Sourate: ANNAHLI 

Verset : 61

وَلَوۡ يُؤَاخِذُ ٱللَّهُ ٱلنَّاسَ بِظُلۡمِهِم مَّا تَرَكَ عَلَيۡهَا مِن دَآبَّةٖ وَلَٰكِن يُؤَخِّرُهُمۡ إِلَىٰٓ أَجَلٖ مُّسَمّٗىۖ فَإِذَا جَآءَ أَجَلُهُمۡ لَا يَسۡتَـٔۡخِرُونَ سَاعَةٗ وَلَا يَسۡتَقۡدِمُونَ

Na lau Allah angewachukulia hatua watu kwasababu ya dhuluma yao, asingemuacha hata mnyama mmoja; Lakini anawasubirisha mpaka muda uliowekwa; Na utakapofika muda wao, hawataweza kuichelewesha saa moja na hawataweza kuiwahisha



Sourate: ANNAHLI 

Verset : 62

وَيَجۡعَلُونَ لِلَّهِ مَا يَكۡرَهُونَۚ وَتَصِفُ أَلۡسِنَتُهُمُ ٱلۡكَذِبَ أَنَّ لَهُمُ ٱلۡحُسۡنَىٰۚ لَا جَرَمَ أَنَّ لَهُمُ ٱلنَّارَ وَأَنَّهُم مُّفۡرَطُونَ

Na wanampa Allah yale wasiyoyachukua (wao katika nafsi zao), na ndimi zao zinasema uongo kwamba wao watapata mwisho mwema. Bila shaka wamewekewa Moto, nao wataachwa (humo milele)



Sourate: ANNAHLI 

Verset : 63

تَٱللَّهِ لَقَدۡ أَرۡسَلۡنَآ إِلَىٰٓ أُمَمٖ مِّن قَبۡلِكَ فَزَيَّنَ لَهُمُ ٱلشَّيۡطَٰنُ أَعۡمَٰلَهُمۡ فَهُوَ وَلِيُّهُمُ ٱلۡيَوۡمَ وَلَهُمۡ عَذَابٌ أَلِيمٞ

Naapa kwajina la Allah hakika tulipeleka (Mitume) kwa umma zilizokuwa kabla yako, na shetani akawapambia matendo yao (mabaya wakayaona mazuri), basi yeye (shetani) leo ni rafiki yao, nao watapata adhabu iumizayo mno (Siku ya Kiyama)



Sourate: ANNAHLI 

Verset : 64

وَمَآ أَنزَلۡنَا عَلَيۡكَ ٱلۡكِتَٰبَ إِلَّا لِتُبَيِّنَ لَهُمُ ٱلَّذِي ٱخۡتَلَفُواْ فِيهِ وَهُدٗى وَرَحۡمَةٗ لِّقَوۡمٖ يُؤۡمِنُونَ

Na hatukukuteremshia kitabu - isipokuwa tu uwabainishie yale ambayo wanahitilafiana humo, na (kiwe) muongozo na rehema kwa watu wanaoamini



Sourate: ANNAHLI 

Verset : 65

وَٱللَّهُ أَنزَلَ مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءٗ فَأَحۡيَا بِهِ ٱلۡأَرۡضَ بَعۡدَ مَوۡتِهَآۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةٗ لِّقَوۡمٖ يَسۡمَعُونَ

Na Allah ameteremsha maji kutoka mbinguni na akahuisha kwa maji hayo ardhi baada ya kufa kwake (kwa ukame). Kwa hakika katika hayo (ya kuteremsha mvua na kuhuisha ardhi) kuna ishara ya wazi (juu ya uwepo wa Allah) kwa watu wanaosikia (na kuzingatia)



Sourate: ANNAHLI 

Verset : 66

وَإِنَّ لَكُمۡ فِي ٱلۡأَنۡعَٰمِ لَعِبۡرَةٗۖ نُّسۡقِيكُم مِّمَّا فِي بُطُونِهِۦ مِنۢ بَيۡنِ فَرۡثٖ وَدَمٖ لَّبَنًا خَالِصٗا سَآئِغٗا لِّلشَّـٰرِبِينَ

Na hakika katika wanyama howa (wa kufugwa) nyinyi mna funzo. Tunawanywesheni katika vile vilivyomo matumboni mwao, kati ya kinyesi na damu, (yanatoka) maziwa halisi, yaburudishayo wanywaji



