Sourate: AL-HIJRI 

Verset : 91

ٱلَّذِينَ جَعَلُواْ ٱلۡقُرۡءَانَ عِضِينَ

Ambao waliifanya (hii) Qur’ani vipande vipande



Sourate: AL-HIJRI 

Verset : 92

فَوَرَبِّكَ لَنَسۡـَٔلَنَّهُمۡ أَجۡمَعِينَ

Basi Naapa kwa Mola wako Mlezi, tutawahoji wote



Sourate: AL-HIJRI 

Verset : 93

عَمَّا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ

Kwa waliyokuwa wanayatenda



Sourate: AL-HIJRI 

Verset : 94

فَٱصۡدَعۡ بِمَا تُؤۡمَرُ وَأَعۡرِضۡ عَنِ ٱلۡمُشۡرِكِينَ

Basi wewe yatangaze uliyoa-mrishwa, na jitenge na washirikina



Sourate: AL-HIJRI 

Verset : 95

إِنَّا كَفَيۡنَٰكَ ٱلۡمُسۡتَهۡزِءِينَ

Hakika Sisi tunatosha kukukinga na (shari za) wanaokejeli



Sourate: AL-HIJRI 

Verset : 96

ٱلَّذِينَ يَجۡعَلُونَ مَعَ ٱللَّهِ إِلَٰهًا ءَاخَرَۚ فَسَوۡفَ يَعۡلَمُونَ

Hao wemefanya muabudiwa mwingine pamoja na Allah. Basi, watakuja kujua



Sourate: AL-HIJRI 

Verset : 97

وَلَقَدۡ نَعۡلَمُ أَنَّكَ يَضِيقُ صَدۡرُكَ بِمَا يَقُولُونَ

Na kwa hakika, Sisi tunajua kuwa wewe kifua chako kinaona dhiki kwa hayo wayasemayo



Sourate: AL-HIJRI 

Verset : 98

فَسَبِّحۡ بِحَمۡدِ رَبِّكَ وَكُن مِّنَ ٱلسَّـٰجِدِينَ

Basi mtakase Mola wako Mlezi kwa kumhimidi, na uwe miongoni mwa wanao msujudia



Sourate: AL-HIJRI 

Verset : 99

وَٱعۡبُدۡ رَبَّكَ حَتَّىٰ يَأۡتِيَكَ ٱلۡيَقِينُ

Na muabudu Mola wako Mlezi mpaka mauti yakufike