Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 181

فَمَنۢ بَدَّلَهُۥ بَعۡدَ مَا سَمِعَهُۥ فَإِنَّمَآ إِثۡمُهُۥ عَلَى ٱلَّذِينَ يُبَدِّلُونَهُۥٓۚ إِنَّ ٱللَّهَ سَمِيعٌ عَلِيمٞ

Na atakayeubadilisha wasia huo baada ya kuusikia, basi ilivyo ni kwamba dhambi yake ipo kwa wale watakaoubadilisha. Hakika, Allah ni Msikiaji mno[1], Mjuzi mno[2]


1- - Wa kauli ya mtoa wasia.


2- - Wa kitendo chake na atamlipa.


Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 182

فَمَنۡ خَافَ مِن مُّوصٖ جَنَفًا أَوۡ إِثۡمٗا فَأَصۡلَحَ بَيۡنَهُمۡ فَلَآ إِثۡمَ عَلَيۡهِۚ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٞ

Na mwenye kuchelea kwa mtoa wasia kupotoka au dhambi akarekebisha baina yao, basi hatakuwa na dhambi. Hakika, Allah ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa kurehemu



Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 183

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ كُتِبَ عَلَيۡكُمُ ٱلصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِكُمۡ لَعَلَّكُمۡ تَتَّقُونَ

Enyi mlioamini, mmeandikiwa funga kama walivyoandikiwa waliokuwepo kabla yenu ili mpate kumcha Allah



Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 184

أَيَّامٗا مَّعۡدُودَٰتٖۚ فَمَن كَانَ مِنكُم مَّرِيضًا أَوۡ عَلَىٰ سَفَرٖ فَعِدَّةٞ مِّنۡ أَيَّامٍ أُخَرَۚ وَعَلَى ٱلَّذِينَ يُطِيقُونَهُۥ فِدۡيَةٞ طَعَامُ مِسۡكِينٖۖ فَمَن تَطَوَّعَ خَيۡرٗا فَهُوَ خَيۡرٞ لَّهُۥۚ وَأَن تَصُومُواْ خَيۡرٞ لَّكُمۡ إِن كُنتُمۡ تَعۡلَمُونَ

Ni siku chache za kuhesabika tu. Na atakayekuwa mgonjwa miongoni mwenu au safarini, basi[1] atimize hesabu katika siku nyingine. Na wale wasioiweza (funga), watoe fidia kwa kumlisha maskini. Na atakayefanya wema kwa ridhaa ya nafsi yake, basi ni bora kwake, na kufunga ni bora kwenu, ikiwa mnajua


1- - Anaruhusiwa kuacha kufunga na atimize.


Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 185

شَهۡرُ رَمَضَانَ ٱلَّذِيٓ أُنزِلَ فِيهِ ٱلۡقُرۡءَانُ هُدٗى لِّلنَّاسِ وَبَيِّنَٰتٖ مِّنَ ٱلۡهُدَىٰ وَٱلۡفُرۡقَانِۚ فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ ٱلشَّهۡرَ فَلۡيَصُمۡهُۖ وَمَن كَانَ مَرِيضًا أَوۡ عَلَىٰ سَفَرٖ فَعِدَّةٞ مِّنۡ أَيَّامٍ أُخَرَۗ يُرِيدُ ٱللَّهُ بِكُمُ ٱلۡيُسۡرَ وَلَا يُرِيدُ بِكُمُ ٱلۡعُسۡرَ وَلِتُكۡمِلُواْ ٱلۡعِدَّةَ وَلِتُكَبِّرُواْ ٱللَّهَ عَلَىٰ مَا هَدَىٰكُمۡ وَلَعَلَّكُمۡ تَشۡكُرُونَ

Ni mwezi wa Ramadhani ambao ndani yake imeteremshwa Qur’aniwe muongozo kwa watu, na hoja zilizo wazi za uongozi na upambanuzi. Basi atakayeshuhudia mwezi (huo) miongoni mwenu afunge. Na mwenye kuwa mgonjwa au safarini, basi[1] atimize hesabu katika siku nyingine[2]. Allah anakutakieni wepesi na hakutakieni uzito, na ili mumtukuze Allah kwa kukuongozeni na ili mpate kushukuru


1- - Anaruhusiwa kutofunga na kutimiza.