Sourate: ANNAHLI 

Verset : 67

وَمِن ثَمَرَٰتِ ٱلنَّخِيلِ وَٱلۡأَعۡنَٰبِ تَتَّخِذُونَ مِنۡهُ سَكَرٗا وَرِزۡقًا حَسَنًاۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةٗ لِّقَوۡمٖ يَعۡقِلُونَ

Na katika matunda ya mitende na mizabibu ambayo mnatengenezea kileo na chakula kizuri. Hakika katika hayo kuna ishara kwa watu wenye akili



Sourate: ANNAHLI 

Verset : 68

وَأَوۡحَىٰ رَبُّكَ إِلَى ٱلنَّحۡلِ أَنِ ٱتَّخِذِي مِنَ ٱلۡجِبَالِ بُيُوتٗا وَمِنَ ٱلشَّجَرِ وَمِمَّا يَعۡرِشُونَ

Na Mola wako mlezi amem-funulia (amempa Ilham) nyuki kwamba fanya baadhi ya majabali kuwa makazi na baadhi ya miti na mizinga wanayoitundika



Sourate: ANNAHLI 

Verset : 69

ثُمَّ كُلِي مِن كُلِّ ٱلثَّمَرَٰتِ فَٱسۡلُكِي سُبُلَ رَبِّكِ ذُلُلٗاۚ يَخۡرُجُ مِنۢ بُطُونِهَا شَرَابٞ مُّخۡتَلِفٌ أَلۡوَٰنُهُۥ فِيهِ شِفَآءٞ لِّلنَّاسِۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةٗ لِّقَوۡمٖ يَتَفَكَّرُونَ

Kisha kula kila aina ya matunda, na zifuate kwa unyenyekevu njia za Mola wako mlezi. Kinatoka katika matumbo yao kinywaji chenye rangi mbalimbali. Ndani yake kuna shifaa kwa watu. Hakika katika hayo kuna ishara kwa watu wenye kutafakari (na kuzingatia)



Sourate: ANNAHLI 

Verset : 70

وَٱللَّهُ خَلَقَكُمۡ ثُمَّ يَتَوَفَّىٰكُمۡۚ وَمِنكُم مَّن يُرَدُّ إِلَىٰٓ أَرۡذَلِ ٱلۡعُمُرِ لِكَيۡ لَا يَعۡلَمَ بَعۡدَ عِلۡمٖ شَيۡـًٔاۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلِيمٞ قَدِيرٞ

Na Allah amewaumbeni, kisha atawafisheni, na miongoni mwenu wapo wanaorudishwa katika umri wa udhaifu (ukongwe), matokeo yake anakuwa hajui chochote baada ya elimu aliyokua nayo. Kwa hakika Allah ni mjuzi sana na ni muweza



Sourate: ANNAHLI 

Verset : 71

وَٱللَّهُ فَضَّلَ بَعۡضَكُمۡ عَلَىٰ بَعۡضٖ فِي ٱلرِّزۡقِۚ فَمَا ٱلَّذِينَ فُضِّلُواْ بِرَآدِّي رِزۡقِهِمۡ عَلَىٰ مَا مَلَكَتۡ أَيۡمَٰنُهُمۡ فَهُمۡ فِيهِ سَوَآءٌۚ أَفَبِنِعۡمَةِ ٱللَّهِ يَجۡحَدُونَ

Na Allah amewapa ubora (ziada) baadhi yenu kwa wengine katika riziki[1]. Lakini wale walio fadhilishwa hawarudishi riziki zao kwa wale walio wamiliki kwa mikono yao ya kuume ili wawe sawa katika (riziki) hiyo. Hivo basi, wanazipinga neema za Allah?


1- - Allah katika Aya hii anaelezea dhana ya Washirikishaji na ubaya wao,. Allah amewafadhilisha watu wao kwa wao akawafanya baadhi matajiri na wengine mafakiri, masikini, watumwa na walio huru. Kisha anawauliza matajiri walio washirikishaji hivi ni kwanini wanavishirikisha na yeye Allah katika kuviabudu hivyo kama wanavyo muabudu yeye ilhali wao hawawashirikishi watumwa wao katika matumizi ya mali wanazo zimiliki wakawa sawasawa anamalizia kwa kusema hii ni dhuluma kubwa ambayo wao wameikataa kwa watumwa wao na wameiridhia kwa Allah.


