إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ سَوَآءٌ عَلَيۡهِمۡ ءَأَنذَرۡتَهُمۡ أَمۡ لَمۡ تُنذِرۡهُمۡ لَا يُؤۡمِنُونَ
Hakika, waliokufuru, ni sawa kwao umewahadharisha au hukuwahadharisha; hawaamini
خَتَمَ ٱللَّهُ عَلَىٰ قُلُوبِهِمۡ وَعَلَىٰ سَمۡعِهِمۡۖ وَعَلَىٰٓ أَبۡصَٰرِهِمۡ غِشَٰوَةٞۖ وَلَهُمۡ عَذَابٌ عَظِيمٞ
Allah amefunga nyoyo zao na usikivu wao, na katika uonaji wao kuna kifuniko, na watastahiki adhabu kubwa
وَمِنَ ٱلنَّاسِ مَن يَقُولُ ءَامَنَّا بِٱللَّهِ وَبِٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِ وَمَا هُم بِمُؤۡمِنِينَ
Na miongoni mwa watu wapo wanaosema[1] kuwa: “Tumemuamini Allah na Siku ya Mwisho” na[2] sio waumini (wa kweli)
1- - Kwa maneno tu.
2- - Ukweli ni kwamba…
يُخَٰدِعُونَ ٱللَّهَ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَمَا يَخۡدَعُونَ إِلَّآ أَنفُسَهُمۡ وَمَا يَشۡعُرُونَ
Wanamhadaa Allah na wale walioamini. Na hawahadai isipokuwa nafsi zao tu na wao hawatambui
وَمَثَلُ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ كَمَثَلِ ٱلَّذِي يَنۡعِقُ بِمَا لَا يَسۡمَعُ إِلَّا دُعَآءٗ وَنِدَآءٗۚ صُمُّۢ بُكۡمٌ عُمۡيٞ فَهُمۡ لَا يَعۡقِلُونَ
Na mfano wa waliokufuru ni kama mfano wa anayemwita asiyesikia ila (ni) sauti na kelele tu. Ni viziwi, mabubu, vipofu kwa sababu hiyo hawatumii akili[1]
1- - Wakayazingatia yale wanayo ambiwa.
زُيِّنَ لِلَّذِينَ كَفَرُواْ ٱلۡحَيَوٰةُ ٱلدُّنۡيَا وَيَسۡخَرُونَ مِنَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْۘ وَٱلَّذِينَ ٱتَّقَوۡاْ فَوۡقَهُمۡ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِۗ وَٱللَّهُ يَرۡزُقُ مَن يَشَآءُ بِغَيۡرِ حِسَابٖ
Makafiri wamepambiwa maisha ya dunia, na wanawadharau walioamini. Na Wacha Mungu watakuwa juu yao Siku ya Kiama. Na Allah anamruzuku amtakaye bila ya hesabu
ٱللَّهُ وَلِيُّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ يُخۡرِجُهُم مِّنَ ٱلظُّلُمَٰتِ إِلَى ٱلنُّورِۖ وَٱلَّذِينَ كَفَرُوٓاْ أَوۡلِيَآؤُهُمُ ٱلطَّـٰغُوتُ يُخۡرِجُونَهُم مِّنَ ٱلنُّورِ إِلَى ٱلظُّلُمَٰتِۗ أُوْلَـٰٓئِكَ أَصۡحَٰبُ ٱلنَّارِۖ هُمۡ فِيهَا خَٰلِدُونَ
Allah ni Mwenye kuwanusuru wale walioamini; huwatoa gizani na kuwapeleka kwenye mwangaza. Na ambao wamekufuru, watetezi wao ni Matwaghuti; huwatoa katika nuru na kuwaingiza kwenye giza. Hao ndio watu wa Motoni, wao humo watasalia milele
إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ بَعۡدَ إِيمَٰنِهِمۡ ثُمَّ ٱزۡدَادُواْ كُفۡرٗا لَّن تُقۡبَلَ تَوۡبَتُهُمۡ وَأُوْلَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلضَّآلُّونَ
Hakika, wale waliokufuru baada ya kuamini kisha wakazidisha ukafiri, toba zao hazitakubaliwa, na hao ndio hasa wapotevu
قُلۡ يَـٰٓأَهۡلَ ٱلۡكِتَٰبِ لِمَ تَكۡفُرُونَ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ وَٱللَّهُ شَهِيدٌ عَلَىٰ مَا تَعۡمَلُونَ
Sema: Enyi Watu wa Kitabu, kwanini mnazikanusha Aya za Allah na ilhali Allah ni Shuhuda wa mnayoyatenda?