2- - Kwa kufunga zile siku ambazo hakufunga.


Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 186

وَإِذَا سَأَلَكَ عِبَادِي عَنِّي فَإِنِّي قَرِيبٌۖ أُجِيبُ دَعۡوَةَ ٱلدَّاعِ إِذَا دَعَانِۖ فَلۡيَسۡتَجِيبُواْ لِي وَلۡيُؤۡمِنُواْ بِي لَعَلَّهُمۡ يَرۡشُدُونَ

Na waja wangu wakikuuliza kuhusu mimi, kwa yakini kabisa mimi nipo karibu; naitikia ombi la muombaji anaponiomba. Basi nawaniitikie na waniamini ili wapate kuongoka



Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 187

أُحِلَّ لَكُمۡ لَيۡلَةَ ٱلصِّيَامِ ٱلرَّفَثُ إِلَىٰ نِسَآئِكُمۡۚ هُنَّ لِبَاسٞ لَّكُمۡ وَأَنتُمۡ لِبَاسٞ لَّهُنَّۗ عَلِمَ ٱللَّهُ أَنَّكُمۡ كُنتُمۡ تَخۡتَانُونَ أَنفُسَكُمۡ فَتَابَ عَلَيۡكُمۡ وَعَفَا عَنكُمۡۖ فَٱلۡـَٰٔنَ بَٰشِرُوهُنَّ وَٱبۡتَغُواْ مَا كَتَبَ ٱللَّهُ لَكُمۡۚ وَكُلُواْ وَٱشۡرَبُواْ حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَكُمُ ٱلۡخَيۡطُ ٱلۡأَبۡيَضُ مِنَ ٱلۡخَيۡطِ ٱلۡأَسۡوَدِ مِنَ ٱلۡفَجۡرِۖ ثُمَّ أَتِمُّواْ ٱلصِّيَامَ إِلَى ٱلَّيۡلِۚ وَلَا تُبَٰشِرُوهُنَّ وَأَنتُمۡ عَٰكِفُونَ فِي ٱلۡمَسَٰجِدِۗ تِلۡكَ حُدُودُ ٱللَّهِ فَلَا تَقۡرَبُوهَاۗ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ ٱللَّهُ ءَايَٰتِهِۦ لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمۡ يَتَّقُونَ

Mmehalalishiwa usiku wafunga kukutana kimwili na wake zenu. Wao ni vazi lenu, na nyinyi ni vazi lao. Allah amejua kwamba mlikuwa mkizihini nafsi zenu. Kwa hivyo, amekukubalieni toba yenu na amekusameheni. Basi sasa kutaneni nao kimwili natakeni aliyokuandikieni Allah. Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu weupe wa Alfajiri dhidi ya weusi wa usiku. Kisha timizeni funga mpaka usiku. Wala msikutane nao kimwili, na hali mmekaa Itikafu misikitini. Hiyo ni mipaka ya Allah, basi msiisogelee. Hivi ndivyo Allah anavyobainisha hoja zake kwa watu ili wapate kumcha



Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 188

وَلَا تَأۡكُلُوٓاْ أَمۡوَٰلَكُم بَيۡنَكُم بِٱلۡبَٰطِلِ وَتُدۡلُواْ بِهَآ إِلَى ٱلۡحُكَّامِ لِتَأۡكُلُواْ فَرِيقٗا مِّنۡ أَمۡوَٰلِ ٱلنَّاسِ بِٱلۡإِثۡمِ وَأَنتُمۡ تَعۡلَمُونَ

Na msile mali zenu baina yenu kwa batili na kuzipeleka kwa mahakimu ili mpate kula sehemu ya mali ya watu kwa dhambi na ilhali mnajua



Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 189

۞يَسۡـَٔلُونَكَ عَنِ ٱلۡأَهِلَّةِۖ قُلۡ هِيَ مَوَٰقِيتُ لِلنَّاسِ وَٱلۡحَجِّۗ وَلَيۡسَ ٱلۡبِرُّ بِأَن تَأۡتُواْ ٱلۡبُيُوتَ مِن ظُهُورِهَا وَلَٰكِنَّ ٱلۡبِرَّ مَنِ ٱتَّقَىٰۗ وَأۡتُواْ ٱلۡبُيُوتَ مِنۡ أَبۡوَٰبِهَاۚ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ لَعَلَّكُمۡ تُفۡلِحُونَ

Wanakuuliza kuhusu miezi miandamo. Sema (uwaambie): Hiyo (miezi miandamo) ni vipimo vya nyakati kwa watu na Hija. Na si katika wema kuingia (katika) nyumba kwa nyuma lakini wema ni kumcha Allah. Na ingieni majumbani kupitia kwenye milango yake, na mcheni Allah ili mpate kufaulu



Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 190

وَقَٰتِلُواْ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ ٱلَّذِينَ يُقَٰتِلُونَكُمۡ وَلَا تَعۡتَدُوٓاْۚ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُحِبُّ ٱلۡمُعۡتَدِينَ

Na piganeni na wanaokupigeni katika njia ya Allah, na msivuke mipaka (mkawashambulia wasiohusika), kwa sababu Allah hawapendi wavukao mipaka



Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 191

وَٱقۡتُلُوهُمۡ حَيۡثُ ثَقِفۡتُمُوهُمۡ وَأَخۡرِجُوهُم مِّنۡ حَيۡثُ أَخۡرَجُوكُمۡۚ وَٱلۡفِتۡنَةُ أَشَدُّ مِنَ ٱلۡقَتۡلِۚ وَلَا تُقَٰتِلُوهُمۡ عِندَ ٱلۡمَسۡجِدِ ٱلۡحَرَامِ حَتَّىٰ يُقَٰتِلُوكُمۡ فِيهِۖ فَإِن قَٰتَلُوكُمۡ فَٱقۡتُلُوهُمۡۗ كَذَٰلِكَ جَزَآءُ ٱلۡكَٰفِرِينَ

Na waueni popote mtaka-powakuta, na wafukuzeni popote watakapo kufukuzeni. Na fitina ni mbaya zaidi kuliko kuua. Na msipigane nao mbele ya Msikiti Mtukufu mpaka wao wapigane nanyi humo. Wakipigana nanyi humo, basi waueni. Hivyo ndivyo yatakiwavyo kuwa malipo ya makafiri



Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 192

فَإِنِ ٱنتَهَوۡاْ فَإِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٞ

Ikiwa wataacha[1] basi Allah ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa kurehemu


1- - Kukuchokozeni au kupambana nanyi


Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 193

وَقَٰتِلُوهُمۡ حَتَّىٰ لَا تَكُونَ فِتۡنَةٞ وَيَكُونَ ٱلدِّينُ لِلَّهِۖ فَإِنِ ٱنتَهَوۡاْ فَلَا عُدۡوَٰنَ إِلَّا عَلَى ٱلظَّـٰلِمِينَ

Na piganeni nao mpaka pasiwepo na fitina na dini iwe ya Allah tu. Ikiwa wataacha (kukufanyieni uadui) basi hapatakiwi kuwepo na uadui isipokuwa kwa madhalimu tu



Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 194

ٱلشَّهۡرُ ٱلۡحَرَامُ بِٱلشَّهۡرِ ٱلۡحَرَامِ وَٱلۡحُرُمَٰتُ قِصَاصٞۚ فَمَنِ ٱعۡتَدَىٰ عَلَيۡكُمۡ فَٱعۡتَدُواْ عَلَيۡهِ بِمِثۡلِ مَا ٱعۡتَدَىٰ عَلَيۡكُمۡۚ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّ ٱللَّهَ مَعَ ٱلۡمُتَّقِينَ