Sourate: ANNAHLI 

Verset : 72

وَٱللَّهُ جَعَلَ لَكُم مِّنۡ أَنفُسِكُمۡ أَزۡوَٰجٗا وَجَعَلَ لَكُم مِّنۡ أَزۡوَٰجِكُم بَنِينَ وَحَفَدَةٗ وَرَزَقَكُم مِّنَ ٱلطَّيِّبَٰتِۚ أَفَبِٱلۡبَٰطِلِ يُؤۡمِنُونَ وَبِنِعۡمَتِ ٱللَّهِ هُمۡ يَكۡفُرُونَ

Na Allah amewafanyieni wake kutokana na nyinyi wenyewe, na akawafanyieni watoto kutokanana wake zenu hao na wajukuu, na akawaruzuku miongoni mwa vitu vilivyo vizuri. Basi je, wanaamini batili na neema za Allah wanazipinga?



Sourate: ANNAHLI 

Verset : 73

وَيَعۡبُدُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ مَا لَا يَمۡلِكُ لَهُمۡ رِزۡقٗا مِّنَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ شَيۡـٔٗا وَلَا يَسۡتَطِيعُونَ

Na wanaabudu kinyume cha Allah wasio na uwezo wa kuwapatia wao riziki yoyote mbinguni na ardhini, na hawana uwezo



Sourate: ANNAHLI 

Verset : 74

فَلَا تَضۡرِبُواْ لِلَّهِ ٱلۡأَمۡثَالَۚ إِنَّ ٱللَّهَ يَعۡلَمُ وَأَنتُمۡ لَا تَعۡلَمُونَ

Na msimpigie Allah mifano. Hakika Allah anajua na ninyi hamjui (chochote)



Sourate: ANNAHLI 

Verset : 75

۞ضَرَبَ ٱللَّهُ مَثَلًا عَبۡدٗا مَّمۡلُوكٗا لَّا يَقۡدِرُ عَلَىٰ شَيۡءٖ وَمَن رَّزَقۡنَٰهُ مِنَّا رِزۡقًا حَسَنٗا فَهُوَ يُنفِقُ مِنۡهُ سِرّٗا وَجَهۡرًاۖ هَلۡ يَسۡتَوُۥنَۚ ٱلۡحَمۡدُ لِلَّهِۚ بَلۡ أَكۡثَرُهُمۡ لَا يَعۡلَمُونَ

Allah amepiga mfano wa mtumwa anayemilikiwa; asiyeweza chochote, na (mfano wa mtu mwingine) tuliyemruzuku riziki njema (mali nyingi), akawa anatoa katika mali hiyo kwa siri na dhahiri. Hivi, watu hao watakuwa sawa? Alhamduli LLahi! Kila sifa njema anastahiki Allah Lakini wengi wao hawajui



Sourate: ANNAHLI 

Verset : 76

وَضَرَبَ ٱللَّهُ مَثَلٗا رَّجُلَيۡنِ أَحَدُهُمَآ أَبۡكَمُ لَا يَقۡدِرُ عَلَىٰ شَيۡءٖ وَهُوَ كَلٌّ عَلَىٰ مَوۡلَىٰهُ أَيۡنَمَا يُوَجِّههُّ لَا يَأۡتِ بِخَيۡرٍ هَلۡ يَسۡتَوِي هُوَ وَمَن يَأۡمُرُ بِٱلۡعَدۡلِ وَهُوَ عَلَىٰ صِرَٰطٖ مُّسۡتَقِيمٖ

Na Allah anapiga mfano wa watu wawili: Mmoja wao bubu, hawezi chochote, naye ni mzigo juu ya bwana wake, popote amtumapo haleti heri. Hivi, huyu anaweza kuwa sawa na yule anayeamuru kwa uadilifu naye yupo katika njia iliyonyoka?[1]


1- - Aya inaelezea ubora wa aliye na elimu na asiye na elimu kuwa asiye na elimu ni sawa na bubu hana kheri yeyote itakayo mnufaisha Allah. Lakini pia mwenye elimu akaacha kuifanyia kazi katika daawa elimu yake sawa na kutokuwa nayo hana tofauti na bubu.