ٱلَّذِينَ يَبۡخَلُونَ وَيَأۡمُرُونَ ٱلنَّاسَ بِٱلۡبُخۡلِ وَيَكۡتُمُونَ مَآ ءَاتَىٰهُمُ ٱللَّهُ مِن فَضۡلِهِۦۗ وَأَعۡتَدۡنَا لِلۡكَٰفِرِينَ عَذَابٗا مُّهِينٗا
Ambao wanaofanya ubahili na wanawaamuru watu wawe mabahili, na wanaficha fadhila alizowapa Allah. Na tumewaandalia makafiri adhabu inayodhalilisha
وَٱلَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمۡوَٰلَهُمۡ رِئَآءَ ٱلنَّاسِ وَلَا يُؤۡمِنُونَ بِٱللَّهِ وَلَا بِٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِۗ وَمَن يَكُنِ ٱلشَّيۡطَٰنُ لَهُۥ قَرِينٗا فَسَآءَ قَرِينٗا
Na ambao wanatoa mali zao kwa kujionesha (na kujitangaza) kwa watu, na hawamuamini Allah na Siku ya Mwisho. Na yeyote atakayemfanya shetani kuwa rafiki yake, basi (ajue kuwa huyo ni) rafiki mbaya sana
إِنَّ ٱلَّذِينَ يَكۡفُرُونَ بِٱللَّهِ وَرُسُلِهِۦ وَيُرِيدُونَ أَن يُفَرِّقُواْ بَيۡنَ ٱللَّهِ وَرُسُلِهِۦ وَيَقُولُونَ نُؤۡمِنُ بِبَعۡضٖ وَنَكۡفُرُ بِبَعۡضٖ وَيُرِيدُونَ أَن يَتَّخِذُواْ بَيۡنَ ذَٰلِكَ سَبِيلًا
Hakika, ambao wanamkufuru Allah na Mitume wake na wanataka kutenganisha kati ya Allah na Mitume wake, na wanasema: Tunaamini baadhi na tunakufuru baadhi, na wanataka kushika baina ya hayo njia (ya kati ambayo ni dini mseto inayochanganya baina ya Imani na ukafiri).[1]
1- - Aya inawakataza Waislamu kutofautisha baina ya Mitume ya Allah kama ilivyokuwa kwa Wayahudi ambao wamemuamini Mtume Mussa lakini wakataa kumuamini Mtume Isa na Mtume Muhammad, na kama ilivyo kwa Wakristo ambao wamemuamini Mtume Isa na kukataa kumuamini Mtume Muhammad. Pia aya inakataza kufanya ujanja wa kutaka kuunganisha dini zote hizo ili zionekane ni sahihi na zina mrengo mmoja unaopaswa kuwa pamoja.
أُوْلَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡكَٰفِرُونَ حَقّٗاۚ وَأَعۡتَدۡنَا لِلۡكَٰفِرِينَ عَذَابٗا مُّهِينٗا
Hao ndio makafiri kweli, na tumewaandalia makafiri adhabu yenye kukudhalilisha
وَٱلَّذِينَ كَفَرُواْ وَكَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَآ أُوْلَـٰٓئِكَ أَصۡحَٰبُ ٱلۡجَحِيمِ
Na waliokufuru na kuzikanusha Aya zetu (tulizoziteremsha kwa Mitume wetu), hao ndio watu wa Motoni
لَّقَدۡ كَفَرَ ٱلَّذِينَ قَالُوٓاْ إِنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلۡمَسِيحُ ٱبۡنُ مَرۡيَمَۚ قُلۡ فَمَن يَمۡلِكُ مِنَ ٱللَّهِ شَيۡـًٔا إِنۡ أَرَادَ أَن يُهۡلِكَ ٱلۡمَسِيحَ ٱبۡنَ مَرۡيَمَ وَأُمَّهُۥ وَمَن فِي ٱلۡأَرۡضِ جَمِيعٗاۗ وَلِلَّهِ مُلۡكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَمَا بَيۡنَهُمَاۚ يَخۡلُقُ مَا يَشَآءُۚ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٞ
Kwa yakini kabisa, wamekufuru wale waliosema: “Hakika Allah (Mungu) ndio Masihi bin Mariamu.” Sema: “Ni nani anayemiliki kuzuia jambo lolote litokalo kwa Allah akitaka kumuangamiza Masihi Mwana wa Mariamu na mama yake na wote waliomo ardhini (duniani)? Na ufalme wa mbinguni na ardhini na vilivyomo kati yake ni wa Allah (tu peke yake); anaumba atakacho. Na Allah ni Muweza wa kila kitu
لَقَدۡ كَفَرَ ٱلَّذِينَ قَالُوٓاْ إِنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلۡمَسِيحُ ٱبۡنُ مَرۡيَمَۖ وَقَالَ ٱلۡمَسِيحُ يَٰبَنِيٓ إِسۡرَـٰٓءِيلَ ٱعۡبُدُواْ ٱللَّهَ رَبِّي وَرَبَّكُمۡۖ إِنَّهُۥ مَن يُشۡرِكۡ بِٱللَّهِ فَقَدۡ حَرَّمَ ٱللَّهُ عَلَيۡهِ ٱلۡجَنَّةَ وَمَأۡوَىٰهُ ٱلنَّارُۖ وَمَا لِلظَّـٰلِمِينَ مِنۡ أَنصَارٖ
Kwa hakika kabisa, wamekufuru waliosema: Hakika, Allah ni Masihi Mwana wa Mariamu. Na Masihi (mwenyewe) alisema: Enyi Wana wa Israili, muabuduni Allah, Mola wangu Mlezi na Mola wenu Mlezi. Ilivyo ni kwamba, yeyote anayemfanyia ushirika Allah, hakika Allah amemharamishia Pepo, na makazi yake ni Motoni. Na madhalimu hawatakuwa na watetezi wowote
لَّقَدۡ كَفَرَ ٱلَّذِينَ قَالُوٓاْ إِنَّ ٱللَّهَ ثَالِثُ ثَلَٰثَةٖۘ وَمَا مِنۡ إِلَٰهٍ إِلَّآ إِلَٰهٞ وَٰحِدٞۚ وَإِن لَّمۡ يَنتَهُواْ عَمَّا يَقُولُونَ لَيَمَسَّنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ مِنۡهُمۡ عَذَابٌ أَلِيمٌ
Kwa hakika kabisa, wamekufuru waliosema: Allah ni Watatu wa utatu. Na (ilivyo ni kwamba) hakuna yeyote mwenye haki ya kuabudiwa isipokuwa Muabudiwa Mmoja tu. Na wasipokoma (kusema) hayo wanayoyasema, kwa yakini kabisa itawashika wale waliokufuru miongoni mwao adhabu iumizayo sana
أَوَمَن كَانَ مَيۡتٗا فَأَحۡيَيۡنَٰهُ وَجَعَلۡنَا لَهُۥ نُورٗا يَمۡشِي بِهِۦ فِي ٱلنَّاسِ كَمَن مَّثَلُهُۥ فِي ٱلظُّلُمَٰتِ لَيۡسَ بِخَارِجٖ مِّنۡهَاۚ كَذَٰلِكَ زُيِّنَ لِلۡكَٰفِرِينَ مَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ
Hivi aliyekuwa maiti, kisha tukampa uhai na tukamjaalia nuru ambayo anatembea nayo kati ya watu; (hivi) mfano wake atakuwa sawa na aliye gizani (ambaye) si mwenye kutoka humo? Kama hivyo tumewapambia makafiri yale waliyokuwa wanayatenda
تِلۡكَ ٱلۡقُرَىٰ نَقُصُّ عَلَيۡكَ مِنۡ أَنۢبَآئِهَاۚ وَلَقَدۡ جَآءَتۡهُمۡ رُسُلُهُم بِٱلۡبَيِّنَٰتِ فَمَا كَانُواْ لِيُؤۡمِنُواْ بِمَا كَذَّبُواْ مِن قَبۡلُۚ كَذَٰلِكَ يَطۡبَعُ ٱللَّهُ عَلَىٰ قُلُوبِ ٱلۡكَٰفِرِينَ
