Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 249

فَلَمَّا فَصَلَ طَالُوتُ بِٱلۡجُنُودِ قَالَ إِنَّ ٱللَّهَ مُبۡتَلِيكُم بِنَهَرٖ فَمَن شَرِبَ مِنۡهُ فَلَيۡسَ مِنِّي وَمَن لَّمۡ يَطۡعَمۡهُ فَإِنَّهُۥ مِنِّيٓ إِلَّا مَنِ ٱغۡتَرَفَ غُرۡفَةَۢ بِيَدِهِۦۚ فَشَرِبُواْ مِنۡهُ إِلَّا قَلِيلٗا مِّنۡهُمۡۚ فَلَمَّا جَاوَزَهُۥ هُوَ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مَعَهُۥ قَالُواْ لَا طَاقَةَ لَنَا ٱلۡيَوۡمَ بِجَالُوتَ وَجُنُودِهِۦۚ قَالَ ٱلَّذِينَ يَظُنُّونَ أَنَّهُم مُّلَٰقُواْ ٱللَّهِ كَم مِّن فِئَةٖ قَلِيلَةٍ غَلَبَتۡ فِئَةٗ كَثِيرَةَۢ بِإِذۡنِ ٱللَّهِۗ وَٱللَّهُ مَعَ ٱلصَّـٰبِرِينَ

Basi Twaluti alipoondoka na majeshi alisema: Hakika Allah atakufanyieni mtihani kwa mto, basi atakayekunywa humo si pamoja nami, na asiye yanywa bila shaka yupo pamoja nami, ila atakayeteka kiasi cha kiganja cha mkono wake. Basi walikunywa humo isipokuwa wachache miongoni mwao. Basi alipovuka yeye na walioamini pamoja naye, walisema: Leo hatumuwezi Jaluti na majeshi yake. Wakasema: wale ambao wana yakini ya kukutana na Allah: Makundi mangapi machache yameyashinda makundi mengi kwa idhini ya Allah? Na Allah yupo pamoja na wafanyao subira



Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 250

وَلَمَّا بَرَزُواْ لِجَالُوتَ وَجُنُودِهِۦ قَالُواْ رَبَّنَآ أَفۡرِغۡ عَلَيۡنَا صَبۡرٗا وَثَبِّتۡ أَقۡدَامَنَا وَٱنصُرۡنَا عَلَى ٱلۡقَوۡمِ ٱلۡكَٰفِرِينَ

Na walipotoka (hadharani) kupambana Na Jaluti Na majeshi yake, walisema: Mola wetu! Tumi-minie subira, na uiimarishe miguu yetu na utupe ushindi dhidi ya watu makafiri



Sourate: AL-BAQARAH 

Verset : 251

فَهَزَمُوهُم بِإِذۡنِ ٱللَّهِ وَقَتَلَ دَاوُۥدُ جَالُوتَ وَءَاتَىٰهُ ٱللَّهُ ٱلۡمُلۡكَ وَٱلۡحِكۡمَةَ وَعَلَّمَهُۥ مِمَّا يَشَآءُۗ وَلَوۡلَا دَفۡعُ ٱللَّهِ ٱلنَّاسَ بَعۡضَهُم بِبَعۡضٖ لَّفَسَدَتِ ٱلۡأَرۡضُ وَلَٰكِنَّ ٱللَّهَ ذُو فَضۡلٍ عَلَى ٱلۡعَٰلَمِينَ

Basi waliwashinda kwa idhini ya Allah na Daudi akamuua Jaluti, na Allah akampa (Daudi) ufalme na utume na akamfundisha aliyoyataka. Na kama Allah asingewakinga watu baadhi yao kwa wengine, bila shaka ardhi ingeliharibika, lakini Allah ni Mwenye hisani kubwa mno kwa walimwengu