Mwezi mtukufu kwa mwezi mtukufu. Na kila kilicho kitukufu kitalipiwa kisasi. Na yeyote atakaye fanya uadui juu yenu, basi mlipeni sawa na uadui alioufanya kwenu. Na mcheni Allah na jueni kwamba Allah yupamoja na wamchao



Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 195

وَأَنفِقُواْ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ وَلَا تُلۡقُواْ بِأَيۡدِيكُمۡ إِلَى ٱلتَّهۡلُكَةِ وَأَحۡسِنُوٓاْۚ إِنَّ ٱللَّهَ يُحِبُّ ٱلۡمُحۡسِنِينَ

Na toeni katika njia ya Allah, na msijiingize kwenye maangamizi kwa mikono yenu. Na fanyeni mazuri, hakika Allah anawapenda wafanyao mazuri



Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 196

وَأَتِمُّواْ ٱلۡحَجَّ وَٱلۡعُمۡرَةَ لِلَّهِۚ فَإِنۡ أُحۡصِرۡتُمۡ فَمَا ٱسۡتَيۡسَرَ مِنَ ٱلۡهَدۡيِۖ وَلَا تَحۡلِقُواْ رُءُوسَكُمۡ حَتَّىٰ يَبۡلُغَ ٱلۡهَدۡيُ مَحِلَّهُۥۚ فَمَن كَانَ مِنكُم مَّرِيضًا أَوۡ بِهِۦٓ أَذٗى مِّن رَّأۡسِهِۦ فَفِدۡيَةٞ مِّن صِيَامٍ أَوۡ صَدَقَةٍ أَوۡ نُسُكٖۚ فَإِذَآ أَمِنتُمۡ فَمَن تَمَتَّعَ بِٱلۡعُمۡرَةِ إِلَى ٱلۡحَجِّ فَمَا ٱسۡتَيۡسَرَ مِنَ ٱلۡهَدۡيِۚ فَمَن لَّمۡ يَجِدۡ فَصِيَامُ ثَلَٰثَةِ أَيَّامٖ فِي ٱلۡحَجِّ وَسَبۡعَةٍ إِذَا رَجَعۡتُمۡۗ تِلۡكَ عَشَرَةٞ كَامِلَةٞۗ ذَٰلِكَ لِمَن لَّمۡ يَكُنۡ أَهۡلُهُۥ حَاضِرِي ٱلۡمَسۡجِدِ ٱلۡحَرَامِۚ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّ ٱللَّهَ شَدِيدُ ٱلۡعِقَابِ

Na timizeni Hija na Umra kwa ajili ya Allah. Na ikiwa mmezuiwa[1], basi chinjeni wanyama watakaokuwa rahisi kupatikana. Na wala msinyoe vichwa vyenu, hadi mnyama afike mahali pake. Basi ambaye atakuwa mgonjwa miongoni mwenu, au ana tatizo kichwani kwake, basi atoe fidia ya kufunga au sadaka au mnyama. Na mtakapokuwa katika hali ya amani, atakayefanya Umra kabla ya Hija[2] basi afunge siku tatu katika Hija na siku saba mtakaporejea kwenu. Hizo ni siku kumi kamili. Hilo ni kwa ambaye familia yake sio wakazi wa (mji wa) Msikiti Mtukufu (wa Makka). Na mcheni Allah, na jueni kwamba, Allah ni mkali wa kuadhibu


1- - Kutimiza ibada hizo


2- - Bila kuunganisha Umra na Hija


Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 197

ٱلۡحَجُّ أَشۡهُرٞ مَّعۡلُومَٰتٞۚ فَمَن فَرَضَ فِيهِنَّ ٱلۡحَجَّ فَلَا رَفَثَ وَلَا فُسُوقَ وَلَا جِدَالَ فِي ٱلۡحَجِّۗ وَمَا تَفۡعَلُواْ مِنۡ خَيۡرٖ يَعۡلَمۡهُ ٱللَّهُۗ وَتَزَوَّدُواْ فَإِنَّ خَيۡرَ ٱلزَّادِ ٱلتَّقۡوَىٰۖ وَٱتَّقُونِ يَـٰٓأُوْلِي ٱلۡأَلۡبَٰبِ