Hiyo ni miji tunakusimulia miongoni mwa habari zake. Na kwa hakika kabisa, Mitume wao waliwajia na hoja za wazi wazi. Basi hawakuyaamini yale waliyoyakadhibisha hapo kabla. Kama hivyo Allah anazipiga lakini nyoyo za makafiri
إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ يُنفِقُونَ أَمۡوَٰلَهُمۡ لِيَصُدُّواْ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِۚ فَسَيُنفِقُونَهَا ثُمَّ تَكُونُ عَلَيۡهِمۡ حَسۡرَةٗ ثُمَّ يُغۡلَبُونَۗ وَٱلَّذِينَ كَفَرُوٓاْ إِلَىٰ جَهَنَّمَ يُحۡشَرُونَ
Hakika wale waliokufuru hutoa mali zao ili kuzuia (kuiwekea vikwazo) njia ya Allah (Uislamu usimakinike na watu wasiufuate). Basi watazitoa (mali zao hizo), kisha zitakuwa majuto kwao, kisha watashindwa. Na waliokufuru watakusanywa katika Jahanamu tu
وَٱلَّذِينَ كَفَرُواْ بَعۡضُهُمۡ أَوۡلِيَآءُ بَعۡضٍۚ إِلَّا تَفۡعَلُوهُ تَكُن فِتۡنَةٞ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَفَسَادٞ كَبِيرٞ
Na wale waliokufuru baadhi yao ni watetezi wa wengine (hawawezi kumuhami Mwislamu). Msipofanya hayo (niliyokuamrisheni) itatokea fitina katika ardhi (katika nchi) na uovu mkubwa sana
إِنَّمَا ٱلنَّسِيٓءُ زِيَادَةٞ فِي ٱلۡكُفۡرِۖ يُضَلُّ بِهِ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ يُحِلُّونَهُۥ عَامٗا وَيُحَرِّمُونَهُۥ عَامٗا لِّيُوَاطِـُٔواْ عِدَّةَ مَا حَرَّمَ ٱللَّهُ فَيُحِلُّواْ مَا حَرَّمَ ٱللَّهُۚ زُيِّنَ لَهُمۡ سُوٓءُ أَعۡمَٰلِهِمۡۗ وَٱللَّهُ لَا يَهۡدِي ٱلۡقَوۡمَ ٱلۡكَٰفِرِينَ
Bila ya shaka yoyote, ubadili-shwaji (ucheleweshwaji) wa miezi mitukufu[1]) ni ukafiri ulio zidi walio kufuru wanautumia kuwapoteza watu wasijuwe miezi mitukufu; wanahalalisha mwaka mmoja na kuharamisha mwaka mwingine, ili wafanye kuwa sawa idadi ya ile (miezi) aliyoitukuza Allah. Kwa hivyo watahalalisha alivyo viharimisha Allah. Wamepambiwa vitendo vyao viovu. Na Allah hawa-ongozi watu makafiri
1- - Allah katika Aya iliyotangulia kabla ya hii ametaja kuwa katika miezi kumi na miwili ya mwaka ameteua miezi mine na kuifanya mitukufu. Ndani ya miezi hiyo mitukufu ameharamisha mambo mengi ikiwemo kupigana vita. Makafiri, kwa ukafiri wao, walikuwa wanaufanyia ukarabati utaratibu huu uliowekwa na Allah na kufanya mabadiliko ya miezi mitukufu kwa kuipa majina ya miezi mitukufu miezi mingine ili wapate fursa ya kufanya yale yaliyokatazwa katika miezi mitukufu. Allah anahesabu kitengo hiki ni ukafiri juu ya ukafiri.
