وَمَآءٖ مَّسۡكُوبٖ
Na maji yenye kumiminwa
Partager :
وَفَٰكِهَةٖ كَثِيرَةٖ
Na matunda mengi
لَّا مَقۡطُوعَةٖ وَلَا مَمۡنُوعَةٖ
Hayana kikomo na wala hayakatazwi
وَفُرُشٖ مَّرۡفُوعَةٍ
Na matandiko ya kupumzikia yaliyoinuliwa
إِنَّآ أَنشَأۡنَٰهُنَّ إِنشَآءٗ
Hakika Sisi Tutawaumba (Mahurulaini) upya
فَجَعَلۡنَٰهُنَّ أَبۡكَارًا
Na tukawafanya kuwa bikra
عُرُبًا أَتۡرَابٗا
Wenye mahaba kwa waume zao, na wana umri unaolingana
لِّأَصۡحَٰبِ ٱلۡيَمِينِ
Ni kwaajili ya watu wa kuliani
ثُلَّةٞ مِّنَ ٱلۡأَوَّلِينَ
Kundi kubwa katika watu wa mwanzo
وَثُلَّةٞ مِّنَ ٱلۡأٓخِرِينَ
Na kundi kubwa katika watu wa mwishoni
وَأَصۡحَٰبُ ٱلشِّمَالِ مَآ أَصۡحَٰبُ ٱلشِّمَالِ
Na watu wa kushotoni, je, ni wepi watu wa kushotoni?
فِي سَمُومٖ وَحَمِيمٖ
(Watakuwa) Kwenye moto ubabuao na maji yachemkayo
وَظِلّٖ مِّن يَحۡمُومٖ
Na kivuli cha moshi mweusi mnene wa joto kali mno
لَّا بَارِدٖ وَلَا كَرِيمٍ
Si cha baridi na wala si cha kunufaisha
إِنَّهُمۡ كَانُواْ قَبۡلَ ذَٰلِكَ مُتۡرَفِينَ
Hakika walikua kabla ya hapo kwenye maisha ya neema na anasa
وَكَانُواْ يُصِرُّونَ عَلَى ٱلۡحِنثِ ٱلۡعَظِيمِ
Na walikuwa wakishikilia kufanya dhambi kubwa mno
وَكَانُواْ يَقُولُونَ أَئِذَا مِتۡنَا وَكُنَّا تُرَابٗا وَعِظَٰمًا أَءِنَّا لَمَبۡعُوثُونَ
Na walikuwa wakisema: Je, hivi tutakapo kufa na tukawa udongo na mifupa, je hivi sisi hakika tutafufuliwa?
أَوَءَابَآؤُنَا ٱلۡأَوَّلُونَ
Au na wazee wetu wa mwanzo?
قُلۡ إِنَّ ٱلۡأَوَّلِينَ وَٱلۡأٓخِرِينَ
Sema; Hakika wa mwanzo na wa mwisho,
لَمَجۡمُوعُونَ إِلَىٰ مِيقَٰتِ يَوۡمٖ مَّعۡلُومٖ
Hakika watakusanywa kwenye wakati na siku maalumu
ثُمَّ إِنَّكُمۡ أَيُّهَا ٱلضَّآلُّونَ ٱلۡمُكَذِّبُونَ
Kisha hakika nyinyi enyi wapotovu mnaokadhibisha
لَأٓكِلُونَ مِن شَجَرٖ مِّن زَقُّومٖ
Hakika mtakula chakula kitokanacho na mti wa mzakoum
فَمَالِـُٔونَ مِنۡهَا ٱلۡبُطُونَ
Basi mtajaza kutokana na mti huo matumbo yenu
فَشَٰرِبُونَ عَلَيۡهِ مِنَ ٱلۡحَمِيمِ
Na mtakunywa juu yake maji ya moto ya chemkayo
فَشَٰرِبُونَ شُرۡبَ ٱلۡهِيمِ
Tena mtakunywa unywaji wa ngamia mwenye kiu kubwa
هَٰذَا نُزُلُهُمۡ يَوۡمَ ٱلدِّينِ
Haya ndio mapokezi yao Siku ya Malipo! (Kiyama)
نَحۡنُ خَلَقۡنَٰكُمۡ فَلَوۡلَا تُصَدِّقُونَ
Sisi Tumekuumbeni, basi kwa nini hamsadikishi hilo?
أَفَرَءَيۡتُم مَّا تُمۡنُونَ
Je, mnaona mbegu ya uzazi mnayo imwagia kwa nguvu?
ءَأَنتُمۡ تَخۡلُقُونَهُۥٓ أَمۡ نَحۡنُ ٱلۡخَٰلِقُونَ
Je, nyinyi ndio mnaiumba au sisi ndio Waumbaji?
نَحۡنُ قَدَّرۡنَا بَيۡنَكُمُ ٱلۡمَوۡتَ وَمَا نَحۡنُ بِمَسۡبُوقِينَ
Sisi tumekadiria kati yenu umauti na haikua sisi wenye kukimbiwa