Hija ina miezi maalumu. Basi yeyote atakayeingia katika wajibu wa kutekeleza Hija katika miezi hiyo asiseme maneno yaliyokatazwa wala vitendo vilivyokatazwa wala asifanye mabishano katika Hija. Na wema wowote mnaoufanya Allah anaujua. Na jiandaeni, hakika maandalizi bora ni Ucha Mungu. Basi niogopeni enyi wenye akili



Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 198

لَيۡسَ عَلَيۡكُمۡ جُنَاحٌ أَن تَبۡتَغُواْ فَضۡلٗا مِّن رَّبِّكُمۡۚ فَإِذَآ أَفَضۡتُم مِّنۡ عَرَفَٰتٖ فَٱذۡكُرُواْ ٱللَّهَ عِندَ ٱلۡمَشۡعَرِ ٱلۡحَرَامِۖ وَٱذۡكُرُوهُ كَمَا هَدَىٰكُمۡ وَإِن كُنتُم مِّن قَبۡلِهِۦ لَمِنَ ٱلضَّآلِّينَ

Hakuna ubaya wowote kwenu kutafuta fadhila za Mola wenu. Basi mtakapomiminika kutoka Arafa, mtajeni Allah kwenye eneo la Mash-arilharam. Na mtajeni kama alivyokupeni muongozo. Na hakika, kabla yake mlikuwa katika watu waliopotea



Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 199

ثُمَّ أَفِيضُواْ مِنۡ حَيۡثُ أَفَاضَ ٱلنَّاسُ وَٱسۡتَغۡفِرُواْ ٱللَّهَۚ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٞ

Kisha miminikeni kutokea pale walipomiminika watu, naombeni msamaha kwa Allah, hakika Allah ni Mwingi wa kusamehe, Mpole mno



Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 200

فَإِذَا قَضَيۡتُم مَّنَٰسِكَكُمۡ فَٱذۡكُرُواْ ٱللَّهَ كَذِكۡرِكُمۡ ءَابَآءَكُمۡ أَوۡ أَشَدَّ ذِكۡرٗاۗ فَمِنَ ٱلنَّاسِ مَن يَقُولُ رَبَّنَآ ءَاتِنَا فِي ٱلدُّنۡيَا وَمَا لَهُۥ فِي ٱلۡأٓخِرَةِ مِنۡ خَلَٰقٖ

Mtakapomaliza ibada zenu, basi mtajeni Allah, kama mnavyowataja baba zenu au zaidi. Na miongoni mwa watu wapo wanaosema: “Ewe Mola wetu tupe katika dunia, na hawatakuwa na fungu lolote Akhera



Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 201

وَمِنۡهُم مَّن يَقُولُ رَبَّنَآ ءَاتِنَا فِي ٱلدُّنۡيَا حَسَنَةٗ وَفِي ٱلۡأٓخِرَةِ حَسَنَةٗ وَقِنَا عَذَابَ ٱلنَّارِ

Na baadhi yao wapo wanaosema: Ewe Mola wetu, tupe katika dunia wema, na Akhera wema na utukinge na adhabu ya Moto



Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 202

أُوْلَـٰٓئِكَ لَهُمۡ نَصِيبٞ مِّمَّا كَسَبُواْۚ وَٱللَّهُ سَرِيعُ ٱلۡحِسَابِ

Hao wanalo fungu katika waliyoyachuma. Na Allah ni Mwepesi wa kuhesabu



Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 203

۞وَٱذۡكُرُواْ ٱللَّهَ فِيٓ أَيَّامٖ مَّعۡدُودَٰتٖۚ فَمَن تَعَجَّلَ فِي يَوۡمَيۡنِ فَلَآ إِثۡمَ عَلَيۡهِ وَمَن تَأَخَّرَ فَلَآ إِثۡمَ عَلَيۡهِۖ لِمَنِ ٱتَّقَىٰۗ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّكُمۡ إِلَيۡهِ تُحۡشَرُونَ