Sourate: ANNAHLI 

Verset : 77

وَلِلَّهِ غَيۡبُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۚ وَمَآ أَمۡرُ ٱلسَّاعَةِ إِلَّا كَلَمۡحِ ٱلۡبَصَرِ أَوۡ هُوَ أَقۡرَبُۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٞ

Na ni Allah tu anayejua visivyoo-nekana mbinguni na ardhini na halikua jambo la kutokea Kiyama (uharaka wa kutokea) kwake isipokuwa tu ni kama kupepesa jicho au ni haraka zaidi ya hivyo. Hakika Allah ni muweza wa kila kitu



Sourate: ANNAHLI 

Verset : 78

وَٱللَّهُ أَخۡرَجَكُم مِّنۢ بُطُونِ أُمَّهَٰتِكُمۡ لَا تَعۡلَمُونَ شَيۡـٔٗا وَجَعَلَ لَكُمُ ٱلسَّمۡعَ وَٱلۡأَبۡصَٰرَ وَٱلۡأَفۡـِٔدَةَ لَعَلَّكُمۡ تَشۡكُرُونَ

Na Allah amewatoeni katika matumbo ya mama zenu ikiwa hamjui chochote, na amewajaalieni masikio na macho na mioyo ili mpate kushukuru



Sourate: ANNAHLI 

Verset : 79

أَلَمۡ يَرَوۡاْ إِلَى ٱلطَّيۡرِ مُسَخَّرَٰتٖ فِي جَوِّ ٱلسَّمَآءِ مَا يُمۡسِكُهُنَّ إِلَّا ٱللَّهُۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَٰتٖ لِّقَوۡمٖ يُؤۡمِنُونَ

Hivi hawaoni ndege waliowezeshwa kuogelea angani? Hakuna anayewashikilia isipokuwa Allah. Bila shaka katika hayo kuna ishara kwa watu wanaoamini



Sourate: ANNAHLI 

Verset : 80

وَٱللَّهُ جَعَلَ لَكُم مِّنۢ بُيُوتِكُمۡ سَكَنٗا وَجَعَلَ لَكُم مِّن جُلُودِ ٱلۡأَنۡعَٰمِ بُيُوتٗا تَسۡتَخِفُّونَهَا يَوۡمَ ظَعۡنِكُمۡ وَيَوۡمَ إِقَامَتِكُمۡ وَمِنۡ أَصۡوَافِهَا وَأَوۡبَارِهَا وَأَشۡعَارِهَآ أَثَٰثٗا وَمَتَٰعًا إِلَىٰ حِينٖ

Na Allah ameyafanya majumba yenu kuwa sehemu ya kupum-zika (wakati usio wa safari), na amewafanyieni wakati wa safari ngozi za wanyama howa (wa kufugwa), ni rahisi kwenu kubeba wakati wa safari zenu, na wepesi kwenu kuchomeka kwake (mahema) wakati wa kutua kwenu baada ya safari zenu; na katika sufi (za kondoo), na mikojo ya (ngamia na manyoya ya (mbuzi), (mnatengeneza) vyombo na vifaa vya kutumia (busati, mifuko na mapambo mbali mbali) kwa muda



Sourate: ANNAHLI 

Verset : 81

وَٱللَّهُ جَعَلَ لَكُم مِّمَّا خَلَقَ ظِلَٰلٗا وَجَعَلَ لَكُم مِّنَ ٱلۡجِبَالِ أَكۡنَٰنٗا وَجَعَلَ لَكُمۡ سَرَٰبِيلَ تَقِيكُمُ ٱلۡحَرَّ وَسَرَٰبِيلَ تَقِيكُم بَأۡسَكُمۡۚ كَذَٰلِكَ يُتِمُّ نِعۡمَتَهُۥ عَلَيۡكُمۡ لَعَلَّكُمۡ تُسۡلِمُونَ

Na Allah amewafanyieni katika vile alivyoviumba, vitiavyo kivuli (kama miti na milima) na amewafanyieni milima kuwa sehemu ya kukimbilia, na amewafanyieni kanzu zinazowakingeni na joto, na dereya[1] zinazowakingeni katika vita vyenu. Hivi ndivyo (Allah) anatimiza neema zake kwenu ili mpate kutii


1- - Ni vazi la chuma linalovaliwa vitani kujikinga na mikuki na silaha zote (proof)


Sourate: ANNAHLI 

Verset : 82

فَإِن تَوَلَّوۡاْ فَإِنَّمَا عَلَيۡكَ ٱلۡبَلَٰغُ ٱلۡمُبِينُ

Na endapo watakengeuka basi hakika huna jukumu isipokuwa kufikisha (ujumbe) waziwazi tu



Sourate: ANNAHLI 

Verset : 83

يَعۡرِفُونَ نِعۡمَتَ ٱللَّهِ ثُمَّ يُنكِرُونَهَا وَأَكۡثَرُهُمُ ٱلۡكَٰفِرُونَ

Wanazijua neema za Allah kisha wanazipinga na wengi wao ni makafiri



Sourate: ANNAHLI 

Verset : 84

وَيَوۡمَ نَبۡعَثُ مِن كُلِّ أُمَّةٖ شَهِيدٗا ثُمَّ لَا يُؤۡذَنُ لِلَّذِينَ كَفَرُواْ وَلَا هُمۡ يُسۡتَعۡتَبُونَ