يَحۡلِفُونَ بِٱللَّهِ مَا قَالُواْ وَلَقَدۡ قَالُواْ كَلِمَةَ ٱلۡكُفۡرِ وَكَفَرُواْ بَعۡدَ إِسۡلَٰمِهِمۡ وَهَمُّواْ بِمَا لَمۡ يَنَالُواْۚ وَمَا نَقَمُوٓاْ إِلَّآ أَنۡ أَغۡنَىٰهُمُ ٱللَّهُ وَرَسُولُهُۥ مِن فَضۡلِهِۦۚ فَإِن يَتُوبُواْ يَكُ خَيۡرٗا لَّهُمۡۖ وَإِن يَتَوَلَّوۡاْ يُعَذِّبۡهُمُ ٱللَّهُ عَذَابًا أَلِيمٗا فِي ٱلدُّنۡيَا وَٱلۡأٓخِرَةِۚ وَمَا لَهُمۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ مِن وَلِيّٖ وَلَا نَصِيرٖ
(Wanafiki) Wanaapa kwa (jina la) Allah kuwa hawakusema (hayo maneno yaliyokufikia). Na kwa hakika kabisa, walisema neno la ukafiri na wamekufuru baada ya kusilimu kwao na walikusudia kufanya ambayo hawakuyapata (ya kutaka kumuua Mtume na kuwafukuza Waislamu) na hawakuchukia ila tu kwa sababu Allah na Mtume wake wamewatajirisha (Waislamu kwa kuwapa neema mbali mbali) kutokana na fadhila zake. Basi iwapo watatubu itakuwa heri kwao na wakikengeuka, Allah atawaadhibu adhabu inayoumiza mno (hapa) duniani na (kesho) Akhera, na hawana katika ardhi yeyote wa kuwalinda wala wa kuwanusuru
إِنَّ ٱلَّذِينَ حَقَّتۡ عَلَيۡهِمۡ كَلِمَتُ رَبِّكَ لَا يُؤۡمِنُونَ
Hakika, wale ambao neno la Mola wako Mlezi limethibiti kwao, kamwe hawaamini
وَلَوۡ جَآءَتۡهُمۡ كُلُّ ءَايَةٍ حَتَّىٰ يَرَوُاْ ٱلۡعَذَابَ ٱلۡأَلِيمَ
Na (hawaamini) hata ziwajie Aya zote (miujiza ya kila aina) mpaka waione adhabu iumizayo mno
أَفَمَنۡ هُوَ قَآئِمٌ عَلَىٰ كُلِّ نَفۡسِۭ بِمَا كَسَبَتۡۗ وَجَعَلُواْ لِلَّهِ شُرَكَآءَ قُلۡ سَمُّوهُمۡۚ أَمۡ تُنَبِّـُٔونَهُۥ بِمَا لَا يَعۡلَمُ فِي ٱلۡأَرۡضِ أَم بِظَٰهِرٖ مِّنَ ٱلۡقَوۡلِۗ بَلۡ زُيِّنَ لِلَّذِينَ كَفَرُواْ مَكۡرُهُمۡ وَصُدُّواْ عَنِ ٱلسَّبِيلِۗ وَمَن يُضۡلِلِ ٱللَّهُ فَمَا لَهُۥ مِنۡ هَادٖ
Je, (analingana sawa yule) Msimamizi wa kila nafsi (na Mjuzi) wa wachumayo, na wakamfanyia Allah washirika! Sema watajeni. Au ndio mnampa (Allah) habari ya (washirika) asio na habari nao katika (mbingu na) ardhi; au (ndio mnawasifu hao washirika) kwa maneno matupu? Bali waliokufuru wamepambiwa vitimbi vyao na wamezuiliwa njia (ya haki). Na ambaye Allah amemuacha apotee basi hana wa kumuongoa
مَّثَلُ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ بِرَبِّهِمۡۖ أَعۡمَٰلُهُمۡ كَرَمَادٍ ٱشۡتَدَّتۡ بِهِ ٱلرِّيحُ فِي يَوۡمٍ عَاصِفٖۖ لَّا يَقۡدِرُونَ مِمَّا كَسَبُواْ عَلَىٰ شَيۡءٖۚ ذَٰلِكَ هُوَ ٱلضَّلَٰلُ ٱلۡبَعِيدُ
Mfano (wa kutisha wa) waliomkufuru Mola wao Mlezi, vitendo vyao (vyema ikiwemo kuunga udugu n.k Siku ya Kiyama havitawafaa) ni kama jivu linalopeperushwa kwa nguvu za upepo katika siku ya dhoruba. Hawawezi kupata chochote katika waliyoyachuma. Huo ndio upotevu wa mbali
۞أَلَمۡ تَرَ إِلَى ٱلَّذِينَ بَدَّلُواْ نِعۡمَتَ ٱللَّهِ كُفۡرٗا وَأَحَلُّواْ قَوۡمَهُمۡ دَارَ ٱلۡبَوَارِ
Kwani hukuwaona wale (maka-firi) waliobadilisha neema za Allah kuwa kufuru, na wakawafikisha watu wao kwenye nyumba ya maangamivu?
جَهَنَّمَ يَصۡلَوۡنَهَاۖ وَبِئۡسَ ٱلۡقَرَارُ
(Nao wataingia) Jahanamu, maovu yaliyoje makazi hayo!?
وَجَعَلُواْ لِلَّهِ أَندَادٗا لِّيُضِلُّواْ عَن سَبِيلِهِۦۗ قُلۡ تَمَتَّعُواْ فَإِنَّ مَصِيرَكُمۡ إِلَى ٱلنَّارِ
Na walimfanyia Allah washirika ili wapoteze watu kwenye Njia yake. Sema: Stareheni, kwani marejeo yenu ni Motoni