Na mtajeni Allah katika siku chache. Atakayefanya haraka[1] ndani ya siku mbili, basi hakuna dhambi yoyote kwake. Na atakayechelewa hakuna dhambi kwake; kwa mwenye kumcha Allah. Na mcheni Allah najueni kuwa bila ya shaka nyinyi mtakusanywa kwake tu


1- - Kuondoka Mina


Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 204

وَمِنَ ٱلنَّاسِ مَن يُعۡجِبُكَ قَوۡلُهُۥ فِي ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا وَيُشۡهِدُ ٱللَّهَ عَلَىٰ مَا فِي قَلۡبِهِۦ وَهُوَ أَلَدُّ ٱلۡخِصَامِ

Na miongoni mwa watu wapo ambao zinakuvutia kauli zao katika maisha ya dunia, na wanamshuhudisha Allah juu ya yaliyo moyoni mwake hali yeye ni mpingaji mno



Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 205

وَإِذَا تَوَلَّىٰ سَعَىٰ فِي ٱلۡأَرۡضِ لِيُفۡسِدَ فِيهَا وَيُهۡلِكَ ٱلۡحَرۡثَ وَٱلنَّسۡلَۚ وَٱللَّهُ لَا يُحِبُّ ٱلۡفَسَادَ

Na anapoondoka (kwako) anahangaika huku na kule ardhini ili kufanya ufisadi humo na kuangamiza mimea na vizazi. Na Allah hapendi ufisadi



Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 206

وَإِذَا قِيلَ لَهُ ٱتَّقِ ٱللَّهَ أَخَذَتۡهُ ٱلۡعِزَّةُ بِٱلۡإِثۡمِۚ فَحَسۡبُهُۥ جَهَنَّمُۖ وَلَبِئۡسَ ٱلۡمِهَادُ

Na wanapoambiwa; Muogopeni Allah hupandwa na mori wa kufanya uovu. Basi kitakachowatosha ni Jahanamu na ni makazi mabaya mno



Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 207

وَمِنَ ٱلنَّاسِ مَن يَشۡرِي نَفۡسَهُ ٱبۡتِغَآءَ مَرۡضَاتِ ٱللَّهِۚ وَٱللَّهُ رَءُوفُۢ بِٱلۡعِبَادِ

Na miongoni mwa watu wapo ambao huuza nafsi zao kwa ajili ya kutafuta radhi za Allah na Allah ni Mpole sana kwa waja



Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 208

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱدۡخُلُواْ فِي ٱلسِّلۡمِ كَآفَّةٗ وَلَا تَتَّبِعُواْ خُطُوَٰتِ ٱلشَّيۡطَٰنِۚ إِنَّهُۥ لَكُمۡ عَدُوّٞ مُّبِينٞ

Enyi mlioamini, ingieni kwenye Uislamu wote (wazima wazima), na msifuate nyayo za shetani, hakika yeye kwenu ni adui aliye wazi



Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 209

فَإِن زَلَلۡتُم مِّنۢ بَعۡدِ مَا جَآءَتۡكُمُ ٱلۡبَيِّنَٰتُ فَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّ ٱللَّهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ

Na kama mtateleza[1] baada ya kukujieni hoja za wazi, basi jueni kwamba, Allah ni mwenye nguvu nyingi mwingi wa hekima


1- - Kwa kuacha baadhi ya sheria na hukumu


Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 210

هَلۡ يَنظُرُونَ إِلَّآ أَن يَأۡتِيَهُمُ ٱللَّهُ فِي ظُلَلٖ مِّنَ ٱلۡغَمَامِ وَٱلۡمَلَـٰٓئِكَةُ وَقُضِيَ ٱلۡأَمۡرُۚ وَإِلَى ٱللَّهِ تُرۡجَعُ ٱلۡأُمُورُ

Hakuna wanachongojea isipokuwa kuwajia Allah na Malaika kwenye vivuli vya mawingu na jambo lishakatiwa shauri. Na kwa Allah pekee ndipo yanaporudishwa mambo