Na (wakumbushe ewe Mtume) siku tutakapofufua shahidi (Mtume wao) kwa kila umma, kisha wale waliyokufuru hawataruhusiwa (kujisahihisha kutokana na waliyoyafanya) na hawata kubaliwa udhuru



Sourate: ANNAHLI 

Verset : 85

وَإِذَا رَءَا ٱلَّذِينَ ظَلَمُواْ ٱلۡعَذَابَ فَلَا يُخَفَّفُ عَنۡهُمۡ وَلَا هُمۡ يُنظَرُونَ

Na wale waliodhulumu watakapoiona adhabu, basi hawata punguziwa (adhabu) na hawatasubiriwa



Sourate: ANNAHLI 

Verset : 86

وَإِذَا رَءَا ٱلَّذِينَ أَشۡرَكُواْ شُرَكَآءَهُمۡ قَالُواْ رَبَّنَا هَـٰٓؤُلَآءِ شُرَكَآؤُنَا ٱلَّذِينَ كُنَّا نَدۡعُواْ مِن دُونِكَۖ فَأَلۡقَوۡاْ إِلَيۡهِمُ ٱلۡقَوۡلَ إِنَّكُمۡ لَكَٰذِبُونَ

Na pindi wale washirikina watakapo waona washirika wao (walio washirikisha na Allah), watasema: Mola wetu mlezi, hao ndio washirika wetu ambao tulikuwa tunawaabudu badala yako. Basi watawatupia neno (kwa kusema): hakika ninyi ni waongo kabisa



Sourate: ANNAHLI 

Verset : 87

وَأَلۡقَوۡاْ إِلَى ٱللَّهِ يَوۡمَئِذٍ ٱلسَّلَمَۖ وَضَلَّ عَنۡهُم مَّا كَانُواْ يَفۡتَرُونَ

Na siku hiyo (washirikishaji) watadhihirisha utii mbele ya Allah, na yatawapotea yote waliyokuwa wakiyatunga



Sourate: ANNAHLI 

Verset : 88

ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ وَصَدُّواْ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ زِدۡنَٰهُمۡ عَذَابٗا فَوۡقَ ٱلۡعَذَابِ بِمَا كَانُواْ يُفۡسِدُونَ

(Ama) wale waliokufuru na wakawazuia (watu) njia ya Allah, tutawazidishia adhabu juu ya adhabu kwa yale waliokuwa wakiyaharibu



Sourate: ANNAHLI 

Verset : 89

وَيَوۡمَ نَبۡعَثُ فِي كُلِّ أُمَّةٖ شَهِيدًا عَلَيۡهِم مِّنۡ أَنفُسِهِمۡۖ وَجِئۡنَا بِكَ شَهِيدًا عَلَىٰ هَـٰٓؤُلَآءِۚ وَنَزَّلۡنَا عَلَيۡكَ ٱلۡكِتَٰبَ تِبۡيَٰنٗا لِّكُلِّ شَيۡءٖ وَهُدٗى وَرَحۡمَةٗ وَبُشۡرَىٰ لِلۡمُسۡلِمِينَ

Na siku tutakayomfufua shahidi (Mtume) katika kila umma kutoka miongoni mwao atakayethibitisha (kuwa aliwafikishia ujumbe wa Allah wakampinga), na tutakuleta wewe kuwa shahidi wa (watu) hawa. Na tumekuteremshia kitabu kikibainisha kila kitu, na rehema na bishara kwa Waislamu



Sourate: ANNAHLI 

Verset : 90

۞إِنَّ ٱللَّهَ يَأۡمُرُ بِٱلۡعَدۡلِ وَٱلۡإِحۡسَٰنِ وَإِيتَآيِٕ ذِي ٱلۡقُرۡبَىٰ وَيَنۡهَىٰ عَنِ ٱلۡفَحۡشَآءِ وَٱلۡمُنكَرِ وَٱلۡبَغۡيِۚ يَعِظُكُمۡ لَعَلَّكُمۡ تَذَكَّرُونَ

Kwa hakika Allah anaamuru uadilifu, na ihsani, na kuwapa (sadaka) ndugu wa karibu na anakataza uchafu, na uovu, na uasi. Anawanasihini ili mpate kukumbuka