَهَآءُ وَلَٰكِن لَّا يَعۡلَمُونَ
Na wanapoambiwa: Kuweni wenye kuamini kama walivyoamini watu, wanasema: Ah! Hivi tuamini kama walivyoamini wapumbavu? Elewa! Wao ndio wapumbavu hasa na lakini hawajui
وَإِذَا لَقُواْ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ قَالُوٓاْ ءَامَنَّا وَإِذَا خَلَوۡاْ إِلَىٰ شَيَٰطِينِهِمۡ قَالُوٓاْ إِنَّا مَعَكُمۡ إِنَّمَا نَحۡنُ مُسۡتَهۡزِءُونَ
Na wanapokutana na walioamini wanasema: Tumeamini. Na wanapokuwa faragha na mashetani wao wanasema: Sisi tuko pamoja nanyi, tunachokifanya sisi tunacheza shere tu
ٱللَّهُ يَسۡتَهۡزِئُ بِهِمۡ وَيَمُدُّهُمۡ فِي طُغۡيَٰنِهِمۡ يَعۡمَهُونَ
Allah anawacheza shere wao, na anawapa muda zaidi katika kupotoka kwao huku wakiwa wanatangatanga
أُوْلَـٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ ٱشۡتَرَوُاْ ٱلضَّلَٰلَةَ بِٱلۡهُدَىٰ فَمَا رَبِحَت تِّجَٰرَتُهُمۡ وَمَا كَانُواْ مُهۡتَدِينَ
Hao ndio walioununua upotevu kwa uongofu. Biashara yao haikuleta faida, na hawakuwa waongofu
مَثَلُهُمۡ كَمَثَلِ ٱلَّذِي ٱسۡتَوۡقَدَ نَارٗا فَلَمَّآ أَضَآءَتۡ مَا حَوۡلَهُۥ ذَهَبَ ٱللَّهُ بِنُورِهِمۡ وَتَرَكَهُمۡ فِي ظُلُمَٰتٖ لَّا يُبۡصِرُونَ
Mfano wao ni kama mfano wa mtu aliyewasha moto. Kila moto ulipomuangazia maeneo yanayomzunguka, Allah akaondoa mwanga wao na kuwaacha katika kiza kinene; hawaoni
صُمُّۢ بُكۡمٌ عُمۡيٞ فَهُمۡ لَا يَرۡجِعُونَ
Ni viziwi, mabubu, vipofu. Kwa sababu hiyo, hawarudi
أَوۡ كَصَيِّبٖ مِّنَ ٱلسَّمَآءِ فِيهِ ظُلُمَٰتٞ وَرَعۡدٞ وَبَرۡقٞ يَجۡعَلُونَ أَصَٰبِعَهُمۡ فِيٓ ءَاذَانِهِم مِّنَ ٱلصَّوَٰعِقِ حَذَرَ ٱلۡمَوۡتِۚ وَٱللَّهُ مُحِيطُۢ بِٱلۡكَٰفِرِينَ
Au ni kama mvua iteremkayo kwa kasi kutoka mawinguni, ndani yake mna kiza kinene na radi na umeme wanaweka vidole vyao masikioni mwao kutokana na radi kwa kuhadhari kifo. Na Allah amewazunguka makafiri wote
يَكَادُ ٱلۡبَرۡقُ يَخۡطَفُ أَبۡصَٰرَهُمۡۖ كُلَّمَآ أَضَآءَ لَهُم مَّشَوۡاْ فِيهِ وَإِذَآ أَظۡلَمَ عَلَيۡهِمۡ قَامُواْۚ وَلَوۡ شَآءَ ٱللَّهُ لَذَهَبَ بِسَمۡعِهِمۡ وَأَبۡصَٰرِهِمۡۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٞ
Umeme unakaribia kupofoa macho yao. Kila unapowaangazia wanatembea katika mwanga huo, na pale unapowazimikia wanasimama. Na kama Allah angelitaka basi, kwa yakini kabisa, angeondoa kusikia kwao na macho yao. Hakika, Allah ni muweza wa kila kitu
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ ٱعۡبُدُواْ رَبَّكُمُ ٱلَّذِي خَلَقَكُمۡ وَٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِكُمۡ لَعَلَّكُمۡ تَتَّقُونَ
Enyi watu, muabuduni Mola wenu ambaye amekuumbeni na (ameumba) waliokuwepo kabla yenu ili muwe Wacha Mungu
ٱلَّذِي جَعَلَ لَكُمُ ٱلۡأَرۡضَ فِرَٰشٗا وَٱلسَّمَآءَ بِنَآءٗ وَأَنزَلَ مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءٗ فَأَخۡرَجَ بِهِۦ مِنَ ٱلثَّمَرَٰتِ رِزۡقٗا لَّكُمۡۖ فَلَا تَجۡعَلُواْ لِلَّهِ أَندَادٗا وَأَنتُمۡ تَعۡلَمُونَ
Ambaye amekuumbieni ardhi ikiwa imetandazwa, na mbingu ikiwa sakafu na ameteremsha kutoka mawinguni maji (mvua), akatoa kwa maji hayo riziki zenu kutoka kwenye matunda. Basi msimfanyie Allah washirika ilihali mnajua (kuwa Allah hana mshirika)
وَإِن كُنتُمۡ فِي رَيۡبٖ مِّمَّا نَزَّلۡنَا عَلَىٰ عَبۡدِنَا فَأۡتُواْ بِسُورَةٖ مِّن مِّثۡلِهِۦ وَٱدۡعُواْ شُهَدَآءَكُم مِّن دُونِ ٱللَّهِ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ
Na ikiwa mna shaka na kile tulichomteremshia mja wetu, basi leteni Sura (moja tu) iliyo mithili yake, na waleteni mashahidi wenu badala ya Allah ikiwa nyinyi ni wa kweli
فَإِن لَّمۡ تَفۡعَلُواْ وَلَن تَفۡعَلُواْ فَٱتَّقُواْ ٱلنَّارَ ٱلَّتِي وَقُودُهَا ٱلنَّاسُ وَٱلۡحِجَارَةُۖ أُعِدَّتۡ لِلۡكَٰفِرِينَ
Na msipofanya (hivyo) na kamwe hamtaweza kufanya (hivyo), basi uogopeni Moto ambao nishati yake ni watu na mawe, ulioandaliwa kwa ajili ya makafiri
وَبَشِّرِ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّـٰلِحَٰتِ أَنَّ لَهُمۡ جَنَّـٰتٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُۖ كُلَّمَا رُزِقُواْ مِنۡهَا مِن ثَمَرَةٖ رِّزۡقٗا قَالُواْ هَٰذَا ٱلَّذِي رُزِقۡنَا مِن قَبۡلُۖ وَأُتُواْ بِهِۦ مُتَشَٰبِهٗاۖ وَلَهُمۡ فِيهَآ أَزۡوَٰجٞ مُّطَهَّرَةٞۖ وَهُمۡ فِيهَا خَٰلِدُونَ
Na wape bishara wale walioamini na kufanya matendo mema kuwa, watapata bustani zitiririkazo mito chini yake. Kila wanapopewa riziki ya matunda humo wanasema: Hii ndio ile riziki tuliyopewa kabla. Na wamepewa riziki hiyo ikiwa inafanana. Na watapata humo wake waliotwaharishwa, na watabaki humo daima
۞إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَسۡتَحۡيِۦٓ أَن يَضۡرِبَ مَثَلٗا مَّا بَعُوضَةٗ فَمَا فَوۡقَهَاۚ فَأَمَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ فَيَعۡلَمُونَ أَنَّهُ ٱلۡحَقُّ مِن رَّبِّهِمۡۖ وَأَمَّا ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ فَيَقُولُونَ مَاذَآ أَرَادَ ٱللَّهُ بِهَٰذَا مَثَلٗاۘ يُضِلُّ بِهِۦ كَثِيرٗا وَيَهۡدِي بِهِۦ كَثِيرٗاۚ وَمَا يُضِلُّ بِهِۦٓ إِلَّا ٱلۡفَٰسِقِينَ
Hakika, Allah haoni aibu kutoa mfano wowote; wa mbu na (mfano) zaidi (ya mbu). Ama walioamini wanajua kuwa mfano huo ni haki kutoka kwa Mola wao. Na ama waliokufuru, wanasema kuwa: Allah amekusudia nini kwa mfano huu? Allah, kwa mfano huu, anawaacha wengi wapotee na anawaongoza wengi. Na (Allah) hawaachi kupotea kwa mfano huu isipokuwa waovu tu
ٱلَّذِينَ يَنقُضُونَ عَهۡدَ ٱللَّهِ مِنۢ بَعۡدِ مِيثَٰقِهِۦ وَيَقۡطَعُونَ مَآ أَمَرَ ٱللَّهُ بِهِۦٓ أَن يُوصَلَ وَيُفۡسِدُونَ فِي ٱلۡأَرۡضِۚ أُوْلَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡخَٰسِرُونَ
Ambao wana vunja ahadi za Allah baada ya kuwekwa, na wanakataa alichoamuru Allah kiungwe, na wanafanya uharibifu ardhini. Hao tu ndio wenye hasara
كَيۡفَ تَكۡفُرُونَ بِٱللَّهِ وَكُنتُمۡ أَمۡوَٰتٗا فَأَحۡيَٰكُمۡۖ ثُمَّ يُمِيتُكُمۡ ثُمَّ يُحۡيِيكُمۡ ثُمَّ إِلَيۡهِ تُرۡجَعُونَ
Vipi mnamkufuru Allah, na ilhali mlikuwa wafu akakupeni uhai? Kisha atakufisheni, kisha atakupeni uhai. Na kisha ni kwake tu ndiko mtakakorejeshwa
هُوَ ٱلَّذِي خَلَقَ لَكُم مَّا فِي ٱلۡأَرۡضِ جَمِيعٗا ثُمَّ ٱسۡتَوَىٰٓ إِلَى ٱلسَّمَآءِ فَسَوَّىٰهُنَّ سَبۡعَ سَمَٰوَٰتٖۚ وَهُوَ بِكُلِّ شَيۡءٍ عَلِيمٞ
Ni yeye tu aliye kuumbieni vyote vilivyomo ardhini. Kisha akakusudia mbingu na kuziumba zikiwa mbingu saba zilizo sawa. Na yeye ni mjuzi wa kila kitu
وَإِذۡ قَالَ رَبُّكَ لِلۡمَلَـٰٓئِكَةِ إِنِّي جَاعِلٞ فِي ٱلۡأَرۡضِ خَلِيفَةٗۖ قَالُوٓاْ أَتَجۡعَلُ فِيهَا مَن يُفۡسِدُ فِيهَا وَيَسۡفِكُ ٱلدِّمَآءَ وَنَحۡنُ نُسَبِّحُ بِحَمۡدِكَ وَنُقَدِّسُ لَكَۖ قَالَ إِنِّيٓ أَعۡلَمُ مَا لَا تَعۡلَمُونَ
Na (kumbuka) Mola wako alipowaambia Malaika kuwa: Kwa yakini, mimi nitamuweka Khalifa ardhini. Wakasema: Hivi unamuweka humo atakayefanya uharibifu humo na kumwaga damu, na wakati sisi tunakutakasa kwa kukusifu? (Allah) Akasema: Mimi ninajua msichokijua